Subcribe to our RSS feeds Join Us on Facebook Follow us on Twitter Add to Circles

Alhamisi, 12 Juni 2014

UTAMBAJI WA HADITHI JUKWAANI.

Utambaji wa Hadithi Jukwaani

   Okpewho anajadili usimulizi wa hadithi katika Afrika. Anaeleza kuwa msimulizi wa kijadi ni tofauti na msimulizi anayepatikana katika maandishi. Usimulizi katika Afrika unafanyika wakati maalumu hasa wakati wa jioni au usiku watu wanapokuwa katika mapumziko baada ya vipindi maalumu vya kazi.

Usimulizi wa hadithi katika Afrika hufuata fomula maalumu. Usimulizi wa hadithi hizi huwa na mianzo na miisho ya kifomula ingawa mianzo na miisho hiyo hutofautiana toka jamii moja hadi nyingine. Kwa mfano matumizi ya paukwa pakawa, hadithi hadithi n k kutegemeana na utanzu husika.

Pia usimulizi wa hadithi unaambatana na ushiriki wa hadhira ambaye huonyesha kuwa anafuatilia simulizi hiyo.


Kwa jumla, utambaji wa hadithi jukwaani huwa na sifa kadhaa zinazoutambulisha. Sifa hizi huzitenga hadithi za mapokeo na zile tunazozisoma vitabuni. Utendaji huu unaandamana na sifa zifuatazo;

Usemi halisi. msemaji anasema moja kwa moja

Michepuko: msimuliaji hutoa kauli za pembeni au maoni yake. Anaiacha hadithi na kusema mambo ya pembeni au kando kabla ya kuendelea tena kuisimulia. Michepuko hii inaweza kuwa na jukumu la viliwazo hasa katika hadithi za kusikitisha au za kitanzia.

Urudiaji

Matumizi ya wakati uliopo kihistoria/ au uliopita kisimulizi. Utambaji au usimulizi huwa katika wakati uliopita lakini huchanganya pia na sifa zinazohusishwa na wakati uliopo ili kuhakikisha kuwa umbali uliopo kati ya hadhira na hadithi yenyewe umepunguzwa.

Kubadilisha muundo wa hadithi: mtambaji anauwezo wa kuubadilisha muundo wa hadithi kwa kuongeza vitushi fulani, kurudia visa fulani, kubadilisha msamiati, kurahisisha kisa, kutia ucheshi n.k. Kwa hakika kila utambaji hadithi moja huwa ni tofauti na utambaji wa hadithi hiyo wa mwanzoni yaani inafaraguliwa.

NADHARIA ZA FASIHI SIMULIZI

Nadharia huchukuliwa kuwa dira ya kumwongoza mtafiti au mchambuzi kulikabili na kulielezea vyema jambo fulani kwa tazamao unaotazamiwa kuwa imara zaidi kuliko ule wa nadharia nyingine. Nadharia hutoa mwongozo katika utatuzi wa jambo fulani ambalo halijaweza kuhakikishwa ukweli wake. Ni mawazo, maelezo au mwongozo uliopangwa ili kusaidia kutatua au kutekeleza jambo fulani, kwa upande wetu jambo la kifasihi simulizi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni