Maana ya Nadharia
ya isimumuundo. Mbinu za kimuundo katika uchanganuzi wa vipengele vya fonolojia.
Katika makala hii tutajadili maana ya
fonolojia na maana ya isimumuundo kasha usuli wa nadharia ya isimumuundo. Katika
kiini cha makala hiii ni Ubainishaji wa vipengele vya kifonojia na Ubainishaji
wa mbinu za kimuundo pamoja na ufafanuzi wa mbinu hizo katika vipengele vya
kifonolojia. Kisha tutahitimisha mjadala wetu.
Kwa mujibu wa Mugulu (1999)
akimrejelea Fudge (1973) anasema kwamba fonolojia ni kiwango kimojawapo cha
lugha fulani kilicho na vipashio vidogo zaidi kuliko vipashio vingine vyote vya
lugha. Vipashio vya kifonolojiani fonimu na alofoni zake.
Dosari ya fasili hii ni kwamba
haijafafanua kiwango kipi cha lugha ambacho kinahusika na fonolojia kwani lugha inaviwango mbalimbali.
Massamba (2010) anasema kuwa fonolojia
ni tawi la isimu linalojishughulisha na mfumo wa sauti (asilia) za lugha. Hii
inamaana kwamba, kila lugha mahususi inamfumo wake wa sauti ambamo maneno hujengwa.
Ki ukweli fonolojia hujihusisha na namna sauti zinavyotumika katika maneno ya
lugha mahususi katika kuleta maana.
Massamba na wenzake (2004) wanafafanua
kuwa, fonolojia ni tawi la isimu ambalo hujishughusha na uchunguzi, uchambuzi
na uainishaji wa sauti pambanuzi ambazo hutumika katika mifumo mbalimbali ya
sauti za lugha za binadamu.
Massamba (2010), pamoja naMassamba na
wenzake (2004), wanaonekana kufanana katika fasili zao juu ya fonolojia
isipokuwa, Massamba na wenzake (2004), wameonesha kuwa fonolojia si tawi
linalojihusisha na mfumo wa sauti tu, bali huzichunguza, huzichambua pamoja na
kuziainisha sauti hizo.
TUKI (1990) wanasema kuwa, fonolojia
ni tawi la isimu ambalo hushughulikia uchambuzi wa mfumo wa sauti zinazotumiwa
katika lugha fulani.
Vilevile dosari ya fasili hii ni
kwamba, imeegemea upande mmoja tu yaani uchambuzi wa mfumo wa sauti za lugha fulani
na kusahau kuwa taaluma hii ya fonolojia haijikiti tu katika uchambuzi bali
huzingatia uchambuzi, uchunguzi pamoja na uainishaji wa sauti hizo kama asemavyo
Massamba na wenzake (2004). “fonolojia ni tawi la isimu ambalo hujishughusha na
uchunguzi, uchambuzi na uainishaji wa sauti pambanuzi ambazo hutumika katika
mifumo mbalimbali ya sauti za lugha za binadamu.”
Kwa mujibu waMatthews (2001)anafafanua
kwamba, Isimumuundo ni tawi la isimu ambalo hutumika kama kihuzi cha kinadharia
kinachochunguza au kuchambua na kuelezea muundo wa lugha kwa kuzingatia
vipengele vya lugha pamoja na uhusiano wake katika kuunda kitu kikubwa zaidi.
Pia isimumuundo ni mkabala unaochambua
na kufafanua mfumo wa lugha kama unavyojibainisha ukilinganisha na kipindi
maalum katika historia.
Baada ya kuangalia fasili hizo ufuatao
ni usuli wa nadharia ya isimumuundo kwa mujibu waMatthews (kishatajwa).
Nadharia ya umuundo ilianzia Ufaransa miaka ya 1900 na mwanzilishi wake ni
Ferdinand de Saussure katika dhana yake ya langue (umilisi) na parole (utendi).
Nadharia ya isimumuundo imejadiliwa na
matapo makuu mawili yaani tapo la Ulaya na tapo la Marekani
Awali ya yote wanasimu wa awali
walijaribu kuchunguza lugha kwa kulinganisha zaidi na historia. Ferdinand
hakuridhika na ulinganishaji huo kwani aliona kwamba ulikuwa unajibu swali kuwa
asili ya lugha hiyo ni wapi, lakini haikujibu swali kuwa hiyo lugha inamfumo
gani.
Tapo la Ulaya lilitoa hoja kuu
zifuatazo katika nadharia hii:
Lugha inamfumo, yaani lugha ni mfumo
ambao una elemeti zinazotagusana.
Lugha ni mfumo wa alama: kwa mfano
kelele ni lugha endapo tu zitawasilisha au kuelezea mawazo fulani, mfano dhana
(dhahania), kiashiria na kiashiriwa.
Lugha hushughulika katika viwango
viwili ambavyo ni langue (umilisi) na parole (utendi)
Baada ya tapo la Ulaya lilifuata tapo
la Marekani ambalo nalo lilifafanua dhana ya umuundo au nadharia hii ya isimu
muundo kama ifuatavyo: Hapo awali watu walijishughulisha na uchunguzi wa lugha
za Marekani yenye asili ya kihindi, walikuwa wanaanthropolojia, lakini
ilionekana kuwa hawakuwa na mbinu mahususi ambazo wangezifuata ili kuweza
kufafanua lugha hizo.
Kutokana na mapungufu hayo wakatokea
wanaumuundo wa kimarekani walioongozwa na Bloomfield ambaye yeye aliona kuwa
uchunguzi wa lugha unapaswa kujikita katika kile watu wanachokisema. Hivyo basi
walipendekeza hoja kuu zifuatazo.
Isimu ni sayansi fafanuzi; yaani
inafafanua kile watu wanachokisema na sio kile wanachotakiwa kusema.
Kila lugha ni mfumo ulio na taratibu
zake: lugha haipaswi kuchambuliwa kwa kutumia lugha nyingine, bali inapaswa
kuchambuliwa kwa kutumia mfumo wake wenyewe.
Lugha ni mfumo ambao vipashio
vidogovidogo zaidi huunganika kimpangilio ili kuunda vipashio vikubwa zaidi.
Wanamuundo hawa walipendekeza taratibu ambazo walianza kuzitumia kwa kuchambua
vipashio vidogo kabisa na kuviainisha na kuvipambanua katika ruwaza ambazo
zilitumika kuunganisha ilikuunda vipashio vikubwa zaidi.
Maana haipaswi kuwa sehemu ya
ufafanuzi wa kiisimu. Bloomfield na wafuasi wengine wa tapo hili waliona kuwa
maana ni dhana ya kinasibu ambayo haiwezi kuchunguzika, kwa hiyo si ya
kisayansi.
Taratibu za kutambua vipashio katika
lugha ni lazima ziwe halisi na zenye kufuata taratibu maalum.
Baada ya usuli wa nadharia ya
isimumuundo, vifuatavyo ni vipengele vya kifonolojia pamoja na mbinu za
kimuundo katikaufafanuzi wa vipengele hivyo(kifonolojia) kwa mifano. Vipengele
hivyo ni sauti (foni), alofoni, fonimu na silabi. Pia mbinu zitumikazo na
wanaisimumuundo katika ufafanuzi wa vipengele hivyo ni mbinu ya uainishaji,
sintagmatiki, paradigmatiki, moza, jozi pekee, mpishano huru, mgawanyo
kamilishani, mgawanyo wa kiutoano, na ubadala.
Kwa kuanza na mbinu ya uainishaji. Kwa
mujibu wa Kamusi ya Karne ya 21(2011), uainishaji ni “upangaji wa vitu au
viumbe katika makundi kwa mujibu wa jinsi vinavyohusiana.”
Hivyo basi, katika muktadha wa
kifolonojia tunaweza kusema kuwa, uanishaji ni upangaji wa vipashio katika
makundi kulingana na nduni zake bainifu au uhusiano wake. Kwa mfano: kosonanti
za Kiswahili ziliainishwa kulingana na namna zinavyotamkwa, mahali pa matamshi
na hali ya nyuzi sauti.
Kwa mfano: konsonanti “m”, “n”, “g” waliziainisha
kama nazali pamoja na kuzipa sifa zake kama vile; [m] [n]
+kons +kons
+nazali +nazali
+midomo +ufizi
+ghuna +ghuna
Hivyo kila sauti waliipa nduni za
ziada na nduni bainifu, zilizotofautisha fonimu moja na nyingine. Kwa mfano
fonimu; “s” na “l”
[s]=kikwamizi [l]= kitambaza
+kons +kons
+kikwa +kitambaza
+ufizi +ufizi
-unazali
-unazali
-ghuna +ughuna
Mbinu ya pili sintagmatiki;
sintagmatiki ni ubadilishanaji wa nafasi ya vipashio vya kifonolojia (fonimu)
kwa njia ya mlalo. Hivyo katika lugha ya Kiswahili vipashio kwa kawaida
hupangwa katika mfuatano maalum wenye mahusiano, ambao ni;
K+I – b+a = ba mfano katika neno “baba”
K+K+I – c+h+a = cha mfano katika neno “chama”
K+K+K+I – m+b+w+a = mbwa mfano katika neno “mbwa”
Hivyo basi mbinu hii ya sintagmatiki
imejikita zaidi katika kuangalia mpangilio sahihi wa sauti katika lugha husika
kiulalo. Na kamwe huwezi kukuta neno “ngoma”limeandikwa ngmoa, au kata – ktaa.
Vilevile hata muundo wa silabi za
Kiswahili hubainishwa idadi yake kwa kufuata mbinu ya kisintagmatiki, yaani
kuhesabu kwa ulalo kuanzia kushoto kuelekea kulia. Mfano neno “Anajichekelesha”
neno hili lina silabi 7 ambazo ni $$ A$$ na $$ ji $$ che $$ ke $$ le $$ sha $$
1 2 3
4 5 6
7
Mbinu ya tatu ni mbini ya
paradigmatiki, neno paradigmatiki limetokana na neno paradigm likiwa na maana
ya kundi la vitu vinavyoweza kukaa pamoja kutokana na mahusiano yao.
Hivyo paradigmatiki kwa mujibu wa The
New American Dictionary paradigmatiki ni mahusiano wima baina ya vipengele vya
kiisimu vinavyounda muundo mkubwa zaidi kama vile sentensi. Kwa hiyo, nadharia
hii hubainisha vipashio kiuwima zaidi. Kwa mfano;
m
mw
nafasi iliyokaliwa na /m/ inaweza kukaliwa na mu pia mw
w
Pia katika muundo wa lugha ya
Kiswahili sauti huweza kubadilishana nafasi kiparadigmatiki (wima) na kuunda
neno jingine lenye maana tofauti na lile la awali. Kwa mfano katika neno “pata”
tunaweza kupata maneno yafuatayo kwa kubadilisha fonimu (konsonanti) kiuwima;
/p/+/a/+/t/+/a/ = (pata)
/b/+/a/+/t/+/a/ = (bata)
/k/+/a/+/t/+/a/ = (kata)
/n/+/a/+/t/+/a/ = (nata)
Vilevile tunaona kwamba katika maneno
hayo kama tutatoa kosonanti au sauti /p/ na kuweka irabu au sauti /e/ ni
dhahiri kwamba maneno hayo hayatakuwa na maana yoyote katika lugha ya Kiswahili
kwa sababu lugha ya Kiswahili haina mfuatano wa I+I+K+I katika kuunda silabi
badala yake inamfuatano wa K+K+I
Mbinu ya nne ni mbinu ya moza, kwa
mujibu wa McCarthy (1989), moza ni mapangilio wa vipashio ulio katika mkururo.
Mbinu hii huangalia mpangilio wa kimfuatano katika fonimu. Kwa mfano; foni “abc”
zitafuatana na fonimu “xyz” inategemewa kwamba mpangilio wa “abc” unaweza tu
kufanana na “xyz” na sio “yxz” nk.
Mfano.1mama, baba, kaka lala
walewale, kulekule, vilevile,
imba, cheza, kula, oga
Maneno haya katika mfano.1 yapo katika
mfuatano na mpangilio wa sauti unaokubalika katika lugha ya Kiswahili.
Mfano.2 mmaa, bbaa, kkaa, aall
wlwlaeae, klkluuee, vvlliiee
iamb, chzea, uakl, oag
Maneno katika mfano.2 hayapo katika
mfuatano na mpangilio wa sauti unaokubalika katika lugha ya Kiswahili.
Mbinu nyingine ya kimuundo inayotumika
katika utambuzi wa vipengele vya kifonolojia kama vile fonimu ni mbinu ya jozi
sahili au jozi pekee.
Hapa wanamuundo huchukua maneno mawili
yanayofanana kwa idadi mfano, bata [bata] = sauti nne na bati [bati] = sauti
nne. Katika maneno haya sauti zinazotofautiana ni /a/ na /i/ kwa sababu hizi ni
fonimu mbili tofauti.
Pia maneno haya yana maana mbili
tofauti kutokana na sauti tofauti yaani /a/ na /i/. Vilevile maneno kata na
bata tunapata maana mbili tofauti kutokana na sauti mbili tofauti yaani /k/ na
/b/
Mbinu nyingine ni ile ya mgawanyo
kamilishani; mbinu hii inadai kwamba kuna mazingira ambapo kuna sauti mbili
zinazofanana ambapo sauti hizo mbili zinagawana mazingira ya kutokea. Kwa
mfano: kama “A” ikitaokea katika mazingira ya kwanza basi haiwezi kutokea
katika mzaingira ya pili. Kamwe haziingiliani. Lakini katika lugha ya Kiswahili
hakuna sifa kama hii. Sifa hii tunaipata katika lugha ya Ciruri/chiruri.
Kwa mfano neno “Imbusi” – mbuzi = “Ogubusi”
– mbuzi mkubwa.
Mbinu nyingine ni mbinu ya mpishano
huru, katika mbinu hii kuna kuwa na sauti mbili ambazo zinaweza kutokea sehemu
yoyote au mazingira yoyote bila ya kikwazo. kwa mfano; Gari – ghari
Zambi – dhambi
Agenda – ajenda
Mbinu hii hutumika katika kubainisha
alofoni za fonimu moja.
Mgullu (1999) akimrejelea Hyman (1975)
anaeleza kuwa mbinu nyingine ambayo hutumiwa wakati wa kuchambua sauti ambazo
ni fonimu au alofoni za lugha fulani ni ile ya mgawanyo wa kiutoano. Utoano ni
dhana ambayo imeelezwa vizuri na Hyman kuwa, katika fonolojia ni dhana ambayo
hutumiwa kuelezea uhusiano uliopo baina ya sauti mbili au zaidi ambazo haziwezi
kutokea katika mazingira sawa.
Mfano, katika lugha ya Kiingereza kuna
sauti /P / yenye mpumuo na sauti /P/ isiyo na mpumuo ambazo tunaelewa wazi kuwa
[P ] hutokea mwanzoni mwa neno tu, kwa
mfano, katika /pin/, /pen/, /put/, nk. Kwa upande mwingine /p/ isiyo na mpumuo
hutokea sehemu yoyote ya neno isipokuwa mwanzoni. Hapa tunapata kigezo muhimu
sana cha kutofautisha fonimu na alofoni.
Hivyo basi, mbinu walizotumia
wanamuundo katika uchambuzina ufafanuzi wa vipengele vya kifonolojia zimekuwa
msingi mkubwa sana katika uchambuzi wa data mbalimbali za lugha duniani na
ndizo zimekuwa chanzo cha kuwafanya wanaisimu yaliofuatia kupata mahali pa
kuanzia katika kufanya uchunguzi wa lugha mbalimbali duniania.
MAREJEO:
Jewell, E. J and A. Frank. (2005). The
New Oxford American Dictionary. (2nd Edit).Oxford University Press.
New York.
Mdee, J. S. na wenzake (2011). Kamusi
ya Karne ya 21.Longhorn Publishers (K) Ltd. Nairobi.
Massamba, D.P.B na wenzake. (2009).Fonolojia
ya Kiswahili Sanifu (Fokisa): Sekondari na Vyuo.Taasisi
ya Uchunguzi wa Kiswahili. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Massamba, D.P.B. (2010). Phonological
Theory: History and Development. Institute of Kiswahili Studies
(IKS). Dar es Salaam.
Metthews, P. (2001). A short History
of Structural Linguistics. Cambridge University Press. British.
McCarthy, J.J. (1989). “Linear Order
in Phonological Representation.”Linguistics Department
Faculty Publication Series Paper 45.http:// scholarworks.umass.ed/linguist_faculty_pubs/45
Mgullu, R.S. (1999).Mtalaa wa isimu:
Fonetiki, Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili.
Longhornpublishers.Ltd. Nairobi.
TUKI, (1990).Kamusi Sanifu ya Isimu na
Lugha. Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mambo
yaliyosababisha kuibuka kwa nadharia Ya mofofonemiki kwa mifano kutoka katika lugha mbalimbali.
Makala
hii itajadili Maana ya mofofonemiki, Historia fupi ya mofofonemiki, Mambo
yaliyosababisha kuibuka kwa nadharia ya mofofonemiki kisha hitimisho na
marejeo.
Kwa kuanza na fasili ya mofofonemiki kwa mujibu wa mtandao wa Wikipedia wanafafanua
mofofonemiki kuwa ni tawi la isimu linalojishughulisha na mwingiliano wa
mishakato ya kimofolojia na kifonolojia au kifonetiki. Pia hujishughulisha na
mabadiliko ya sauti yanayotokea katika mofimu wakati zinapoungana kuunda
maneno. (Tafsiri yetu).
Fasili hii ina mapungufu fulani kwani,
mofofonemiki haijishughulishi na michakato yote ya kifonolojia na kimofolojia
bali ni baadhi tu ya michakato hiyo ambayo ilishindwa kufafanuliwa kwa kutumia
data za kifonolojia au kifonetiki peke yake.
The
New Oxford American Dictionary inafafanua kwamba, mofofonolojia/mofofonemiki ni tawi la
isimu linalojishughulisha na uwakilishi wa kifonolojia wa mofimu.
Hivyo basi tunaweza kusema kuwa, mofofonemiki
ni tawi la isimu linaloshughulikia matumizi ya kimofolojia katika kueleza
baadhi ya tofauti za kifonolojia ambazo isingewezekana kuzielezea kwa kutumia
data za kifonetiki au kifonolojia peke yake.
Baada ya kuangalia fasili ya neno
mofofonemiki ifuatayo ni historia fupi ya nadharia ya mofofonemiki.
Kwa mujibu wa Massamba (2010:82)
akimrejelea Martnet (1965) anafafanua kwamba, istilahi hii
mofofonemiki/mofofonolojia ilipendekezwa kwa mara ya kwanza na N.S. Trubetzkoy
(1929). Trubetzkoy alitumia istilahi hii kwa maana ya tawi la isimu
ilinaloshughulikia matumizi ya mafolojia katika kuelezea baadhi ya tofauti za
kifonolojia ambazo isingewezekana kuzielezea kwa kutumia data za kifonolojia au
kifonetiki peke yake.
Baada ya kuangalia historia fupi ya mofofonemiki
yafuatayo ni mambo yaliyosababisha kuibuka kwa nadharia ya mofofonemiki.
Kuchunguza
ubadilikaji wa sauti ambao usingeweza kuelezwa kwa kutumia data za kifonolojia
peke yake. Baadhi yao wakapendekeza kuwapo kwa kiwango cha kimofofonemiki
pamoja na kipashio umbo kiini kama kiwakilishi cha mofimu, kwa hiyo
walipendekeza hivyo baada ya kushindwa kujua ipi ni alofoni ya fonimu ipi kwa
kutumia kigezo cha kifonetiki pekee Kwa
mfano; walishindwa kujua /k/ ni alofoni
ya /c/ au /c/ ni alofoni ya /k/ Kwa mfano hata katika lugha ya kurusi –
ruka = “mkono”
ručnoj = “a
mkono”
Mzizi ni – ruk na ruč
Wanamofofonemiki walichunguza wakagundua
kuwa katika mazingira fulani /k/ hubadilika kuwa /č/ baada ya kufuatiwa na “noj”.
Hivyo wakapendekeza umbo kiini la maneno haya ni ruKa au ruČnoj umbo kiini lake
lilitambulika kama {K} au {Č}
Katika
lugha ya Kiswahili kuna mabadiliko ya sauti yanayotokea katika baadhi ya maneno
baada ya sauti fulani kufuatiwa na kiambishi cha unominishaji (i) kwa mfano
katika maneno yafuatayo;
Fuata – fuasi
Penda – Penzi
Cheka – Cheshi
Pika – Pishi
Pia wanamofofonemiki walichunguza
ubadilishanaji huu wa sauti kwani walishindwa kujua ipi ni alofoni ya fonimu
ipi. Ndipo wakagundua kuwa katika mazingira fulani /t/ hubadilika kuwa /s/
baada ya kufuatwa na mofimu ya unominishaji “i” pia sauti /d/ hubadilika na
kuwa /z/ baada ya kufuatwa na mofimu ya unominishaji “i”.
Baada ya kupendekeza umbo kiini maneno
haya yakaandikwa kama ifuatavyo: kwa mfano neno {fuaTa} umbo {T} likawa umbo
kiini ambalo linawakilisha sauti zote mbili yaani /t/ na /s/, pia neno {piKa}
umbo kiini lake ni {K} ambalo linawakilisha sauti /k/ na /ʃ/
Kuchunguza mabadiliko ya sauti
yanayotokea mofimu zinapoungana. Kwa mfano; katika lugha ya Kiswahili,
U + ima – wima
I + etu – yetu
Mu + alimu – Mwalimu
U + imbo – wimbo
Vi
+ ake –
vyake
Wanamofofonemiki wakagundua kuwa sauti
fulani huweza kuungana na kuunda sauti moja na kubadili umbo la neno.
Chunguza muundo wa kifonolojia wa
mofimu katika lugha. Kwa mfano katika lugha ya Kiswahili;
Mu + huni – Mhuni
Mu + gonjwa – Mgonjwa
Mu + guu – Mguu
Mu + uguzi – Muuguzi
Mu
+ tu – Mtu
Wanamofofonemiki wakagundua kwamba
mofimu fulani huweza kuungana na mofimu nyingine na kuunda umbo la neno.
Kuchunguza ubadilishanaji wa sauti
ambao una una uamilifu wa kimofolojia lakini husababisha mabadiliko fulani ya
kifonetiki. Kwa mfano katika lugha ya kiingereza;
Play + s – [pleiz]
Dog + s – [dogz]
Since – [sins]
Else – [els]
Place
– [pleis]
Wanamofofonemiki wakachunguza kinachosababisha
kuwepo na maumbo tofauti tofauti ya mofimu ya wingi. Kwa mfano; /s/, /iz/, /z/
Wakagundua kuwa kuna mchakato zaidi ya ule wa kifonolojia ambao ni wa
kimofolojia unaosababisha umbo ‘s’ kutamkwa /z/ au /iz/ au /s/
MAREJEO:
The New Oxford American Dictionary. (2005), (2ndEdit), Oxford University
Press. New York.
Swali:Kwa kutumia data ifuatayo bainisha mabadiliko ya sauti yaliyosababishwa
na mazingira ya kifonolojia pekee, kimofolojia pekee na kimofofonolojia. Onesha
kwa mifano kutoka katika data jinsi wanamofofonolojia walivyofanikisha kutatua
matatizo ya kimofofonolojiaData.
Iba
|
Wizi
|
Cheka
|
Mcheshi
|
Mguu
|
Miguu
|
Nkindiza
|
Nkindiza
|
Mkuki
|
Mkuki
|
Mvuvi
|
Mvuvi
|
Katika
kujibu swali hili tumeligawanya katika sehemu tatu. Katika sehemu ya kwanza
tumetolea maana ya istilahi mbalimbali kwa mujibu wa wataalamu mbalimbali.
Istilahi hizo ni pamoja na maana ya fonolojia, mofolojia na mofofonolojia,
sehemu ya pili tumejadili kiini cha swali ambapo tumeonesha mazingira
mbalimbali ya utokeaji wa data tulizopewa na suluhisho la wanamofofonolojia katika
kutatua matatizo ya kimofofonolojia na sehemu ya tumehitimisha kazi na kutoa
marejeo.
Kwa kuanza na maana ya istilahi hizo watalaamu wanatueleza kama
ifuatavyo;
Massamba
na wenzake (2004) wanaeleza kuwa; fonolojia kama tawi la isimu ambalo
hujishughulisha na uchunguzi, uchambuzi na uainishaji wa sauti pambanuzi ambazo
hutumika katika mifumo mbalimbali ya sauti za lugha za binadamu. Hii ina maana
kwamba fonolojia kama tawi la isimu hujishughulisha hasa na zile sauti ambazo
sauti ambazo hutumika kutofautisha maana za maneno katika lugha mahususi.
John
Habwe na Peter Karanja (2004) wanaeleza kuwa; fonolojia ni utanzu wa isimu
unaochunguza jinsi sauti za lugha zinavyofanya kazi katika lugha mbalimbali.
Fonolojia huchunguza jinsi sauti hizo zinavyotumika, zinavyounganishwa na
kupangwa katika lugha yoyote mahususi ili kuunda tungo zenye maana.
Hivyo
kutokana na maana za wataalamu hawa tuanaweza kueleza kuwa; fonolojia ni tawi
la isimu linalojishughulisha na uchunguzi, uchambuzi na ufafanuzi wa sauti
katika lugha mahususi. Mfano Kiswahili, Kiingereza Kichina, Kijerumani na
Kihaya.
Baada ya kueleza maana ya fonolojia tuangalie maana ya mofolojia
kulingana na wanataalamu mbalimbali.
Massamba na wenzake (2004) wanaeleza kuwa; mofolojia ni tawi
la isimu linalojishughulisha na uchunguzi, uchambuzi na uainishaji wa maneno
katika lugha.
John Habwe na Peter Karanja (2004) wanatueleza kuwa;
mofolojia ni neno linalotumiwa kumaanisha utanzu wa isimu unaoshughulikia
muundo wa maneno. Fasili hii inamapungufu kwani katika mofolojia
hatushughulikii miundo ya maneno katika lugha bali kinachoshughulikiwa ni
maumbo ya maneno. Miundo ya maneno katika taaluma ya isimu inashughulikiwa na
tawi na sintaksia.
Kutokana na fasili za wataalamu hawa tunaweza kueleza kuwa;
mofolojia ni tawi la isimu linalojishughulisha na uchunguzi, uchambuzi na
ufafanuzi wa maumbo ya maneno katika lugha. Baada ya kuangalia maana ya
fonolojia na mofolojia ifuatayo ni maana ya mofofonolojia;
Massamba (2010) akimnukuu Martinet (1965) ambapo Martinet
alinukuu kutoka kwa Trubetzkoy (1929) anatueleza kuwa; mofofonolojia kama
ilivyotumiwa na Trubetzkoy ilimanisha sehemu ya isimu ambayo ingeweza kutumia
mofolojia kuelezea tofauti fulani za kifonolojia ambazo zisingeweza kuelezwa
kwa kutumia data za kifonolojia peke yake.
Baada ya kuangalia maana za istilahi mbalimbali zilizotumika
katika swali hili, kifuatacho ni kiini cha swali kinachoonesha mabadiliko ya
sauti yaliyotokea katika data tuliyopewa ambayo ni mabadiliko kifonolojia pekee, kimofolojia pekee na kimofofonolojia.
Tukianza na mabadiliko ya kifonolojia pekee, haya hutokea
kwa namna tofauti au katika mazingira tofauti. Kwa mfano mazingira hayo ni;
udondoshaji, uyeyushaji, muungano wa sauti, nazali kuathiri konsonanti na
konsonanti kuathiri nazali.
Hivyo
kutokana na data yetu katika kubainisha mazingira ya mabadiliko ya sauti kifonolojia pekee ni kama ifuatavyo;
Mvuvi [ ɱ vuvi ]
Badiliko
lililotokea hapa ni la kifonolojia katika mchakato wa usilimishaji wa nazali
yaani konsonanti kuathiri nazali. Hapa tunaona kuwa sauti ya midomo /m/
imesilimishwa na kubadili sehemu yake ya kutamkia na kuchukua sifa ya
midomomeno / ɱ / baada ya kukabiliana na sauti ya midomomeno /v/. Hivyo
sauti /m/ imebadilika na kuwa / ɱ /.
Katika
mabadiliko ya sauti ya sauti ya kitambaza /l/ kubadilika na kuwa kipasuo /d/
pia ni mabadiliko ya kifonolojia hii ni katika neno;
n-limi [
ndimi ]
Utokeaji
wake ni kutokana na kanuni ya nazali
kuathiri konsonanti. Mazingira ya utokeaji wake ni sauti / l / inapokabiliana na nazali / n
/ yenye sifa ya kutamkiwa sehemu moja yaani kwenye ufizi hubadilika na kuwa
/ d /.
Pia mabadiliko nazali /n/ kipasuo cha kaa laini [ ŋ ] ni ya kifonolojia ambayo utokeaji wake
ni wakiusilimishaji au kanuni ya konsonanti kuathiri nazali. Mazingira ya
utokeaji wake ni sauti ya nazali kuathiriwa na konsonanti inayoiandamia hivyo
kuifanya nazali kuifuata konsonanti mahali pa kutamkia. Mabadiliko hayo
yameathiri sauti ya nazali /n/ na kutamkwa kama nazali ya kaa laini [ ŋ ].
Hivyo katika uwakilishi
litakuwa;
Umbo
la ndani [ ŋkindiza ]
Umbo
la nje nkindiza.
Baada
ya kueleza mabadiliko ya kifonolojia, tutazame mabadiliko ya kimofolojia.
Kutokana na data hii tunapata maumbo kama;
Mguu mi-guu
Haya
ni mabadiliko ya kimofolajia. Mazingira ya utokeaji wake ni mabadiliko ya
uongezaji au upachikaji wa mofimu ya
umoja na wingi ambapo; mofimu m- ya umoja imebadilika na kuwa mofimu mi- katika
wingi.
M-guu umbo
la umoja
Mi-guu
— umbo la wingi.
Pia katika neno mkuki
mkuki, mabadiliko yaliyotokea ni
ya kimofolojia tu kwani hakuna mabadiko ya umbo na kinachoonekana ni uwepo wa
mofimu m- ya umoja katika umbo hili pamoja na mzizi -kuki. hivyo kilichofanyika
ni kuongeza -kuki katika mofimu hiyo ya umoja na kupata neno m-kuki. Hivyo umbo
hili linabakia na umbo lake ambalo hubakia kuwa vilevile.
M-kuki
m-kuki, maumbo yote haya yako katika umoja
Vilevile katika neno M-dalasini m-dalasini, hakuna mabadiliko ya kimofolojia bali umbo
limeendelea kuwa vilevile la umoja.
Baada
ya kuangalia mabadiliko ya kifonolojia na kimofolojia katika data tulitopewa,
kipengele kinachofuatia ni kubainisha mabadiliko ya sauti yaliyotokea kwa mabadiliko
ya kimofofonolojia.
Kutokana
na data yetu maneno;
Iba mwizi
Cheka mcheshi
Haya
ni mabadiliko ya kimofofonolojia. Sababu ya kuwepo kwa mchakato huu ni uwepo wa mbadilishano wa
sauti ambayo hayakuweza kufafanuliwa kwa utaratibu wa fonolojia pekee na
utaratibu wa mofolojia pekee hivyo kukawa na hitaji kubwa kuwa na kiwango
kingine cha kuweza kutatua changamoto hiyo. Kwa hiyo kuibuka kwa mofofonolojia
kulikuwa na lengo la kumaliza changamoto hiyo iliyokuwepo.
Hivyo katika mabadiliko iba wizi,
sauti ya kipasuo cha midomo /b/ kubadilika kuwa sauti ya kikwamizi cha ufizi
/z/ imesababishwa na kuwepo kwa irabu /i/ ya unominishaji mwishoni mwa sauti
/b/. Kutokana na kitendo cha “kuiba” tungetarajia kupata nomino “mwibi” kutokana
na mofimu {mu-ib-i}. Lakini tunapata neno [w-iz-i]. Hapa konsonanti ya kipasuo
cha midomo /b/ hudhoofika na kuwa konsonanti ya kikwamizi cha ufizi [ z ]
katika mazingira ya kutanguliwa na irabu ya unominishaji /i/.
iba [ w-iz-i ]
Pia
katika neno cheka mcheshi, mabadiliko
yaliyotokea hapa ni ya kimofofonolojia ambapo sauti ya kipasuo cha kaakaa laini
/k/ inabadilika na kuwa sauti ya kikwamizi cha kaakaa gumu [ ∫ ] baada ya
kufuatiwa na irabu ya unominishaji /i/.
Cheka [ mče∫i ]
Uwepo
wa mabadiliko sauti na umbo ambayo hayawezi kuelezwa, kwa mchakato wa fonolojia
na mchakato wa kimofolojia ndipo
palipoibuka mchakato wa kimofofonolojia.
Katika
utatuzi wao wanamofofonolojia walikuja na dhana ya umbo kiini. Umbo kiini hili
liliwakilisha fonimu mbili. Waliteua umbo kiini kwenye neno la msingi. Na
liliwekewa mabano mchirizi { }.
Kwa mfano katika
cheka mcheshi
Neno
la msingi ni “cheka” ambapo waliteua sauti {K} kuwa umbo kiini. Fonimu {K} iliteuliwa
kuwakilisha /k/ yenyewe katika neno
cheka ambalo ni kitenzi na inawakilisha sauti [ ∫ ] kwenye
“mcheshi” ambayo ni nomino. [k]
{K}
[ ∫ ]
Umbokiini {K}
linawakilisha sauti /k/ na [
∫ ]
Pia
katika neno iba na wizi umbokiini ambalo liliteuliwa ni {B} ambayo kuwakilisha
sauti /b/ na sauti sauti /z/.
[ b ]
{B}
[ z ]
Baada
ya utatuzi huu baadhi ya wataalamu walitoa
maoni yao juu ya umbokiini. Baadhi yao ni Linhtner (1970) akinukuliwa na
Massamba (2010) anaeleza kuwa umbo kiini sio halisi ni la kidhahania na
kinasibu kwani halioneshi mchakato na namna ambavyo sauti na umbo hubadilika na
kuwa katika sauti nyingine na kitu gani hasa husababisha mabadiliko hayo ya
sauti. Umbokiini huishia tu katika kuteua sauti moja kuwakilisha sauti
nyingine. Basi huo ukawa udhaifu wa dhana ya umbokiini.
Hitimisho,
kutokana na wanamofofonolojia kushindwa kutatua matatizo ya kifonolojia
wakaibuka wanafonolojia zalishi ambao waliokuja na mitazamo mipya katika
utatuzi wa matatizo ambayo yalishindwa kutatuliwa na wanamofofonolojia ambapo
walikuja na dhana ya misingi na mihimili ya kufuata ili kubainisha mabadiliko
yaliyokuwa yanatokea yaliyoshindwa kuelezeka.
Marejeo.
Habwe,
J. na P, Karanja (2004) Misingi ya Sarufi
ya Kiswahili. Nairobi: Phoenix Publishers
Ltd.
Massamba,
D.P.B. na wenzake (2004) Fonolojia ya
Kiswahili Sanifu (FOKISA): Sekondari
na Vyuo. Dar es Salaam. TUKI.
Massamba,
D.P.B. (2010) Phonological Theory:
History and Development. Dar es Salaam:
TUKI.
Michakato ya
kiusilimisho katika fonolojia.
Katika
kujadili mada hii tutalenga kuangalia michakato ya kiusilimisho namna inavyotumika
katika kuyakokotoa maumbo ya ndani kwenda maumbo ya nje katika lugha ya
Kiswahili. Lakini kabla ya kuonesha ukokotozi huo ni vyema kwanza tuangalie
maana ya mchakato, maana ya usilimisho, umbo la ndani na nje, kisha tutaelekea
kwenye hitimisho pamoja na marejeo.
Tuki
(2004) inaeleza kuwa mchakato ni mfululizo wa shughuli unaosababisha kitu
fulani kufikiwa.
Hivyo
katika uwanja huu wa fonolojia tunaweza
kusema kuwa mchakato utakuwa unafanyika pale ambapo mofimu mbili
zinapokutanishwa huweza kutokeza mabadiliko fulani katika mofimu mojawapo au
kutotokea badiliko lolote. Mfano viungu hubadilikia kuwa vyungu,kietu
hubadilika kuwa chetu hapa tunaona kuwa mabadiliko yametokea lakini miti
hubakia kuwa miti, kiti hubakia kuwa kiti na hapa tunaona kuwa hakuna
mabadiliko yoyote yaliyotokea.
Massamba
(2011) anaeleza kuwa kuna aina mbili za michakato asilia yaani mchakato
usilimisho na mchakato sio-usilimisho. Lakini katika mjadala huu tutajikita kwa
kuangalia mchakato mmoja tu yaani ule wa kiusilimisho, ambao Massamba anasema muwa
usilimisho ni pale ambapo kitamkwa kimoja hufanywa kifananefanane na kitamkwa
kilicho jirani yake kwa maana kwamba hupata baadhi ya sifa za kipande sauti
chenziye kilicho jirani. Kwa mfano, konsonanti inaweza kupata baadhi ya sifa za
irabu au irabu ikapata baadhi ya sifa za konsonanti, na konsonanti moja huweza
kuathiri konsonanti nyenziye au irabu moja huweza kuathiri irabu nyenziye. Pia anaendelea
kusema kuwa usilimisho unaweza kuhusisha michakato kadhaa kama
vile,unazalishaji wa irabu, utamkiaji pamwe wa nazali, ukaakaishaji,
ughunishaji kati irabu, uhafifishaji kati irabu, tangamano la irabu,
ughunishaji konsonanti shadda, muungano.
Habwe
na Karanja (2004), wanaeleza kuwa usilimisho ni kule kufanana kwa fonimu kwa
kiasi au kikamilifu kutokana na kuathiriana. Hapa sauti jirani katika neno
huathiriana kiasi kwamba fonimu hupokea ama kupoteza sifa za kifonetiki kwa
fonimu jirani, na matokeo yakiwa kuwa fonimu hizi hukabiliana sana katika
kufanana. Pia wanaendelea kusema kuwa usilimisho unaweza kuhusisha kuimarika,
kodhoofika, kuingizwa, kudondoshwa, au kuungana kwa fonimu katika neno.
Hivyo
tunaweza kusema kuwa usilimisho ni kule kufanana kwa fonimu kwa kiasi au
kiukamilifu kutokana na kuathiriana kwake kunakosababishwa na fonimu iliyo
jirani.
Baada ya kuangalia utangulizi huo sasa
ni wakati wa kukokotoa michakato hiyo ya kiusilimisho kutoka umbo la ndani
kwenda la nje.
Lakini
kabla ya kukokotoa kwanza tuangalie umbo la ndani kuwa ni namna umbo lenyewe
linavyoumbwa na mofimu zake au tunaweza kusema kuwa ni umbo la neno ambalo
halijafanyiwa michakato yoyote ya mabadiliko. Na umbo la nje ni lile
lililofanyiwa mabadiliko au michakato na mara nyingi huakisi umbo la ndani.
Michakato itakayooneshwa ni ile ambayo imeorodheshwa na wataalamu lakini ambayo
inahusiana na lugha ya Kiswahili tu kwani mingine inahusiana na lugha zingine
kwa mfano michakato ya Massamba ameingiza michakato miwili inayohusiana na
lugha za kigeni ambayo ni ughunishaji
kati irabu na uhafifishaji kati
irabu, hivyo hiyo hatajadiliwa.
Unazalishaji wa irabu
Massamba (2011) anadai kuwa unazalishaji wa
irabu ni aina ya usilimisho ambao irabu hupata sifa ya unazali kutokana na
irabu yenyewe kutangamana na konsonanti ambayo ni nazali. Hivyo irabu nyingi
hupewa sifa za unazali kutokana na ama kufuatiwa kwa nazali ama kutanguliwa na
nazali. Na alama inayowakilisha unazalishaji ni alama ya kiwimbi [ ̴ ] ,zaidi tuangalie mifano ifuatayo.
Mifano
umbo
la ndani
|
umbo
la nje
|
/nondo/
|
[nondo]
|
/penya/
|
[penya]
|
/mama/
|
[mama]
|
/ngambo/
|
[ ambo]
|
/nyumba/
|
[ umba]
|
/muwa/
|
[muwa]
|
Hivyo sauti zote zilizowekewa alama ya
kiwimbi ( ̴
) zina unazali kwa sababu zimefuatana na nazali na hivyo zimefanywa kuwa unazali.
Kanuni
katika Kiswahili
I I
N
Kanuni
ya jumla.
+kons
+naz -kos
+naz
|
+naz
|
|
|
Ukaakaishaji
Mgullu
(1999) akimnukuu Les (1984), anadai kuwa ukaakaishaji wa fonimu hutokea ambapo
fonimu zisizo za kaakagumu zinapobadilika na kuwa za kaakagumu. Yeye anadai
kuwa katika Kiswahili sauti za kaakagumu zipo mbili tu yaani /ɟ/ na /ʧ/ ambazo ni vizuiwa kwamizwa. Anamalizia
kwa kusema kuwa ukaakaishaji wa fonimu hutokea wakati ambapo fonimu zisizo
vizuiwa kwamizi hubadilika na kuwa vizuiwa kwamizwa. Hii katika ukokotozi wake
unakuwa kama ifuatavyo.
umbo
la ndani
|
umbo
la nje
|
umbo
la nje
|
/ki+enu/
|
[kjenui]
|
[ enu]
|
/ki+eusi/
|
[kjeusi]
|
[ eusi]
|
/ki+ombo/
|
[kjombo]
|
[ ombo]
|
/ki+umba/
|
[kjumba]
|
[ umba]
|
/ambaki+o/
|
[ambakjo]
|
[amba o]
|
Hapa
tunaona kwamba kipasuo cha kaakaalaini /k/ hubadili mahali pa matamshi na kuwa
kizuiwa kwamizi /ʧ/ cha kaakaagumu katika mazingira ya kufuatiwa na sauti /ϳ/.
Kanuni yake /i/ [ ]
I =
kisha inabadilika kuwa
/k/ [
] /i/
Kanuni ya jumla.
-sila +stn’d +sila
+juu + juu -kons
+nyuma +k’gumu -nyuma
-fulizwa +juu
-ghuna
|
|
Uyeyushaji
Uyeyushaji,
wataalamu wengine huita irabu kuwa nusu irabu Mgullu (1999). Huu ni mchakato
ambapo irabu irabu za juu /u/ na /i/ hubadlika na kuwa /w/ au / j/ katika
mazingira ya kufuatiwa na irabu zisizofana nazo. Kwa kifupi ni kwamba /u/
inapofuatiwa na irabu yoyote isiyofanana nayo hubadilika kuwa [w] na /i/
ikifuatiwa na irabu yoyote isiyofanana nayo hubadilika na kuwa [j].
Hivyo
tunaweza kusema kuwa uyeyushaji ni kanuni inayoelezea mabadiliko ya sauti
(irabu) na kuwa kiyeyusho aidha [w] au [j] hii ni kwa irabu zote za juu
zinapofuatana na sauti zingine zisizofanana nazo. Na sauti hizo hubadilika
katika mazingira ya /u/ hubadilika kuwa [w] inapofuatana na irabu nyingine
isiyofanana nayo na / i/ inabadilika na kuwa [ϳ]
pia inapofuatana na irabu isiyofanana nayo.
Mfano
wa /u/
umbo
la ndani
|
umbo
la nje
|
/mu+aminifu/
|
[mwe:mbamba]
|
/ku+enu/
|
[kwe:nu]
|
/mu+
anafunzi/
|
[mwa:nafunzi]
|
/mu+eupe/
|
[mwe:upe]
|
/mu+embe/
|
[mwe:mbe]
|
Hivyo tunaona wazi kabisa kuwa irabu ya juu nyuma /u/ imebadilika na kuwa kiyeyusho [w] katika
mazingira ya kuatiwa na irabu isiyofanana nayo ambayo ni /a/ na /e/ kwa hapo juu lakini hata ikiwa
ni /o/ huweza kubadilisha.
Kanuni /u/ [w] I = u
Mfano
wa irabu /i/
/umbo
la ndani/
|
[umbo
la nje]
|
/mi+embe/
|
[mje:mbe]
|
/mi+endo/
|
[mje:ndo]
|
/mi+ezi/
|
[mje:zi]
|
/mi+anzo/
|
[mja:nzo]
|
/mi+eusi/
|
[mwe:usi]
|
/mi+oyo/
|
[mjo:jo]
|
Hivyo
tunaona kuwa irabu ya juu mbele /i/ hubadilika na kuwa [j] inapofuatana na
irabu nyingine isiyofanana nayo ambayo ni /e,a na o/.
Kanuni yake /i/
[j] I/= i
Kanuni ya jumla.
+juu -sila
+sila
+mbele + juu
+juu
+juu -sila
+juu
+nyuma +juu +nyuma
+nyuma
|
|
|
Tangamano la irabu (usilimisho wa irabu
pekee)
Huu
ni mchakato wa kiusilimisho baina ya irabu na irabu katika kuathiriana kiasi
kwamba hulazimika kufuatana. Katika mchakato huu kinachotokea ni kwamba, kama
irabu ya mzizi ni /i, u au a/ basi irabu ya kiambishi cha utendea lazima
kiwe ni [i] , wakati irabu ya mzizi ikiwa ni/ e au o/ katika hali ya utendea kiambishi chake
kitakuwa ni [e]. Mfano.
umbo
la ndani
|
umbo
la nje
|
/imb+a/
|
[Imb-i-a]
|
/andik+a/
|
[andik-i-a]
|
/dak+a/
|
[dak-i-a]
|
/chun+a/
|
[ un-i-a]
|
/og+a/
|
[og-e-a]
|
/ ez+a/
|
[ ez-e-a]
|
/kom+a/
|
[kom-e-a]
|
Hapa tumeona kuwa
mofimu ya utendea ina alomofu mbili ambazo ni /i/ na /e/ ambapo alomofu /i/
tunaona inatokea pale ambapo irabu ya mzizi inakuwa na /i,u na a/ wakati ambapo
alomofu /e/ inatokea wakati irabu ya mzizi ikiwa ni /e na o/. kinachoonekana
hapa ni kwamba irabu zinatangamana kwa kufuata mahali pa matamshi. Kwa mfano
kama irabu ya mzizi ni ya juu basi irabu ya utendea pia itakuwa ni ya juu, na
irabu ya mzizi ikiwa ni ya kati basi irabu ya utendea pia itakuwa ya kati,na
irabu ya chini siku zote inaonekana kuwa ni ya juu.
Kanuni.
+sila
+juu +sila
-kons
-nyuma -kati
-juu +K
-nyuma +sila
- chini -juu
-chini
|
Utamkaji pamwe wa nazali.
Huu ni mchakato ambapo katika mkururo wa nazali na
konsonanti hupelekea nazali kuathiriwa na konsonanti inayofuatana nayo.
Usilimisho huu hutokea pale ambapo nazali hufuata mahali pa matamshi pa
konsonanti inayofuatana nayo. Mifano yake ni kama ifuatayo;
umbo la ndani
|
umbo la nje
|
/n+buzi/
|
[mbuzi]
|
/n+bwa/
|
[mbwa]
|
/n+bu/
|
[mbu]
|
/n+gongo/
|
[mgo go]
|
/n+gozi/
|
[ gozi]
|
/n+vua/
|
[ vua]
|
/n+vivu/
|
[ vivu]
|
Hivyo katika mifano
hii tunaona kuwa nazali zimebadilika kwa kufuata mahali pa matamshi pa
konsonanti zilizokaribiana nazo. Mfano /n+gozi/ imebadilika kuwa [ɳgozi] ambayo huweza kuoneshwa kwa kanuni ifuatayo;
/n / [ ] /g/
Kanuni ya jumla.
s
+kons
-sila [ mahali] -sila
+naz
mahali
|
Kwa
kuhitimisha tunaona kuwa michakato ya kiusilimisho katika lugha ya Kiswahili
ipo na inatumika kukokotoa umbo la ndani kwenda umbo la nje. Huweza kufanya
mabadiliko ya karibu au moja kwa moja kuliko michakato isiyo ya kiusilimisho
ambayo haionyeshi mabadiliko ya moja kwa moja.
MAREJEO
Habwe,
J na Peter K. (2004) Misingi ya sarufi ya
Kiswahili. Phoenix Publishers: Nairobi.
Massamba,D.P.B.
(2011) Maendeleo Katika Nadharia ya
Fonolojia. Taasisi ya Taaluma za
Kiswahili (TUKI): Dar
es Salaam.
Mgullu,
R.S. (1999) Mtalaa wa isimu: Fonetiki,
Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili. Longhorn Publishers Ltd: Nairobi.
TUKI, (2004) Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Oxford University Press: Nairobi.
MIFANO YA MISAMIATI YA LAHAJA
ZA KISWAHILI NA MAANA YAKE KATIKA LUGHA SANIFU.
Kitika kujadili mada hii
tutaanza na maana ya Lahaja, Maana ya Lugha Sanifu, pia tutaangalia tofauti
kati ya lahaja na lugha sanifu, ufanano kati ya lahaja na lugha sanifu na sababu
za kuwepo kwa lahaja. Baada ya hapo tutaangalia Mifano ya misamiati ya lahaja
za Kiswahili na maana yake katika lugha sanifu. Kisha tutahitimisha mada hii.
Dhana ya lahaja na Kiswahili
sanifu zimejadiliwa na wataalamu mbalimbali katika mitazamo tofauti tofauti
kama ifuatavyo;
King’ei (2010) anasema kuwa
lahaja ni tofauti za kimatamshi zinazodhihirika miongoni mwa wanajamii lugha
wanaoishi katika maeneo mbalimbali ya kijiografia.
Msanjila na wenzake (2011)
wanasema kuwa lahaja ni lugha mojawapo kati ya lugha ambazo kimsingi huhesabiwa
kuwa lugha moja isipokuwa zinatofautiana katika baadhi ya vipengele fulani
fulani kama vile lafudhi, fonolojia, msamiati usiokuwa wa msingi au miundo
kutoka na eneo lugha hiyo inapozungumzwa .
TUKI (2004) inasema kuwa lahaja
ni tofauti katika matamshi maumbo na matumizi ya maneno katika maeneo
mbalimbali kwa lugha yenye asili moja.
Fasili zote hizi ni sahihi
kwani zimegusia mambo muhimu kama vile utofauti wa kifonolojia, kimsamiati na
lafudhi.
Kwa misingi hiyo lahaja za Kiswahili zimegawanyika katika
makundi mawili ambazo ni lahaja za kijiografia na lahaja za kijamii.
Pamoja na wataalamu hapo juu
kufasili dhana ya lahaja, pia dhana ya
Lugha sanifu imeweza kufasiliwa na wataalam mbalimbali kama ifuatavyo;
Msanjia na wenzake (2011)
wanasema kuwa lugha sanifu ni lugha ambayo imekubaliwa na serikali itumike
katika shughuli rasmi.
TUKI (2004) inasema kuwa lugha
sanifu ni lugha yenye kufuata taratibu au kanuni zilizokubaliwa.
Hivyo basi tunaweza kusema kuwa
lugha sanifu ni lugha yenye kufuata taratibu na kanuni zilizokubaliwa na
mamlaka husika ili itumike katika shughuli za kiserikali mfano, Bungeni,
maofisini na katika shughuli za kimahakama. Pia katika shughuli za kijamii kwa
mfano, katika elimu na vyombo vya habari.
Baada ya kuangalia fasili
zilizotolewa na wataalam mbalimbali kuhusu lahaja na lugha sanifu, zifuatazo
ni tofauti na ufanano ulizopo kati ya lahaja na lugha sanifu.
Tofauti
ya kwanza ipo katika fasili; ambapo
lugha sanifu imefasiliwa (ameshatajwa) kuwa ni lugha ambayo imekubaliwa na
serikali ili itumike katika shughuli rasmi wakati lahaja ni tofauti za
kimatamshi zinazodhihirika miongoni mwa wanajamii lugha wanaoishi katika maeneo
mbalimbali ya kijiografia.
Tofauti
ya pili ipo katika idadi ya wazungumzaji; Lugha sanifu inawatumiaji wengi kuliko lahaja,
hii ni kutokana na sababu kwamba lugha sanifu imeteuliwa kutoka katika lahaja
mbalimbali ili itumike katika shughuli zote za kiserikali na kijamii hivyo
husaidia kuwajumuisha wanajamii wenye kutumia lahaja tofauti tofauti na
kupelekea lugha sanifu kuwa na wazungumzaji wengi kuliko lahaja.
Tofauti
ya tatu ipo katika idadi;
Lugha sanifu ni moja katika jamii fulani mfano katika jamii ya kitanzania lugha
sanifu ni Kiswahili, wakati lahaja zipo nyingi katika jamii fulani. Kwa mfano
katika jamii ya kitanzania kuna lahaja kama vile Kimtang’ata, Kipemba na
Kiunguja.
Tofauti
nyingine ni
kwamba lugha sanifu inaweza kuwa rasmi lakini lahaja haiwezi kuwa lugha rasmi
pasipo kusanifishwa.
Vile
vile tofauti nyingine ipo katika maandishi; Lugha sanifu hutumika katika maandishi rasmi
wakati lahaja haiwezi kutumika katika maandishi rasmi ila inakuwa katika
maongezi ya kila siku.
Pia lugha sanifu ina hadhi ya juu kuliko lahaja kwa sababu
imesanifishwa na kutumika katika mawasiliano rasmi.
Ufanano kati ya lugha sanifu na
lahaja;
Zote ni lugha kutokana na
kwamba zinakidhi haja ya mawasiliana miongoni mwa wanajamii.
Pia zote zinatunza utamaduni wa
jamii husika. Kwa mfano wimbo wa Taifa katika jamii ya watanzania huimbwa kwa
lugha ya Kiswahili na kurithishwa kizazi kimoja kwenda kingine.Pia shughuli
mbalimbali za kijamii kama vile jando na unyago katika jamii tofauti tofauti
hufanyika kwa kutumia lahaja za jamii husika, hivyo hutumika kuhifadhi
utamaduni wa jamii husika.
Vilevile zote hutumika kama kitambulisho
cha jamii husika. Kwa mfano lugha ya Kiswahili hutumika kama kitambulisho cha
waswahili pale wanapozungumza Kiswahili katika jamii ambayo si ya waswahili.
Pia lahaja humtambulisha mtu kuwa ni wa jamii fulani pale anapozungumza, mfano
lahaja ya Kiunguja ni ya watu wa Unguja.
Pamoja na hayo, hata hivyo kuna
sababu mbalimbali zinazopelekea kutokea kwa lahaja. Sababu hizo ni kama vile;
Vikwazo
vya kijiografia;
Mipaka ya kijiografia huweza kutenganisha lahaja moja na lahaja nyingine,
mipaka hiyo ya kijiografia huweza kusababishwa na mito, milima, mabonde,
maziwa, bahari na misitu. Mfano lahaja ya Kiunguja na lahaja ya Kipemba
imetenganishwa na bahari ya Hindi.
Matukio
ya kihistori;
haya ni yale mambo yanayowafanya watu kuhama na kuingiliana kutoka sehemu moja
na kwenda sehemu nyingine, matukio hayo ya kihistoria ni kama vile njaa, vita,
na majanga mbalimbali ambayo kwa namna moja au nyingine husababisha kutokea kwa
lahaja.
Uhamiaji; hii ni hali ya jamii moja au
kundi la watu kuhama au kuhamia katika jamii nyingine na kusababisha kutokea
kwa lahaja, na uhamiaji huo huweza kusababishwa na biashara, kuoana, na
ufugaji.
Kutokana na sababu hizo
zimepelekea mgawanyiko wa lahaja katika makundi mawili ambayo ni lahaja za
kijiografia na lahaja za kijamii.
Lahaja
za kijiografia
ni zile lahaja ambazo husababishwa na mipaka ya kijiografia kama vile misitu,
mito, maziwa, mabonde na bahari. Mfano wa lahaja hizo ni kama vile; Kihadimu,
Kitumbatu, Kiunguja, Kingazija na Kiamu.
Lahaja
za kijamii
hizi ni zile lahaja ambazo hutokana na tofauti za kijamii ambazo huweza
kusababisha kuwepo kwa matabaka, umri, jinsia, cheo na hadhi.
Ifuatayo ni mifano ya misamiati
ya lahaja za kiswahili za kijiografia na kijamii pamoja na maana zake katika
Kiswahili sanifu
Lahaja za kijiografia;
Lahaja
ya Kimtang’ata;
hii ni lahaja inayozungumzwa maeneo ya Tanga. Mfano ya misamiati yake ni;
Msamiati katika lahaja ya Kimtang’ata
|
Kiswahili sanifu.
|
Tombo
|
Ziwa
|
Kifugutu
|
Kisu
(ki)butu
|
Kuwanga
|
Kuhesabu
|
Mbeko
|
Akiba
ya nafaka
|
Uwanda
|
Tambarare
|
Lahaja
ya Kitumbatu;
hii ni lahaja inayozunguzwa katika kisiwa cha Tumbatu kaskazini mwa Unguja.
Mfano wa misamiati ya lahaja hii ni;
Msamiati katika lahaja ya
Kitumbatu
|
Kiswahili sanifu
|
Ulanda
|
Kisu
kikali
|
Kifuto
|
Kisu
kibutu
|
Agulia
|
Piga
bao (ramli)
|
Chuchu
|
Ziwa
|
Yula
|
Yule
|
Lahaja
ya Kiunguja ni
ile lahaja inayozungumzwa katika kisiwa cha Unguja. Mfano wa misamiati ya
lahaja hiyo ni;
Msamiati katika lahaja ya
Kiuguja
|
Kiswahili sanifu
|
Mbatata
|
Viazi
mviringo
|
Tungule
|
Nyanya
|
Mfereji
|
Bomba
|
Maritiki
|
Sokoni
|
|
|
Lahaja
Kihadimu; hii
ni lahaja inayozungumzwa kisiwani Unguja. Mifano ya msamiati wa lahaja hii ni;
Msamiati katika lahaja ya
Kihadimu
|
Kiswahili sanifu
|
Kule
|
Mbali
|
Rikacha
|
Pikicha
|
Vacha
|
Pacha
|
Lahaja
za kijamii;
hizi ni lahaja zinazotokana na jinsia, umri, matabaka na hadhi ya wazungumzaji.
Mfano katika kigezo cha kijinsia wanawake hutumia neno shostina wanaume hutumia
neno msela,
wote wakiwa na maana ya rafiki katika Kiswahili sanifu.
Pia kuna kigezo cha kiumri
ambapo tunapata msamiati wa lahaja za kijamii kama vile; demu kwa vijana na binti
kwa wazee ambapo wote wakiwa na maana ya msichana katika Kiswahili sanifu.
Kwa kuhitimisha lugha ya
Kiswahili inazo lahaja nyingi lakini lahaja iliyosanifiwa ni lahaja ya Kiunguja
kutokana na kukidhi vigezo. Kutokana na kusanifiwa kwa lahaja hiyo
kumesababisha lahaja nyingine kuadhiriwa na hata kudumaa.
MAREJEO:
King’ei, K. (2010). Misingi ya Isimujamii.Taasisi ya Taaluma
za Kiswahili. Chuo Kikuu
cha Dar es salaam.
Mlacha, S.A.K. na Hurskainen,
A. (1995). Lugha, Utamaduni Na Fasihi
Simulizi ya Kiswahili. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Idara ya Taaluma za
Asia na Afrika na Chuo Kikuu cha Helsinki. TUKI
Msanjila, Y.P na wenzake.
(2011). Isimujamii: Sekondari na Vyuo.
TUKI. Dar es salaam.
TUKI, (2004).Kamusi ya Kiswahili Sanifu. (Toleo la Pili). East Africa: Oxford University
Press na Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI).
Ulahajia ni
nini?
Dhana ya
ulahajia inafaa vipi katika kuelezea utendaji wa lugha?
Swali hili limegawanyika katika
sehemu ‘a’ na sehemu ‘b’. Na katika kulijibu swali hili
tukianza na kipengele ‘a’ tutajadili dhana
ya ulahaji kutokana na wataalamu mbalimbali huku tukitoa fasili yetu kwa
ujumla. Pia katika kipengele ‘b’ tutajadili kuhusu dhana ya utendi kwa mujibu wa wataalamu, pia tutajadili maana
mazungumzo huku tukitoa fasili yetu. Na katika kujadili kiini chetu cha swali
tutajadili dhana ya ulahajia jinsi inavyotumika katika kuelezea utendaji wa lugha na mwishoni tutatoa
hitimisho la kazi yetu.
Dhana ya ulahajia imefasiliwa
na wataalamu mbalimbali ambao wameifafanua dhana hii kama ifuatavyo:-
Crystal, D (2000) anafasili
ulahajia kuwa ni taaluma inayohusu mfumo wa lahaja za kimkoa.
Wikipedia wanasema kuwa,
ulahajia ni tawi la isimu linalojihusisha na taaluma ya lahaja.
Kwa hiyo dhana ya ulahajia
hufafanuliwa kuwa ni taaluma inayojihusisha na uchunguzi wa lahaja za kimkoa.
Taaluma hii huchunguza utofauti
wa lahaja kati ya mkoa mmoja na mkoa mwingine. Zamani taaluma hii ilijikita
zaidi katika kufanya uchunguzi kwa wazee walioishi sehemu moja bila kuhama
tangia kuzaliwa kwao, lakini kwa sasa taaluma hii uchunguzi wake umejikita
zaidi katika maeneo ya mjini kutokana na kuchanganyika kwa makundi ya watu
tofauti tofauti kutoka mikoa tofautitofauti.
Dhana
ya utendi imefafanuliwa na wataalamu mbalimbali ambao wamefasili dhana hii kama
ifuatavyo:-
Wikipedia wanafasili utendi kuwa ni uzungumzaji wa lugha
katika muktadha halisi, nini hasa mzungumzaji husema kwa kuzingatia makosa ya
kisarufi.
Kwa hiyo utendi huweza
kufasiliwa kuwa ni utumiaji wa lugha katika mazingira halisi. Lugha inayotumika
lazima iendane na mazingira yaliyopo.
Vile vile mazungumzo
yamefasiliwa na Oxford (2004) kuwa ni jambo linalojadiliwa na watu au kikundi
cha watu kwa lengo fulani. Kwa mfano maongezi.
Halliday (1990) anasema
mazungumzo huweza kuwa na makosa mbalimbali katika mpangilio wa sentensi au
katika mtindo wa matamshi. Vile vile Halliday anasema lugha ya mazungumzo
inasifa zake bainifu ambazo ni tofauti na zile sifa za lugha ya maandishi.
Kwa hiyo tunaweza kufasili
mazungumzo kuwa ni jambo fulani linalojadiliwa na watu wawili au kundi la watu
kwa lengo fulani.
Baada ya kujadili dhana hizo, sasa
tunaweza kujadili ni kwa jinsi gani dhana ya ulahajia inavyoweza kuelezea utendaji
wa lugha hususani katika lugha ya mazungumzo kwa kuzingatia lugha ya Kiswahili.
Utofauti wa matamshi. Ulahajia huchunguza matamshi
ya wazungumzaji wa lugha kutoka mikoa tofauti tofauti. Kwa mfano wazungumzaji
kutoka mikoa ya kanda ya ziwa. Mfano wahaya kutoka mkoa wa Kagera katika
matamshi yao hawana kitamkwa ng’ kwa
hiyo wanapotamka maneno kama vile ng’ombe wao hutamka ngombe, neno ng’ang’ania
hutamka ngangania, neno ung’amuzi wao hulitamka kama ungamuzi. Vile vile watu
kutoka mkoa wa Mara ambao ni wakurya hutumia kitamkwa r badala ya l
kwa mfano neno kula wao hulitamka kura, neno kulala hulitamka kurara,
kulalamika wao hulitamka kuraramika. Pia wazungumzaji kutoka mikoa ya kusini
mfano kutoka mkoa wa mtwara na lindi ambao ni Wamakonde wao hutumia kitamkwa n
badala ya m kwa mfano mtoto hutamka kama ntoto, msichana hutamka kama
nsichana, mchana hutamka nchana. Vile vile wazungumzaji kutoka mkoa wa mbeya
ambao ni wanyakyusa wao hutamka f badala ya v kwa mfano neno viatu vyangu
hutamka kama fiatu fyangu, uvivu hutamka ufifu, viazi hutamka fiasi.
Wazungumzaji wa kutoka mikoa ya kaskazini mfano wapare kutoka mkoa wa moshi
hutumia kitakmwa th badala ya s kwa mfano badala ya kusema sisi
sote ni wasichana wao hutamka thithi thote ni wathichana. Kwa hiyo tofauti hizo
za kimatamshi zinatokana na athari za lahaja za mikoa waliyotoka.
Msamiati. Dhana ya ulahajia huweza
kutumika katika kuchunguza msamiti mbalimbali wa wazungumzaji wa lugha moja
kutoka mikoa tofauti tofauti. Kwa mfano watu kutoka Zanzibar wao hutumia
msamiati tofauti na wazungumzaji wa mikoa ya bara, kwa mfano husema neno
tungule kwa kumaanisha nyanya, neno malikiti humaanisha sokoni, mferejini
humaanisha bombani, vile vile kabila la Wamakonde kutoka mkoa Mtwara hutumia
neno kumaanika kwa kumaanisha kudharirika, kwa hiyo wazungumzaji hawa hutumia
msamiati wa lahaja zao kutokana na
athari za lahaja hizo.
Muundo wa sentensi, vile vile dhana ya ulahajia
huweza kuelezea utendaji wa lugha kwa kuchunguza muundo wa sentensi wa
wazungumzaji wa lugha moja, kwa kuchunguza muundo wa sentensi utaweza kubaini
kuwa wazungumzaji wa lugha hii wanatokea mkoa gani, kwa mfano wazungumzaji wa
mkoa wa Tabora hutumia wingi mahala pa nomino ya umoja wakiashiria heshima. Kwa
mfano husema baba wanakuja badala ya kusema baba anakuja, mmefika salama?
Badala ya kusema umefika salama?. Kwa hiyo mtu wa heshima kwao hutumia nomino
ya wingi na hii yote ni kutokana na kuathiriwa na lahaja za mikoa watokayo.
Kiimbo. Ulahajia huweza kuchunguza
kupanda na kushuka kwa mawimbi ya sauti ya wazungumzaji wa lugha, kwa mfano
kabila la Waluguru kutoka mkoa wa Morogoro wao huzungumza kwa kupandisha na
kushusha mawimbi ya sauti. Kwa mfano, “baba amekuja”. kwa hiyo athari hizo
zimetokana na lahaja ya mkoa waliotokea.
Mkazo, mkazo ni kule kutumia nguvu
zaidi katika kutamka maneno au sentensi. Yaani ni hali ya neno au silabi katika
neno kusikika kuwa na nguvu zaidi kuliko silabi au maneno mengine. Kwa hiyo
ulahajia huweza kuelezea utofauti wa mkazo uliopo katika baadhi ya wazungumzaji
wa lugha moja. Kwa mfano kabila la Wasukuma kutoka mkoa wa Mwanza huweka
msisitizo katika mazungumzo, kwa mfano “baba anakujaa”, pia wanaongeza vitamkwa ambavyo si vya msingi katika maneno
yanayojitosheleaza. kwa mfano neno amekuja wao huongezea kitamkwa ga, = amekujaga, neno ameenda + ga, = ameendaga, hakuna + ga.=hakunaga.
Kwa hiyo mtu huweza kuwa na
umilisi wa lugha fulani lakini asiwe mtendaji hususani katika lugha ya
mazungumzo na hii ni kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuathiriwa na lahaja
ya mkoa atokao, athari hizi hujidhihirisha zaidi katika lugha ya mazungumzo
kama tulivyojadili hapo juu, lakini katika lugha ya maandishi athari hizi
huweza kujidhihirisha kwa kiasi kidogo sana au zisitokee kabisa.
Kwa kuhitimisha tunaweza kusema
kuwa dhana ya ulahajia huweza kuelezea utendaji wa lugha husasani katika lugha
ya mazungumzo kwani ndio rahisi sana kuchunguza tofauti za wazungumzaji wa
lugha moja watokao sehemu tofauti tofauti, ambayo ni tofauti sana na kuelezea
utendaji wa lugha katika lugha ya maandishi kwani ni vigumu sana kubainisha
makosa ya kisarufi kama vile matamshi, kiimbo, mkazo, msamiati na hata muundo
wa sentensi. Mara nyingi maandishi huandikwa kwa ufasaha zaidi ukilinganisha na
mazungumzo na ndio maana ulahajia huweza kuelezea utendaji wa lugha hususani
katika lugha ya mazungumzo.
Marejeo;
Crystal, D. (2002). The Cambridge of Encyclopedia of Language:
Second edition. London. Cambridge University Press.
Halliday, M.A.K. (1990). Spoken and Written Language. London.
Oxford University Press.
Kamusi ya Kiswahili Sanifu,
(2004). Nairobi. Oxford University Press.
Lugha ya mazungumzo haina muundo
rasmi?. Huku ukijikita katika nduni za lugha ya mazungumzo, jadili kauli hii.
Katika kujadili swali hili,
tutaanza kujadili nini maana ya lugha kwa mujibu wa wataalam mbalimbali, pia
tutatoa maana ya lugha ya mazungumzo, maana ya muundo rasmi na hatimaye
tutaingia katika kiini cha swali ambapo tutakubaliana na swali kwa kutumia
uthibitisho wa nduni (sifa) za lugha ya mazungumzo jinsi zinavyofanya lugha ya
mazungumzo isiwe na muundo rasmi. Yaani tutaangalia ni kwa vipi sifa za lugha
ya mazungumzo zinavyopelekea lugha ya mazungumzo kukosa sifa ya kuwa na muundo
rasmi. Na mwisho tutatoa hitimisho.
Massamba (2009) anaeleza kuwa,
lugha ni mfumo wa sauti nasibu ambazo zimekubaliwa na jamii kwa madhumuni ya
mawasiliano yao.
Mgullu (1999) kama alivyomnukuu
Trudgil (1974) anafafanua kuwa, lugha ni mfumo wa sauti za nasibu zinazotumiwa
kwa mawasiliano miongoni mwa watu wa jamii fulani wenye utamaduni wake.
Kwa ujumla tunaweza kusema
kwamba, lugha ni mfumo wa sauti nasibu ambazo zimebuniwa na jamii kwa madhumuni
ya mawasiliano miongoni mwao.
Dhana yingine tuliyoiangalia
kulingana na swali hili ni lugha ya mazungumzo. Kwa mujibu wa Wikipedia,
wanasema lugha ya mazungumzo ni utaratibu wa kuongea baina ya pande mbili, kwa
kawaida wahusika ni watu. Lugha ya mazungumzo huwa na mitindo mbalimbali kama
vile rejesta, misimu, jagoni na agoti.
Kisha tukaangalia dhana ya
muundo, kwa mujibu wa Concise Oxford Dictionary (2001) (toleo la 10) muundo ni
mpangilio na uhusiano wa vitu katika kuunda kitu kizima;
Katika muktadha wa mazungumzo,
muundo rasmi ni ule mpangilio unaohusisha kanuni na taratibu zilizowekwa katika
uzungumzaji ambapo kila mzungumzaji hana budi kuzingatia wakati wa mazungumzo.
Vilevile tunapozungumzia muundo
rasmi katika lugha huangalia mpangilio wa maneno na muundo wa sentensi na namna
maneno na sentensi hizo zinavyopangiliwa na kuleta mtiririko wenye maana na
uliokamilika na unaoweza kueleweka na watu wote.
Kutokana na fasili hii lugha ya
mazungumzo haina muundo rasmi, hii ni kwa sababu haizingatii vigezo hivyo
wakati wa uzungumzaji na hivyo kuonekana kutokuwa na muundo rasmi na hii ndiyo
sifa mojawapo kati ya sifa zinazojidhihirisha katika lugha ya mazungumzo.
Hivyo basi tunaweza
kuthibitisha kauli hii kwamba, lugha ya mazungumzo haina muundo rasmi kwa
kujikita katika sifa au nduni za lugha ya mazungumzo kama ifuatavyo;
Kwa
mujibu wa King’ei (2010), anaorodhesha sifa zinazojitokeza katika lugha ya
mazungumzo ambazo ni kama ifuatavyo;
Ubadilikaji
wa kila mara wa maudhui, na uteuzi usiotabirika wa maneno, kauli au usemi. Hivyo katika sifa hii tunaona kwamba hakuna muundo
rasmi kutokana na kwamba mzungumzaji ana uteuzi wa maneno na kauli
zisizotabirika, hivyo anaamua mwenyewe nini cha kusema bila kufuata muundo au
kanuni zozote. Mfano anaweza kuanza na aina yoyote ya neno katika sentensi.
Utokezaji
wa makosa wa aina tofauti katika mazungumzo, mfano kukosea matamshi, kusitasita, kusahau
baadhi ya maneno, kuchanganya hoja, wazungumzaji kusema kwa pamoja na hivyo
kupoteza uzi au mtiririko sahihi wa mazungumzo. Jambo hili hutokea kutokana na
kukosekana kwa muundo rasmi unaowaongoza wazungumzaji. Kimsingi muundo rasmi
hufuata kanuni madhubuti na utokeaji wa makosa haupo kwa sababu ya urasmi wake.
Pia
kuwepo kwa uradidi /
marudio na msisitizo kwa wingi katika mazungumzo na pia mazungumzo kukatishwa
kwa vichekesho, miguno ama matumizi ya lugha ya ishara, hali hii hutokana na
kutokuwepo na muundo maalum unaomwongoza mzungumzaji, ndiyo maana wazungumzaji
hujikuta wakirudia rudia maneno wakati wa mazungumzo.
Masahihisho
ya kila namna na pia ufafanuzi na maelezo hutolewa mara kwa mara pale utata unapotokea. Hii ni kwa sababu ya kutokuwepo kwa muundo
maalum kama vile mpangilio wa mawazo, sentensi na mtiririko wa mawazo katika
mada ndivyo vinapelekea kutokea kwa utata na kusababisha masahihisho ya mara
kwa mara.
Matumizi
ya sentensi fupi fupi,
sentensi za neno moja moja au maneno yasiyokamilika hutokea kwa wingi katika
mazungumzo pindi mzungumzaji anapozungumza kwa huweza kutumia sentensi fupi
fupi, au kutumia maneno yasiyokamilika. Yote hii hutokana na kutokuwepo kwa
muundo rasmi wa lugha ya mazungumzo. Katika hali ya muundo rasmi hauruhusu
udondoshaji wa maneno au tungo au matumizi ya sentensi fupifupi ambazo
hazijajitosheleza.
Msamiati
mwepesi na unaofahamika kwa urahisi,
pindi mzungumzaji wa lugha anapoongelea mada fulani mbele ya hadhira yake
huangalia mandhari pamoja na uhusiano baina yake na wasikilizaji wake, hivyo
anaweza kubadilika kulingana na hali halisi anayokutana nayo. Hii
haijidhihirishi katika muundo rasmi kama vile lugha ya maandishi, mwandishi
hazingatii muktadha au uhusiano baina yake na wasomaji wake, yeye huandika kazi
yake bila kujua watakaosoma ni akina nani. Hivyo basi ubadilikaji huu wa
msamiati kulingana na hadhira ya mzungumzaji unatuthibitishia kwamba lugha ya
mazungumzo haina muundo rasmi.
Vilevile
kuna uvunjaji wa kanuni za sarufi na matumizi sanifu kutegemeana na uhusiano wa wazungumzaji, katika lugha ya mazungumzo hakuna
kanuni ambazo zinamfanya/kumbana mzungumzaji, hivyo basi kwa sababu ya
kutokuwepo kwa kanuni hizo ni wazi kwamba lugha hii haitakuwa na muundo rasmi
unaomuongoza mzungumzaji ndiyo maana mzungumzaji hujikuta akivunja kanuni.
Mfano; mtu anaweka viambishi sehemu ambayo haihitajiki kiambishi kama vile neno
nilikuwepo – nilikuwepogi, alimpaga au hakunaga. Pia wapare husema thatha
ni thaa thaba kamili wakimaanisha
kuwa sasa ni saa saba kamili. Vilevile Wahaya husema ngombe badala ya ng’ombe.
Pia katika lugha ya mazungumzo hakuna muda au nafasi ya kufikiria jambo la
kuzungumza, hapa mzungumzaji hana
muda wa andalio la anachotaka kusema, hutamka tu bila kufikiria jambo analotamka.
Jambo hili la kutokuwa na muda wa kujiandaa ndilo hupelekea kutokea kwa miguno
na makosa ya kimantiki. Lakini katika muundo rasmi mambo haya huwa hayajitokezi
kwa sababu kuna maandalizi ya kutosha.
Kwa kuhitimisha tunaweza kusema
kuwa, muundo wa lugha ya mazungumzo hauwezi kujidhihirisha moja kwa moja kwa
watumia lugha isipokuwa huweza kuhusisha utaratibu fulani unaozingatia mada,
muktadha na mahusiano ya wazungumzaji. Aidha hoja inasisitiza kuwa hakuna mada
rasmi zilizozoeleka na zinazotumika na watu wote, vivyo hivyo kwa muktadha na
mahusiano. Pia lugha hiyo haiwezi kuwa na mpangilio maalum wa kile
kinachozungumzwa na maelezo yake kwa wazungumzaji baina yao.
MAREJEO:
Smith, T. (2001). Concise Oxford English Dictionary. (10th
Edt). Oxford University Press. UK.
King’ei, K. (2010). Misingi ya Isimujamii. Taasisi ya
Taaluma za Kiswahili. Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
Massamba, D.P.B. (2009). Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha.TUKI,
Dar es Salaam.
Mgullu, R.S. (1999). Mtalaa wa isimu: Fonetiki, Fonolojia na
Mofolojia ya Kiswahili. Longhorn publishers.
Ltd. Nairobi
MBINU
MBALIMBALI ZA KUBAINI AU KUTAMBUA FONIMU.
Katika kujadili mada hili sehemu ya kwanza tutajikita katika
kuangalia maana ya fonolojia na fonimu
kwa mujibu wa wataalamu mbalimbali, katika sehemu ya pili tutaangalia mbinu
mbalimbali za kubainisha fonimu kwa mujibu wa wataalamu mbalimbali na sehemu ya
tatu tutahitimisha na mwisho marejeo.
Kwa kuanza na maana ya fonolojia imejadiliwa na
wataalam mbalimbali kama ifutavyo:-
Massamba, (2004), Habwe na
Karanja (2007) kama walivyomnukuu Ladefoged (1975:23) wanaelekea kuwa na fasili
zinazokaribiana kuhusu fonolojia. Wanafafanua kuwa fonolojia ni tawi la isimu ambalo hushughulika na
ufafanuzi , uchunguzi na uchanganuzi wa mfumo wa sauti za lugha mahsusi.
Hivyo basi tunaweza kusema
fonolojia kwa ujumla tunaweza kufasili kama ni nyanja mojawapo ya isimu
inayoshughulika na uchambuzi, uchunguzi wa sauti za lugha mahususi kama vile fonolojia ya
Kiswahili, Kingereza, Kisafwa na Kihehe.
Pia
dhana ya fonimu imejadiliwa na wataalamu mbalimbali
kama ifuatavyo;
Massamba (2004) anasema fonimu
ni kipande kidogo kabisa katika mfumo wa sauti za lugha ambacho kina sifa
pambanuzi za kuweza kukitofautisha na vipande vingine vya aina yake.
Habwe na Karanja, (2007) wanasema
kuwa fonimu ni kipashio kidogo kabisa cha sauti katika lugha kinachokuwa na
uwezo wa kubadili maana ya neno.
Massamba na wenzake (2004)
wanaema kuwa fonimu ni kipande sauti ambacho hutumika katika kujenga maneno ya
lugha, kwa mfano vitamkwa kama /p/,/b/,
/u/, /m/, /t/,/d/,/a/,/k/ na /n/ tunaweza kujenga maneno kama tunda, pumba, taka, muda, dunda, kama na
kuta.
Hivyo kwa ujumla fonimu
tunaweza kufasili kama kipashio kidogo kabisa cha kifonolojia ambacho huwa na
uwezo wa kujenga neno mfano /k/, /a/ na /a/ zinajenga neno “kaa,” /t/,/i/ na /a/-zinajenga neno “tia” au
kubadili maana ya neno moja na nyingine mfano pia, bia,tia, kata,pata na
bata,hivyo fonimu /p/, /b/, /t/ na /k/ zinabadili maana ya neno moja na
jingine.
Wataalamu
mbalimbali wamebainisha mbinu mbalimbali za kubainisha fonimu, mbinu hizo ni
kama zifuatazo:-
Mgawanyo wa kimtoano au
mgawanyo kamilishani,
Mgullu (1999) akimnukuu Hyman (1975) anaeleza utoano kuwa ni dhana ambayo
hutumiwa kuelezea uhusiano uliopo baina ya sauti mbili au zaidi za fonimu moja
ambazo haziwezi kutokea katika mazingira sawa, hii ina maana ya kwamba kila
sauti huwa na mazingira yake maalumu ya utokeaji ambayo hayawezi kukaliwa na
sauti nyingine,kwa mfano kutoka lugha ya Kiingereza sauti /ph/ yenye mpumuo na /p/
isiyo na mpumuo haziwezi kutokea katika mazingira yanayofanana mfano tunaona
kuwa /ph/ yenye mpumuo
mara zote hutokea mwanzoni mwa maneno tu kwa mfano /put/, /pin/ na /pen/ na /p/ isiyokuwa na mpumuo hutokea sehemu nyingine yoyote katika neno
isipokuwa mwanzoni mwa neno, kwa mfano /spell/na /spin/.
Pia mbinu hii imeungwa mkono na
Massamba (2010) akimnukuu Hocket (1958)
anasema kwamba sauti mbili zinaweza kuwakilisha fonimu zinazofanana kama
zitakua na mazingira tofauti ya utokeaji, sauti zinazotokea katika mgawanyo
kamilishani hujulikana kama alofoni za fonimu moja. Mfano kutoka lugha ya
Ci-Ruuri:
Imbusi “mbuzi”
Oguβusi “mbuzi mkubwa”
Imbogo “nyati”
oguβogo “nyati kubwa”
Kutokana na mifano ya maneno
hayo, tunaona kuwa fonimu /b/ na /β/ hugawana mazingira ya
utokeaji, sehemu ambapo /b/ hutokea,
/β/ haiwezi kutokea, huwa /β/ hutokea katikati ya irabu na
mahala pengine popote, wakati /b/ hutokea tu pale inapokuwa imetanguliwa na
nazali kama vile /m/.
Mpishano huru , kwa mujibu wa Mgullu (1999)
akimnukuu Martinent anaeleza kuwa dhana ya mpishano huru ni maneno mawili
yanayoweza kuwa na tofauti ya fonimu moja tu lakini tunapozitazama fonimu hizo
zilizotofauti, tunaona wazi kuwa kwanza fonimu hizo ni tofauti sana Kifonetiki
au haziwezi kuwa alofoni za fonimu moja, pia tunaona kwamba fonimu hizo
zilizotofauti kifonetiki hazipo katika ule uhusiano wa kimtoano, yaani zote
zinaweza kutumika katika mazingira yaleyale kwenye neno lakini fonimu hizo
ingawa ni tofauti hazisababishi tofauti za maneno katika maneno zinamotokea
yaani kila moja inaweza kutumiwa badala ya nyingine (katika maneno maalumu)
bila kubadili maana katika maneno hayo.
Mifano:
Alimradi ilimradi /a/ na /i/
Baibui buibui /a/ na /u/
Amkia amkua /i/ na /u/
Bawabu bawaba /a/ na /u/
Wasia wosia /a/ na /o/
Benua binua /e/ na /i/
Heri kheri /h/ na /kh/ au /x/.
Mfanano wa kifonetiki, Mgullu (1999) akimnukuu Jones (1957) anaeleza
kuwa fonimu fulani katika lugha fulani huwa ni ujumuisho wa udhahanishaji wa
sauti kadhaa au tuseme kundi la sauti zinazofanana sana kifonetiki ni sauti
zilizo na sifa bainifu zinazofanana. Kwa mfano irabu huwa na sifa zake bainifu
ambazo ni tofauti na konsonanti, mfano irabu /i/ na /u/ hatuwezi kusema kuwa ni
fonimu moja kwa sababu sauti hizi zinatofautiana sana kifonetiki, kwa hiyo hizi
ni fonimu mbili tofauti.
Mfano;
/i/ /u/
+
irabu +irabu
+mbele +nyuma
+juu
+juu
-mviringo +mviringo
Hivyo irabu /i/
na /u/ zinafanana tu katika sifa
mbili ambapo zote ni irabu na zote ni irabu za juu na zinatofautiana katika
sifa mbili ambapo irabu /i/ ni irabu ya mbele si viringe na irabu /u/ ni irabu
ya nyuma viringe. Hivyo hatuwezi kusema zinafanana kifonetiki kutokana na
kutofautian kwa baadhi ya sifa bainifu.
Besha (2007) anasema kuwa
uainishaji wa fonimu tunaangalia mfanano
wa kifonetiki. Anasema kuchanganua mifumo ya sauti za lugha mbalimbali
mfanano wa kifonetiki kati ya sauti ni muhimu sana kwa vile mahusiano ya
kifonetiki, kanuni pamoja na minyumbuo yote inategemea katika sifa hii
kuainisha sauti za lugha ili kugundua zipi ni fonimu za lugha hiyo pamoja na
alofoni zake. Umuhimu huwekwa katika kuangalia uhusiano uliopo katika makundi
ya sauti kufuatana na mahali pa kutamkia na namna za utamkaji , makundi makubwa
yanayohusiana sana ni matatu ambayo ni Vipasuo, vikwamizi na ving’ong’o,ndani
ya makundi haya umuhimu mkubwa huwekwa katika mahali pa kutamkia . Hivyo basi
mifano inayotolewa na wataalamu mbalimbali haibainishi mfanano wa kifonetiki
kwani sifa za kila sauti zinatofautiana na nyingine, sifa kuu ya mfanano wa
kifonetiki ni lazima sauti hizo zifanane kwa sifa zote.
Jozi sahili / jozi ya mlinganuo
finyu, kwa
mujibu wa mgullu (1999) kama alivyomnukuu Fischer (1975) anasema mlinganuo
finyu ni tofauti ndogo kabisa ya kifonolojia iliyopo baina ya maneno
fulani,aghalabu maneno hayo huwa yana idadi sawa za fonimu, fonimu zinazofanana
isipokuwa fonimu moja na mpangilio wa fonimu ulio sawa.Katika lugha ya
kiswahili maneno kama /pia/ na
/tia/ ni mfano wa mlinganuo
finyu kwa sababu idadi ya fonimu ni sawa, aina ya fonimu zilizopo ni zilezile
isipokuwa moja, maneno yote yana /a/ na /i/ isipokua tofauti
katika fonimu /p/ na /t/ na mpangilio wa sauti ni sawa
ambapo /p/ na /t/ zipo mwanzoni mwa neno
zikifatiwa na irabu /a/
na irabu /u/.Pia kutoka lugha ya kiswahili maneno kama
pata
na bata
kata
na kati
dua
na tua
Katika maneno haya fonimu /p/,
/b/, /a/, /i/,/d/ na /t/ ndio zinazotofautisha maana
za maneno baina
ya neno moja na jingine. Mbinu
hii pia imeungwa mkono na wataalamu wengine kama Besha (2007) na Massamba
(2010) kwani wametoa maelezo yao na mifano inayofanana sana na ya Mgullu (1999)
alivyonukuu kutoka kwa Fischer (1975)
Kwa
kuhitimisha,ni vigumu kubainisha fonimu kwa kutumia mbinu moja, hivyo basi ni
vyema fonimu zikabainishwa kwa kujumuisha mbinu zote kama zilivyobainishwa na
wataalam mbalimbali ili kuweza kupata mbinu moja ambayo ni sahihi katika kubaini
fonimu.
Marejeo
Besha,
R.M. (2007) Utangulizi wa Lugha na Isimu.Macmillan
Aidan L.t.d: Dar es Salaam.
Habwe,
J. na Karanja, P (2007) Misingi ya Sarufi
ya Kiswahili.Phoenix: Nairobi
Massamba,
D.P.B (2004) Phonological Theory: History and Development. TUKI: Dar es
Salaam
Massamba,
D.P.B (2010) Kamusi ya Isimu na Falsafa
ya Lugha. TUKI: Dar es Salaam
Massamba,
D.P.B na wenzake (2004) Fonolojia ya
Kiswahili Sanifu
(FOKISA). TUKI: Dar es Salaam.
Mgullu,
S.R. (1999), Mtalaa wa Isimu.Longhorn:Nairobi
KWA KUWA
MSAMIATI MWINGI ULIOPO KATIKA LUGHA YA KISWAHILI UNATOKANA NA LUGHA YA KIARABU NI
DHAHIRI KUWA LUGHA HII INATOKANA NA KIARABU. JADILI.
Katika kujadili swali hili tutaanza na
utangulizi kwa kueleza maana ya asili,
maana ya msamiati na baada ya hapo tutaangalia jinsi kigezo cha msamiati
kinavyotumiwa kudai kuwa Kiswahili ni
kiarabu na tutaonesha udhaifu wake na mwisho tutakanusha madai haya kwa
kuonesha kuwa Kiswahili ni kibantu na sio kiarabu.
Mjadala kuhusu asili ya Kiswahili umejadiliwa
na wataalam mbalimbali na wametumia vigezo mbalimbali kuthibitisha madai yao.
Wapo wanaodai kuwa Kiswahili ni kiarabu, wanaoshadidia dai hili, kigezo
kimojawapo wanchokitumia ni kigezo cha msamiati, kwamba lugha ya Kiswahili ina
msamiati mwingi wa kiarabu na kwa hiyo kwa kuwa Kiswahili kina msamiati mwingi
wa kiarabu basi pia Kiswahili ni kiarabu, kwa kweli dai hili halina mashiko.
Kabla hatujaanza kufafanua kwamba kwa nini dai hili halina mashiko ni vema tukaangalia fasili ya dhana muhimu
kama zinavyojitokeza katika swali la mjadala. Dhana hizo ni kama zifuatazo:
‘Istilahi asili,’ kwa mujibu wa Massamba na wenzake (1999)
asili ni jinsi kitu au jambo
lilivyotokea au lilivyoanza. Fasili hii
ni nzuri na inajitosheleza kwa maana kwamba jambo au kitu kinaweza kutokea
kibahati kama ilivyo katika lugha au linaweza kuanzishwa.
Msamiati pia unaelezwa na TUKI (2004) kuwa ni jumla ya
maneno katika lugha. Fasili hii iko wazi kwamba jumla ya maneno yote katika
lugha ndio huunda msamiati wa lugha husika.
Wataalam wanaodai kuwa Kiswahili ni kiarabu
kwa kutumia kigezo cha msamiati, hoja zao ni kama zifuatazo:
Khalid (2005) anasema kuwa neno lenyewe
Kiswahili limetokana na neno la kiarabu sahil katika umoja ambalo wingi
wake ni sawahili likiwa na maana
ya pwani au upwa. Hivyo kutoka na jina la lugha hii ya Kiswahili kuwa na asili
ya neno la kiarabu sahil hivyo hudai kuwa Kiswahili ni kiarabu.
Khalid anaendelea kusema kuwa Kiswahili kina
msamiati mwingi wenye asili ya kiarabu. Hapa ni baadhi ya mifano ya msamiati wa
Kiswahili wenye asili ya kiarabu kama alivyobainisha Khalid:
Maneno yanayoonesha muda.
Asubuhi dakika
Wakati alfajiri
Karne alasiri
Magharibi saa
Maneno yanayowakilisha namba.
Nusu robo
Sita saba
Tisa ishirini
Thelathini arubaini
Hamsini sitini
Sabini themanini
Tisini mia
Elfu
Mtandao wa jamiiforum pia wameonesha mifano ya msamiati wa Kiswahili wenye asili
ya kiarabu kama ifuatavyo:
Kiswahili Kiarabu
Dirisha drisha
Karatasi kartasi
Debe dabba
Samaki samak
Mustakabali mustakabal
Madrasa madrasa
Lodh (2000) naye anasema kiasi kikubwa cha
nomino za Kiswahili zimetokana na mizizi ya maneno ya kiarabu. Mifano ya maneno
hayo ni kama yafuatayo:
Hesabu/hisabu mahisabu/hisabati
Harka harakati
Safiri - msafiri
Safari -
msafara
Fikiri - fikara/fikra
Hata hivyo kigezo hiki cha msamiati kina
udhaifu; Massamba (2002) ameonesha udhaifu wa kigezo hiki kuwa ni pamoja na
kwamba:
Hakuna ushahidi wowote wa kitakwimu ambao
unaonesha idadi ya maneno ya kiarabu yaliyopo katika lugha ya Kiswahili
yanayoweza kuhitimisha kuwa Kiswahili ni kiarabu.
Kigezo cha msamiati peke yake hakijitoshelezi
kuelezea kuwa Kiswahili ni kiarabu, walipaswa waangalie vigezo vingine kama
vile kigezo cha kihistoria kwa kuchunguza masimulizi mbalimbali ya kale na
kigezo cha kiisimu; katika kigezo hiki walipaswa kuchunguza fonolojia,
mofolojia , na sintaksia ya Kiswahili kwa kulinganisha na kiarabu na ndipo
wangepata hitimisho sahihi la madai yao.
Vilevile kigezo hiki cha msamiati hakina
mashiko kwa sababu lugha ina tabia ya kuathiriana, lugha huathiriana na lugha
nyingine endapo kutakuwa na mwingiliano baina ya wanajamii lugha hizo. Kwa mfano Kiswahili kimetokea kuathiriana na
kiarabu kutokana na uhusiano uliokuwepo hapo zamani katika biashara kati ya
waarabu na watu wa upwa wa Afrika Mashariki na hii ikapelekea msamiatia wa
kiarabu kuingia katika lugha ya Kiswahili, hivyo kwa hoja hii hatuwezi kusema
Kiswahili ni kiarabu kwa sababu msamiati wa kiarabu unaonekana katika lugha ya
Kiswahili.
Hata hivyo si lugha ya kiarabu tu ambayo
msamiati wake unaonekana katika lugha ya Kiswahili vilevile kunamsamiati wa
lugha zingine za kigeni katika lugha ya Kiswahili kwa mfano, neno lenye asili
ya kireno katika Kiswahili ni kama vile meza,
leso pia yapo maneno yenye asili ya kijerumani kwa mfano schule kwa Kiswahili shule na maneno yenye asli ya kiingereza
ni kama vile mashine, televisheni,
sekondari, redio, kompyuta na maneno mengine yenye asli hiyo. Basi ingekuwa
msamiati wa kigeni kuonekane kwenye lugha fulani huifanya hiyo lugha kuwa na
asili ya lugha ya kigeni basi tungesema pia Kiswahili ni kiingereza kwa sababu tu msamiati mwingi wa kiingereza
unonekana katika Kiswahili.
Pia kigezo hiki kinaonekana kuwa ni dhaifu kwa
sababu hawakufanya utafiti katika nyanja zote za matumizi ya lugha kwa mfano
msamiti unaotumika katika nyanja ya elimu, afya, utamaduni na kadhalika. Kwa
hiyo madai haya yanaonekana kutokuwa na mashiko kwa ufinyu wa utafiti wake.
Kutoka na kigezo hiki cha msamiati kutokuwa na
mashiko kuhitimisha kuwa Kiswahili ni kiarabu, basi hatuna budi kusema kuwa
Kiswahili sio kiarabu bali ni kibantu. Katika kuthibitisha madai haya tutajikita zaidi katika kigezo
cha kiisimu ambacho tunaamini kuwa ni kigezo pekee kinachoweza
kutupatia taarifa sahihi kwani ni kigezo cha kisayansi lakini pia tutaangalia
kwa ufupi vigezo ambavyo vinatoa ushahidi juu ya ubantu wa Kiswahili ambavyo ni
ushahidi wa kihistoria, kiakiolojia na kiethinolojia.
Kigezo hiki cha kiisimu kimetumiwa na wataalam
mbalimbali katika kuonesha ubantu wa Kiswahili Massamba (ameshatajwa) amewataja
wataalam mbalimbali ambao wamehusika na utafiti juu ya ubantu wa Kiswahili,
wataalam hao ni pamoja na Carl Meinhof
katika kitabu chake cha Introduction to
the phonology of the Bantu language, Duke
(1935 – 1945), Malcom Guthrie
(1967), Dereck Nurse na Thomas Spear
(1985). Hawa walijadili ubantu wa Kiswahili kwa kutumia kigezo cha kiisimu,
kihistoria na kiakiolojia.
Kwa kuanza na
kigezo cha kiisimu tutaangalia
vipengele kama vile kufanana kwa msamiati wa msingi, muundo wa kifonolojia,
muundo wa kimofolojia, muundo wa kisintaksia mpangilio wa ngeli za majina.
Mizizi ya msamiati wa msingi wa lugha za
kibantu na Kiswahili hufanana kwa kiasi kikubwa, mifano ifuatayo huweza
kuonesha ukweli huu.
Mfano,
Kiswahili
|
Kikurya
|
Kinyiha
|
Kijita
|
Maji
|
Amanche
|
Aminzi
|
Amanji
|
Jicho
|
Iriso
|
Iryinso
|
Eliso
|
Katika mifano hiyo hapo juu tunaona mifano
hiyo hapo juu tunaona kuwa mizizi maji, manche, minzi, manji inafanana kwa
kiasi kikubwa, kwa hiyo huu ni ushahidi tosha kutuonesha kuwa kuna uhusiano wa
kinasaba kati ya Kiswahili na lugha za kibantu.
Pia mofolojia ya Kiswahili na lugha za kibantu
hufanana kwa kiasi kikubwa, yaani mfumo wa
maumbo ya maneno ya lugha ya Kiswahili na lugha za kibatu hufanana. Kwa mfano,
namna viambishi vinavyopachikwa katika mzizi wa maneno hufuata kanuni ileile
kama inavyotumika katika lugha ya Kiswahili yaani viambishi vinaweza kupachikwa
kabla au baada ya mzizi na uwa na uamilifu bayana. Hebu tuchunguze mifano
ifuatayo:
Kiswahili
|
Kisukuma
|
Kisimbiti
|
Kinyiha
|
A-na-lim-a
|
a-le-lem-a
|
a-ra-rem-a
|
i-nku-lim-a
|
a-na-chek-a
|
A-le-sek-a
|
a-ra-sek-a
|
a-ku-sek-a
|
Kwa kuangalia mifano hii utagundua kwamba
katika kutenganisha viambishi hufuata kanuni moja kwamba mahali kinapokaa
kiambishi kwa mfano cha njeo, ndipo pia hukaa kwa upande wa lugha za kibantu,
kwa mfano –na- na –ra- katika lugha ya kisimbiti. Hivyo tunaweza kusema kuwa
kuna unasaba baina ya lugha hizi.
Vilevile sintaksia ya lugha ya Kiswahili na
lugha za kibantu hufanana kwa karibu sana. Kwa mfano jinsi ya mpangilio wa vipashio na
kuunda sentensi hufanana yaani mpangilio wa maneno hufuata kanuni maalum ambazo
hufanana katika Kiswahili na lugha za kibantu. Katika Kiswahili sentesi ina
kuwa na pande mbili yaani upande wa kiima na upande wa kiarifu, katika upande
wa kiima kipashio chake kikuu ni nomino na katika upande wa kiarifu kipashio
chake kikuu ni kietnzi. Hii inamaana kwamba katika kuunda sentensi ni lazima
nomino ianze na baadaye kitenzi. Hebu tuangalie mifano ifuatayo:
Kiswahili
|
Mama / anakula
N (K) T (A)
|
Kijita
|
Mai / kalya
N(K) T (A)
|
Kihehe
|
Mama/ ilya
N(K) T(A)
|
Kihaya
|
Mama / nalya
N(K) T(A)
|
Katika mifano hii tumeona kwamba muunndo wa
kiima-kiarifu katika lugha za kibantu unafanana sana na ule wa Kiswahili yaani
nomino hukaa upande wwa kiima halikadhalika kitenzi hukaa upande wa kiarifu,
kwa hiyo kwa mifano hii tunaweza kusema kuwa lugha ya Kiswahili ni jamii ya
lugha za kibantu.
Pia mfumo wa sauti (fonolojia) wa lugha za kibantu unafana sana
na ule wa Kiswahili, yaani mpangilio wa sauti katika kuunda silabi, na miundo
ya silabi kwa ujumla hufanana. Kwa mfano katika lugha ya Kiswahili hakuna
muundo wa silabi funge yaani silabi ambayo inaishia na konsonanti, muundo
asilia wa silabi za Kiswahili ni ule unaoishia na irabu vilevile katika lugha
za kibantu hufuata muundo wa silabi wazi, yaani silabi zote huishia na irabu.
Mifano ifuatayo hufafanua zaidi:
Kisawhili
|
Baba
|
K+I+K+I
|
Kikurya
|
Tata
|
K+I+K+I
|
Kiha
|
Data
|
K+I+K+I
|
Kijita
|
Rata
|
K+I+K+I
|
Kipare
|
Vava
|
K+I+K+I
|
Tanbihi: K= konsonanti I= irabu.
Kwa mifano hii tunaona kwamba mifumo ya sauti
katika lugha za kibantu hufanana na ule wa Kiswahili, kwa hiyo tunaweza
kuhitimisha kwa kusema kuwa lugha hizi ni za familia moja.
Pia vilevile mfumo wa ngeli za majina katika
lugha ya Kiswahili hufanana sana na ule wa kibantu hususani katika upachikaji
wa maumbo ya umoja na wingi na maumbo ya upatanisho wa kisarufi. Katika lugha ya Kiswahili viambishi vya
umoja na wingi hupachikwa mwanzoni kabla ya mzizi wa neno, hivyohivyo katika
lugha za kibantu. Kwa mfano:
|
Umoja
|
Wingi
|
Kiswahili
|
m-tu
|
wa-tu
|
Kikurya
|
mo-nto
|
abha-nto
|
Kiha
|
umu-ntu
|
abha-ntu
|
Kikwaya
|
mu-nu
|
abha-nu
|
Mifano hiyo hapo juu inadhihirisha wazi kwamba
vipashio vyote vya umoja na wingi hujitokeza kabla ya mzizi wa neno, hivyo ni
dhahiri lugha hizi zina uhusiano wa nasaba moja.
Vilevile katika upatanisho wa kisarufi
lugha za kibantu na Kiswahili huelekea
kufanana viambishi vya upatanisho wa kisarufi hususani viambisha vya nafsi.
Kwa mfano:
Kiswahili
|
Mtoto a-nalia
|
Kizanaki
|
Umwana a-rarira
|
Kisukuma
|
Ng’wana
a-lelela
|
Kikurya
|
Omona a-rakura
|
Tunaona hapo juu kwamba kiambishi ‘a’ cha upatanisho wa kisarufi hujitokeza
katika lugha zote, hivyo tunashawishika kusema kuwa Kiswahili kina uhusiano
mkubwa na kibantu.
Pamoja na
ushahidi wa kiisimu kutupatia vithibitisho tosha juu ya ubantu wa Kiswahili pia
kuna ushahidi mwingine kama vile ushahidi wa kihistoria, kiakiolojia na
kiethinolojia.
Ushahidi wa
kihistoria huchunguza
masimulizi na vitabu mbalimbali vya kale ambavyo huelezea asili na chimbuko la
wakazi wa upwa wa Afrika Mashariki. Vilevile ugunduzi wa kiakiolojia huonesha kuwa kulikuwa na wakazi
wa asili wa upwa wa Afrika Mashariki ambao walikuwa na utamaduni wao na
maendeleo yao hata kabla ya kuja kwa wageni. Katika ushahidi wa kiethinolojia,
huchunguzwa tarihi mbalimbali zinazojaribu kutoa historia ya watu pwani ya Afrika
Mashariki na lugha yao.
Kwa ujumla vyanzo hivi vyote huonesha kuwa
pwani ya Afrika mashariki ilikuwa na wakazi wake wa asili ambao walikuwa na
lugha yao, utamaduni wao na pia maendeleo yao, vyanzo hivi pia huhitimisha kwa
kusema kuwa lugha ya wakazi hawa ilikuwa ni Kiswahili.
Kwa hiyo, kwa hoja hizi tunaweza kuhitimisha
kwa kusema kuwa, madai ya kusema kwamba msamiati mwingi wa kiarabu katika lugha ya Kiswahili hayana mashiko;
Kwani hakuna ushahidi wa kutosha kusimamia hoja hiyo. Kama ilvyojadiliwa hapo
juu,vigezo vya kiisimu, kihistoria, kiakiolojia na kiethnolojia ndivyo vitoavyo
ushahidi wa kina na kutoa hoja za mashiko kuthibitisha kuwa Kiswahili sio kiarabu na bali ni kibantu.
MAREJEO.
Khalid (2005) “Swahili words of Arabic
origin” katika
Lodh, A.Y (2000) Oriental influences in Swahili: A study in language. Götenbog.
Sweden.
Massamba, D.P.B na wenzake (1999) Sarufi miundo ya Kiswahili Sanifu. TUKI.
Dar es salaam.
Massamba, D.P.B (2002) Historia ya Kiswahili 50BK hadi 1500BK.
The Jomo Kenyatta Foundation.
TUKI (2004) kamusi ya Kiswahili sanifu. TUKI. Dar es salaam.
TOFAUTI
KATI YA NYANJA ZA ISIMU NA MATAWI YA ISIMU KATIKA KISWAHILI.