Subcribe to our RSS feeds Join Us on Facebook Follow us on Twitter Add to Circles

Jumanne, 9 Septemba 2014

MATUMIZI YA MISEMO MAGAZETINI:

 
         Misemo magazetini hutumika kwa namna tofauti. Matumizi haya ya misemo hutumiwa moja kwa moja kwenye vichwa vya habari au katika maelezo. Baadhi ya vichwa vya habari hutofautiana na mada ambazo huwa zinakuwemo  ndani ya habari.Hii ina maana kuwa misemo inayotumika huwa na maana iliyotofauti kabisa na maana inayoonekana magazetini.Misemo mingine tumeionyesha kwenye kiambatisho.  Ngoja uangalie mifano ifuatayo:
a)      Nesi  Kitete ajikaanga (Mtanzania, mei, 23,2011.)
b)      Sarakakasi za Sitta Mwakyembe CCJ (Mtanzania, Mei 9, 2011).
c)      Vigogo CCM  wakaangwa (Manzania, Mei,23,2011)  .
d)     Spika, Zitto jino kwa jino, Mkulo  apigilia msumali wa mwisho(Uhulu, Juni, 14, 2011).
e)      Ujamaa wampofusha Mukama(Rai,mei 19-25,2011).
f)       Lady Jaydee kutembea uchi live(Sani,Mei, 14,2011).
g)      Akina Ukwa waja tena (Kiu, ya jibu Juni, 23,2011).
h)      Ngeleja kitanzini(Uhuru, Juni; 6, 2011).
i)        Mashabiki Yanga wafurika kushuhudia majembe yao (Bingwa, Juni, 14, 2011).
j)        Ulimwengu ndiye muuaji (Uhuru Juni 6, 2011).
k)      Morocco yafanya mauaji (Uhuru, Juni 6, 2011).
l)        Mbowe balaa Dar (Majira, juni,6, 2011) .
m)    Mganda awasili kumvaa Mwakyembe(Bingwa Mei, 20 , 2011).
n)      Lowassa amkatia Kiwete rufaa (Mwananchi, juni, 16, 2011).
o)      UPDP kuunguruma Dar kesho (Mtanzania,Mei,25,2011).
p)      CDA yakabwa koo na kamati ya bunge(Bingwa,Mei, 20,2011).
Katika mifano hii, ni dhahili kuwa maana inayoonekana katika msemo hii sivyo ilivyo katika maelezo au habari nzima. Mfano, katika (a) siyo kwamba ‘nesi alijikaanga kiaangoni’ bali alijiweka katika mazingira magumu ya kuendelea na kazi baada yahuduma  kumzalisha mama
                                                                         8.
 na mwanae kufichwa. Pia katika (f) haimaanishi Ukwa waigizaji wa Nigeria bali kuna vijana waliojifananishwa na waigizaji hao. Katika (h) ‘majembe’ haimaanishi majembe vifaa bali anamaanisha wachezaji wapya waliosajiliwa na timu ya Yanga.Mifano mingine mingi tutaitolea maana katika sehemu inayofuatwa.
                                                                     
4.1.KWA NINI MAGAZETI HUTUMIA MISEMO:
Kihole (2004) anasema kuwa ; ‘ni kwa hali hii ya kushangaza kile kinachotajwa katika mada hiyo ama hufanya baadhi ya wasomaji kukosa hata hamu ya kufikiria kununua magazeti haya au kuwachochea watu kufanya juhudi za kuyapata magazeti hayo’. Hivyo baadhi ya magazeti hutumia misemo ili kuvuta umakini wa wasomaji. Ngoja sasa tuangalie baadhi ya misemo ambayo huweza kuvuta wasomaji.
a)      Nilitema big G kwa karanga za kuonjeshwa
b)      Ray C akimbia nchi.
c)      Ngono Big Brother sasa(Kiu ya Jibu,juni,22,2011).
d)     Nilipopiga ramri kumtafuta Mungu(Kiu ya jibu,Juni,22,2011).
e)      Lady  Jay dee kutembea uchi(Ku ya jibu,Juni,22,2011).
f)       Kituo cha kuoshea nyeti za kike Dar(Sani,Mei,11-14).
g)      Mganda awasili kumvaa Mwakyembe (Bingwa Mei,20,2011).
h)      Spika Makinda mbumbumbu anasimamia asichokijua (Rai,Juni,20,2011).
i)        Freemason na ugaidi katika kanzu ya uislamu (Mtanzania,Juni,17,2011).
j)        Wanaume kumeza vidonge vya kuzuia mimba(Uhuru, Juni, 7-14,2011).
k)      Sauti ya radi awa makamu wa Rais(Ijumaa mei, 20, 2011).
l)        Waziri, changu wateta kwa nusu saa Dom(Ijuma,Julai,15,2011).
m)    90% mastaa wauza ngono bei chee(Ijumaa, Julai,15,2011).
n)      Badra aanika chachandu zake adatisha midume(Ijumaa,Julai,15,2011).
o)      Mchumba aliyevua nguo (Dimba, Juli,17,2011).
p)      Linah sina mtu sasa niko single(Sani,juni,12,2011).
q)      Mrembo anaswa akichimba dawa hadharani(Iumaa,Julai,15,2011).
                                                            9.
Kwa kuitazama  misemo hii katika vichwa vya magazeti  tunaweza kubaini kuwa inavutia wasomaji hata kununua magazeti ili kupata taarifa iliyomo ndani ya gazeti hilo. Kutokana maoni ya Kihole (2004) anaposema kuwa ni kutokana na matumizi ya misemo hiyo wasomaji huweza kukatishwa tamaa au kufanya juhudi za kuyapata magazeti hayo, tumeshuhudia magazeti mengi yakitumia misemo hiyo ili kufanikisha
nia ya wasomaji. Mfano gazeti la sani, Ijumaa na Kiu.

1.1.KUSISITIZA JAMBO:
Katika utafiti wetu tumegundua kuwa magazeti hutumia misemo, na misemo hiyo huwa inajirudiarudia katika magazeti mengi. Misemo hii hulenga kuweka msisitizo juu ya jambo lilopita, lililopo au lijalo. Mfano misemo tuliyoitumia katika utafiti wetu baadhi inasisitiza juu ya mambo yaliyokuwepo katika kipindi hicho cha utafiti ulipofanyika. Ngoja sasa tuione baadhi ya misemo hiyo.
a)      Tibaijuka ang’aka(Mtanzania,Mei,20,2011).
-Hi ilkuwa kipindi cha mchakato wa watu kurudisha ardhi walizochukua na wananchi bila kukubaliwa na serikali.
b)      Wabunge CCM wakaangwa (Mtanzania, Mei,23,2011).
Misemo hii imesikika sana kipindi cha wabunge wanahusihwa na migogoro ya chama   ilyojulikana kama (kujivua gamba).
c)      DC walimu wa shule za kata wasiitwe Voda fasta.
d)     Kujivua gamba hakutoshi.
Katika mifano hii misemo mingine huibuka kulingana na mada iliyopo na baadae misemo hiyo haisikiki tena. Hivyo ni kutokana na msisitizo huo wasomaji huweza kuwa na ufuatilizi juu ya tukio fulani kulingana na jinsi linavyotokea mara kwa mara.


                                                                 
1.2.MAANA YA MISEMO MAGAZETINI:
 Katika utafiti huu tumegundua kuwa magazeti hutumia misemo mbalimbali yenye maana tofauti. Kulingana na nadhalia iliyotumika kuchambua utafiti huu tumeona kuwa kazi ya fasihi huwa haina maana moja hivyo maana inaweza kutokana na kazi iliyopo au kulingana mukutadha uliopo. Hivyo maana ya misemo mingine hutokana na mukutadha wa kazi iliyopo. Hivyo katika maana ya misemo  hii tuliyotoa tumezingatia jinsi misemo hii ilivyotokea magazetini.  Mfano wa ,misemo hii ni kama ifuatavyo;
a)      Kalenga aipiga tafu Vodacom miss Bagamoyo(Mtanzania,Mei, 20,2011).
-‘Kupiga tafu’       kusidia .
b)      Aahidi kuanika hadharani vielelezo walivyoshiriki(Mtanzania,Mei, 20, 2011).
                -‘Kuanika’ maana yake ni kuweka wazi.
c)      Azzani asiwe mbuzi wa kafara CCM (Rai, Mei, 19-25,2011).
-‘Kuwa mbuzi wa kafara maana yake’ asiangaliwe kama mkosaji kutokana na makosa
                    yanayofanywa na wakuu wake wa kazi.   
d)     TAKUKURU inabweka lakini haing’ati(Rai, mei, 19-25, 2011)
-‘Hii ina maana kuwa takukuru inatishia lakini haitendi.

e)      Niyonzima aotambawa jangwani(Bingwa, Mei, 20,2011).
-Kuota mbawa maana yake ni kushindwa kufikia mwafaka.

f)       Nyota wa Man U walipoanika vifaa vyao kwenye ‘pati’Bingwa, (Mei,19-25,2011).
           -Kuanika vifaa maana yake walikuusanyika na nakujumuisha wake zao. Vifaa ni
wanawake.
g)      Mshindi wa Tanzania ajishebedua ‘BBA’.(Bingwa, Mei,19-25,2011).
-Kujishebedua maana yake kujifanya hutaki kitu fulani huku unakitaka.

h)      Blatter amekalia kutikavu FIFA? (Majira,23,2011).
-Kukalia kuti kavu maana yake amejiweka katika nafasi ngumu ya kazi yake.
i)        Bimman abwaga manyanga (Majira,Mei,23,2011).
-Kubwaga manyanga maana yake kuacha kazi.
                                                           11.

j)        Harambee ya Yanga yadoda (Uhuru, Mei, 3,2011).
-Kudoda maana yake kushindwa.

k)      Wadai hukumu inanuka rushwa(Majira,Mei,23,2011).
-Kunuka rushwa ina maana kuwa kuna hali ya kutoa rushwa katika hukumu hiyo.
l)        Mwakalebela aibwaga TAKUKURU.
-‘Kuibwaga’ ina maana ya alishinda kesi iliyomkabili kuhusu TAKUKURU.
Hivyo kama tulivyoeleza kabla hatujaanza kutoa mifano hii kuwa kazi ya fasihi huwa haina maana moja, nidhahili kuwa maana nyingine katika mifano hii imetolewa kulingana na muktadha wa kazi yenyewe au taarifa ilivyo kwenye magazeti.
Waandishi wa magazeti nchini Tanzania wanatumia misemo katika magazeti, kwanza ni kwa sababu ya kutaka siko la magazeti yao,hii ni kwa mujibu wa mwafunzi mmoja mwenye namba ya usajiri (2009-04-03894). Anasema kuwa waandishi hutumia misemo katika vichwa vya habari kwa kudokezea kile kitakachokuwa ndani ya habari yenyewe.Mfano ‘endelea na habari hii ndani upate uhondo’ ‘usijinyime uhondo huu’ Hivyo misemo hii imekuwa chanzo cha waandishi kuuza kazi zao. Mfano gazeti la SaniIjumaa, Kiu.
Pia kwa muuza gazeti katika kituo cha mabasi kilichoko ubungo jijini Dar es salaam namba ya simu 0713750941)  anasema kuwa amekuwa akiuza magazeti kwa muda mrefu na kusema kuwa magazeti yanayonunuliwa saana ni yale yenye maneno yanayovutia.
hivyo tukizingatia maoni na maelezo ya watu hawa tunaweza kukubaliana nao kwani tunaona maagazeti mengi yakitumia misemo mingi.   


                                                    HITIMISHO:
        Kwa kuhitimisha tunaweza kusema kuwa misemo ni kipengele ambacho ni kipana sana kwani katika utafiti wetu tumegusia tu misemo bila kangalia dhima zake, fani na maudhui yake. Hivyo ni bora zaidi kufanyike uchunguzi mwingine ili kuweza kubaini vipengele hivyo vya fani na maudhui. Vile vile misemo mingi huanza kama misimu na ikitumiwa sana huweza kuwa na mashiko na kutumika maeneo tofauti.
                                                                       

                                                          
KIAMBATISHO.
1.      Tibaijuka ang’aka.
2.      Nesi kitete ajikaanga.
3.      Kalenga aipiga tafu Vodacom miss Bagamoyo.
4.      Sarakasi za sitta Mwakyembe CCJ.
5.      Akili kuanika hadharani vielelezo walivyoshiriki.
6.      Vigogo CCM wakaangwa.
7.      Wafumania nyavu 10 kukumbukwa.
8.      UPDP kuunguruma Dar kesho.
9.      Ujamaa wampofusha Mkama.
10.  Azzan asiwe mbuzi wa kafara.
11.  Wizara ya elimu imulikwe.
12.  Takukuru inabweka lakini haing’at.i
13.  Gamba laCCM halivuliki, ibueni mafisadi.
14.  Mganda awasili kumvaa Mwakyembe.
15.  Nyota wa Man U walipoanika vifaa vyao.
16.  Mshiriki wa Tanzania BBA ajishebedua.
17.  Mbowe balaa Dar.
18.  Bimman abwaga manyanga.
19.  Wadai hukumu inanuka rushwa.
20.  CDA yakabwa koo na kamati ya bunge.
21.  Mwakalebela aibwaga TAKUKURU.
22.  Harambee ya Yanga yadoda.
23.  DC walimu wa shule za kata wasiitwe Vodafasta
24.  Ris wa zamani wa FIFA amkingia Blatter kifua
25.  Wamer amkaanga Bin Hamman
26.  Sauti ya radi awa makamu wa Rais
27.  Kujivua gamba hakutoshi
28.  Balozi wa Tanzania UK katikati ya mkutano.
29.  CCM itambue ugumu na urefu wa gamba.
30.  Mkata  tawi Gbagbo hakumsikiliza Odinga kawasikliza mijusi
31.  Basi lakanyaga kombe la Real Madrid
32.  Ulimwengu ndiye muuaji
33.  Kauli hizi za viongozi CHADEMA mauti yetu
34.  Mateja wageuza kituo cha mabasi ‘Gesti bubu’
35.  Kiburi chamuondoa duniani
36.  Spika Zitto jino kwa jino
37.  Kujivua gamba si ndoto ya mchana
                                                                      15.
38.  Tulivyozunguka kuitafuta vaselini Kampara
39.  Mashabiki wafurika kushuhudia majembe yao.
40.  Basena akunwa na beki wa Motema pembe.
41.  Wyne Rooney apandikiza nywele.
42.  Ngeleja kitanzini.
43.  Wanaume kuanza kumeza vidonge vya kuzuia mimba.
44.  Ikulu – viongozi wa dini si Malaika.
45.  Lady Jaydee kutembea uchi live.
46.  Kituo cha kuoshea nyeti za kike Dar.
47.  Wabunge wamchefua Spika Makinda awafananisha na watu wa kariakoo.
48.  CCM mnahangaika na Lowassa CHADEMA haoooo..
49.  Pinda hajui idadi ya mawaziri wanaoishi hotelini.
50.  Freemasoni na ugaidi ndani ya kanzu yabuislamu.
51.  Julio amtolea nje nyota wa Chelsea.
52.  Jenerali mchana nyavu ageuka balozi Japan.
53.  Mjadara wa posho waitikisa nchi.
54.  Dr. Slaa pakacha na chujio hayahifadhi maji.
55.  Abebwaye hukitazama kisogo cha ambebaye.
56.  Nani mwanamke shujaa ajitokeze tumuone?
57.  CCM ikiwatimua mapacha watatu tutawapokea AFP.
58.  Spika Makinda mbumbumbu asimamia asichokijua.
59.  Lowassa amkatia Kikwete rufaa.
60.  Munge arusha mpira Masijala.
61.   Mlema sijiudhulu ng’o.
62.  Bajeti iliyotolewa na Zitto haina masilahi kwa taifa.
63.  Ngono Big Brother sasa.
64.  Aliyezama baharini kusaka mwili wa osama aibukia patupu.
65.  Nilivyopiga ramli kumtafuta Mungu.
66.  Aki na Ukwa waja tena.
67.  Nilitema big ‘G’ kwa karanga za kuonjeshwa.
68.  Ray c akimbia nchi.
69.  Waziri, changu wateta kwa nusu saa Dom.
70.  Mainda, Steve Nyerere Mhhhh!.
71.  90% Mastaa wauza ngono bei cheee.
72.  Mrembo anaswa.
73.  Badra aanika chachandu zake adatisha midume.
74.  Asha Bakari vimwana Twanga pepeta ni zaidi ya miss.
75.  Mchumba aliyevua nguo shereheni.
76.  Lina sina mtu kwa sasa niko single.
                                                                              16.
77.  Belina alizwa viatu, atangaza dau.
78.  Kalala Juniour bifu za kijinga siyo ishu.
79.  Kuolewa si kila kitu dada’ngu vuta subila.
80.  Aliyemwaga radhi hadharani aachwa kwa taraka tatu.
81.  Jenifer Aniston amwenzi mbwa wake kwa totoo!
82.  Wanaomjua waanika siri zke.
83.  Mrembo anaswa akichimba dawa hadharani.
84.  Lina sina wakumpa penzi.
85.  Mbunge CHADEMA amlipua Sitta.
86.  Lowassa alizwa na kujiudhuru kwa Rostam.
87.  Mikopo ya elimu ya juu yaitafuna wizara ya elimu.
88.  Lowassa amlilia Rostam.
89.  Rostam adaiwa kumkejeli Kikwete.
90.  Ngeleja uso kwa uso na wabunge leo.
91.  Uamuzi wa Rostam kuachia ngazi watikisa nchi.




            
                                                            
                                                           MAREJEO.
Kihole, Y.M.(2004) Maswala ya kisarufi katika magazeti ya mitaani ya kiswahili: Tanzania.
              Mtandao www.ifeas-uni-mainz.de/SwaFo/SF11%20 kihore.pdf
King’ei, K.(2000) Matumizi ya Lugha kwenye vyombo vya habari. Kenya:  Mtandao
Mgazeti, Mtanzania, Kiu ya jibu, Ijumaa, Rai, Majira, Uhuru, Nipashe, Mwananchi, Bingwa,
             Mwananchi,Sani,: ya kuanzia Mei-Julai (2011).
Mulokozi .M.M.(1996)Utangulizi  wa  Fasihi. Dar  es  salaam:Taasisi  ya  Uchunguzi wa
               Kiswahili.
Wafula. R.M. na K.  Njogu (2002) Nadharia za Uhakiki wa Fasihi. Nairobi: Jomo Kenyatta
               Publishers Ltd.
Wamitila. K.W. (2006)Uhakiki wa Fasihi:Misingi na Vipengele Vyake. Nairobi:Kenya Litho
                Ltd.
  www.landmark.edu/library/citation-guides/apa.cfm Iliyosomwa Tarehe 23 juni 2011 saa
                11:41
                                                                        14
  

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni