Aina za Vitenzi
- Vitenzi Halisi
- Vitenzi Visaidizi + Vitenzi Vikuu
- Vitenzi Vishirikishi
- Vitenzi Sambamba
Vitenzi Halisi
Hivi
ni vitenzi vinavyorejelea kitendo moja kwa moja. Vitenzi hivi
haziambatanishwi na vitenzi vingine katika sentensi. Vitenzi halisi
vinaweza kuambatanishwa na vitenzi
Kwa mfano soma, kula, sikiza
- Waziri Mwasimba aliwasili jana kutoka ng'ambo.
- Kawia atapikia wageni.
- Funga mlango wa dirisha.
Vitenzi Visaidizi na Vitenzi Vikuu
Vitenzi visaidizi hutumika kusaidia vitenzi vikuu katika sentensi ili kuleta maana inayokusudiwa kulingana na wakati au hali.
Kwa mfano -kuwa, -ngali,
- Jua lilikuwa limewaka sana.
- Bi Safina angali analala
Vitenzi Vishirikishi
Vitenzi vishirikishi hutumika kuelezea hali iliyopo au mazingira. Kuna aina mbili za vitenzi vishirikishi:
a) Vitenzi Vishirikishi Vikamilifu - havichukua viambishi vyovyote.
- Kaka yako ni mjanja sana.
- Huyo si mtoto wangu!
- Paka wake yu hapa.
b)
Vitenzi Vishirikishi Vipungufu - huchukua viambishi vya nafsi au ngeli.
Vitenzi hivi vinaweza kusimama peke yake au vinaweza kufuatiliwa na
vitenzi vikuu.
Kwa mfano ndiye, ndio, ndipo
- Sanita ndiye mkurugenzi wa kampuni
- Huku ndiko kulikoibiwa
Vitenzi Sambamba
Vitenzi
vikuu viwili au zaidi vinapoandamana katika sentensi huitwa vitenzi
sambamba. Aghalabu mojawapo ya vitenzi hivi hutumia viungo vingine kama
vile KI, KA, PO, KU n.k
Kwa mfano - alicheka akioga, alikula akashiba
- Kidori alilima akachoka.
- Mama ameenda kumtafuta baba.
- Mwalimu alikuwa ameanza kufundisha Juma alipoingia darasani.
Aina za Viwakilishi
Viwakilishi vya Nafsi
Viwakilishoi hivi hutumika kwa niaba ya nafsi kwa umoja na kwa wingi
Kwa mfano mimi, wewe, yeye, sisi, nyinyi, wao
Nafsi | Umoja | Wingi |
Nafsi ya Kwanza | mimi | sisi |
Nafsi ya Pili | wewe | nyinyi/ninyi |
Nafsi ya Tatu | yeye | wao |
- Sisi tuliwatangulia nyinyi kufika hapa.
- Mimi si mjinga kama vile yeye anavyofikiria
Viwakilishi Viashiria
Viwakilishi viashiria (vionyeshi) hutumika badala ya nomino kwa kutumia kuonyesha nomino inayorejelewa bila kuitaja.
Kwa mfano huyu, yule, hapa, n.k
- Hiki hakina maandishi yoyote.
- Hao hawajui tofauti ya viwakilishi na vivumishi
- Tumekuja hapa ili kuwaburudisha kwa nyimbo tamu tamu.
Viwakilishi Visisitizi
Hutumika kwa niaba ya nomino kwa kutumia kiashiria chake mara mbili mfululizo.
Kwa mfano yuyu huyu, wawa hawa, kiki hiki, papo hapo, mumu humu,
- Zizi hizi ndizo zilizovunjika wiki jana
- Yule yule aliyekamatwa juzi, ameiba tena
Viwakilishi vya Sifa
Husimama badala ya nomino kwa kurejelea sifa yake.
Kwa mfano -eupe, -zuri, -tamu, -embamba, -rembo
- Vyekundu vimehamisha
- Warembo wamewasili.
- Kitamu kitaliwa kwanza.
Viwakilishi vya Idadi
Hutumika kusimama badala ya nomino kwa kurejelea idadi yake.
a) Idadi Kamili - hutumia nambari kuelezea idadi ya nomino
Kwa mfano saba, mmoja, ishirini
- Wawili wamepigwa risasi polisi leo jioni.
- Alimpatia mtoto wake hamsini kununua chakula
b) Idadi Isiyodhihirika - huelezea kiasi cha nomino kwa ujumla, bila kutaja idadi kamili
Kwa mfano chache, nyingi, kadhaa, kidogo, wastani
- Tutazungumza na wachache kabla ya kuanzisha maonyesho yetu.
- Kadhaa zimeripotiwa kupotea.
Viwakilishi Viulizi
Viwakilishi viulizi hutumika kwa niaba ya nomino katika kuulizia swali.
Baadhi ya viwakilishi viulizi huchukua viambishi vya ngeli
Kwa mfano -ngapi?, -pi?
- Vingapi vinahitajika? - kuulizia idadi
- Zipi zimepotea?
Kunavyo viwakilishi viulizi vingine ambavyo havichukui viambishi vyovyote.
Kwa mfano wapi?, gani?, nini?, vipi?
- Gani imefunga bao hilo?
- Wapi hapana majimaji?
- Yule mvulana alikupatia nini?
- Uliongea naye vipi? - kuulizia namna
Viwakilishi Vimilikishi
Viwakilishi hivi hurejelea nomino kwa kutumia vimilikishi.
Kwa mfano -angu, -ako, -ake, -etu, -enu, -ao
- Kwetu hakuna stima.
- Lake limekucha.
- Zao zimeharibika tena
Viwakilishi Virejeshi
Hutumia O-rejeshi kurejelea na kusimamia nomino
Kwa mfano ambaye, ambao, ambalo, ambacho, huyo, yule
- Ambalo lilipotea limepatikana.
- Ambaye hana mwana, aeleke jiwe
Viwakilishi Vya A-Unganifu
Huwakilishi nomino kwa kutaja kinachomiliki nomino hiyo. Huundwa kwa kuambatanisha kiambishi cha nafsi/ngeli pamoja na kiambishi -a cha a-unganifu, kisha nomino nyingine
Kwa mfano cha, la, kwa, za, ya
- Cha mlevi huliwa na mgema
- Za watoto zitahifadhiwa.
|
Muundo wa Vitenzi
- Vitenzi vya Silabi Moja
- Vitenzi vya Kigeni
- Vitenzi vya Kawaida
Vitenzi vya Silabi Moja
Hivi
ni vitenzi vyenye silabi moja pekee. Ili kuleta maana kamili, vitenzi
hivi huambatanishwa na kiungo KU- katika kauli ya kutenda. Kama vitenzi
vingine, vitenzi vya silabi moja vinaweza kunyambuliwa.
mfano:
- -cha - kucha - jua linapochomoza asubuhi k.m kumekucha
- -fa - kufa - kuacha kupumua, kupoteza uhai k.m amekufa
- -ja- kuja - fika mahali hapa k.m nimekuja
- -la- kula - kutia chakula mdomoni k.m anakula
- -nya- kunya - kutoa mabaki ya chakula toka tumboni k.m mtoto amekunya
- -nywa- kunywa - kutia kinywaji kama vile maji au maziwa mdomoni k.m ninakunywa uji
- -pa- kupa - kumkabithi/kumpatia mtu kitu k.m amenipa pesa
- -pwa- kupwa - kujaa hadi pomoni - k.m kisima kimekupwa maji
- -ta- kuta -
- -twa- kutwa - jua linapozama magharibi na usiku kuingia k.m kumekutwa
- -wa- kuwa - kutokea katika hali au mahali fulani k.m alikuwa
Angalia mengi zaidi kuhusu vitenzi vya silabi moja katika ukurasa huu wa Mnyambuliko
Vitenzi Vya Kigeni
Hivi
ni vitenzi vyenye asili kutoka kwa lugha nyingine badala ya Kibantu.
Baadhi ya lugha hizo ni Kiarabu, Kizungu, Kireno, Kihispania n.k.
Vitenzi hivi havifuatilii muundo wa kawaida wa vitenzi vya Kiswahili
ambavyo huishia kwa sauti -a. Badala yake, vitenzi hivi huishia kwa
sauti nyingine kama vile -e, i, -o, na u
mfano:
-
- tubu
-
-
- thamini
- amini
- samehe
- baleghe
Vitenzi Vya Kibantu
Hivi
ni vitenzi vyenye asili ya Kibantu na ambavyo huishia kwa sauti -a.
Kitengo hiki hujumuisha asilimia kubwa zaidi ya vitenzi vya Kiswahili
mfano:
- simama
- shika
- tembea
- beba
- soma
- lia
|