Subcribe to our RSS feeds Join Us on Facebook Follow us on Twitter Add to Circles

Jumanne, 9 Septemba 2014

VYANZO VYA KUKUSANYA DATA YA KUUNDA KAMUSI.



   Katika mjadala huu tumeugawa katika sehemu  kuu tatu, sehemu ya kwanza  itaelezwa   maana  ya vipengele muhimu katika swali  kutokana na wataalamu  kama vile kamusi, na data, sehemu ya pili ni   kiini cha swali  ambalo itaelezwa vyanzo mbalimbali vya ukusanyaji data katika kuundia kamusi, na sehemu yatatu na mwisho itaelezwa hitimisho na marejeo ya swali.
Zgusta (1971) akinukuliwa na Mdee (2010)  anaeleza kuwa; Kamusi ni kitabu cha marejeo chenye msamiati uliokusanywa kutoka kwa wazungumzaji wa jamii fulani na kupangwa katika utaratibu maalumu, kisha kufafanuliwa kwa namna ambayo  wasomaji wanaweza kuelewa.
Pia Tuki (2004)  wanasema kuwa  Kamusi ni kitabu  cha maneno yaliyopangwa kwa utaratibu wa kialfabeti na kutolewa maana ya maelezo mengine. Fasili hizi kwa kiasi fulani inamapungufu kwani kwa  kuwa kamusi ni kitabu lakini sio kwamba kamusi zote zipo katika muundo wa maandishi ya kitabu bali kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, kamusi  zinaweza kuwa  katika mfumo wa elekroniki kama vile kwenye simu, santuri na kompyuta.
Hivyo tunaweza kueleza kuwa; kamusi ni orodha ya maneno yaliyopangiliwa kialfabeti na kuhifadhiwa katika kitabu, santuri, simu au eletroniki na kufafanuliwa kwa maneno marahisi  namna ambavyo wasomaji waweze kuelewa kwa urahisi.
Kuhusu maana ya data  TUK(I2004)wanaeleza kuwa data ni  taarifa  au takwimu  inayotumiwa kuelezea au kuthibitisha hoja fulani. Hivyo kwa ujumla tunaweza kusema kuwan  data ni  mkusanyiko wa  maneno (msamiati) vielelezo, picha,  na takwimu zinazokusanywa na wanaleksografia  kwa lengo la kuundia kamusi.
Hivyo tanaweza kusema kuwa ukusanyaji data ni hatua muhimu katika uundaji wa kamusi na hivyo ndivyo hatua ya muhimu  ambayo inahitaji kuzingatia   sera za kamusi  na mahitaji ya  watumiaji.Kwa hiyo tunasema kuwa kamusi bora kwa kiasi kikubwa hutegemea  ubora wa wakusanyaji data na ukusnyaji wenyewe.  Vyanzo hivyo vya   ukusanyaji data zimegawanyika katika makundi makuu  mawili  ambayo ni makundi simulizi na makundi andishi  na  makundi hayo yamegwanywa katika makundi  madogomadogo kama ifuatvyo.
Kutokana  na mawazo  ya Kipfer (1984) akinukuliwa na Habwe (1995) katika  makala yake  kitabu cha utafi na utungaji kamusi anasema kuwa “tunaweza kupata vyanzo mbalimbali  ukusa nyaji  wa data katika makundi makuu mawili ambazo ni  makundi  mazimulizi na mandishi na hizo makundi zimegwanywa katika makundi madogomadogo”. Tukijikita  katika makundi haya tunawefafanua vyanzo hivyo za yaliyoko katika kundi la kwanza ambayo ni vyanzo simulizi. Katika kundi hili tunaweza  kupata  vyanzo  mbalimb  vya data nazo.
Kwenda uwandani: Kutokana na wazungumzaji wa lugha husika au walengwa ..Hivyo mwanalekiksografia  anapaswa kwenda katika  jamii ya wazungumzaji wa lugha husika  ili kupata data mbalimbali ambazo wanjamii wanazitumia. Data hizo ndizo zitakazomsaidia  katika utungaji  wake wa kamusi.
Majadiliano:Kutokana na majadiliano mbalimbali katika makundi mbalimbali  ya jamii  kutokana na mada mbalimbali, makundi haya yanaweza kuwa ya  wanasayansi, wanasiasa.  wanafasihi na wanaisimu  hivyo wanalekiksografia  huweza kuchambua  msamiati  mbalimbali na kuziorodhesha  katika kamusi anayoilenga.
Mahubiri ya kidini: Kuwepo kwa mikutano mbalimbali ya kidini kama vile  mikutano ya kiinjili katika dini ya kikritu na mawaida katika dini ya kiislamu kutokana matumizi mengi ya maneno  katika shughuli hizo kunakuwepo maneno ambayo mwanalekiksografia kukusanya  data zake kutokana na  mahubiri haya huku akizichambua  na kuzitumia   katika kuundia kamusi.
Masimulizi ya visa na utambaji wa hadithiti: Kutokana na visa mbalimbali  vya matukio  zinazosimuliwa  na watu mbalimbali kama vile kisa cha kibo na mawezi, na kisa ch Sungura kuwa na mkia mfupi. na visa vingine. Mwanalekiksografia  huchambua  maneno mbalimbali na kuyatumia katika kuundia   kamusi anayoilenga .
Maongezi ya kawaida:Kutokana na mazungunzo yanayofanyika  katika shughuli za  kila siku katika jamii  kunakuwepo misimiati  mbalimbali inayotumika  na ambayo wanalekiksografia  hukusanya  data hizo na  kuzichambua na kuingiza katika kamusi.
Baada ya kuangalia vyanzo mbalimbali  vya  ukusanyaji  data  katika kundi la  masimulizi  basi ni vyema  kutalii  vyanzo  katika kundi la maandishi.Upatikanaji data  kimaandishi ni data zinazopatikana katika maandishi  mbalimbali  za waandishi wengine na kuhifadhiwa maktabani.  Mwanalekiksografia   huweza kwenda  maktabani  kusoma maandiko mbalimbali ambapo huweza kumsaidia kukusanya data zake na data zinaweza katika;
Katika kazi za  tafsiri: Kutokana na kazi za waandishi maarufu walioandika  katika lugha mbalimbali  huweza kutafsiriwa katika lugha  nyingine  kama vile tafsiri za kazi za kiingereza kwenda katika kazi za Kiswahili mfano kazi za “Shujaa Okonkwo,”  “Mtaa Mweusi,” na “Nitaolewa  Nikipenda.” tafsiri za kazi hizi humsaidia  mwanaleksografia  kufahamu maendeleo ya tamaduni  mbalimbali  za jamii  na baadhi ya msamiati  itumiwayo katika jamii hizo ambayo  humsaidia mwanalikiksogrfia kupata data  ambazo humsaidia katika kuundia kamusi yake.
Katika kumbukumbu mbalimbali,kama vile.makongamano, mikutano, na shughuli za bunge: Kutokana na  kumbukumbu hizo  pamoja na warsha,  mwanaleksografia  hukusanya data zilizoandikwa  kama kumbukumbu zao  na kuziingiza katika kamusi lengwa alilokusudia.
Makala mbalimbali za kidini: Kuwepo kwa makala mbalimbali za  kidini zilizoandikwa kwa lengo au kutoa msimamo wa dini zao au kueneza dini hiyo. Mwanalekiksogrfia anapswa  kuyaangalia makala hayo pamoja na vitabu vya kidini kama vile Bibilia Takatifu na Kuruani Tukufu  na magazeti ya kidini kama vile “Tumaini letu” Upendo” Kiongozi” na An-nuar. Hivyo  kupitia makala hizi mwanaleksografia  hupata maneno mbalimbali  ambayo humsaidia yanayotumika katika kuundia  kamusi lengwa.
Kutumia kongoo:Hii ni data za lugha ambazo huhifadhiwa katika kompyuta bila kujali ni maneno ya lugha gani na huhifadhiwa kadri inavyohitaji mtaalamu.  Katika  kongoo kuna nyanja    mbalimbali  kama vile nyanja  mimea,Afya sheria, wanyama,  uchumi, fasihi na isimu.Hivyo mwanaleksografia huchambua baadhi ya msamiati anayohitaji ya nyanja na kuziingiza katika kamusi anayoilenga.
Hotuba.Pia mwanalekiksografia huweza kupata data zake kwa kusoma  hotuba  za viongozi mbalimbali maarufu kama vile  Hayati mwalimu Nyerere,  Mkapa, Lowasa, Mwinyi Neson Mandela wa Afrika Kusini  na Jomo Kenyatta wa Kenyia. Hotuba hizo huandikwa na kuhifadhiwa katika maktaba ambapo mwanaleksografia huchumbua misamiati mbalimbali ambazo humsaidia  kuundia kamusi.
Kamusi za awli. Kamusi za  awali pia ni muhimu kwa mwanalekiksografia  katika kupatia data zake kwani humsaidia kuonyesha  maneno ambayo yapo katika kamusi za awali  na pia maana ya matumizi yake kulingana  na kamusi hizo.
Kutoka katika kazi za kifasihi: Kutokana  na kusoma kazi mbalimbali za  fasihi kama vile riwaya,  Tamthiliya na ushairi hasa za watu mashuhuri kama zilizoaandikwa  na  Shaaba Robert , Mathias  Mnampala, Amri Abeid, Mulokozi,  na Kezilahabi  mwanalekiksografia  anapswa  kuzichambu kazi hizo  kwa undani na kuzinukuu baadhi ya misamiati zilijitokeza ili apate data  za kuundia kamusi yake.
Magazeti na majarida:  hii ni vyanzo ambavyo   mkusanyaji data anaweza kupata data zake kwa kutumia  njia hii kwa sababu  magazeti hushughulikia nyanja  mbalimbali katika  jamii na ni rahisi kupata maneno yanayozunguzwa na makundi mbalimbali za jamii na waandishi wake  hujitahidi kutumia  lugha sanifu iwezekanvyo. Mifano  ya magazeti haya ni kama vile  Rai, Mwananchi Nipashe,Mtanzania ,Tanzania daima Habari leo Mwanaspoti Bingwa na The Guardian na Majira. Pia kuna majarida mbalimbali kama vile  Mulika Kioo cha Lugha, na Jarida la femina. Kutokana na misamiati inayopatikana katika majarida haya na magazeti haya mwanalekiksografia huchambua  misamiati anayohitaji katika kuundia kamusi.
Kwa  kuhitimisha  tunaweza kusema kuwa  ili mwanalekiksografia aweze kukusanya  data zilizobora zaidi ni vyema kuwa mmilisi wa lugha husika

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni