Subcribe to our RSS feeds Join Us on Facebook Follow us on Twitter Add to Circles

Jumanne, 9 Septemba 2014

MAANA IBUKIZI KWA WAZUNGUMZAJI WA KISWAHILI ZAMA ZA UTANDAWAZI (MAANA YA KINGONOSHI).



                    Wazungumzaji wa Kiswahili wanaweza kuibua maana mbalimbali kulingana na wanavyotumia maneno. Maana hii huibuliwa mara nyingi na msikilizaji. Wakati msemaji akimaanisha maana fulani msikilizaji huweza kuibua maana ya ziada ambayo msemaji hajamaanisha. mtaalamu mmoja aliyaita maneno hayo ibukizi maneno ya kiungonoshaji. yaani nanafungamana na fikra za kingono. Ashakumu si matusi, maneno yatakayotumika ni makali zaidi kwani tumeyachukua jinsi yalivyo kutoka kwa wazungunzaji wa lugha.
      Yafuatayo ni baadhi ya maneno ya Kiswahili ambayo yakitumika kati ya wazungumzaji na wasikilizaji huweza kuibua maana ya ziada. Maneno haya  tutayaainisha kwa kuyatungia sentensi  na kufafanua utata wa maana zake.Kwa uhakika maneno haya hutumika katika mazingira ya kawaida lakini haijulikani ni kitu gani humsukuma msikilizaji kuibua maana ya ziada bada la ya maana ya msingi. Endelea
(i) Sentensi hizo ni kama ifuatavyo;
1.      Juma amemkata Asha jana.
Maana ya msingi; Juma ametumia kifaa chenye ncha kali kama vile sindano, kisu, panga na vinginevyo kumuweka jeraha mwilini mwa Asha.
Maana ibukizi; Juma amefanya mapenzi na Asha.
2.      Yeye alimwambia rose “naomba tigo
Maana ya msingi; Alimuomba Rose ampatie aidha vocha ya mtandao au kampuni ya mawasiliano ya tigo au laini ya tigo
Maana ibukizi; Yeye alimuomba Rose afanye naye mapenzi kinyume cha maumbile.
3. Nilipokuwa nasafiri kwa daladala kwenda mbagala nilisikia mama mmoja akimwambia kondakta wa daladala “nitakupa ikisimama”.
Maana ya msingi: Alimwambia atatoa nauli endapo gari litakuwa limesimama kituoni.
Maana inambukizi; ana kwamba watafanya nae mapenzi endapo uume utakuwa imesimama.
4.      Rafiki yangu aliniambia “atanipa mbele”.
Maana ya msingi; Rafiki yangu atanipa kitu fulani tulichoaidiana mbele ya safari tunapoelekea.
Maana ibukizi; Rafiki yangu atanipa sehemu ya mbele yaani uke au uume wakati tukifanya mapenzi.
5.      Naomba usinitie hapa tafadhali.
Maana ya msingi; Anaomba usimhusishe au usimjumuishe au kumuhusisha na tendo au tukio lolote.
Maana ibukizi; Anaomba usifanye naye mapenzi katika eneo hilo labda kwa sababu lipo wazi sana au halifai.
6.      Raheli alimwambia Kanyamaishwa kuwa  “ndizi yake” ni kubwa kuliko ya Jabiri.
Maana ya msingi; Tunda aina ya  ndizi alilokuwa nalo Kanyamaishwa lilikuwa ni kubwa kuliko la  Jabiri.
Maana ibukizi; Kanyamaishwa ana uume mkubwa kuliko wa Jabiri.
7.      Jamila ana shimo kubwa sana
Maana ya msiingi; Jamila ana sehemu  kubwa aliyoichimba kwenda chini kwa ajili ya kuweka vitu kama vile takataka.
Maana ibukizi; Jamila ana uke mkubwa sana (mpana)
8.      Amina alimwambia Jabiri kuwa “watafanya”.
Maana ya msingi; Wakikutana watatekeleza mambo fulani ya msingi waliyokuwa wameahidiana.
Maana ibukizi; Watakapo kutana hawatafanya mapenzi.
9.      Pita amemchoma Meri
Maana ya msingi; Pita ametumia kitu chenye ncha kali kwa kumjeruhi meri kama vile sindano.
Maana ibukizi; Pita amefanya mapenzi na Meri hadi akaridhika.
10.  Asha alimwambia Deo “leo umenifikisha kileleni”.
Maana ya msingi; Asha ailmwambia Deo kuwa leo amekwea naye hadi mwishoni mwa  kikomo au tamati ya mlima.
Maana ibukizi; Asha alimwambia Deo kuwa leo amefanya nae mapenzi akaridhika.
11.  Juma alimwambia Asha apanue aingize vizuri.
Maana ya msingi; Juma alimwambia  Asha afungue vizuri kitu kama mfuko au gunia ili aweke kitu fulani kwa uangalifu.
Maana ibukizi; Juma alimwambia Asha atanue vizuri miguu ili sehemu zake za siri yaani uke uonekane vizuri ili aingeze uume vizuri.
12.  Jana shangazi alimwambia mjomba achomoe taratibu.
Maana ya msingi; Shangazi alimwambia mjomba atoe kitu fulani kilichokuwa kimeingizwa mahali fulana kama vile msumari ukutani taratibu.
Maana ibukizi;  Shangazi alimwambia mjomba utoe uume wake taratibu kwenye uke wa shangazi.
13.  Daaa!!!! Rafiki yangu anamtambo mkubwa sana.
Maana ya msingi; Rafiki nyangu ana mashine kubwa sana ya kurahisishia kazi kama vile jenereta na n.k.
Mmana ibukizi; Rafiki yangu ana uume mkubwa.
14.  Jabiri amelala na Asha.
Maana ya msingi; Jabiri alipumzika pamoja na Asha kitandani au chini.
Maana ibukizi;  Jabiri alifanya mapenzi na Asha.
15.  Dada alimwambia kondakta “nikikaa vizuri nitakupa”.
Maana ya msingi; Dada atamwambia kondakta atampa nauli aliwa amekaa vizuri.
Maana ibukizi; Dada atampa konda uke akikaa vizuri.
16.  Siku hizi bakari anatembea na dada yangu.
Maana ya msingi; Bakari anaongozana na dada yangu katika matembezi yao.
Maana ibukizi; Bakari anamahusiano ya kimapenzi na dada yangu.
17.  Musa ameacha kusimamisha siku hizi.
Maana ya msingi; Musa ameacha tabia yake ya kuzuia kitu fulani kama vile gari, pikipiki au baisikeli visiendelee na safari.   
Maana ibukizi; Musa, uume wake haufanyi kazi kama mwanaume kamili.
18.  Yeye amemwagia Dada mbegu kichwani.
Maana ya msingi; Ina maana yeye alimmwagia nafaka kama vile mahindi, maharage na kadhalika kichwani.
Maana ibukizi; Yeye alimmwagia manii/ shahawa kichwani.
19.  Alinitaka sana mara ya kwanza nikakataa lakini mara ya pili nilikuballi.
Maana ya msingi; Kunihitaji tushirikiane naye sana katika kufanikisha jambo au mabo fulani aliyokuwa nayo mfano kazi.
Maana ibukizi; Kumwomba awe na uhusiano wa kimapenzi naye.
20.  Jana nilikunwa vizuri sana kuliko siku zote.
Maaana ya msingi; Jana alinikwangua kwangua au kunisugua sugua kwa kutumia kitu kama kucha au kijiti kuliko siku zote.
Maana ibukizi; Jana alinidhisha kimapenzi kuliko siku zote.
21.  Halima hatamwacha Munisi kwa sababu alimsugua vizuri.
Maana ya msingi; Munisi alimkuna / alimsugua vizuri alipokuwa anawashwa.
Maana ibukizi;  Halima alifanya naye mapenzi hadi aridhike
22.  Hapo mwanzo alitulia sana siku hizi anagawa sana.
Maana ya msingi; Alikuwa hatoi vitu kama vile msaada kwa watu.
Maaana ibukizi; Alikuwa hajihusishi na masuala ya mapenzi lakini kipindi hiki anafanya sana mapenzi kwa kila mtu.
23.  Pale nimepita lakini sijafurahi kabisa.
Maana ya msingi; Kuendelea na safari kwa kupitia njia ile ile lakini hufurahii safari.
Maana ibukizi; Kufanya mapenzi na mtu fulani bila kupata raha yoyote.
24.  Juma ndie aliyewabandua wale wasichana wawili.
Maana ya msingi; Kutoa mabango au vipeperushi vya wasichana wawili vilivyokuwa vimewekwa sehemu fulani kama kwenye mbao za matangazo.
Maana ibukizi; Juma ndiye aliyewatoa bikira wasichana wale wawili.
25.  Alipotoka pale alikuwa tayari kaloana.
Maana ya msingi; Nguo alizokuwa amevaa zilikuwa na majimaji.
Maana ibukizi; Alipotoka pale nguo zake zilikuwa zimeloa shahawa.
26.  Juma hajui kulenga mpaka aongozwe.
Maana ya msingi; Hana shabaha hadi aongozwe .
Maana ibukizi; Juma hawezi kuingiza uume wake kwenye uke hadi aongozwe.
27.  Ingawa ya kwangu ni nyembamba lakini ya kwake ni nene zaidi.
Maana ya msingi;  Maneno “ya kwake” na “ya kwangu” yanarejelea nomino yoyote iliyomo katiaka ngeli ya mofolojia ya nomino. Kwa mfano simu, nyumba, chupa na n.k.
Maana ibukizi; Maneno “ya kwangu” na “ya kwake” huweza kurejelea na kumaanisha sehemu za siri za mwanamke au mwnaume. (uke na uume)
28.  Leo nina hamu sana kwasababu nimemkosa siku nyingi.
Maana ya msingi; Nina shauku ya kumuona kwa sababu sijamuona siku nyingi.
Maaana ibukizi; Nina nyege naye za kufanya naye mapenzi kwa sababu sijafanya naye siku nyingi.
29.  Joni hupenda sana kuzama chumvini.
Maana ya msingi; Joni anapenda kuingia sehemu yenye majimaji yenye asili ya chumvi.
Maana ibukizi; Joni anapenda sana kunyonya au kulamba sehemu za siri za mwanamke yaani uke.
30.  Ingawa alinishughulikia vizuri sikuridhika.
Maana ya msingi; Ingaw alifanya haraka katika kufanikisha jambo fulani / kujitahidi kufanikisha jambo fulani.
Maana ibukizi; Ingawa alinipa mapenzi vizuri lakini sikiridhika
31.  Ingawa anamtaimbo mkubwa hawezi kuutumia
Maana ya msingi; Ingawa ana fimbo kubwa ya chuma ya kuvunjia miamba hawezi kuitumia.
Maana ibukizi; Ana uume mkubwa lakini hawezi kuutumia.
32.  Japokuwa amenichokonoa hakufanikiwa.
Maana ya msingi; Japokuwa alinidadisi kwa kuniuliza maswali lakini hakifanikiwakupata majibu aliyoyahitaji.
Maana ibukizi; Aliingiza uume au kidole kwenye uke bila kutimiza haja ya mwanamke.
33.  Jana alinikaza kuliko siku zote.
Maana ya msingi;  Jana alinifanyia uimara kuliko siku zote
Maana ibukizi;  Alinifanyia mapenzi mazuri kuliko siko zote
34.  Ingawa alimpa kidogo ila alikojoa sana.
Maana ya msingi;  Ingawa alipata kinywaji kidogo alienda haja ndogo mara nyingi.
Maana ibukizi;  Alitumia sehemu za siri (uke au uume) kidogo lakini alitoa shahawa nyingi.
35.  Aise! Siku hizi huoni mtu anayefyeka ovyo ovyo.
Maana ya msingi; Siku hizi huoni mtu anayejua kukata miti au  majani ili yawe mafupi ovyo ovyo.
Maana ibukizi; Siku hizi huwezi kuona mtu akifanya mapenzi na kila msichana bila kuchagua.
36.  Yeye ananimegea vizuri kuliko wewe.
Maana ya msingi; Yeye ananivunjia kitu au kunikatia kitu kinacholiwa vizuri kuliko wewe.
Maana ibukizi; Yeye alinipa mapenzi mazuri yasiyokuwa na choyo kuliko wewe.
37.  Kutokana na tundu lako dogo nilishindwa kutimiza haja yangu.
Maana ya msingi; Kutokana na uwazi mdogo mfano tundu la choo nilishindwa kutimiza haja yangu.
Maana bukizi; Kutokana na uke wako mdogo nilishindwa kufanya mapenzi vizuri nikatimiza haja yangu.
38.  Juma hupenda kunyonya maziwa kila siku kabla hajalala.
Maana ya msingi; Juma hupenda kunywa maziwa yaliyosindikwa katika pakiti au mifuko.
Maana ibukizi; Juma hupenda kunyonya matiti kila siku usiku.
39.  Jana yeye alimtafuna kutwa nzima.
Maana ya msingi; Jana alisaga kwa meno kitu fulani kutwa nzima.
Maana bukizi; Jana alifanya nae mapenzi siku nzima.
40.  Juma alipochomoa nilihisi maumivu makali.
Maana ya msingi; Juma alipotoa kitu kama sindano matakoni mwangu nilipata maumivu makali.
Maana bukizi; Juma alipochomoa uume kwenye uke nilihisi maumivu.
41.  Mama alimwambia dada kuwa “usafi unaanzia chini”.
Maana ya  msingi; Mama alimwambia dada usafi huanzia sehemu ya kawaida kabisa tenga katika ngazi ya chini.
Maana ibukizi; Mama alimwambia dada kuwa usafi unaanzia sehemu za siri yaani uke au uume.
42.  Ikiingia huwa ninasinzia.
Maana ya msingi; Ikipenya kuingia ndani kitu kama sindano ya usingizi huwa ninasinzia.
Maana ibukizi; Kila uume uingiapo ndani ya uke wangu huwa ninasinzia
43.  Alipoiweka ilizama yote.
Maana ya msingi; Baada ya kuingia au kuzama ndani ya kitu kama vile  kimiminika ilizama yote.
Maana ibukizi; Uume ulipoingia ndani ya uke ilizama yote.
44.  Kila nikifikia katikati huwa nndio ninapata utamu.
Maana ya msingi; Kila nikifika katikati ndio nanogawa kwa kitu au jambo.
Maana bukizi; Kila nikiingiza kwenye uke (katikati) ndio napata utamu.
45.  Wewe unapenda nyeti.
Maana ya msingi; Wewe unapenda kudeka
Maana bukizi. Wewe unapenda sehemu za siri ( uke au uume)
46.  Mchi wake unatwanga vizuri.
Maaana ya msingi. Kifaa chake cha  kutwangia vitu kama nafaka na madawa kwenye kinu unatwanga vizuri.
Maana ibukizi; Uume wake unaweza kufanya mapenzi vizuri.
47.  Akina mama huko mbele mtanipa. (aliuliza mgombea). Na akina baba je huko nyuma mtanipa.     
Maana ya msingi; Akina mama mliokaa mbele na akina baba mliokaa nyuma mtanipia kura.
Maana ibukizi;   Neno “mbele” na “nyuma” yana maana sehemu za  siri yaana “mbele” ni “uke” na “nyuma” ni “mkundu”.
48.   Sina hamu kabisa na yule kaka maana kitendo alichonifanyia huko nyuma sitakisahau kabisa.
Maana ya msingi: Sina hamu kabisa na yule kaka, kwani  kuni  jambo alilonifanyi hapo zamani sitalisahau kabisa.
Maana ibukizi: Sina hamu kabisa na yule kaka maana kitendo alichonifanyia kwenye matako/ mkundu sitakisahau.

49.  Jamaa wa lori alilazimishia mpaka akafanikisha  kumchomekea kwa mbele yule dada aliyekuwa anaendesha gari aina ya  Prado.
Maana ya msingi: Jamaa wa lori alilazimisha mpaka akafanikisha kutanguliza gari lake aina ya lori  katika nafasi ya mbele ya gari la yule dada  mwenye Prado.
Maana ibukizi: Jamaa wa lori alilazimisha mpaka akafanikisha  kuingiza uume wake katika uke wa dada yule mwenye  Prado.
50.  Dada  mwenye pikipiki  alimwambia yule kijana yule pale sheli, “ingiza vizuri pipe yako usije ukamwaga nje”.

Maana ya msingi: Dada mwenye pikipiki alimwambia yule kijana pale sheli, “weka mpaka ndani bomba la mafuta  usije ukamwaga mafuta nje.

Maana ibukizi: Dada mwenye pikipiki alimwambia yule kijana pale sheli,
“ingiza uume wako mpaka ndani usije akamwaga shahawa nje”.
 
(ii) Kutokana na data ya kwanya kategoria zinazongonoishwa zaidi ni pamoja na;
·         Vitenzi. Kwa  mfano choma, liwa , ingiza, chomoa ,liwa, tia, tiwa.
·         Nomino. Kwa mfano shimo, tundu, mtaimbo, mchi.
·         Vivumishi. Kwa mfano, yake nene, pana.
·         Vihusishi. Kwa mfano, ya kwake, ya Asha
Kategoria zinazongonoishwa zaidi ni vitenzi kwa sababu ndio msingi na muhimili wa sentensi. Vile vile ndio msingi unaobeba utendaji katika tungo.
Kategoria ambazo haziwezi kungonoshwa ni viunganishi na vielezi.
(iii) Wazungumzaji wa Kiswahili hupenda sana kuibua maneno kwa sababu hufikiria zaidi ya maana ya msingi ya neno husika kutokana na maendeleo ya sayansi na tekinolojia na kusababisha dhana ya ngono kukaa akilini mwa watu hasa vijana.
(iv) Kati ya msemaji na msikilizaji anayengonosha maneno yanayosemwa ni msikilizaji kwani yeye ndiye mlengwa na mfasiri wa dhana inayosemwa. Yeye ndiye anayetafuta maana ya lile lisemwalo.
(v) Hakuna ruwaza maalumu na dhabiti ya ungonoishaji.
(vi)  Kundi la watu wanaongonoisha zaidi ni kundi la vijana kwa misingi ya rika kwa sababu rika hili huwa na mawazo yalivofungamana zaidi na mambo ya ngono.
(vii) Anayeelewa maana ngonoshi za maneno ya Kiswahili ni wazungumzaji na watu waliofungamana na maana hizo za ngono. Wasioelewa maana ya ngonoshi ni wale ambao wapo nje ya muktadha  na rika hilo la vijana. Mfano baadhi ya wazee.
(viii) Katika taaluma ya isimu ungonoshi una mchango kama ufuatao;
·         Huonyesha uhusiano wa maana za maneno. Kwa mfano unaweza kujua ni neno lipi lina maana ya msingi na lipi lina maana ngonoshi.
·         Husidia katika kuonyesha ukubalifu wa maana za maneno kulingana na matumizi. Yaani neno linapata maana kutokana na jinsi linavyotumika, watumiaji wenyewe katika mzingira fulani.
·         Hutusaidia kupata maana za ziada. Kwa mfano neno “mbele” inaweza kuwa na maana ya “kutangulia” na maana ya ziada  ikawa  ni “sehemu za siri” yaani uke au uume.
Athari za maana ibukizi / ungonoishaji ni pamoja na;
·         Kwanza athari ni kupotosha maana ya msingi. Kwa mfano msemaji alikusudia kuomba kura kwa kusema “kina mama hapo mbele mtanipa” kama kuwauliza wanaompiga kura lakini wao wakapata maana potofu ya kuwaomba sehemu za siri yaani uke
·         Pili ni kuongeza uziada dufu katika lugha. Ungonoishaji huaongeza maana ya ziada katika neno. Maana isiyo ya msingi katika neno.
·         Tatu ni kuleta utata katika tungo. Kwa mfano “ikiingia huwa nafumba macho”. Mtu anaweza kujiuliza nini inayoingia.
·         Pia huibua mgogoro katika jamii. Kwa mfano msemajia anapomwambia msikilizaji (kwa mfano wa kike) ambaye hana mzoea naye utungo kama “unashimo kubwa”, kauli hii yaweza kuleta malumbano baina ya msemaji na msikilizaji.
·         Hupelekea uzalilishaji wa kijinsia.
(ix) Ungonoishaji wa maneno ya Kiswahili ni jambo jipya lililoibuka ingawa maneno yanayotumika yalikuwepo. Kimsingi maneno haya yalizingatia maana za msingi za maneno husika. lakini kutokana na maendeleo ya sayansi na tekinolojia pamoja na utandawazi maneno haya yameanza kupewa maana ya ziada inayofungamana na ngono yaani ungonoishaji. Na hii hutokana na mawazo ya watumiaji kufungamana na ngono.
(x) Suala la ungonoishaji ni suala la kukemewa na kubezwa kwani linapotosha maadili na uwezo wa kukamilisha mawasiliano na lengo lililokusudiwa. Kwa mfano kama mtu anafundisha anaweza kujikuta anachekwa baada ya kutumia neno liloibua dhana ya ungonoishi kwa wanafunzi au wasikilizaji. Hivyo suala hili likiendelezwa mwisho wake maana ya msingi imefifizwa na wanatumia maana ungongoshi tu.



Marejeo.
TUKI,  (2004), Kamusi ya Kiswahi Sanifu. Oxford University Press: Nairobi





Jumatatu, 21 Julai 2014

MAENDELEO YA LUGHA YA KISWAHILI.


MAENDELEO YA KISWAHILI.
Kiswahili ni lugha inayozungumzwa katika eneo kubwa la Afrika ya Mashariki. Lugha hii ina utajiri mkubwa wa misamiati, misemo, mithali, mashairi, mafumbo, vitendawili na nyimbo. Kiswahili hutumika mashuleni, katika mawasiliana na kuna vitabu vingi vilivyotungwa kwa kutumia lugha hiyo, vikiwa pamoja na vile vya hadithi, hekaya au riwaya.
Lugha ilianza takriban miaka 800-1000 iliyopita katika pwani ya Afrika Mashariki.Wakazi wa Pwani hii waliokuwa wasemaji wa lugha za Kibantu tofauti tofauti mfano; kisukuma, kihaya, kijita, kikurya, kimakonde, kingoni, kihehe, kizigua, kibena n.k.katika shughuli mbalimbali kama biashara ambazo zilikuwa zikiwakutanisha watu hawa wakiwa wanaozungumza lugha tofauti tofauti, iliwabidi waweze kuchukua msamiati mbalimbali kutoka katika lugha zao ili waweze kuwasiliana katika shughuli zao. Walipopokea maneno mengi hasa ya Kibantu katika mawasiliano yao, ikachangia kuwa msingi wa Kiswahili ni sarufi na msamiati wa Kibantu.
Kwakua tumeona kuwa Kiswahili ni lugha sasa basi, lugha nini?
Lugha ni sauti za nasibu zilizo katika mpangilio maalumu na zilizo kubaliwa na jamii ya watu zitumike kama chombo cha mawasiliano.
Au
Ni mfumo wa sauti za nasibu za kusemwa zinazotumiwa na watu wa jamii fulani wenye utamaduni unaofanana kwa madhumuni ya mawasiliano katika jamii hiyo.
Au
Katika kamusi ya kiswahili sanifu TUKI 1981 oxford press uk. 86, inafafanua kuwa lugha ni mfumo wa sauti nasibu ambazo hutumiwa na jamii kwa madhumini ya mawasiliano kati yao.
Sifa / tabia za lugha.
(a)Lugha huzaliwa.
Lugha huzaliwa kutokana na mwingiliana kati ya lugha mbili au zaidi nakutengeneza lugha moja. Kwa mfano lugha ya Kiswahili imetokana na mwingiliano wa lugha mbalimbali za kibantu.
(b)Lugha hukua.
Lugha hukuwa kutokana na kuongezeka kwa msamiati mbalimbali ambayo hutumiwa katika lugha husika katika shughuli mbalimbali.
(c)Lugha huathiliwa.
Lugha huathiliwa kutokana na mwingiliano wa lugha mbili tofauti  na kusababisha ukiukwaji wa kanuni na matumizi sahihi ya lugha mojawapo. Kwamfano Kiswahili kinaweza kuathiliwa na kiingeleza pale ambapo mtumiaji au watumiaji wanapochangaya maneno ya kiingereza katika Kiswahili, pia kutumia sarufi ya lugha ya kiingereza pindi atumiapo lugha ya Kiswahili.
(d)Lugha hufa.
Lugha hufa kutokana na kukosekana kwa msamiati wa lugha husika.
(e)Lugha ina ubora.
Ubora wa lugha hupatikana kwa watumiaji wa lugha yenyewe. Kwa mfano,kiwahili kinaubora kwa Wakazi wa Afrika Mashariki kwasababu ndio watumiaji wa lugha hiyo.
(f)Lugha ni sauti za kusemwa na binadamu.
Mwanadamu hutumia alama za sauti kimsingi hakuna kiumbe ambacho si binadamu kinachoweza kuzunghumza lugha.
CHIMBUKO LA LUGHA YA KISWAHILI.
Chimbuko ni asili ya kitufulani, tunaposema chumbuko la lugha ya kiswahili tunaangalia asili ya lugha ya kiswahili. Yawezekana kabisa kuwa kila jamii inahistoria yake jinsi lugha yake ilivyozuka, vivyo hivyo hata kiswahili kina asili yake kamaifuatavyo:
KISWAHILI NI KIKONGO, katika hoja hii tunaona kuwa hapo zamani Pwani ya Afrika Mashariki ilikuwa ombwe (hapakuwa na kitu) wakongo walifika wakiwa katika misafara yao na kuweka kambi kisha makazi. Baada ya wakongo hawa kuwa na makazi imegundulika kuwa lugha iliyokuwa ikizungumzwa ilihusiana na lugha ya Kiswahili. Katika hoja hii tunapata ukakasi unaosababisha tushindwe kupata uthibitisho wakisayansi unaoonesha kuwa kiswahili nikikongo.
KISWAHILI NI LUGHA YA VIZALIA, Vizalia ni watoto ambao walitokana baada ya mwingiliano wa wanawake wa Afrika mashariki na waarabu waliokuwa wakifika Pwani ya Afrika Mashariki kwa madhumuni ya kufanya biashara. Baada ya mwingiliano huo walioaona na kuzaa watoto ambao walichukuwa baadhi ya maneno (misamiati) kutoka kwa Baba zao na kwa Mama zao kisha kutumia katika mawasiliano na kuwa lugha moja iliyojulikana kama lugha ya vizalia.

KISWAHILI NI PIJINI,  wakazi wa afrika Mashariki waliingiliana na Waarabu waliofika kwa ajili ya biashara zao wakakuta lugha inayozungumzwa ni tofauti na lugha yao ndipo ilipozuka lugha ya Kiswahili kwa kuchukua maneno kutoka katika lugha zote mbili na kuunda lugha moja ambayo ni pijini ambayo waliitumia katika mawasiliani yao. Kwakua lugha hii ilikuwa ikitumiwa na wakazi hawa ilionekana kuwa ndilo chimbuko la kaswahili, lakini hoja hii inakosa mashiko kwani inatupatia uthibitisho wa nadharia pekee hatujapata uthibitisho wa kisayansi unaoonesha kuwa pijini ndilo chimbuko la kiswahili.

KISWAHILI NI KRIOLI,  hii ni pijini iliyokomaa. Baada ya pijini kuendelea kutumika na watumiaji wake na kuwa lugha Mama ya jamii husika huitwa krioli.
KISWAHILI NIKIARABU, kuna thibitisho mbalimbali ambazo zinathibitisha kuwa Kiswahili kimetokana na lugha ya kiarabu, uthibitisho huo ni:
•Kutokana na neno lenyewe KISWAHILI neno hili limetokana na neno la kiarabu “sahili”umoja na wingi wake ni “Swahili”lenye maana ya Pwani ya Afrika mashariki. Kwakua neno hili ni lakiarabu na warabu walifika Pwani ya Afrika Mashaiki kwaajili ya biashara zao ikathibitiashwa kuwa kiswahili asili yake ni kiarabu.
•Kiswahili kilitumika katika dini ya kiislam, baada ya Waarabu kufika uwanda wa Pwani ya Afrika mashariki kuendesha biashara zao pia walikuja kueneza dini ambayo ni kiislamu. Dini hiyo ilienezwa kwa lugha ya kiswahili kwa wakazi wa Pwani. Kufuatia kuenea kwa dini hiyo ikachangia kueneza lugha ya kiswahili na kuthihirika kuwa kiswahili chimbuko lake ni kiarabu.
•Baadhi ya maneno yaliyomo na yanayotumika katika lugha ya Kiswahili ni ya kiarabu. Kwamfano maneno kama siri, gati, sukari nk, maneno haya yanatumika katika lugha ya kiswahili na nimisamiati sanifu. Inakadiliwa kuwa lugha ya kiarabu inamaneno asilimia 31 katika lugha ya Kiswahili ambayo hutumika katika muktadha mbalimbali. Kutokana na uthibitisho huo inadhihilishwa Kiswahili ni kiarabu.

KISWAHILI NIKIBANTU
Neno KIBANTU limetokana na neno BANTU maana yake ni WATU. Wabantu hupatikana Afrika haswa Afrika mashariki na kati ikihusisha mataifa kama Tanzania, Rwanda, Burundi, Kongo, Kenya  n.k
Tunaposema kiswahili ni kibantu ina maana kuwa, lugha ya kiswahili ni lugha ambayo imetokana na muunganiko wa misamiati ya lugha za makabila mbalimbali yanayopatikana afika mashariki na kati, kwamfano Kisukuma, kihaya, kijita, kingoni kihehe na n.k.
Dhana hii imeonekana kuwa na mashiko na kuweza kutoa udhibitisho wakisayansi unaothihilisha asili ya kiswahili nikibantu, yaani kimetokana na muunganiko wa misamiati kutoka katika lugha mbalimbali. Ili kuthibitisha hoja hii kunauthibitishoi wa KIISIMU na ule wa KIHISTORIA
USHAHIDI WA KIISIMU.
Isimu ni sayansi ya lugha. Tunaposema sayansi ya lugha ni jinsi ambavyo lugha ilivyopangiliwa ki muundo, kimatamshi, kimaana na kimtindo.





 

Jumatatu, 16 Juni 2014

UTENDAJI KAZI WA FONIMU.


FONIMU INAVYOWEZA KUVUKA MPAKA WA FONIMU NA KUINGIA           KATIKA FONIMU NYINGINE.

Dhana ya fonimu ni dhana ambayo imejadiliwa na wataalamu mbalimbali wakitumia mitazamo tofauti tofauti. Wataalamu wafuatao wameeleza maana ya fonimu:-

Massamba, (2004) anasema fonimu ni kipande kidogo kabisa katika mfumo wa sauti za lugha ambacho kina sifa pambanuzi  kuweza kukitofautisha na vipande vingine vya aina yake. Sauti pambanuzi katika mfumo wa lugha.
Massamba na wenzake, (2004) wanasema fonimu ni kitamkwa kilicho bainifu katika lugha fulani maalumu.
Mgullu, akimnukuu Jones, (1975) anaeleza kuwa Fonimu ni kundi la sauti katika lugha fulani, lenye sauti muhimu (phonemes) pamoja na sauti zinazohusiana na ambazo hutumiwa mahali peke katika muktadha maalumu.
Tunaweza kusema kuwa wataalamu hawa wametofautiana katika kuelezea dhana nzima ya fonimu, wakati Massamba (2004), anasema fonimu ni kipande kidogo kabisa katika mfumo wa sauti za lugha, Jones (1975) akinukuliwa na Mgullu anasema kuwa fonimu ni kundi la sauti katika lugha fulani.
Hivyo  tunaweza kusema kuwa fonimu kipashio kidogo cha kifonolojia kinachoweza kubadili maana ya neno katika lugha fulani (mahususi). Kwa mfano pata – baba.
Dhana ya fonimu kuvuka mipaka na kuingia katika fonimu nyingine ni pale fonimu fulani inapoliacha umbo lake la asilia na kuingia katika umbo jingine. Dhana hii imenukuliwa na Massamba (2010) kutoka kwa mtaalamu Bloch (1941).
Bloch (1941) anashawishi kwa kiasi kikubwa kuwa fonimu kuvuka mipaka ni tukio la kawaida katika lugha ya asili kutokana na ushahidi kuwa alofoni za fonimu moja zinaweza kutofautiana kwa kiasi kikubwa kifonetiki. Wakati mwingine zinakuwa na uhusiano na alofoni za fonimu nyingine tofauti na fonimu zilimotokea. Vile vile kifonetiki, sauti fulani inaweza kutokea kuwa katika fonimu mbili au zaidi katika lugha moja.  Anaendelea kusema kuwa kuna aina mbili za fonimu kuvuka mipaka ambazo ni:-
Uvukaji mipaka usiokamili, unaamanisha hali ya fonimu ya aina moja kutokea katika fonimu mbili katika mazingira ya hali tofauti.
Kwa mfano;
Sauti [x] inaweza ikawa /a/ katika mazingira fulani na sauti [x] katika mazingira tofauti inaweza ikawa /b/, katika lugha ya Kidenimaki ( Jakoboson, Fant na Halle 1952) fonimu /t/ na /d/ zinakuwa na tabia tofauti mwishoni mwa silabi /t/ kutamkwa kama /d/ zinakuwa na mfano /hat/ kwenda /had/ wakati fonimu /d/ inakuwa / ð / . Kwa  mfano /had/ inakuwa /hað/ japokuwa katika Kidenimaki neno roof (paa) ni sawa sawa na tag wakati day (siku) ni dag. Hii inamaanisha kwamba mwanzoni mwa silabi fonimu /t/ na /d/ hazibadiliki. Kwa maana nyingine kuna /d/ inayotokana na /t/ pia kuna /d/inayotokana na /d/ yenyewe. 
Katika lugha ya Kiswahili uvukaji wa mipaka usiokamili wa fonimu hutokea katika hali zifuatazo:-
Kwa mfano:
 Udogo                          Ulimi                              Loa
Undugu                         Ndimi                      Ndoana
Ndugu
Hivyo katika Kiswahili sauti /d/ hujitokeza kama /d/ wakati mwingine huvuka mipaka na kuwa /l/. Sauti /l/ huwa /d/ endapo inatanguliwa na nazali /n/. Endapo tutajikita kifonetiki ni ngumu kutabiri /d/ kama ni alofoni ya fonimu /d/ au fonimu /l/ itakuwa rahisi.
Mfano mwingine wa Kiswahili ni pale:
Ki + ti  = ki+eusi (kiti cheusi) katika mifano ya Kiswahili tutaona mabadiliko ya kifonimu yakijitokeza katika mfano wa fonimu /k/ inapofuatiwa na irabu halafu kuwa katika mpaka wa mofimu kisha ikafuatiwa na irabu /e/ hubadilika na kuwa /ch/ yaani (ki+eusi) = cheusi.
Mfano mwingine katika Kiswahili ni:-
N + buzi  (mbuzi)  /n/ inakuwa /m/ ikifuatiwa na /b/
N+dama  (ndama)   /n/ inabakia kuwa /n/ ikifuatiwa na /d/
N+gombe (ng’ombe)  /n/ inabadilika na kuwa /n’g/
Pia tunaona kuwa nazali /n/ inapofuatiwa na kitamkwa /b/ hubadilika na kuwa /m/ inapofuatiwa na kitamkwa /d/ hubakia kuwa /n/ inapofuatiwa na kitamkwa /g/ hubadilika na kuwa [ ŋ ]. Hii inamaana kuwa katika mazingira haya sauti /m/, /n/ na [ŋ] ni alofoni za fonimu /N/
Uvukaji wa mipaka uliokamili. Huu ni uvukaji wa mipaka wa sauti moja kwenda sauti nyingine katika mazingira ya aina moja.
Kwa mfano:-
Katika lugha ya kiingereza uvukaji wa mipaka uliokamili unahusisha fonimu /t/ na /d/ inapotokea katikati ya irabu. Wamarekani hutamka sawa sauti ya ufizi [d].
Mfano:- Butter, Betting, Kitty ukiyatofautisha na Budden, Bedding, Kiddy katika mifano yote hiyo fonimu /t/ na /d/ hutamkwa sawa.
Kwa mfano:- /betting/ - [ beDiŋ] na /bedding/ = [beDiŋ]. Unapotamka haya maneno hautamki moja kwa moja /d/ wala /t/ bali inakuwa sauti katikati ya /t/ na /d/. Kwa msingi huo fonimu /t/  na /d/ hupoteza uhalisia wake katika matamshi. Baada ya ule uhalisia kupotea sauti inayokuja huziwakilisha haizitofautishi sauti  /t/ na /d/. aina hii ya uvukaji ndio huitwa uvukaji wa mipaka wa fonimu uliokamili.
Kutokana na mifano tajwa hapo juu ni dhahiri kuwa fonimu inaweza kutokea katika umbo lake asilia na kwenda katika umbo jingine la fonimu au alofoni ambazo hutokana na fonimu moja. Hii husababishwa na mazingira ya utokeaji wake au sifa za kifonolojia.
MAREJEO:

Massamba, D.P.B. (2004). Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha. Taaasisi ya
                  Uchunguzi wa Kiswahili. Dar es salaam.
Massamba, D.P.B na wenzake. (2004). Fonolojia ya Kiswahili Sanifu. Taasisi ya
   Uchunguzi wa Kiswahili. Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
Massamba, D.P.B. (2010). Phonological Theory: History and development.
   TUKI. Dar es saalam.