Subcribe to our RSS feeds Join Us on Facebook Follow us on Twitter Add to Circles

Alhamisi, 12 Juni 2014

HISTORIA YA NADHARIA YA FASIHI SIMULIZI.

HISTORIA YA NADHARIA YA FASIHI SIMULIZI

            Historia ya nadharia ya fasihi simulizi ilianza katika elimu ya ushairi, balagha n.k. ya Wagiriki toka karne ya 18. Katika karne ya 20 nadharia hii imekuwa ni mkabala mkubwa katika usomaji wa matini. Kuna nadharia mbalimbali za kifasihi kama vile Umuundo, Umarksi, Ufeministi nk.

     Hivyo, tunaweza kujumuisha kuwa nadharia ya fasihi simulizi ni chombo kinachotoa mwongozo kuhusu mwelekeo wa jamii fulani. Hii ina maana kwamba ni mwangaza unaoimulika jamii juu ya mazingira na fikra zake. Kwa hali hiyo basi, nadharia hii haina budi kuzibainisha sifa na ushirikiano wa jamii husika.

Kuingia kwa ukoloni mamboleo kumefanya fikra na maarifa kutoka nje zitukuzwe na kuabudiwa huku fikra za ndani zikidumazwa kila kukicha. Kwa kufanya hivyo nadharia hizi zimeweza kuleta mabadiliko katika nadharia asilia zilizokuwepo. Kwa mfano; utamaduni wetu wa asili kama vile ususi, ufinyanzi, jando na unyago, nk zimebadilika baada ya kuingia kwa ukoloni mamboleo.

Hata hivyo, wahakiki wa Magharibi na Kiafrika wameangalia mambo mengi yaliyoikabili fasihi simulizi ya Kiafrika kama tutavyoona katika nadharia za fasihi simulizi tutakazopitia.

Nadharia za Fasihi simulizi tutakazojadili katika kozi hii ni hizi zifuatazo:

1: Nadharia za kitandawazi

Nadharia ya Ubadilikaji Taratibu (Evolutionalism Theory)
Nadharia ya Msambao (Diffusionism Theory)
Nadharia ya Kisosholojia (Sociological Theory)

2: Nadharia za kitaifa
3: Nadharia Hulutishi
1. Nadharia za Kitandawazi

Ubadilikaji Taratibu “Evolutionalism”

Mfuasi wa nadharia hii ni Charles Darwin (1809-1882) ambapo hoja zake zilikuwa na ushawishi mkubwa kwa wanafunzi waliokuwa wakijifunza kuhusu utamaduni kama vile Edward Burnet Tylor (1832-1917) na James George Frazer (1854-1941). Wote hawa waliamini juu ya misingi anuwai kuhusu kanuni zinazoongoza asili na maendeleo ya utamaduni wa mwanadamu.

Kundi hili liliona kuwa dhana ya ubadilikaji taratibu misingi yake mikuu ni viumbe hai. Wanaona kwamba viumbe hai vyote vinakuwa katika mchakato wa mabadiliko mbalimbali hadi kufikia maumbo vilivyonayo sasa.

Wanaedelea kusema kuwa kuna kanuni ambazo ni muhimu sana zinazochangia makuzi ya kanuni za binadamu. Wakaona kuwa kuna ukoo, akili au asili au jamii moja ambayo imezagaa ulimwenguni kote, na kama uchunguzi utafanywa wa kuchunguza jamii mbili kiutamaduni katika kipindi kilekile cha mabadiliko, itabainika kuwa elimu zao zina tabia zinazofanana.

Wanaendelea kusema kwamba, ili kuelewa jamii moja kwa ujumla ni vyema kulinganisha na jamii nyingine ya aina hiyo kwa kipindi kilekile cha ukuaji. Kwa mfano kuchunguza ngano za kijadi katika makabila mbalimbali ya Kusini kama vile uchawi na miviga na kulinganisha na jamii za Kiafrika.

Kwa ujumla katika nadharia hii tunabaini kuwa nadharia hii ilitawaliwa na mbinu linganishi (comparative methods).

Kwa mfano Frazer (kazi yake ni The Golden Bough ambayo ilikuwa katika majuzuu 13), alitafiti sanaa jadi ya Waitalia. Katika utafiti wake yeye alijihusisha na kutafiti chimbuko la matambiko ya uchawi na dini huko Italia. Alichokuwa anataka kuthibitisha kuhusu jamii ya Waitalia ni kwamba asili ya dini inapatikana katika magical rites za mtu wa kale.

Pamoja na watafiti wenzake, walikuja kama watawala na kuchunguza mila na desturi za Kiafrika ili kuzilinganisha na utafiti kama huo aliokuwa akiufanya huko kwao. Walitafiti na kuchunguza jamii ndogo ndogo za Kiafrika na kisha kufanya ulinganishi. Kwa ujumla wataalamu hao walikusanya, walitathimni fani mbalimbali za Kiafrika kama vile ngano, nyimbo, vitendawili, methali na aina nyingine, za FS katika jamii mbalimbali za Kiafrika. Baadhi ya watawala wataaluma wa kikoloni walitafiti kuhusu fasihi simulizi ya Kiafrika chini ya usimamizi wa Frazer ni pamoja na;
John Roscoe ambaye alitafiti jamii ya Baganda- Uganda.
Edwin Smith & Andrew Dale ambao walitafiti jamii ya Ila- Zambia.
Reverend Henri Junod- Tonga, Afrika Kusini
Robert Rattray- Akan-Ghana, pia Hausa- Nigeria
P. Amaury Talbot- Ekoi- Nigeria (Southeastern Nigeria)

H. Chatelain- Angola. Chatelain akichunguza kuhusu ngano za Angola na za Afrika kwa jumla, aligundua kuwa ngano za Kiafrika ni tawi toka mti mmoja wa ulimwengu.

Mwisho, wote kwa pamoja walihitimisha kuwa watu wa Afrika ni sawa na watu wengine popote pale ulimwenguni.

CHANGAMOTO

Dhana hii ya ubadilikaji taratibu iliathiri mbinu na matokeo ya utafiti wao kwa njia tofautitofauti kama vile:

Ø Kila kilichokusanywa katika fasihi simulizi kilihesabika kama masalia ya zamani au mabaki ya fasihi zilizotangulia.

Ø Kadri fani hizo zilivyorithishwa kwa njia ya mdomo toka kizazi kimoja hadi kingine ndivyo zilivyozidi kupoteza sifa mahsusi za ubora, zilichuja na kuchujuka

Ø Chochote kilichosalia lazima kitakuwa na dosari fulani tofauti na kitu halisi cha zamani

Ø Walijihusisha mno na maudhui na kamwe hawakujihusisha na sifa za kifani kama vile miundo na mitindo ya fani husika. Hii ni kutokana na ukweli kwamba lengo lao lilikuwa ni kufahamu hali halisi ya utamaduni wa jamii za watu wasiostaarabika na historia yao. Ili kuyafahamu haya waliona kuwa ni bora kupata muhtasari tu wa maudhui yanayojadiliwa ndani ya fasihi simulizi ya jamii husika na sio kujihusisha na fani ya fs hiyo

Ø Hawakuoa umuhimu wa fanani na mtambaji: “no creator, no author of such tales,…….as a product of joint or communal authorship.”

Ø Pia waliziona kazi za fasihi simulizi za Kiafrika kwamba hazina mwenyewe kwa kuwa ni mali ya jamii nzima. Walisema kwamba, ijapokuwa fasihi simulizi ni mali ya jamii, lakini sio kwa kiwango hicho walichokisema wao. Walisisitiza kuwa si kila mzungumzaji anaweza kuwa fanani wa fasihi simulizi. Wao walilipuuza suala la upekee wa muktadha.

HITIMISHO
Kimsingi, ilikuwa vigumu sana kupata matokeo sahihi katika uchunguzi ulioongozwa na misingi ya kiuibukaji. Hii ni kutokana na mbinu batili zilizotumika pamoja na kuongozwa na malengo muflisi na finyu kuhusu umbile la jamii za Kiafrika kwa jumla. Leo hii nadharia hii haitumiki tena katika mijadala ya fasihi simulizi. Wakoloni waliitumia kama njia ya kuhalalisha suala la uvamizi na ukoloni barani Afrika.

Nadharia ya Msambao “Diffusionism Theory”

Iliongozwa na mawazo na ushawishi wa Grimms na Thompson

Ni nadharia iliyopingana na nadharia ya ubadilikaji taratibu tuliyoona hapo juu. Wana ubadilikaji taratibu waliamini kuwa;
Ikiwa ngano mbili kutoka katika jamii mbili tofauti zimeonyesha kufanana kwa namna fulani za kimuundo au kimaudui ni kwa sababu wanadamu ulimwenguni kote wanamkondo mmoja wa mawazo na kufikiri kwao ni kwa namna moja, na kwamba ngano hiyo inasawiri hatua sawa za maendeleo ya kiutamaduni katika jamii husika.

Tofauti na wanaubadilikaji, wanamsambao wangeamini kuwa;

Pale ambapo kufanana kwa namna hiyo kutatokea, sababu ya msingi ya kuwapo kwa mfanano huo ni kuwa katika kipindi fulani hapo zamani sana jamii hizo mbili ziliwahi kukutana kwa namna fulani, makutano baina ya jamii hizo yalisababisha hali ya kuazimana kwa baadhi ya mila na tamaduni (mawazo) mojawapo ya jamii husika.

Watafiti hawa waliangalia mila na desturi za jamii zilivyokuwa zikikua na kusema kuwa zilikua kutokana na msukumo wa asili na lugha za Ulaya. Walikubaliana kwa sehemu kubwa kuwa asili ya mila, desturi na aina nyingine za utamaduni zinapatikana India, na walitaka kutafiti ni kwa kiasi gani utamaduni huu wa Indo-European ulikuwa umesambaa duniani.

Wana msambao nao walitumia mbinu ya ulinganishi kama walivyofanya wanaubadilikaji taratibu. Kazi ya utafiti ilihimizwa na wajerumani ambao ni Jacob na Wilhelm Grimm ambao walikusanya ngano nyingi kutoka India na kutoka katika nchi yao.

Jacob na Wilhelm Grimm: Walitafiti ngano kutoka India na Afrika, na walihitimisha kwamba, kuna kufanana kwa ngano za India na Ulaya. Wakatoa maamuzi ya kwamba, hadithi za Kiafrika ni chimbuko kutoka kwa wazazi wenye asili na utamaduni wa India na Ulaya. Hivyo, dhana yao hiyo waliifikia kutokana na kuifanyia kazi dhana potofu, kwani kila bara lina utamaduni, mila na desturi zake. Aidha waliliona bara la Afrika kama bara ambalo halijastaarabika.

Stith Thompson: Yeye aliwaunga mkono akina Jacob na Wilhelm. Katika kitabu chake cha The Folktale (1946:438) anapendekeza kuwa panapotokea kufanana kati ya ngano/hadithi za Ulaya na za Afrika, zinaweza kuelezewa kuwa huenda hadithi/ngano hizo zililetwa na Wazungu wakati wa utumwa.

Mawazo yao kwa ujumla ni kuwa;
Ø Utamaduni unaweza kusambaa tu kutoka katika jamii imara na maarufu tena yenye nguvu kuelekea kwenye utamaduni wa jamii iliyo kinyume chake “from superior to an inferior people)
Ø Ikiwa kulikuwa na kufanana kwa namna yoyote katika ngano zilizopatikana Afrika na Ulaya kwa mfano, lazima moja kati ya jamii hizo ni dhaifu kuliko nyingine, na jamii dhaifu….Afrika, ilihali jamii imara… ulaya
Ø Yote haya yangeweza kuelezwa tu kwa misingi ya ukweli kuwa jamii za Ulaya zilileta mambo hayo Afrika kutokea Ulaya kipindi cha biashara ya Watumwa (Thompson 1946:438)

Tafiti ziliendelea kufanyika baada ya Jacob, Grimm na Thompson ambapo bara la Afrika lilionekana kuwa bara lenye giza na hivyo kukaonekana haja ya kuanzisha dini ya Kikristo na teknolojia ya Ulaya barani Afrika ili Afrika iondokane na giza hilo.

Kwahiyo tunaweza kuona namna kila kitu cha Afrika ikiwemo fasihi simulizi yake vilivyodidimizwa na watawala hawa wa kikoloni.

Mapungufu

Tunaweza kusema kwamba, ingawa walijitahidi kuipa hadhi fasihi simulizi kwa kusisitiza upekee wa muktadha, hawakuchunguza kwa undani sifa za kisanaa za fasihi simulizi. Pia walijishughulisha na muhtasari tu wa simulizi walizochunguza, na hivyo ni dhahiri kwamba kuna vipengele vingine muhimu vya Fasihi Simulizi ya Kiafrika ambavyo havikutiliwa maanani..

Hitimisho

Ø Bado tafiti za namna hii hapa Afrika zinaendelea lkn mkabala na malengo ni tofauti

Ø Ule upendeleo uliokuwepo hapo zamani sasa umeondoka

Ø Sasa wanajihusisha na kutafiti msambao wa ngano na vipengele (units) vyake ndani ya tamaduni mbalimbali, katika bara la Afrika. Kama vile asili ya ngano za Kiafrika zinazosimuliwa katika Marekani ya Kusini na Kaskazini

Nadhari ya Sosholojia ‘Sociological Theory’

Mihimili ya Nadharia hii

(a) Umahsusi na sio umajumui

· Ilikuwa mahususi zaidi kuliko nadharia zilizotangulia: badala ya kujikita katika taaluma ya sanaa jadi kwa ujumla (maumbile ya mwanadamu na utamaduni wa mwanadamu) kama walivyofanya wanadharia wa zamani, nadharia ya usosholojia ilijikita katika jamii peke yake.

· Hii ilikuwa baada ya kugundua dosari zilizofanywa hapo kabla; dosari za kutoa matamko ya juu juu na ya kijumla zaidi

Ø Kauli hizo mara nyingi zilitupilia mbali vipengele fulani vya maisha kmv lugha na mienendo mingine….. hakika viliitofautisha jamii moja dhidi ya nyingine

Ø Kwao, tofauti zilizokuwepo baina ya jamii moja na nyingine zilikuwa na maana zaidi kuliko kufanana kulikokuwepo

· Kwa hiyo wanasosholojia waliazimia kuchunguza kila jamii kwa wakati na nafasi yake, kwa kurekodi kila kilichopatikana katika jamii husika (sanaa jadi yao).

· Wataalamu mbalimbali walioongoza jitihada hizi ni pamoja na hawa wafuatao

Ø Bronislaw Malinowski na A.R. Radcliffe-Brown (Uingereza)

Hawa walichunguza jamii mbalimbali katika Pasifiki, na waliandika mengi kuhusu jamii hizo. Jamii hizo ni pamoja na visiwa vya Trobriand na Andaman mutawalia

Ø Franz Boas (Marekani)

Huyu alichunguza jamii za wenyeji wa Marekani

· Wapo pia wataalamu wengi waliofanya utafiti wao, na kuandikia kuhusu jamii za Kiafrika ambao ni pamoja na hawa wafuatao

i. E.E. Evans-Pritchard………Nuer (Sudani)

ii. Geoffrey Lienhardt……..Dinka (Sudani)

iii. William Boscom…….Yoruba (Nigeria)

iv. S.F. Nadel………..Nupe (Nigeria)

v. Marcel Griaule……….Dogon (Burkina Faso)

Ingawa hata kabla ya wataalamu hawa, kulikwishakuwepo wataalamu wengine waliotafiti na kuandika kuhusu FS ya kiafrika lakini wataalamu hao waliongozwa na mawazo ya kiubadilikaji taratibu zaidi

(b) Mkazo katika Utendaji
-Tofauti na ilivyokuwa kwa wananadharia wa nadharia zilizotangulia ambao hawaku.... “They were not interested in studying the performers of oral tradition” wanasosholojia waliweka msisitizo katika kuchunguza PERFORMERS/watendaji wa fani mbalimbali za FS. Kutokana na msisitizo wao huu imebainika kuwa
*Fanani wa FS wana ujuzi na ustadi wa kiutendaji katika sanaa husika (ubunifu wao ni mkubwa sana). Jambo hili… limetusogeza mbele kidogo ktk kuielewa FS
*Wanasosholojia walidiriki na kuthubutu kudokeza kuhusu sifa za ndani za kimtindo katika FS ya kiafrika

(c) Msisitizo juu ya dhima ya Fasihi Simulizi katika jamii
Ø Tofauti na ilivyokuwa imedhaniwa hapo mwanzo kuwa FS ni mabaki tu ya zamani na kwamba hayakuwa na umuhimu wowote katika maisha ya jamii katika zama za kisasa, wanasosholojia waliamini kuwa uamilifu wa FS uko hai na haufi na kwamba unabadilika kulingana na maendeleo ya jamii husika. Dhima hizo ni pamoja na “DHIMA ZA KIJAMII ZA FS…KWA MUJIBU WA WANASOSHOLOJIA”
- FS ni kama Encyclopedia ya hekima za jamii husika
Hii ni kwa mujibu wa Bascom 1959 ambaye alifanya utafiti katika Poetry of Divination katika jamii za Wayoruba wa Nigeria
- FS ni nyenzo muafaka ya kurekodia hatua mbalimbali za maendeleo ya jamii husika. Aylward Shorter 1969…..the tales of origin katika jamii ya Wakimbu Tanzania
- FS inasaidia na imeendelea kusaidia kuimarisha ‘authority of statement or a custom in situation kama vile katika mahakama au contests for Chieftaincy. J.C. Massenger…..Anang of Nigeria 1958, J.B. Christenseu……Fante of Ghana 1958. Hawa walichunguza Methali katika jamii zilizotajwa
· CHANGAMOTO ZAKE…….Pamoja na uzuri uliotajwa bado kuna changamoto kadhaa
Ø Given far less time to illuminating and analyzing the artistic properties of African OL
Ø They have published tale, in flat, unimpressive prose, eliminating features of oral style (repetition and exclamation)
Ø They have done few carefully analyses of techniques of the original language that appealed to the audience of the tale in the first place
Ø The circumstances surrounding the performance of the tale (ushiriki wa hadhira, matumizi ya ala za muziki, nk) not reported
Ø Hata pale ambapo wamejaribu kuuleza vyema muktadha huu, umuhimu na nafasi yake katika kufanikisha au kukwamisha ngano husika haujaelezwa
Ø Ilikuwa vigumu sana kwa kutumia mbinu zao kuona ni kwa vipi ngano kwa mfano inaweza kuwa fasihi
Ø Pia kutokana na mbinu yao ya kusisitiza umuhimu wa FOLKLORE katika utamaduni wa watu, wataalamu kmv BOSCOM NA BEN-AMOS walisisitiza kuwa “Any judgement of a folk text must be based on the views of the society from which the text come” Wazo hili ni zuri sana lkn, ikiwa kazi za fs ya kiafrika zitaeleza mawazo ya wageni na si ya wenyeji, kmv boscom na amos, ni kwa sababu sanaa hizo zina sifa fulani fulani ambazo zinaenda na kueleza mambo fulani yaliyo mbali na dhana ya uzuri kwa waafrika. Mazingira km haya yakitokea, ni jukumu la mwandishi, ikiwa kweli wanaelewa vyema lugha husika, kufafanua sanaa husika na sifa za sanaa hiyo ilimuradi wageni waikubali sanaa husika na waipokee. Kwa hiyo mkabala wa MUKTADHA WA KIJAMII waliokuwa nao wanasosholijia ulikuwa FINYU SANA….. changamoto ya kiuhakiki ktk kazi za kifasihi
· HITIMISHO………..Hata kabla ya wataalamu hawa kufanya uchunguzi wa kisosholojia, walishakuwepo wataalamu wa mwanzo kama vile…………………….. ambao walifanya uchunguzi wa kisosholojia.
Ø Tofauti kubwa ni kuwa wale wa mwanzo waliongozwa na mawazo ya kiuibukaji
Ø Waliongozwa na kuhamasishwa na ….kizazi cha Franzer.
Ø Hawa wa baadaye walijihusisha na kuhamasika zaidi na “ HISTORIES OF THE CULTURES THEY STUDIED
Ø PIA waliongozwa na kuhamasishwa na mawazo ya Malinowski
Ø Pia hawa wa baadaye walitilia mkazo matumizi na uamilifu wa sanaa jadi za kiafrika katika jamii “SOCIETAL FUNCTIONS OF OL
Ø Hata hivyo, bado wataalamu hawa hawakufanikiwa au hitimisho lao halikuendana na tathimini ya karibu na kina kuhusu material walizozikusanya. Hii ni kwa sababu hawakuwa na ujuzi wa kutosha katika lugha za jamii za kiafrika


TOFAUTI KATI YA WANASOSHOLOJIA NA WANAUIBUKAJI AU WATAALAMU WENGINE WA MWANZO
· WATAALAMU WA MWANZO They were not interested in studying the performers of oral tradition
Ø Kwa sababu waliamini kuwa watendaji hawa walikariri tu mambo waliyoyapata kutoka kwa mababu zao siku za nyuma na kwamba wao wenyewe hawakuyaelewa mambo hayo, mengi yao. Hawakuyaelewa
Ø Pia waliamini kwamba, watambaji hawa walikuwa wajinga na washamba kabisa kiasi kwamba hawakuwa na uwezo w kuongeza ubunifu wowote katika sanaa hizo
Ø KWA UPANDE WAO wataalamu hawa waliweka msisitizo katika kuchunguza PERFORMERS wa fani mbalimbali za FS
Ø Kutokana na msisitizo wao huu tumebaini mambo murua yaendanayo na FS
i. Wamebainisha ujuzi na ustadi wa watendaji katika sanaa husika (ubunifu wao ni mkubwa sana)
jambo hili… limetusogeza mbele kidogo ktk kuielewa FS
Nadharia za Kitaifa

Utangulizi
· Je tunakumbuka changamoto za Nadhariaa zilizotangulia? Kwa mfano wanasosholojia?

Ø Hawakuwa na uelewa wa kutosha kuhusu lugha za Kiafrika.

Ø Kwa kiwango kikubwa waliathiriwa na dhana za kikoloni na upendeleo wa kibeberu: Afrika ni bara la giza na la washenzi wasiokuwa na aina yoyote ya ustaarabu, na walistahili kustaarabishwa na Wazungu kupitia mlango wa ukoloni.

· Dosari hizi ziliathiri pia uwezo wao katika kuchunguza FS ya Kiafrika

Ø Mara baada ya kutafiti, hawakuwa tayari kuchapisha matokeo halisi ya utafiti wao: waliyahariri

Ø Kwa kutumia msaada wa wenyeji (viongozi na wasomi wa mwanzo) walitafsiri tafiti hizo katika lugha za kigeni

Ø Kila ambacho hawakukielewa, walikifuta kutoka katika data zao

Ø HATIMAYE, sifa na ujumi wa fasihi simulizi ya kiafrika haukudhihirishwa (LITERARY QUALITIES OF AOL WAS NOT APPRECIATED)

· Kutokana na dosari hizo, palihitajika kundi la wanazuoni wenye ujuzi na mtazamo mwingine, tofauti na ule wa kikoloni.

Ø Ndipo walipojitokeza wanazuoni wa Kiafrika kmv. S.Adeboye Babalola wa Nigeria, Daniel Kunene wa Basotho, Kofi Awoonor wa Ghana na J.P. Clark wa Nigeria

Ø Lengo na azma yao ilikuwa ni kukosoa mawazo ya wanazuoni wa Kimagharibi. Kwa kweli walifanya hivyo, tena bila kuyatathmini vilivyo.

Ø Ilifikiriwa kuwa wataalamu hawa walikuwa na sifa maridhawa za kuimarisha uchunguzi katika FS ya Kiafrika. Kwa mfano, mtazamo chanya kuhusu Bara la Afrika, uzoefu wao kuhusu FS ya Kiafrika na ujuzi wao katika lugha za Kiafrika.

Ø Kwa kutumia nyenzo hizi, walijaribu kuboresha tafiti za zamani za kikoloni katika FS ya Kiafrika. Je waliboreshaje?

Waasisi

S. Adeboye Babalola

- Nigeria, aliandika The Content and Form of Yoruba Ijala (1966)

- Ijala ni Ushairi wa Wawindaji katika jamii ya Wayoruba

· Yaliyomo kwenye kitabu hiki ni yapi

Ø Usuli wa kitamaduni wa utendwaji wa Ijala

Ø Sherehe na matukio mengine ambapo aina hii ya ushairi inatambwa

Ø Maudhui ya Ijala

Ø Mafunzo ya Washairi wa Ijala

Ø Utendaji wa Ijala

Ø Mbinu za kimtindo katika Ijala (ladha ya Kishairi)
- Complex structure of imagery and allusion
- The manipulation of sounds and the voice
- Linguistic devices.. (poetic diction)

Ø Matini ya Mashairi ya Ijala katika lugha ya Kiyoruba

Ø Tafsiri ya Mashairi katika lugha ya Kingeraza

Ø Tanbihi (Footnote) inayofafanua mambo muhimu katika tafsiri

Daniel P. Kunene

- Basotho (1971) Heroic Poetry of the Basotho

Yaliyomo kwenye kitabu cha Kunene

Ø Uchambuzi wa kina kuhusu muundo wa sarufi ya Kisotho

Ø Dhana ya Ushujaa kwa Wasotho

Ø Mbinu zitumikazo kuchagua majina muafaka ya mashujaa

Ø Uchambuzi wa majina ya Sifo… praise Names

Ø Kutathmini ruwaza ya Takriri…..(fomula simulizi)

Kutathmini

Ø njia ambazo mshairi anajenga ishara…
- Vitu mbalimbali katika utamaduni unaozunguka
- Mazingira
- Vitu mbalimbali vinavyosifiwa

Ø Uhusiano kati ya Mtindo wa Kishujaa katika FS na athari yake kwa washairi wa Kisotho katika zama za kisasa

Wanazuoni wa Kimarekani: Milman Parry na Albert Lord

- Harakati za kudai uhuru barani Afrika

Ø Ushairi simulizi wa Kishujaa: mashujaa wa tendi Simulizi

J.P. Clark wa Nigeria

Ø Mhariri wa Ozidi Saga (1977)

· Katika Ozidi Saga tunasimuliwa kuwa

Ø Ozidi ni hadithi ya Kijadi inayosimuliwa kwa muda wa siku saba

Ø Inasimulia kuhusu mbinu za kivita za kitamaduni za Shujaa Ozidi

Ø Mambo au vitu vinavyoambatana na hadithi kmv

- muziki,

- nyimbo,

- dansi na

- uigizaji wa matuko au vitushi muhimu

Ø alirekodi kila kitu kilichowezekana kunaswa na tape recoda

- tendo au kauli kutoka kwa mtambaji lililosababisha hadhira kuangua vicheko. Katika hali km hii, fanani alilazimika kufanya uradidi wa kauli au matendo hayo. Hali hii inaonyesha athari ushiriki wa hadhira katika utendaji

- matendo au kauli zenye kuibua hali ya mshangao na mshituko kwa hadhira

- kauli zilizotolewa na watazamaji ktk hadhira kmv maswali na maoni kuhusu utendaji husika

- majibu ya msimuliaji kuhusu kauli hizo

- hali ya utendaji ambapo mziki unachezwa na kisha ladha au midundo Fulani ya kimuziki huimbwa na kikundi cha wanamuziki wa fanani

Hitimisho;

Kutokana na yaliyosemmwa na kutendwa na Wananadharia ya Kitaifa, mambo kadhaa tunaweza kuyasisitiza

Ø Wanazuoni wenyeji walifanikiwa kueleza na kufafanua ufanisi wa mbinu mbalimbali za kimtindo katika FS

Ø Wanazuoni wa kiafrika hawakuwa wa mwanzo kufanya uchunguzi wa namna hii, badala yake hata wazungu walikwishajaribu kufanya hivyo, tatizo lilikuwa kwenye mtazamo (wa kikoloni na wa kitaifa)

Ø Walirekodi hali na muktadha wote wa utendwaji wa FS

Ø Wazungu walikosea kutathmini FS ya kiafrika kwa sababu walitumia vigezo vya FA … yenye misingi na utamaduni wa kimagharibi. Kimsingi, hizi ni Fasihi mbili tofauti, zenye kutoka katika jamii mbili tofauti, na hivyo zinahitaji vigezo tofauti vya utathmini. Zina michakato tofauti ya kiubunifu.

Nadharia hulutishi / HYBRIDITY THEORY

Iliasisiwa na Wanazuoni wa Kiafrika wenye mtazamo kuwa hata wageni wamechangia sana katika kukuza taaluma ya FS ya Kiafrika. Miongoni mwa waasisi na wafuasi hawa ni pamoja na M.M.Mulokozi, Johson na Ngungi wa Thiong

· Katika nadharia zote zilizotangulia, wakiwemo wana nadharia za Kitaifa kulikuwa na changamoto mbalimbali. Hata hivyo, changamoto hizo zilitofautiana kutoka kundi moja la wananadharia hadi lingine. Kwa kuwa changamoto za nadharia nyingine zilikwisha jadiliwa, hapa tutajadili na kugusia tu zinazohusiana na nadharia za kitaifa

Ø Walipinga kabisa mawazo ya wanazuoni wa Kimagharibi

Ø Walidai kuwa Wananadharia wa Kimagharibi hawakutoa jambo lolote la msingi kuhusu Afrika.

· Kimsingi, wazo kuwa Wanazuoni wote na tena mawazo yote yaliyotolewa na Wageni hayafai katika taaluma ya FS ya kiafrika ni batili.

· Huu ndio msingi wa kuibuka kwa Nadharia Hulutishi

· Nadharia hulutishi zinaleta uwiano wa kitaaluma na kuibua mjadala kuwa

Ø Ingawa kwa kiwango kikubwa mawazo ya Wanazuoni wa Kigeni yalitawaliwa na dosari kadhaa, si kila walichokinena kuhusu Afrika, hususani utamaduni na Fasihi ya Kiafrika ni kibaya.

Ø Kwa mujibu wa Mawazo ya Wananazuoni wa Nadharia Hulutishi, yaliyosemwa na Wageni yanahitaji kuchambuliwa na kufanyiwa ufafanuzi wa kina. Ndani mwake mna dosari na pia mna uzuri wa namna fulani. hayapaswi kupuuzwa kabisa.

· Katika utafiti na uchunguzi wa masuala yanayohusu FS ya kiafrika ni vema kuchanganya
- Mbinu bora kutoka kwa kigeni (F ya kigeni na mbinu zao)
- Mbinu bora kutoka kwa wenyeji (F ya Kiafrika kwa kutumia mbinu za kiafrika)
· Matokeo yake, ilipatikana aina fulani ya fasihi yenye sifa Mchanganyiko, ndio maana iliitwa nadharia Hulutishi


Mchango wa Wageni ktk FS ya Kiafrika

1. RUTH FINNEGAN

- Alifanya utafiti na kuandika mengi kuhusu Afrika

- Miongoni mwa kazi zake ni pamoja na Limba Stories & Storytelling (1967), Oral literature in Africa (1970)

- Katika kazi zake hizi Finnegan anafanya yafuatayo kuhusu afrika na fasihi yao kwa ujumla

ü Anaukana muelekeo uliokuwepo wa kulitazama Bara la Afrika na Fasihi yao

Kutotilia maanani ubunifu wa fanani wa fs na bara la Afrika kwa ujumla

ü Anathamini sifa za kiubunifu za FS ya kiafrika

- Hata hivyo, naye hakusafika sana, kwani pamoja na mchango wake mzuri anatenda makosa kadhaa ya kiufafanuzi na kinadharia. Makosa haya yalileta athari kubwa kwa wanazuoni wa baadaye kuhusu umbo na sura halisi ya FS ya Kiafrika. Makosa ayatendayo ni yapi/

ü Afrika hakuna tendi

ü Afrika hakuna Visasili

2 . GORDON INNES

- Amechunguza tendi simulizi za jamii ya Wamandinka huko Gambia

- Katika uchunguzi wake alihimiza wasifu wa kila msimuliaji, na Muktadha wa utambaji wao, kmv matumizi ya ala za muziki

- Kutokana na utafiti wake alithibitisha na kuunga mkono wazo la Finnegan kuwa katika jamii za kiafrika kuna uwezekano kuwa, watambaji au wasimuliaji tofauti wenye kusimulia kisa kimoja kwa namna tofauti tofauti, tofauti hiyo inasababishwa na ujuzi wa mtambaji, uzoefu wa mtambaji na muktadha wa utambaji. Kwa maana hiyo basi, tunapata mawazo kuwa

ü Innes ana imani kuwa watambaji wa FS kwa kawaida hawana mtindo mmoja wa utambaji. Hii ni kwa sababu kila mmoja ana ustadi wake, uzoefu wake na muktadha tofauti na mtambaji mwingine.

2.5 Hitimisho na Tathmini

Katika hatua za hivi karibuni kumekuwapo na mapinduzi makubwa kuhusu FS ya Kiafrika na Bara la Afrika kwa Ujumla. Huu tunaweza kuiita mueleko mpya ambao “giving greater recognition to the literary qualities of African Oral Literature’. Swali ni kuwa je, muelekeo huu mpya umesaidia kwa kiasi gani mustakbali wa FS ya Kiafrika?

Ø Kuondolewa na kufutika kwa dhana potofu kuhusu Bara la Afrika

Ø Kukomaa kwa mtazamo chanya kuhusu FS ya kiafrika
- Methali na vitendawili “depth of wisdom
- Kiwango kikubwa cha ubunifu
- Utamaduni ambapo FS hii imechipuka ni changamani sana

Ø Kukua na kukomaa kwa taaluma ya F ya Kisasa ya Kiafrika

- Hapo mwanzo F ilitazamwa kama sehemu ya sanaa au tawi la Anthropolojia

- Sasa hivi, somo la F linasomwa na kufundishwa katika Vyuo na Taasisi mbalimbali kama somo linalojitegemea. Lina malengo yake, na nadharia zake

- Linaonyesha uhusiano mkubwa kati Fs ya kijadi na F ya kisasa ya kiafrika

Ø Uzuri na umaridadi wa utamaduni wa Kiafrika sasa hivi unatangazwa kwa njia ya kukusanya na kutafsiri mbinu na tanzu za FS ili kupata F ya kisasa. Katika utunzi mpya, mbinu za kisasa na za zamani za FS zinachanganywa pamoja

Ø Sasa, maswali mengi ya kiutafiti yamepatiwa ufumbuzi; sisi ni akina nani? Tuko wapi? Tunafanya nini? Kwa nini tuko hapa? Tumefikaje hapa tulipo leo hii? Je, hatua tuliyofikia inakidhi haja na matakwa ya kijamii katika hali zote (hususani haja ya kisanaa au kiubunifu? Kama haikidhi haja hiyo, tufanyeje ili tusonge mbele?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni