Subcribe to our RSS feeds Join Us on Facebook Follow us on Twitter Add to Circles

Jumatatu, 21 Julai 2014

MAENDELEO YA LUGHA YA KISWAHILI.


MAENDELEO YA KISWAHILI.
Kiswahili ni lugha inayozungumzwa katika eneo kubwa la Afrika ya Mashariki. Lugha hii ina utajiri mkubwa wa misamiati, misemo, mithali, mashairi, mafumbo, vitendawili na nyimbo. Kiswahili hutumika mashuleni, katika mawasiliana na kuna vitabu vingi vilivyotungwa kwa kutumia lugha hiyo, vikiwa pamoja na vile vya hadithi, hekaya au riwaya.
Lugha ilianza takriban miaka 800-1000 iliyopita katika pwani ya Afrika Mashariki.Wakazi wa Pwani hii waliokuwa wasemaji wa lugha za Kibantu tofauti tofauti mfano; kisukuma, kihaya, kijita, kikurya, kimakonde, kingoni, kihehe, kizigua, kibena n.k.katika shughuli mbalimbali kama biashara ambazo zilikuwa zikiwakutanisha watu hawa wakiwa wanaozungumza lugha tofauti tofauti, iliwabidi waweze kuchukua msamiati mbalimbali kutoka katika lugha zao ili waweze kuwasiliana katika shughuli zao. Walipopokea maneno mengi hasa ya Kibantu katika mawasiliano yao, ikachangia kuwa msingi wa Kiswahili ni sarufi na msamiati wa Kibantu.
Kwakua tumeona kuwa Kiswahili ni lugha sasa basi, lugha nini?
Lugha ni sauti za nasibu zilizo katika mpangilio maalumu na zilizo kubaliwa na jamii ya watu zitumike kama chombo cha mawasiliano.
Au
Ni mfumo wa sauti za nasibu za kusemwa zinazotumiwa na watu wa jamii fulani wenye utamaduni unaofanana kwa madhumuni ya mawasiliano katika jamii hiyo.
Au
Katika kamusi ya kiswahili sanifu TUKI 1981 oxford press uk. 86, inafafanua kuwa lugha ni mfumo wa sauti nasibu ambazo hutumiwa na jamii kwa madhumini ya mawasiliano kati yao.
Sifa / tabia za lugha.
(a)Lugha huzaliwa.
Lugha huzaliwa kutokana na mwingiliana kati ya lugha mbili au zaidi nakutengeneza lugha moja. Kwa mfano lugha ya Kiswahili imetokana na mwingiliano wa lugha mbalimbali za kibantu.
(b)Lugha hukua.
Lugha hukuwa kutokana na kuongezeka kwa msamiati mbalimbali ambayo hutumiwa katika lugha husika katika shughuli mbalimbali.
(c)Lugha huathiliwa.
Lugha huathiliwa kutokana na mwingiliano wa lugha mbili tofauti  na kusababisha ukiukwaji wa kanuni na matumizi sahihi ya lugha mojawapo. Kwamfano Kiswahili kinaweza kuathiliwa na kiingeleza pale ambapo mtumiaji au watumiaji wanapochangaya maneno ya kiingereza katika Kiswahili, pia kutumia sarufi ya lugha ya kiingereza pindi atumiapo lugha ya Kiswahili.
(d)Lugha hufa.
Lugha hufa kutokana na kukosekana kwa msamiati wa lugha husika.
(e)Lugha ina ubora.
Ubora wa lugha hupatikana kwa watumiaji wa lugha yenyewe. Kwa mfano,kiwahili kinaubora kwa Wakazi wa Afrika Mashariki kwasababu ndio watumiaji wa lugha hiyo.
(f)Lugha ni sauti za kusemwa na binadamu.
Mwanadamu hutumia alama za sauti kimsingi hakuna kiumbe ambacho si binadamu kinachoweza kuzunghumza lugha.
CHIMBUKO LA LUGHA YA KISWAHILI.
Chimbuko ni asili ya kitufulani, tunaposema chumbuko la lugha ya kiswahili tunaangalia asili ya lugha ya kiswahili. Yawezekana kabisa kuwa kila jamii inahistoria yake jinsi lugha yake ilivyozuka, vivyo hivyo hata kiswahili kina asili yake kamaifuatavyo:
KISWAHILI NI KIKONGO, katika hoja hii tunaona kuwa hapo zamani Pwani ya Afrika Mashariki ilikuwa ombwe (hapakuwa na kitu) wakongo walifika wakiwa katika misafara yao na kuweka kambi kisha makazi. Baada ya wakongo hawa kuwa na makazi imegundulika kuwa lugha iliyokuwa ikizungumzwa ilihusiana na lugha ya Kiswahili. Katika hoja hii tunapata ukakasi unaosababisha tushindwe kupata uthibitisho wakisayansi unaoonesha kuwa kiswahili nikikongo.
KISWAHILI NI LUGHA YA VIZALIA, Vizalia ni watoto ambao walitokana baada ya mwingiliano wa wanawake wa Afrika mashariki na waarabu waliokuwa wakifika Pwani ya Afrika Mashariki kwa madhumuni ya kufanya biashara. Baada ya mwingiliano huo walioaona na kuzaa watoto ambao walichukuwa baadhi ya maneno (misamiati) kutoka kwa Baba zao na kwa Mama zao kisha kutumia katika mawasiliano na kuwa lugha moja iliyojulikana kama lugha ya vizalia.

KISWAHILI NI PIJINI,  wakazi wa afrika Mashariki waliingiliana na Waarabu waliofika kwa ajili ya biashara zao wakakuta lugha inayozungumzwa ni tofauti na lugha yao ndipo ilipozuka lugha ya Kiswahili kwa kuchukua maneno kutoka katika lugha zote mbili na kuunda lugha moja ambayo ni pijini ambayo waliitumia katika mawasiliani yao. Kwakua lugha hii ilikuwa ikitumiwa na wakazi hawa ilionekana kuwa ndilo chimbuko la kaswahili, lakini hoja hii inakosa mashiko kwani inatupatia uthibitisho wa nadharia pekee hatujapata uthibitisho wa kisayansi unaoonesha kuwa pijini ndilo chimbuko la kiswahili.

KISWAHILI NI KRIOLI,  hii ni pijini iliyokomaa. Baada ya pijini kuendelea kutumika na watumiaji wake na kuwa lugha Mama ya jamii husika huitwa krioli.
KISWAHILI NIKIARABU, kuna thibitisho mbalimbali ambazo zinathibitisha kuwa Kiswahili kimetokana na lugha ya kiarabu, uthibitisho huo ni:
•Kutokana na neno lenyewe KISWAHILI neno hili limetokana na neno la kiarabu “sahili”umoja na wingi wake ni “Swahili”lenye maana ya Pwani ya Afrika mashariki. Kwakua neno hili ni lakiarabu na warabu walifika Pwani ya Afrika Mashaiki kwaajili ya biashara zao ikathibitiashwa kuwa kiswahili asili yake ni kiarabu.
•Kiswahili kilitumika katika dini ya kiislam, baada ya Waarabu kufika uwanda wa Pwani ya Afrika mashariki kuendesha biashara zao pia walikuja kueneza dini ambayo ni kiislamu. Dini hiyo ilienezwa kwa lugha ya kiswahili kwa wakazi wa Pwani. Kufuatia kuenea kwa dini hiyo ikachangia kueneza lugha ya kiswahili na kuthihirika kuwa kiswahili chimbuko lake ni kiarabu.
•Baadhi ya maneno yaliyomo na yanayotumika katika lugha ya Kiswahili ni ya kiarabu. Kwamfano maneno kama siri, gati, sukari nk, maneno haya yanatumika katika lugha ya kiswahili na nimisamiati sanifu. Inakadiliwa kuwa lugha ya kiarabu inamaneno asilimia 31 katika lugha ya Kiswahili ambayo hutumika katika muktadha mbalimbali. Kutokana na uthibitisho huo inadhihilishwa Kiswahili ni kiarabu.

KISWAHILI NIKIBANTU
Neno KIBANTU limetokana na neno BANTU maana yake ni WATU. Wabantu hupatikana Afrika haswa Afrika mashariki na kati ikihusisha mataifa kama Tanzania, Rwanda, Burundi, Kongo, Kenya  n.k
Tunaposema kiswahili ni kibantu ina maana kuwa, lugha ya kiswahili ni lugha ambayo imetokana na muunganiko wa misamiati ya lugha za makabila mbalimbali yanayopatikana afika mashariki na kati, kwamfano Kisukuma, kihaya, kijita, kingoni kihehe na n.k.
Dhana hii imeonekana kuwa na mashiko na kuweza kutoa udhibitisho wakisayansi unaothihilisha asili ya kiswahili nikibantu, yaani kimetokana na muunganiko wa misamiati kutoka katika lugha mbalimbali. Ili kuthibitisha hoja hii kunauthibitishoi wa KIISIMU na ule wa KIHISTORIA
USHAHIDI WA KIISIMU.
Isimu ni sayansi ya lugha. Tunaposema sayansi ya lugha ni jinsi ambavyo lugha ilivyopangiliwa ki muundo, kimatamshi, kimaana na kimtindo.





 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni