I.
KATEGORIA ZA KISARUFI KULINGANA NA
MTIZAMO WA WANAMAMBOLEO:-
Kategoria ya Sarufi ya
kimamboleoInaoongozwa na wanasosiolojia ambao unahusisha sarufi mbalimbali kama
vile :- Sarufi msonge , Sarufi miundo virai na Sarufi geuza maumbo zalishi iv.
Sarufi husiano Katika kategoria hii huu ndipo tunapata kuona sarufi kama tafiti na uchambuzi wa miundo
inavyooneka kwenye lugha.
a) Kategoria
ya Muundo wa Kirai;
Kirai ni fungu la
maneno yanayohusiana kimuundo lisilokuwa na muundo wa kiima kiarifu. Maneno
katika kirai humilikiwa na neno moja ambalo ndilo neno kuu. Kirai hubainishwa
na kategoria ya neno kuu. Kwa mfano: KN, KT, KV, KE KH n.k.
Virai huundwa na
viambajengo. Kiambajengo ni kikundi cha maneno au hata neno moja pia inayofanya
kazi kama kitu kimoja. Kirai, kishazi au sentensi ni mkusanyiko wa viambajengo
kadha.
Kirai ni mkusanyiko wa
viambajengo vilivyojengwa kuzunguka neno kuu. Kwa mfano, KN huundwa na nomino
na vivumishi vyake, kwa hivyo muundo wa kirai ni maneno yanayokiunda
yakiwakilishwa na alama za kategoria za maneno hayo.
Kwa mfano: a) ‘Mtoto
mdogo’. Hiki ni Kirai Nomino (KN)
kilichoundwa na N (nomino) na V (kivumishi).
Kwa hivyo KN N+V b)
‘analima shamba’.
Hiki ni kirai kitenzi
(KT) chenye kuundwa na kitenzi (T) na kirai nomino (KN). Kwa hivyo KT T+KN.
b) Kategoria
ya Muundo wa Vishazi na Sentensi
Kishazi ni kikundi cha
maneno kilicho ndani ya sentensi chenye muundo wa kiima na kiarifu. Kishazi
kina muundo sawa na sentensi.
Sentensi ni kikundi cha
maneno chenye maana iliyo kamili. Sentensi ndicho kipashio lugha cha kimuundo
ambacho ni kikubwa kuliko vipashio vingine. Vipashio vya lugha ni pamoja na:
mofimu, neno, kirai, kishazi na sentensi yenyewe. Sentensi na kishazi huundwa
na virai vikuu viwili: KN na KT. KT yaweza kuundwa na kitenzi na nomino,
kitenzi na kielezi .
Kwa hivyo S- KN + KT
c) Kategoria
ya Sarufi geuza umbo zalishi;
Kategoria ya geuza umbo zalishi huonyesha ujuzi alionao
mzungumzaji ambao humwezesha kutunga sentensi sahihi na zisizo na kikomo. Uwezo
wa mzungumzaji kutunga sentensi zisizo na ukomo unatokana na kufahamu kanuni za
kutunga sentensi sahihi ambazo mzawa wa lugha anazijua kutokana na kuwa na
umilisi na lugha yake. Kanuni za kutunga sentensi sahihi hubainisha sentensi
sahihi na zisizo sahihi.
Kwa mujibu wa kategoria
hii, sentensi ina umbo la nje ambalo ndilo linalojitokeza katika usemaji na
hata inapoandikwa, na umbo la ndani ambalo huwa limefichika na hujidhihirisha
katika umbo jingine wakati wa kuongea (maana).
Kategoria hii imeweza
kuonyesha uhusiano wa tungo ambazo japo zilikuwa na umbo la nje tofauti, zina
umbo la ndani sawa.
Kwa mfano:
Juma anacheza mpira
KN KT KN
Mpira unachezwa na Juma
KN KT
KU KN
Mfanano wa tungo hizi
umekitwa katika maana. Japokuwa sentensi a) inaanza na Juma, na ile b) inaanza
na Mpira, mtenda na mtendwa katika sentensi zote ni yule yule.
d) Kategoria
ya Sarufi miundo virai zalishi;
Katika kategoria ya sarufi miundo virai zalishi
muundo wa sentensi huelezwa kwa kuchanganua vijenzi vyake ambavyo ni
viambajengo. Viambajengo hivi huchanganuliwa hadi kufikia neno moja ambalo
hubainishwa kwa kategoria yake ya kisarufi. Uchanganuzi huu wa sentensi
huelezwa kwa kanuni ambazo huwezesha kutunga sentensi nyingi zaidi.
Kanuni za muundo
virai. KN N --- mtoto
Hii ina maana kuwa KN
ina N (yaani Kirai Nomino kina kiambajengo kimoja tu ambacho ni nomino). Hii
yaweza pia kuelezwa hivi:
KN N
Mtoto
Hii ina maana kuwa
kirai hiki ni neno moja. ‘mtoto’Kirai chenye viambajengo zaidi kimoja, yaani
chenye maneno zaidi ya moja huelezwa kwa
kanuni:
KN N V au KN N V Mtoto mzuri Hii ina maana kuwa KN
kinaundwa na maneno mawili, yaani ‘mtoto mzuri’Vivyo hivyo kwa Kirai kitenzi
(KT).
KATEGORIA ZA KISARUFI KULINGANA NA MTAZAMO WA WANAMAPOKEO:-
Kama
ilivyoelezwa hapo mwanzoni kuwa kategoria za kisarufi zinahusu sifa
zinazoambatanishwa katika aina za maneno nazo ni kama ifuatavyo:-
Kategoria za nafsi,
ni sifa ama ni kipashio kinachodhihirisha muhusika katika usemaji nazo zipo za
aina tatu ambazo nafsi ya I, II, na III
ambapo huwakilishwa na ni-tu, u-m na a-wa.viwakilishi katika ngazi hii ni
tegemezi kwani haviwezi kusimama peke yake na kuleta maana iliyokusudiwa.kwa
mfano
Nafsi
ya I ninaimba- tunaimba
Nafsi
II unaimba-
mnaimba
Nafsi
III anaimba – wanaimba
Kategoria za njeo/wakati, ni
viambishi vinavyoambikwa katika mashina ya vitenzi vikionesha au kutoa taarifa
ya tendo lililtendeka, linatendeka au litatendeka muda gani.viambishi hivi ni
vingi lakini vimewekwa katika katika hali ya uyakinishi na viambishi vya tendo
katika hali ya ukanushi, njeo hiyo iliyopo, iliyopita, na ijayo katika hali ya
uyakinishi na ukanushi kwa mfano. Njeo iliyopita Alicheza -
hakucheza
Walicheza –
hawakucheza
Njeo
iliyopo ninasoma - sisomi
Tunasoma – hatusomi
Njeo
ijayo utalima – hautalima
Mtalima- hamtalima
Kategoria za hali,ni
viwakilishi ni viwakilishi vinavyopachikwa katika mashina ya vitenzi ambavyo
huangalia utendekaji wa lile tendo. Kategoria hizi huwa viko karibu sana na
kategoria za njeo.japo zina utofauti kuna aina zaidi ya tatu za hali kwa mfano
hali ya mazoea huwakilishwa na (hu-) hali ya kuendelea huwakilishwa na
kiambishi (na-), hali ya masharti huwakilshwa na kimbishi (-ki-/-nge-/-ngali-/-ngeli-)
na hali timilifu inayowakilishwa na kiambishi (-me-). Katika hali ya kutokea
viambishi hivi havitokei katika shina moja la kitenzi ilavinaweza vikatokea
katika sentensi moja katika mashina tofauti ya vitenzi.kwa mfano mwalimu
alikuwa anafundisha /amefundisha . katika sentensi hii -li- inaonesha njeo na
-na- /-me- inaonesha hali
Kategoria za idadi, hivi
ni viambishi vinavyoambikwa katika aina mbalimbali za maneno vikionesha umoja
na wingi ambapo katika Kiswahili hudhihirika kupitia viambishi ngeli vya
upatanisho wa kisarufi . kwa mfano mwalimu
analima, walimu wanalima (a-wa)
huonesha umoja na wingi hivyo hudokeza idadi.
Kategoria
za kauli, ambalo ni umbo
ni umbo la kitenzi ambalo linadhihirisha uhusiano baina ya kiima na yambwa
mfano kauli ya kutenda na kutendwa