ISIMU.
Maana ya Nadharia ya isimumuundo. Mbinu za kimuundo katika uchanganuzi wa vipengele vya fonolojia.
Katika makala hii tutajadili maana ya fonolojia na maana ya isimumuundo kasha usuli wa nadharia ya isimumuundo. Katika kiini cha makala hiii ni Ubainishaji wa vipengele vya kifonojia na Ubainishaji wa mbinu za kimuundo pamoja na ufafanuzi wa mbinu hizo katika vipengele vya kifonolojia. Kisha tutahitimisha mjadala wetu.
Kwa mujibu wa Mugulu (1999) akimrejelea Fudge (1973) anasema kwamba fonolojia ni kiwango kimojawapo cha lugha fulani kilicho na vipashio vidogo zaidi kuliko vipashio vingine vyote vya lugha. Vipashio vya kifonolojiani fonimu na alofoni zake.Dosari ya fasili hii ni kwamba haijafafanua kiwango kipi cha lugha ambacho kinahusika na fonolojia kwani lugha inaviwango mbalimbali.Massamba (2010) anasema kuwa fonolojia ni tawi la isimu linalojishughulisha na mfumo wa sauti (asilia) za lugha. Hii inamaana kwamba, kila lugha mahususi inamfumo wake wa sauti ambamo maneno hujengwa. Ki ukweli fonolojia hujihusisha na namna sauti zinavyotumika katika maneno ya lugha mahususi katika kuleta maana.Massamba na wenzake (2004) wanafafanua kuwa, fonolojia ni tawi la isimu ambalo hujishughusha na uchunguzi, uchambuzi na uainishaji wa sauti pambanuzi ambazo hutumika katika mifumo mbalimbali ya sauti za lugha za binadamu.Massamba (2010), pamoja naMassamba na wenzake (2004), wanaonekana kufanana katika fasili zao juu ya fonolojia isipokuwa, Massamba na wenzake (2004), wameonesha kuwa fonolojia si tawi linalojihusisha na mfumo wa sauti tu, bali huzichunguza, huzichambua pamoja na kuziainisha sauti hizo.TUKI (1990) wanasema kuwa, fonolojia ni tawi la isimu ambalo hushughulikia uchambuzi wa mfumo wa sauti zinazotumiwa katika lugha fulani.Vilevile dosari ya fasili hii ni kwamba, imeegemea upande mmoja tu yaani uchambuzi wa mfumo wa sauti za lugha fulani na kusahau kuwa taaluma hii ya fonolojia haijikiti tu katika uchambuzi bali huzingatia uchambuzi, uchunguzi pamoja na uainishaji wa sauti hizo kama asemavyo Massamba na wenzake (2004). “fonolojia ni tawi la isimu ambalo hujishughusha na uchunguzi, uchambuzi na uainishaji wa sauti pambanuzi ambazo hutumika katika mifumo mbalimbali ya sauti za lugha za binadamu.”Kwa mujibu waMatthews (2001)anafafanua kwamba, Isimumuundo ni tawi la isimu ambalo hutumika kama kihuzi cha kinadharia kinachochunguza au kuchambua na kuelezea muundo wa lugha kwa kuzingatia vipengele vya lugha pamoja na uhusiano wake katika kuunda kitu kikubwa zaidi.Pia isimumuundo ni mkabala unaochambua na kufafanua mfumo wa lugha kama unavyojibainisha ukilinganisha na kipindi maalum katika historia.Baada ya kuangalia fasili hizo ufuatao ni usuli wa nadharia ya isimumuundo kwa mujibu waMatthews (kishatajwa). Nadharia ya umuundo ilianzia Ufaransa miaka ya 1900 na mwanzilishi wake ni Ferdinand de Saussure katika dhana yake ya langue (umilisi) na parole (utendi).Nadharia ya isimumuundo imejadiliwa na matapo makuu mawili yaani tapo la Ulaya na tapo la MarekaniAwali ya yote wanasimu wa awali walijaribu kuchunguza lugha kwa kulinganisha zaidi na historia. Ferdinand hakuridhika na ulinganishaji huo kwani aliona kwamba ulikuwa unajibu swali kuwa asili ya lugha hiyo ni wapi, lakini haikujibu swali kuwa hiyo lugha inamfumo gani.Tapo la Ulaya lilitoa hoja kuu zifuatazo katika nadharia hii:Lugha inamfumo, yaani lugha ni mfumo ambao una elemeti zinazotagusana.Lugha ni mfumo wa alama: kwa mfano kelele ni lugha endapo tu zitawasilisha au kuelezea mawazo fulani, mfano dhana (dhahania), kiashiria na kiashiriwa.Lugha hushughulika katika viwango viwili ambavyo ni langue (umilisi) na parole (utendi)Baada ya tapo la Ulaya lilifuata tapo la Marekani ambalo nalo lilifafanua dhana ya umuundo au nadharia hii ya isimu muundo kama ifuatavyo: Hapo awali watu walijishughulisha na uchunguzi wa lugha za Marekani yenye asili ya kihindi, walikuwa wanaanthropolojia, lakini ilionekana kuwa hawakuwa na mbinu mahususi ambazo wangezifuata ili kuweza kufafanua lugha hizo.Kutokana na mapungufu hayo wakatokea wanaumuundo wa kimarekani walioongozwa na Bloomfield ambaye yeye aliona kuwa uchunguzi wa lugha unapaswa kujikita katika kile watu wanachokisema. Hivyo basi walipendekeza hoja kuu zifuatazo.Isimu ni sayansi fafanuzi; yaani inafafanua kile watu wanachokisema na sio kile wanachotakiwa kusema.Kila lugha ni mfumo ulio na taratibu zake: lugha haipaswi kuchambuliwa kwa kutumia lugha nyingine, bali inapaswa kuchambuliwa kwa kutumia mfumo wake wenyewe.Lugha ni mfumo ambao vipashio vidogovidogo zaidi huunganika kimpangilio ili kuunda vipashio vikubwa zaidi. Wanamuundo hawa walipendekeza taratibu ambazo walianza kuzitumia kwa kuchambua vipashio vidogo kabisa na kuviainisha na kuvipambanua katika ruwaza ambazo zilitumika kuunganisha ilikuunda vipashio vikubwa zaidi.Maana haipaswi kuwa sehemu ya ufafanuzi wa kiisimu. Bloomfield na wafuasi wengine wa tapo hili waliona kuwa maana ni dhana ya kinasibu ambayo haiwezi kuchunguzika, kwa hiyo si ya kisayansi.Taratibu za kutambua vipashio katika lugha ni lazima ziwe halisi na zenye kufuata taratibu maalum.Baada ya usuli wa nadharia ya isimumuundo, vifuatavyo ni vipengele vya kifonolojia pamoja na mbinu za kimuundo katikaufafanuzi wa vipengele hivyo(kifonolojia) kwa mifano. Vipengele hivyo ni sauti (foni), alofoni, fonimu na silabi. Pia mbinu zitumikazo na wanaisimumuundo katika ufafanuzi wa vipengele hivyo ni mbinu ya uainishaji, sintagmatiki, paradigmatiki, moza, jozi pekee, mpishano huru, mgawanyo kamilishani, mgawanyo wa kiutoano, na ubadala.Kwa kuanza na mbinu ya uainishaji. Kwa mujibu wa Kamusi ya Karne ya 21(2011), uainishaji ni “upangaji wa vitu au viumbe katika makundi kwa mujibu wa jinsi vinavyohusiana.”Hivyo basi, katika muktadha wa kifolonojia tunaweza kusema kuwa, uanishaji ni upangaji wa vipashio katika makundi kulingana na nduni zake bainifu au uhusiano wake. Kwa mfano: kosonanti za Kiswahili ziliainishwa kulingana na namna zinavyotamkwa, mahali pa matamshi na hali ya nyuzi sauti.Kwa mfano: konsonanti “m”, “n”, “g” waliziainisha kama nazali pamoja na kuzipa sifa zake kama vile; [m] [n]+kons +kons+nazali +nazali+midomo +ufizi+ghuna +ghunaHivyo kila sauti waliipa nduni za ziada na nduni bainifu, zilizotofautisha fonimu moja na nyingine. Kwa mfano fonimu; “s” na “l”[s]=kikwamizi [l]= kitambaza+kons +kons+kikwa +kitambaza+ufizi +ufizi-unazali -unazali-ghuna +ughunaMbinu ya pili sintagmatiki; sintagmatiki ni ubadilishanaji wa nafasi ya vipashio vya kifonolojia (fonimu) kwa njia ya mlalo. Hivyo katika lugha ya Kiswahili vipashio kwa kawaida hupangwa katika mfuatano maalum wenye mahusiano, ambao ni;K+I – b+a = ba mfano katika neno “baba”K+K+I – c+h+a = cha mfano katika neno “chama”K+K+K+I – m+b+w+a = mbwa mfano katika neno “mbwa”Hivyo basi mbinu hii ya sintagmatiki imejikita zaidi katika kuangalia mpangilio sahihi wa sauti katika lugha husika kiulalo. Na kamwe huwezi kukuta neno “ngoma”limeandikwa ngmoa, au kata – ktaa.Vilevile hata muundo wa silabi za Kiswahili hubainishwa idadi yake kwa kufuata mbinu ya kisintagmatiki, yaani kuhesabu kwa ulalo kuanzia kushoto kuelekea kulia. Mfano neno “Anajichekelesha” neno hili lina silabi 7 ambazo ni $$ A$$ na $$ ji $$ che $$ ke $$ le $$ sha $$ 1 2 3 4 5 67Mbinu ya tatu ni mbini ya paradigmatiki, neno paradigmatiki limetokana na neno paradigm likiwa na maana ya kundi la vitu vinavyoweza kukaa pamoja kutokana na mahusiano yao.Hivyo paradigmatiki kwa mujibu wa The New American Dictionary paradigmatiki ni mahusiano wima baina ya vipengele vya kiisimu vinavyounda muundo mkubwa zaidi kama vile sentensi. Kwa hiyo, nadharia hii hubainisha vipashio kiuwima zaidi. Kwa mfano;mmw nafasi iliyokaliwa na /m/ inaweza kukaliwa na mu pia mwwPia katika muundo wa lugha ya Kiswahili sauti huweza kubadilishana nafasi kiparadigmatiki (wima) na kuunda neno jingine lenye maana tofauti na lile la awali. Kwa mfano katika neno “pata” tunaweza kupata maneno yafuatayo kwa kubadilisha fonimu (konsonanti) kiuwima;/p/+/a/+/t/+/a/ = (pata)/b/+/a/+/t/+/a/ = (bata)/k/+/a/+/t/+/a/ = (kata)/n/+/a/+/t/+/a/ = (nata)
Vilevile tunaona kwamba katika maneno hayo kama tutatoa kosonanti au sauti /p/ na kuweka irabu au sauti /e/ ni dhahiri kwamba maneno hayo hayatakuwa na maana yoyote katika lugha ya Kiswahili kwa sababu lugha ya Kiswahili haina mfuatano wa I+I+K+I katika kuunda silabi badala yake inamfuatano wa K+K+IMbinu ya nne ni mbinu ya moza, kwa mujibu wa McCarthy (1989), moza ni mapangilio wa vipashio ulio katika mkururo. Mbinu hii huangalia mpangilio wa kimfuatano katika fonimu. Kwa mfano; foni “abc” zitafuatana na fonimu “xyz” inategemewa kwamba mpangilio wa “abc” unaweza tu kufanana na “xyz” na sio “yxz” nk.
Mfano.1mama, baba, kaka lalawalewale, kulekule, vilevile,imba, cheza, kula, ogaManeno haya katika mfano.1 yapo katika mfuatano na mpangilio wa sauti unaokubalika katika lugha ya Kiswahili.Mfano.2 mmaa, bbaa, kkaa, aallwlwlaeae, klkluuee, vvlliieeiamb, chzea, uakl, oagManeno katika mfano.2 hayapo katika mfuatano na mpangilio wa sauti unaokubalika katika lugha ya Kiswahili.
Mbinu nyingine ya kimuundo inayotumika katika utambuzi wa vipengele vya kifonolojia kama vile fonimu ni mbinu ya jozi sahili au jozi pekee.Hapa wanamuundo huchukua maneno mawili yanayofanana kwa idadi mfano, bata [bata] = sauti nne na bati [bati] = sauti nne. Katika maneno haya sauti zinazotofautiana ni /a/ na /i/ kwa sababu hizi ni fonimu mbili tofauti.
Pia maneno haya yana maana mbili tofauti kutokana na sauti tofauti yaani /a/ na /i/. Vilevile maneno kata na bata tunapata maana mbili tofauti kutokana na sauti mbili tofauti yaani /k/ na /b/Mbinu nyingine ni ile ya mgawanyo kamilishani; mbinu hii inadai kwamba kuna mazingira ambapo kuna sauti mbili zinazofanana ambapo sauti hizo mbili zinagawana mazingira ya kutokea. Kwa mfano: kama “A” ikitaokea katika mazingira ya kwanza basi haiwezi kutokea katika mzaingira ya pili. Kamwe haziingiliani. Lakini katika lugha ya Kiswahili hakuna sifa kama hii. Sifa hii tunaipata katika lugha ya Ciruri/chiruri.Kwa mfano neno “Imbusi” – mbuzi = “Ogubusi” – mbuzi mkubwa.
Mbinu nyingine ni mbinu ya mpishano huru, katika mbinu hii kuna kuwa na sauti mbili ambazo zinaweza kutokea sehemu yoyote au mazingira yoyote bila ya kikwazo. kwa mfano; Gari – ghariZambi – dhambiAgenda – ajenda
Mbinu hii hutumika katika kubainisha alofoni za fonimu moja.Mgullu (1999) akimrejelea Hyman (1975) anaeleza kuwa mbinu nyingine ambayo hutumiwa wakati wa kuchambua sauti ambazo ni fonimu au alofoni za lugha fulani ni ile ya mgawanyo wa kiutoano. Utoano ni dhana ambayo imeelezwa vizuri na Hyman kuwa, katika fonolojia ni dhana ambayo hutumiwa kuelezea uhusiano uliopo baina ya sauti mbili au zaidi ambazo haziwezi kutokea katika mazingira sawa.Mfano, katika lugha ya Kiingereza kuna sauti /P / yenye mpumuo na sauti /P/ isiyo na mpumuo ambazo tunaelewa wazi kuwa [P ] hutokea mwanzoni mwa neno tu, kwa mfano, katika /pin/, /pen/, /put/, nk. Kwa upande mwingine /p/ isiyo na mpumuo hutokea sehemu yoyote ya neno isipokuwa mwanzoni. Hapa tunapata kigezo muhimu sana cha kutofautisha fonimu na alofoni.
Hivyo basi, mbinu walizotumia wanamuundo katika uchambuzina ufafanuzi wa vipengele vya kifonolojia zimekuwa msingi mkubwa sana katika uchambuzi wa data mbalimbali za lugha duniani na ndizo zimekuwa chanzo cha kuwafanya wanaisimu yaliofuatia kupata mahali pa kuanzia katika kufanya uchunguzi wa lugha mbalimbali duniania.
MAREJEO:Jewell, E. J and A. Frank. (2005). The New Oxford American Dictionary. (2nd Edit).Oxford University Press. New York.Mdee, J. S. na wenzake (2011). Kamusi ya Karne ya 21.Longhorn Publishers (K) Ltd. Nairobi.Massamba, D.P.B na wenzake. (2009).Fonolojia ya Kiswahili Sanifu (Fokisa): Sekondari na Vyuo.Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.Massamba, D.P.B. (2010). Phonological Theory: History and Development. Institute of Kiswahili Studies (IKS). Dar es Salaam.Metthews, P. (2001). A short History of Structural Linguistics. Cambridge University Press. British.McCarthy, J.J. (1989). “Linear Order in Phonological Representation.”Linguistics Department Faculty Publication Series Paper 45.http:// scholarworks.umass.ed/linguist_faculty_pubs/45Mgullu, R.S. (1999).Mtalaa wa isimu: Fonetiki, Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili. Longhornpublishers.Ltd. Nairobi.TUKI, (1990).Kamusi Sanifu ya Isimu na Lugha. Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mambo yaliyosababisha kuibuka kwa nadharia Ya mofofonemiki kwa mifano kutoka katika lugha mbalimbali.
Makala hii itajadili Maana ya mofofonemiki, Historia fupi ya mofofonemiki, Mambo yaliyosababisha kuibuka kwa nadharia ya mofofonemiki kisha hitimisho na marejeo.
Kwa kuanza na fasili ya mofofonemiki kwa mujibu wa mtandao wa Wikipedia wanafafanua mofofonemiki kuwa ni tawi la isimu linalojishughulisha na mwingiliano wa mishakato ya kimofolojia na kifonolojia au kifonetiki. Pia hujishughulisha na mabadiliko ya sauti yanayotokea katika mofimu wakati zinapoungana kuunda maneno. (Tafsiri yetu).Fasili hii ina mapungufu fulani kwani, mofofonemiki haijishughulishi na michakato yote ya kifonolojia na kimofolojia bali ni baadhi tu ya michakato hiyo ambayo ilishindwa kufafanuliwa kwa kutumia data za kifonolojia au kifonetiki peke yake.
The New Oxford American Dictionary inafafanua kwamba, mofofonolojia/mofofonemiki ni tawi la isimu linalojishughulisha na uwakilishi wa kifonolojia wa mofimu.Hivyo basi tunaweza kusema kuwa, mofofonemiki ni tawi la isimu linaloshughulikia matumizi ya kimofolojia katika kueleza baadhi ya tofauti za kifonolojia ambazo isingewezekana kuzielezea kwa kutumia data za kifonetiki au kifonolojia peke yake.
Baada ya kuangalia fasili ya neno mofofonemiki ifuatayo ni historia fupi ya nadharia ya mofofonemiki.Kwa mujibu wa Massamba (2010:82) akimrejelea Martnet (1965) anafafanua kwamba, istilahi hii mofofonemiki/mofofonolojia ilipendekezwa kwa mara ya kwanza na N.S. Trubetzkoy (1929). Trubetzkoy alitumia istilahi hii kwa maana ya tawi la isimu ilinaloshughulikia matumizi ya mafolojia katika kuelezea baadhi ya tofauti za kifonolojia ambazo isingewezekana kuzielezea kwa kutumia data za kifonolojia au kifonetiki peke yake.
Baada ya kuangalia historia fupi ya mofofonemiki yafuatayo ni mambo yaliyosababisha kuibuka kwa nadharia ya mofofonemiki.
Kuchunguza ubadilikaji wa sauti ambao usingeweza kuelezwa kwa kutumia data za kifonolojia peke yake. Baadhi yao wakapendekeza kuwapo kwa kiwango cha kimofofonemiki pamoja na kipashio umbo kiini kama kiwakilishi cha mofimu, kwa hiyo walipendekeza hivyo baada ya kushindwa kujua ipi ni alofoni ya fonimu ipi kwa kutumia kigezo cha kifonetiki pekee Kwa mfano; walishindwa kujua /k/ ni alofoni ya /c/ au /c/ ni alofoni ya /k/ Kwa mfano hata katika lugha ya kurusi –ruka = “mkono”ručnoj = “a mkono”Mzizi ni – ruk na ručWanamofofonemiki walichunguza wakagundua kuwa katika mazingira fulani /k/ hubadilika kuwa /č/ baada ya kufuatiwa na “noj”. Hivyo wakapendekeza umbo kiini la maneno haya ni ruKa au ruČnoj umbo kiini lake lilitambulika kama {K} au {Č}Katika lugha ya Kiswahili kuna mabadiliko ya sauti yanayotokea katika baadhi ya maneno baada ya sauti fulani kufuatiwa na kiambishi cha unominishaji (i) kwa mfano katika maneno yafuatayo;Fuata – fuasiPenda – PenziCheka – CheshiPika – PishiPia wanamofofonemiki walichunguza ubadilishanaji huu wa sauti kwani walishindwa kujua ipi ni alofoni ya fonimu ipi. Ndipo wakagundua kuwa katika mazingira fulani /t/ hubadilika kuwa /s/ baada ya kufuatwa na mofimu ya unominishaji “i” pia sauti /d/ hubadilika na kuwa /z/ baada ya kufuatwa na mofimu ya unominishaji “i”.Baada ya kupendekeza umbo kiini maneno haya yakaandikwa kama ifuatavyo: kwa mfano neno {fuaTa} umbo {T} likawa umbo kiini ambalo linawakilisha sauti zote mbili yaani /t/ na /s/, pia neno {piKa} umbo kiini lake ni {K} ambalo linawakilisha sauti /k/ na /ʃ/Kuchunguza mabadiliko ya sauti yanayotokea mofimu zinapoungana. Kwa mfano; katika lugha ya Kiswahili,U + ima – wimaI + etu – yetuMu + alimu – MwalimuU + imbo – wimboVi + ake – vyakeWanamofofonemiki wakagundua kuwa sauti fulani huweza kuungana na kuunda sauti moja na kubadili umbo la neno.Chunguza muundo wa kifonolojia wa mofimu katika lugha. Kwa mfano katika lugha ya Kiswahili;Mu + huni – MhuniMu + gonjwa – MgonjwaMu + guu – MguuMu + uguzi – MuuguziMu + tu – MtuWanamofofonemiki wakagundua kwamba mofimu fulani huweza kuungana na mofimu nyingine na kuunda umbo la neno.Kuchunguza ubadilishanaji wa sauti ambao una una uamilifu wa kimofolojia lakini husababisha mabadiliko fulani ya kifonetiki. Kwa mfano katika lugha ya kiingereza;Play + s – [pleiz]Dog + s – [dogz]Since – [sins]Else – [els]Place – [pleis]Wanamofofonemiki wakachunguza kinachosababisha kuwepo na maumbo tofauti tofauti ya mofimu ya wingi. Kwa mfano; /s/, /iz/, /z/ Wakagundua kuwa kuna mchakato zaidi ya ule wa kifonolojia ambao ni wa kimofolojia unaosababisha umbo ‘s’ kutamkwa /z/ au /iz/ au /s/MAREJEO:Swali:Kwa kutumia data ifuatayo bainisha mabadiliko ya sauti yaliyosababishwa na mazingira ya kifonolojia pekee, kimofolojia pekee na kimofofonolojia. Onesha kwa mifano kutoka katika data jinsi wanamofofonolojia walivyofanikisha kutatua matatizo ya kimofofonolojiaData.
Iba Wizi Cheka Mcheshi Mguu Miguu Nkindiza Nkindiza Mkuki Mkuki Mvuvi Mvuvi
Katika kujibu swali hili tumeligawanya katika sehemu tatu. Katika sehemu ya kwanza tumetolea maana ya istilahi mbalimbali kwa mujibu wa wataalamu mbalimbali. Istilahi hizo ni pamoja na maana ya fonolojia, mofolojia na mofofonolojia, sehemu ya pili tumejadili kiini cha swali ambapo tumeonesha mazingira mbalimbali ya utokeaji wa data tulizopewa na suluhisho la wanamofofonolojia katika kutatua matatizo ya kimofofonolojia na sehemu ya tumehitimisha kazi na kutoa marejeo.
Kwa kuanza na maana ya istilahi hizo watalaamu wanatueleza kama ifuatavyo;Massamba na wenzake (2004) wanaeleza kuwa; fonolojia kama tawi la isimu ambalo hujishughulisha na uchunguzi, uchambuzi na uainishaji wa sauti pambanuzi ambazo hutumika katika mifumo mbalimbali ya sauti za lugha za binadamu. Hii ina maana kwamba fonolojia kama tawi la isimu hujishughulisha hasa na zile sauti ambazo sauti ambazo hutumika kutofautisha maana za maneno katika lugha mahususi.
John Habwe na Peter Karanja (2004) wanaeleza kuwa; fonolojia ni utanzu wa isimu unaochunguza jinsi sauti za lugha zinavyofanya kazi katika lugha mbalimbali. Fonolojia huchunguza jinsi sauti hizo zinavyotumika, zinavyounganishwa na kupangwa katika lugha yoyote mahususi ili kuunda tungo zenye maana.
Hivyo kutokana na maana za wataalamu hawa tuanaweza kueleza kuwa; fonolojia ni tawi la isimu linalojishughulisha na uchunguzi, uchambuzi na ufafanuzi wa sauti katika lugha mahususi. Mfano Kiswahili, Kiingereza Kichina, Kijerumani na Kihaya.
Baada ya kueleza maana ya fonolojia tuangalie maana ya mofolojia kulingana na wanataalamu mbalimbali.Massamba na wenzake (2004) wanaeleza kuwa; mofolojia ni tawi la isimu linalojishughulisha na uchunguzi, uchambuzi na uainishaji wa maneno katika lugha.
John Habwe na Peter Karanja (2004) wanatueleza kuwa; mofolojia ni neno linalotumiwa kumaanisha utanzu wa isimu unaoshughulikia muundo wa maneno. Fasili hii inamapungufu kwani katika mofolojia hatushughulikii miundo ya maneno katika lugha bali kinachoshughulikiwa ni maumbo ya maneno. Miundo ya maneno katika taaluma ya isimu inashughulikiwa na tawi na sintaksia.Kutokana na fasili za wataalamu hawa tunaweza kueleza kuwa; mofolojia ni tawi la isimu linalojishughulisha na uchunguzi, uchambuzi na ufafanuzi wa maumbo ya maneno katika lugha. Baada ya kuangalia maana ya fonolojia na mofolojia ifuatayo ni maana ya mofofonolojia;
Massamba (2010) akimnukuu Martinet (1965) ambapo Martinet alinukuu kutoka kwa Trubetzkoy (1929) anatueleza kuwa; mofofonolojia kama ilivyotumiwa na Trubetzkoy ilimanisha sehemu ya isimu ambayo ingeweza kutumia mofolojia kuelezea tofauti fulani za kifonolojia ambazo zisingeweza kuelezwa kwa kutumia data za kifonolojia peke yake.
Baada ya kuangalia maana za istilahi mbalimbali zilizotumika katika swali hili, kifuatacho ni kiini cha swali kinachoonesha mabadiliko ya sauti yaliyotokea katika data tuliyopewa ambayo ni mabadiliko kifonolojia pekee, kimofolojia pekee na kimofofonolojia.
Tukianza na mabadiliko ya kifonolojia pekee, haya hutokea kwa namna tofauti au katika mazingira tofauti. Kwa mfano mazingira hayo ni; udondoshaji, uyeyushaji, muungano wa sauti, nazali kuathiri konsonanti na konsonanti kuathiri nazali.
Hivyo kutokana na data yetu katika kubainisha mazingira ya mabadiliko ya sauti kifonolojia pekee ni kama ifuatavyo;Mvuvi [ ɱ vuvi ]
Badiliko lililotokea hapa ni la kifonolojia katika mchakato wa usilimishaji wa nazali yaani konsonanti kuathiri nazali. Hapa tunaona kuwa sauti ya midomo /m/ imesilimishwa na kubadili sehemu yake ya kutamkia na kuchukua sifa ya midomomeno / ɱ / baada ya kukabiliana na sauti ya midomomeno /v/. Hivyo sauti /m/ imebadilika na kuwa / ɱ /.
Katika mabadiliko ya sauti ya sauti ya kitambaza /l/ kubadilika na kuwa kipasuo /d/ pia ni mabadiliko ya kifonolojia hii ni katika neno;n-limi [ ndimi ]
Utokeaji wake ni kutokana na kanuni ya nazali kuathiri konsonanti. Mazingira ya utokeaji wake ni sauti / l / inapokabiliana na nazali / n / yenye sifa ya kutamkiwa sehemu moja yaani kwenye ufizi hubadilika na kuwa / d /.
Pia mabadiliko nazali /n/ kipasuo cha kaa laini [ ŋ ] ni ya kifonolojia ambayo utokeaji wake ni wakiusilimishaji au kanuni ya konsonanti kuathiri nazali. Mazingira ya utokeaji wake ni sauti ya nazali kuathiriwa na konsonanti inayoiandamia hivyo kuifanya nazali kuifuata konsonanti mahali pa kutamkia. Mabadiliko hayo yameathiri sauti ya nazali /n/ na kutamkwa kama nazali ya kaa laini [ ŋ ].
Hivyo katika uwakilishi litakuwa;Umbo la ndani [ ŋkindiza ]Umbo la nje nkindiza.Baada ya kueleza mabadiliko ya kifonolojia, tutazame mabadiliko ya kimofolojia. Kutokana na data hii tunapata maumbo kama;Mguu mi-guu
Haya ni mabadiliko ya kimofolajia. Mazingira ya utokeaji wake ni mabadiliko ya uongezaji au upachikaji wa mofimu ya umoja na wingi ambapo; mofimu m- ya umoja imebadilika na kuwa mofimu mi- katika wingi.M-guu umbo la umojaMi-guu — umbo la wingi.
Pia katika neno mkuki mkuki, mabadiliko yaliyotokea ni ya kimofolojia tu kwani hakuna mabadiko ya umbo na kinachoonekana ni uwepo wa mofimu m- ya umoja katika umbo hili pamoja na mzizi -kuki. hivyo kilichofanyika ni kuongeza -kuki katika mofimu hiyo ya umoja na kupata neno m-kuki. Hivyo umbo hili linabakia na umbo lake ambalo hubakia kuwa vilevile.M-kuki m-kuki, maumbo yote haya yako katika umoja
Vilevile katika neno M-dalasini m-dalasini, hakuna mabadiliko ya kimofolojia bali umbo limeendelea kuwa vilevile la umoja.Baada ya kuangalia mabadiliko ya kifonolojia na kimofolojia katika data tulitopewa, kipengele kinachofuatia ni kubainisha mabadiliko ya sauti yaliyotokea kwa mabadiliko ya kimofofonolojia.Kutokana na data yetu maneno;Iba mwiziCheka mcheshiHaya ni mabadiliko ya kimofofonolojia. Sababu ya kuwepo kwa mchakato huu ni uwepo wa mbadilishano wa sauti ambayo hayakuweza kufafanuliwa kwa utaratibu wa fonolojia pekee na utaratibu wa mofolojia pekee hivyo kukawa na hitaji kubwa kuwa na kiwango kingine cha kuweza kutatua changamoto hiyo. Kwa hiyo kuibuka kwa mofofonolojia kulikuwa na lengo la kumaliza changamoto hiyo iliyokuwepo.
Hivyo katika mabadiliko iba wizi, sauti ya kipasuo cha midomo /b/ kubadilika kuwa sauti ya kikwamizi cha ufizi /z/ imesababishwa na kuwepo kwa irabu /i/ ya unominishaji mwishoni mwa sauti /b/. Kutokana na kitendo cha “kuiba” tungetarajia kupata nomino “mwibi” kutokana na mofimu {mu-ib-i}. Lakini tunapata neno [w-iz-i]. Hapa konsonanti ya kipasuo cha midomo /b/ hudhoofika na kuwa konsonanti ya kikwamizi cha ufizi [ z ] katika mazingira ya kutanguliwa na irabu ya unominishaji /i/.iba [ w-iz-i ]
Pia katika neno cheka mcheshi, mabadiliko yaliyotokea hapa ni ya kimofofonolojia ambapo sauti ya kipasuo cha kaakaa laini /k/ inabadilika na kuwa sauti ya kikwamizi cha kaakaa gumu [ ∫ ] baada ya kufuatiwa na irabu ya unominishaji /i/.Cheka [ mče∫i ]Uwepo wa mabadiliko sauti na umbo ambayo hayawezi kuelezwa, kwa mchakato wa fonolojia na mchakato wa kimofolojia ndipo palipoibuka mchakato wa kimofofonolojia.Katika utatuzi wao wanamofofonolojia walikuja na dhana ya umbo kiini. Umbo kiini hili liliwakilisha fonimu mbili. Waliteua umbo kiini kwenye neno la msingi. Na liliwekewa mabano mchirizi { }.Kwa mfano katika cheka mcheshi
Neno la msingi ni “cheka” ambapo waliteua sauti {K} kuwa umbo kiini. Fonimu {K} iliteuliwa kuwakilisha /k/ yenyewe katika neno cheka ambalo ni kitenzi na inawakilisha sauti [ ∫ ] kwenye “mcheshi” ambayo ni nomino. [k]{K}[ ∫ ]Umbokiini {K} linawakilisha sauti /k/ na [ ∫ ]Pia katika neno iba na wizi umbokiini ambalo liliteuliwa ni {B} ambayo kuwakilisha sauti /b/ na sauti sauti /z/.[ b ]{B}[ z ]Baada ya utatuzi huu baadhi ya wataalamu walitoa maoni yao juu ya umbokiini. Baadhi yao ni Linhtner (1970) akinukuliwa na Massamba (2010) anaeleza kuwa umbo kiini sio halisi ni la kidhahania na kinasibu kwani halioneshi mchakato na namna ambavyo sauti na umbo hubadilika na kuwa katika sauti nyingine na kitu gani hasa husababisha mabadiliko hayo ya sauti. Umbokiini huishia tu katika kuteua sauti moja kuwakilisha sauti nyingine. Basi huo ukawa udhaifu wa dhana ya umbokiini.Hitimisho, kutokana na wanamofofonolojia kushindwa kutatua matatizo ya kifonolojia wakaibuka wanafonolojia zalishi ambao waliokuja na mitazamo mipya katika utatuzi wa matatizo ambayo yalishindwa kutatuliwa na wanamofofonolojia ambapo walikuja na dhana ya misingi na mihimili ya kufuata ili kubainisha mabadiliko yaliyokuwa yanatokea yaliyoshindwa kuelezeka.
Marejeo.
Habwe, J. na P, Karanja (2004) Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Nairobi: Phoenix Publishers
Ltd.Massamba, D.P.B. na wenzake (2004) Fonolojia ya Kiswahili Sanifu (FOKISA): Sekondarina Vyuo. Dar es Salaam. TUKI.Massamba, D.P.B. (2010) Phonological Theory: History and Development. Dar es Salaam:TUKI.
Michakato ya kiusilimisho katika fonolojia.
Katika kujadili mada hii tutalenga kuangalia michakato ya kiusilimisho namna inavyotumika katika kuyakokotoa maumbo ya ndani kwenda maumbo ya nje katika lugha ya Kiswahili. Lakini kabla ya kuonesha ukokotozi huo ni vyema kwanza tuangalie maana ya mchakato, maana ya usilimisho, umbo la ndani na nje, kisha tutaelekea kwenye hitimisho pamoja na marejeo.
Tuki (2004) inaeleza kuwa mchakato ni mfululizo wa shughuli unaosababisha kitu fulani kufikiwa.Hivyo katika uwanja huu wa fonolojia tunaweza kusema kuwa mchakato utakuwa unafanyika pale ambapo mofimu mbili zinapokutanishwa huweza kutokeza mabadiliko fulani katika mofimu mojawapo au kutotokea badiliko lolote. Mfano viungu hubadilikia kuwa vyungu,kietu hubadilika kuwa chetu hapa tunaona kuwa mabadiliko yametokea lakini miti hubakia kuwa miti, kiti hubakia kuwa kiti na hapa tunaona kuwa hakuna mabadiliko yoyote yaliyotokea.
Massamba (2011) anaeleza kuwa kuna aina mbili za michakato asilia yaani mchakato usilimisho na mchakato sio-usilimisho. Lakini katika mjadala huu tutajikita kwa kuangalia mchakato mmoja tu yaani ule wa kiusilimisho, ambao Massamba anasema muwa usilimisho ni pale ambapo kitamkwa kimoja hufanywa kifananefanane na kitamkwa kilicho jirani yake kwa maana kwamba hupata baadhi ya sifa za kipande sauti chenziye kilicho jirani. Kwa mfano, konsonanti inaweza kupata baadhi ya sifa za irabu au irabu ikapata baadhi ya sifa za konsonanti, na konsonanti moja huweza kuathiri konsonanti nyenziye au irabu moja huweza kuathiri irabu nyenziye. Pia anaendelea kusema kuwa usilimisho unaweza kuhusisha michakato kadhaa kama vile,unazalishaji wa irabu, utamkiaji pamwe wa nazali, ukaakaishaji, ughunishaji kati irabu, uhafifishaji kati irabu, tangamano la irabu, ughunishaji konsonanti shadda, muungano.
Habwe na Karanja (2004), wanaeleza kuwa usilimisho ni kule kufanana kwa fonimu kwa kiasi au kikamilifu kutokana na kuathiriana. Hapa sauti jirani katika neno huathiriana kiasi kwamba fonimu hupokea ama kupoteza sifa za kifonetiki kwa fonimu jirani, na matokeo yakiwa kuwa fonimu hizi hukabiliana sana katika kufanana. Pia wanaendelea kusema kuwa usilimisho unaweza kuhusisha kuimarika, kodhoofika, kuingizwa, kudondoshwa, au kuungana kwa fonimu katika neno.
Hivyo tunaweza kusema kuwa usilimisho ni kule kufanana kwa fonimu kwa kiasi au kiukamilifu kutokana na kuathiriana kwake kunakosababishwa na fonimu iliyo jirani.Baada ya kuangalia utangulizi huo sasa ni wakati wa kukokotoa michakato hiyo ya kiusilimisho kutoka umbo la ndani kwenda la nje.Lakini kabla ya kukokotoa kwanza tuangalie umbo la ndani kuwa ni namna umbo lenyewe linavyoumbwa na mofimu zake au tunaweza kusema kuwa ni umbo la neno ambalo halijafanyiwa michakato yoyote ya mabadiliko. Na umbo la nje ni lile lililofanyiwa mabadiliko au michakato na mara nyingi huakisi umbo la ndani. Michakato itakayooneshwa ni ile ambayo imeorodheshwa na wataalamu lakini ambayo inahusiana na lugha ya Kiswahili tu kwani mingine inahusiana na lugha zingine kwa mfano michakato ya Massamba ameingiza michakato miwili inayohusiana na lugha za kigeni ambayo ni ughunishaji kati irabu na uhafifishaji kati irabu, hivyo hiyo hatajadiliwa.Unazalishaji wa irabuMassamba (2011) anadai kuwa unazalishaji wa irabu ni aina ya usilimisho ambao irabu hupata sifa ya unazali kutokana na irabu yenyewe kutangamana na konsonanti ambayo ni nazali. Hivyo irabu nyingi hupewa sifa za unazali kutokana na ama kufuatiwa kwa nazali ama kutanguliwa na nazali. Na alama inayowakilisha unazalishaji ni alama ya kiwimbi [ ̴ ] ,zaidi tuangalie mifano ifuatayo.Mifano
umbo la ndani umbo la nje /nondo/ [nondo] /penya/ [penya] /mama/ [mama] /ngambo/ [ ambo] /nyumba/ [ umba] /muwa/ [muwa]
Hivyo sauti zote zilizowekewa alama ya kiwimbi ( ̴ ) zina unazali kwa sababu zimefuatana na nazali na hivyo zimefanywa kuwa unazali.Kanuni katika KiswahiliI I NKanuni ya jumla.
+sila+kons +naz -kos+naz +kons+naz
UkaakaishajiMgullu (1999) akimnukuu Les (1984), anadai kuwa ukaakaishaji wa fonimu hutokea ambapo fonimu zisizo za kaakagumu zinapobadilika na kuwa za kaakagumu. Yeye anadai kuwa katika Kiswahili sauti za kaakagumu zipo mbili tu yaani /ɟ/ na /ʧ/ ambazo ni vizuiwa kwamizwa. Anamalizia kwa kusema kuwa ukaakaishaji wa fonimu hutokea wakati ambapo fonimu zisizo vizuiwa kwamizi hubadilika na kuwa vizuiwa kwamizwa. Hii katika ukokotozi wake unakuwa kama ifuatavyo.
umbo la ndani umbo la nje umbo la nje /ki+enu/ [kjenui] [ enu] /ki+eusi/ [kjeusi] [ eusi] /ki+ombo/ [kjombo] [ ombo] /ki+umba/ [kjumba] [ umba] /ambaki+o/ [ambakjo] [amba o]
Hapa tunaona kwamba kipasuo cha kaakaalaini /k/ hubadili mahali pa matamshi na kuwa kizuiwa kwamizi /ʧ/ cha kaakaagumu katika mazingira ya kufuatiwa na sauti /ϳ/.Kanuni yake /i/ [ ] I =kisha inabadilika kuwa/k/ [ ] /i/Kanuni ya jumla.
+kons-sila +stn’d +sila+juu + juu -kons+nyuma +k’gumu -nyuma-fulizwa +juu-ghuna
UyeyushajiUyeyushaji, wataalamu wengine huita irabu kuwa nusu irabu Mgullu (1999). Huu ni mchakato ambapo irabu irabu za juu /u/ na /i/ hubadlika na kuwa /w/ au / j/ katika mazingira ya kufuatiwa na irabu zisizofana nazo. Kwa kifupi ni kwamba /u/ inapofuatiwa na irabu yoyote isiyofanana nayo hubadilika kuwa [w] na /i/ ikifuatiwa na irabu yoyote isiyofanana nayo hubadilika na kuwa [j].Hivyo tunaweza kusema kuwa uyeyushaji ni kanuni inayoelezea mabadiliko ya sauti (irabu) na kuwa kiyeyusho aidha [w] au [j] hii ni kwa irabu zote za juu zinapofuatana na sauti zingine zisizofanana nazo. Na sauti hizo hubadilika katika mazingira ya /u/ hubadilika kuwa [w] inapofuatana na irabu nyingine isiyofanana nayo na / i/ inabadilika na kuwa [ϳ] pia inapofuatana na irabu isiyofanana nayo.Mfano wa /u/
umbo la ndani umbo la nje /mu+aminifu/ [mwe:mbamba] /ku+enu/ [kwe:nu] /mu+ anafunzi/ [mwa:nafunzi] /mu+eupe/ [mwe:upe] /mu+embe/ [mwe:mbe]
Hivyo tunaona wazi kabisa kuwa irabu ya juu nyuma /u/ imebadilika na kuwa kiyeyusho [w] katika mazingira ya kuatiwa na irabu isiyofanana nayo ambayo ni /a/ na /e/ kwa hapo juu lakini hata ikiwa ni /o/ huweza kubadilisha.Kanuni /u/ [w] I = uMfano wa irabu /i/
/umbo la ndani/ [umbo la nje] /mi+embe/ [mje:mbe] /mi+endo/ [mje:ndo] /mi+ezi/ [mje:zi] /mi+anzo/ [mja:nzo] /mi+eusi/ [mwe:usi] /mi+oyo/ [mjo:jo]
Hivyo tunaona kuwa irabu ya juu mbele /i/ hubadilika na kuwa [j] inapofuatana na irabu nyingine isiyofanana nayo ambayo ni /e,a na o/.Kanuni yake /i/ [j] I/= iKanuni ya jumla.
+sila -kons+juu -sila +sila+mbele + juu +juuI = +mbele+sila -kons +sila+juu -sila +juu+nyuma +juu +nyuma+nyuma
Tangamano la irabu (usilimisho wa irabu pekee)Huu ni mchakato wa kiusilimisho baina ya irabu na irabu katika kuathiriana kiasi kwamba hulazimika kufuatana. Katika mchakato huu kinachotokea ni kwamba, kama irabu ya mzizi ni /i, u au a/ basi irabu ya kiambishi cha utendea lazima kiwe ni [i] , wakati irabu ya mzizi ikiwa ni/ e au o/ katika hali ya utendea kiambishi chake kitakuwa ni [e]. Mfano.
umbo la ndani umbo la nje /imb+a/ [Imb-i-a] /andik+a/ [andik-i-a] /dak+a/ [dak-i-a] /chun+a/ [ un-i-a] /og+a/ [og-e-a] / ez+a/ [ ez-e-a] /kom+a/ [kom-e-a]
Hapa tumeona kuwa mofimu ya utendea ina alomofu mbili ambazo ni /i/ na /e/ ambapo alomofu /i/ tunaona inatokea pale ambapo irabu ya mzizi inakuwa na /i,u na a/ wakati ambapo alomofu /e/ inatokea wakati irabu ya mzizi ikiwa ni /e na o/. kinachoonekana hapa ni kwamba irabu zinatangamana kwa kufuata mahali pa matamshi. Kwa mfano kama irabu ya mzizi ni ya juu basi irabu ya utendea pia itakuwa ni ya juu, na irabu ya mzizi ikiwa ni ya kati basi irabu ya utendea pia itakuwa ya kati,na irabu ya chini siku zote inaonekana kuwa ni ya juu.Kanuni.
+sila +juu +sila-kons -nyuma -kati-juu +K-nyuma +sila- chini -juu-chini
Utamkaji pamwe wa nazali.Huu ni mchakato ambapo katika mkururo wa nazali na konsonanti hupelekea nazali kuathiriwa na konsonanti inayofuatana nayo. Usilimisho huu hutokea pale ambapo nazali hufuata mahali pa matamshi pa konsonanti inayofuatana nayo. Mifano yake ni kama ifuatayo;
umbo la ndani umbo la nje /n+buzi/ [mbuzi] /n+bwa/ [mbwa] /n+bu/ [mbu] /n+gongo/ [mgo go] /n+gozi/ [ gozi] /n+vua/ [ vua] /n+vivu/ [ vivu]
Hivyo katika mifano hii tunaona kuwa nazali zimebadilika kwa kufuata mahali pa matamshi pa konsonanti zilizokaribiana nazo. Mfano /n+gozi/ imebadilika kuwa [ɳgozi] ambayo huweza kuoneshwa kwa kanuni ifuatayo;/n / [ ] /g/Kanuni ya jumla.
s +kons-sila [ mahali] -sila+naz mahali
Kwa kuhitimisha tunaona kuwa michakato ya kiusilimisho katika lugha ya Kiswahili ipo na inatumika kukokotoa umbo la ndani kwenda umbo la nje. Huweza kufanya mabadiliko ya karibu au moja kwa moja kuliko michakato isiyo ya kiusilimisho ambayo haionyeshi mabadiliko ya moja kwa moja.MAREJEOHabwe, J na Peter K. (2004) Misingi ya sarufi ya Kiswahili. Phoenix Publishers: Nairobi.Massamba,D.P.B. (2011) Maendeleo Katika Nadharia ya Fonolojia. Taasisi ya Taaluma zaKiswahili (TUKI): Dar es Salaam.Mgullu, R.S. (1999) Mtalaa wa isimu: Fonetiki, Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili. Longhorn Publishers Ltd: Nairobi.TUKI, (2004) Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Oxford University Press: Nairobi.
MIFANO YA MISAMIATI YA LAHAJA
ZA KISWAHILI NA MAANA YAKE KATIKA LUGHA SANIFU.
Kitika kujadili mada hii tutaanza na maana ya Lahaja, Maana ya Lugha Sanifu, pia tutaangalia tofauti kati ya lahaja na lugha sanifu, ufanano kati ya lahaja na lugha sanifu na sababu za kuwepo kwa lahaja. Baada ya hapo tutaangalia Mifano ya misamiati ya lahaja za Kiswahili na maana yake katika lugha sanifu. Kisha tutahitimisha mada hii.Dhana ya lahaja na Kiswahili sanifu zimejadiliwa na wataalamu mbalimbali katika mitazamo tofauti tofauti kama ifuatavyo;King’ei (2010) anasema kuwa lahaja ni tofauti za kimatamshi zinazodhihirika miongoni mwa wanajamii lugha wanaoishi katika maeneo mbalimbali ya kijiografia.Msanjila na wenzake (2011) wanasema kuwa lahaja ni lugha mojawapo kati ya lugha ambazo kimsingi huhesabiwa kuwa lugha moja isipokuwa zinatofautiana katika baadhi ya vipengele fulani fulani kama vile lafudhi, fonolojia, msamiati usiokuwa wa msingi au miundo kutoka na eneo lugha hiyo inapozungumzwa .TUKI (2004) inasema kuwa lahaja ni tofauti katika matamshi maumbo na matumizi ya maneno katika maeneo mbalimbali kwa lugha yenye asili moja.Fasili zote hizi ni sahihi kwani zimegusia mambo muhimu kama vile utofauti wa kifonolojia, kimsamiati na lafudhi.Kwa misingi hiyo lahaja za Kiswahili zimegawanyika katika makundi mawili ambazo ni lahaja za kijiografia na lahaja za kijamii.Pamoja na wataalamu hapo juu kufasili dhana ya lahaja, pia dhana ya Lugha sanifu imeweza kufasiliwa na wataalam mbalimbali kama ifuatavyo;Msanjia na wenzake (2011) wanasema kuwa lugha sanifu ni lugha ambayo imekubaliwa na serikali itumike katika shughuli rasmi.TUKI (2004) inasema kuwa lugha sanifu ni lugha yenye kufuata taratibu au kanuni zilizokubaliwa.Hivyo basi tunaweza kusema kuwa lugha sanifu ni lugha yenye kufuata taratibu na kanuni zilizokubaliwa na mamlaka husika ili itumike katika shughuli za kiserikali mfano, Bungeni, maofisini na katika shughuli za kimahakama. Pia katika shughuli za kijamii kwa mfano, katika elimu na vyombo vya habari.Baada ya kuangalia fasili zilizotolewa na wataalam mbalimbali kuhusu lahaja na lugha sanifu, zifuatazo ni tofauti na ufanano ulizopo kati ya lahaja na lugha sanifu.Tofauti ya kwanza ipo katika fasili; ambapo lugha sanifu imefasiliwa (ameshatajwa) kuwa ni lugha ambayo imekubaliwa na serikali ili itumike katika shughuli rasmi wakati lahaja ni tofauti za kimatamshi zinazodhihirika miongoni mwa wanajamii lugha wanaoishi katika maeneo mbalimbali ya kijiografia.Tofauti ya pili ipo katika idadi ya wazungumzaji; Lugha sanifu inawatumiaji wengi kuliko lahaja, hii ni kutokana na sababu kwamba lugha sanifu imeteuliwa kutoka katika lahaja mbalimbali ili itumike katika shughuli zote za kiserikali na kijamii hivyo husaidia kuwajumuisha wanajamii wenye kutumia lahaja tofauti tofauti na kupelekea lugha sanifu kuwa na wazungumzaji wengi kuliko lahaja.Tofauti ya tatu ipo katika idadi; Lugha sanifu ni moja katika jamii fulani mfano katika jamii ya kitanzania lugha sanifu ni Kiswahili, wakati lahaja zipo nyingi katika jamii fulani. Kwa mfano katika jamii ya kitanzania kuna lahaja kama vile Kimtang’ata, Kipemba na Kiunguja.Tofauti nyingine ni kwamba lugha sanifu inaweza kuwa rasmi lakini lahaja haiwezi kuwa lugha rasmi pasipo kusanifishwa.Vile vile tofauti nyingine ipo katika maandishi; Lugha sanifu hutumika katika maandishi rasmi wakati lahaja haiwezi kutumika katika maandishi rasmi ila inakuwa katika maongezi ya kila siku.Pia lugha sanifu ina hadhi ya juu kuliko lahaja kwa sababu imesanifishwa na kutumika katika mawasiliano rasmi.Ufanano kati ya lugha sanifu na lahaja;Zote ni lugha kutokana na kwamba zinakidhi haja ya mawasiliana miongoni mwa wanajamii.Pia zote zinatunza utamaduni wa jamii husika. Kwa mfano wimbo wa Taifa katika jamii ya watanzania huimbwa kwa lugha ya Kiswahili na kurithishwa kizazi kimoja kwenda kingine.Pia shughuli mbalimbali za kijamii kama vile jando na unyago katika jamii tofauti tofauti hufanyika kwa kutumia lahaja za jamii husika, hivyo hutumika kuhifadhi utamaduni wa jamii husika.Vilevile zote hutumika kama kitambulisho cha jamii husika. Kwa mfano lugha ya Kiswahili hutumika kama kitambulisho cha waswahili pale wanapozungumza Kiswahili katika jamii ambayo si ya waswahili. Pia lahaja humtambulisha mtu kuwa ni wa jamii fulani pale anapozungumza, mfano lahaja ya Kiunguja ni ya watu wa Unguja.Pamoja na hayo, hata hivyo kuna sababu mbalimbali zinazopelekea kutokea kwa lahaja. Sababu hizo ni kama vile;Vikwazo vya kijiografia; Mipaka ya kijiografia huweza kutenganisha lahaja moja na lahaja nyingine, mipaka hiyo ya kijiografia huweza kusababishwa na mito, milima, mabonde, maziwa, bahari na misitu. Mfano lahaja ya Kiunguja na lahaja ya Kipemba imetenganishwa na bahari ya Hindi.Matukio ya kihistori; haya ni yale mambo yanayowafanya watu kuhama na kuingiliana kutoka sehemu moja na kwenda sehemu nyingine, matukio hayo ya kihistoria ni kama vile njaa, vita, na majanga mbalimbali ambayo kwa namna moja au nyingine husababisha kutokea kwa lahaja.Uhamiaji; hii ni hali ya jamii moja au kundi la watu kuhama au kuhamia katika jamii nyingine na kusababisha kutokea kwa lahaja, na uhamiaji huo huweza kusababishwa na biashara, kuoana, na ufugaji.Kutokana na sababu hizo zimepelekea mgawanyiko wa lahaja katika makundi mawili ambayo ni lahaja za kijiografia na lahaja za kijamii.Lahaja za kijiografia ni zile lahaja ambazo husababishwa na mipaka ya kijiografia kama vile misitu, mito, maziwa, mabonde na bahari. Mfano wa lahaja hizo ni kama vile; Kihadimu, Kitumbatu, Kiunguja, Kingazija na Kiamu.Lahaja za kijamii hizi ni zile lahaja ambazo hutokana na tofauti za kijamii ambazo huweza kusababisha kuwepo kwa matabaka, umri, jinsia, cheo na hadhi.Ifuatayo ni mifano ya misamiati ya lahaja za kiswahili za kijiografia na kijamii pamoja na maana zake katika Kiswahili sanifuLahaja za kijiografia;Lahaja ya Kimtang’ata; hii ni lahaja inayozungumzwa maeneo ya Tanga. Mfano ya misamiati yake ni;
Msamiati katika lahaja ya Kimtang’ata Kiswahili sanifu. Tombo Ziwa Kifugutu Kisu (ki)butu Kuwanga Kuhesabu Mbeko Akiba ya nafaka Uwanda TambarareLahaja ya Kitumbatu; hii ni lahaja inayozunguzwa katika kisiwa cha Tumbatu kaskazini mwa Unguja. Mfano wa misamiati ya lahaja hii ni;
Msamiati katika lahaja ya Kitumbatu Kiswahili sanifu Ulanda Kisu kikali Kifuto Kisu kibutu Agulia Piga bao (ramli) Chuchu Ziwa Yula YuleLahaja ya Kiunguja ni ile lahaja inayozungumzwa katika kisiwa cha Unguja. Mfano wa misamiati ya lahaja hiyo ni;
Msamiati katika lahaja ya Kiuguja Kiswahili sanifu Mbatata Viazi mviringo Tungule Nyanya Mfereji Bomba Maritiki Sokoni Lahaja Kihadimu; hii ni lahaja inayozungumzwa kisiwani Unguja. Mifano ya msamiati wa lahaja hii ni;
Msamiati katika lahaja ya Kihadimu Kiswahili sanifu Kule Mbali Rikacha Pikicha Vacha PachaLahaja za kijamii; hizi ni lahaja zinazotokana na jinsia, umri, matabaka na hadhi ya wazungumzaji. Mfano katika kigezo cha kijinsia wanawake hutumia neno shostina wanaume hutumia neno msela, wote wakiwa na maana ya rafiki katika Kiswahili sanifu.Pia kuna kigezo cha kiumri ambapo tunapata msamiati wa lahaja za kijamii kama vile; demu kwa vijana na binti kwa wazee ambapo wote wakiwa na maana ya msichana katika Kiswahili sanifu.Kwa kuhitimisha lugha ya Kiswahili inazo lahaja nyingi lakini lahaja iliyosanifiwa ni lahaja ya Kiunguja kutokana na kukidhi vigezo. Kutokana na kusanifiwa kwa lahaja hiyo kumesababisha lahaja nyingine kuadhiriwa na hata kudumaa.MAREJEO:King’ei, K. (2010). Misingi ya Isimujamii.Taasisi ya Taaluma za Kiswahili. Chuo Kikuu cha Dar es salaam.Mlacha, S.A.K. na Hurskainen, A. (1995). Lugha, Utamaduni Na Fasihi Simulizi ya Kiswahili. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Idara ya Taaluma za Asia na Afrika na Chuo Kikuu cha Helsinki. TUKIMsanjila, Y.P na wenzake. (2011). Isimujamii: Sekondari na Vyuo. TUKI. Dar es salaam.TUKI, (2004).Kamusi ya Kiswahili Sanifu. (Toleo la Pili). East Africa: Oxford University Press na Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI).
Ulahajia ni nini?
Dhana ya ulahajia inafaa vipi katika kuelezea utendaji wa lugha?
Swali hili limegawanyika katika sehemu ‘a’ na sehemu ‘b’. Na katika kulijibu swali hili tukianza na kipengele ‘a’ tutajadili dhana ya ulahaji kutokana na wataalamu mbalimbali huku tukitoa fasili yetu kwa ujumla. Pia katika kipengele ‘b’ tutajadili kuhusu dhana ya utendi kwa mujibu wa wataalamu, pia tutajadili maana mazungumzo huku tukitoa fasili yetu. Na katika kujadili kiini chetu cha swali tutajadili dhana ya ulahajia jinsi inavyotumika katika kuelezea utendaji wa lugha na mwishoni tutatoa hitimisho la kazi yetu.Dhana ya ulahajia imefasiliwa na wataalamu mbalimbali ambao wameifafanua dhana hii kama ifuatavyo:-Crystal, D (2000) anafasili ulahajia kuwa ni taaluma inayohusu mfumo wa lahaja za kimkoa.Wikipedia wanasema kuwa, ulahajia ni tawi la isimu linalojihusisha na taaluma ya lahaja.Kwa hiyo dhana ya ulahajia hufafanuliwa kuwa ni taaluma inayojihusisha na uchunguzi wa lahaja za kimkoa.Taaluma hii huchunguza utofauti wa lahaja kati ya mkoa mmoja na mkoa mwingine. Zamani taaluma hii ilijikita zaidi katika kufanya uchunguzi kwa wazee walioishi sehemu moja bila kuhama tangia kuzaliwa kwao, lakini kwa sasa taaluma hii uchunguzi wake umejikita zaidi katika maeneo ya mjini kutokana na kuchanganyika kwa makundi ya watu tofauti tofauti kutoka mikoa tofautitofauti.Dhana ya utendi imefafanuliwa na wataalamu mbalimbali ambao wamefasili dhana hii kama ifuatavyo:-Wikipedia wanafasili utendi kuwa ni uzungumzaji wa lugha katika muktadha halisi, nini hasa mzungumzaji husema kwa kuzingatia makosa ya kisarufi.Kwa hiyo utendi huweza kufasiliwa kuwa ni utumiaji wa lugha katika mazingira halisi. Lugha inayotumika lazima iendane na mazingira yaliyopo.Vile vile mazungumzo yamefasiliwa na Oxford (2004) kuwa ni jambo linalojadiliwa na watu au kikundi cha watu kwa lengo fulani. Kwa mfano maongezi.Halliday (1990) anasema mazungumzo huweza kuwa na makosa mbalimbali katika mpangilio wa sentensi au katika mtindo wa matamshi. Vile vile Halliday anasema lugha ya mazungumzo inasifa zake bainifu ambazo ni tofauti na zile sifa za lugha ya maandishi.Kwa hiyo tunaweza kufasili mazungumzo kuwa ni jambo fulani linalojadiliwa na watu wawili au kundi la watu kwa lengo fulani.Baada ya kujadili dhana hizo, sasa tunaweza kujadili ni kwa jinsi gani dhana ya ulahajia inavyoweza kuelezea utendaji wa lugha hususani katika lugha ya mazungumzo kwa kuzingatia lugha ya Kiswahili.Utofauti wa matamshi. Ulahajia huchunguza matamshi ya wazungumzaji wa lugha kutoka mikoa tofauti tofauti. Kwa mfano wazungumzaji kutoka mikoa ya kanda ya ziwa. Mfano wahaya kutoka mkoa wa Kagera katika matamshi yao hawana kitamkwa ng’ kwa hiyo wanapotamka maneno kama vile ng’ombe wao hutamka ngombe, neno ng’ang’ania hutamka ngangania, neno ung’amuzi wao hulitamka kama ungamuzi. Vile vile watu kutoka mkoa wa Mara ambao ni wakurya hutumia kitamkwa r badala ya l kwa mfano neno kula wao hulitamka kura, neno kulala hulitamka kurara, kulalamika wao hulitamka kuraramika. Pia wazungumzaji kutoka mikoa ya kusini mfano kutoka mkoa wa mtwara na lindi ambao ni Wamakonde wao hutumia kitamkwa n badala ya m kwa mfano mtoto hutamka kama ntoto, msichana hutamka kama nsichana, mchana hutamka nchana. Vile vile wazungumzaji kutoka mkoa wa mbeya ambao ni wanyakyusa wao hutamka f badala ya v kwa mfano neno viatu vyangu hutamka kama fiatu fyangu, uvivu hutamka ufifu, viazi hutamka fiasi. Wazungumzaji wa kutoka mikoa ya kaskazini mfano wapare kutoka mkoa wa moshi hutumia kitakmwa th badala ya s kwa mfano badala ya kusema sisi sote ni wasichana wao hutamka thithi thote ni wathichana. Kwa hiyo tofauti hizo za kimatamshi zinatokana na athari za lahaja za mikoa waliyotoka.Msamiati. Dhana ya ulahajia huweza kutumika katika kuchunguza msamiti mbalimbali wa wazungumzaji wa lugha moja kutoka mikoa tofauti tofauti. Kwa mfano watu kutoka Zanzibar wao hutumia msamiati tofauti na wazungumzaji wa mikoa ya bara, kwa mfano husema neno tungule kwa kumaanisha nyanya, neno malikiti humaanisha sokoni, mferejini humaanisha bombani, vile vile kabila la Wamakonde kutoka mkoa Mtwara hutumia neno kumaanika kwa kumaanisha kudharirika, kwa hiyo wazungumzaji hawa hutumia msamiati wa lahaja zao kutokana na athari za lahaja hizo.Muundo wa sentensi, vile vile dhana ya ulahajia huweza kuelezea utendaji wa lugha kwa kuchunguza muundo wa sentensi wa wazungumzaji wa lugha moja, kwa kuchunguza muundo wa sentensi utaweza kubaini kuwa wazungumzaji wa lugha hii wanatokea mkoa gani, kwa mfano wazungumzaji wa mkoa wa Tabora hutumia wingi mahala pa nomino ya umoja wakiashiria heshima. Kwa mfano husema baba wanakuja badala ya kusema baba anakuja, mmefika salama? Badala ya kusema umefika salama?. Kwa hiyo mtu wa heshima kwao hutumia nomino ya wingi na hii yote ni kutokana na kuathiriwa na lahaja za mikoa watokayo.Kiimbo. Ulahajia huweza kuchunguza kupanda na kushuka kwa mawimbi ya sauti ya wazungumzaji wa lugha, kwa mfano kabila la Waluguru kutoka mkoa wa Morogoro wao huzungumza kwa kupandisha na kushusha mawimbi ya sauti. Kwa mfano, “baba amekuja”. kwa hiyo athari hizo zimetokana na lahaja ya mkoa waliotokea.Mkazo, mkazo ni kule kutumia nguvu zaidi katika kutamka maneno au sentensi. Yaani ni hali ya neno au silabi katika neno kusikika kuwa na nguvu zaidi kuliko silabi au maneno mengine. Kwa hiyo ulahajia huweza kuelezea utofauti wa mkazo uliopo katika baadhi ya wazungumzaji wa lugha moja. Kwa mfano kabila la Wasukuma kutoka mkoa wa Mwanza huweka msisitizo katika mazungumzo, kwa mfano “baba anakujaa”, pia wanaongeza vitamkwa ambavyo si vya msingi katika maneno yanayojitosheleaza. kwa mfano neno amekuja wao huongezea kitamkwa ga, = amekujaga, neno ameenda + ga, = ameendaga, hakuna + ga.=hakunaga.Kwa hiyo mtu huweza kuwa na umilisi wa lugha fulani lakini asiwe mtendaji hususani katika lugha ya mazungumzo na hii ni kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuathiriwa na lahaja ya mkoa atokao, athari hizi hujidhihirisha zaidi katika lugha ya mazungumzo kama tulivyojadili hapo juu, lakini katika lugha ya maandishi athari hizi huweza kujidhihirisha kwa kiasi kidogo sana au zisitokee kabisa.Kwa kuhitimisha tunaweza kusema kuwa dhana ya ulahajia huweza kuelezea utendaji wa lugha husasani katika lugha ya mazungumzo kwani ndio rahisi sana kuchunguza tofauti za wazungumzaji wa lugha moja watokao sehemu tofauti tofauti, ambayo ni tofauti sana na kuelezea utendaji wa lugha katika lugha ya maandishi kwani ni vigumu sana kubainisha makosa ya kisarufi kama vile matamshi, kiimbo, mkazo, msamiati na hata muundo wa sentensi. Mara nyingi maandishi huandikwa kwa ufasaha zaidi ukilinganisha na mazungumzo na ndio maana ulahajia huweza kuelezea utendaji wa lugha hususani katika lugha ya mazungumzo.Marejeo;Crystal, D. (2002). The Cambridge of Encyclopedia of Language: Second edition. London. Cambridge University Press.Halliday, M.A.K. (1990). Spoken and Written Language. London. Oxford University Press.Kamusi ya Kiswahili Sanifu, (2004). Nairobi. Oxford University Press.Lugha ya mazungumzo haina muundo rasmi?. Huku ukijikita katika nduni za lugha ya mazungumzo, jadili kauli hii.Katika kujadili swali hili, tutaanza kujadili nini maana ya lugha kwa mujibu wa wataalam mbalimbali, pia tutatoa maana ya lugha ya mazungumzo, maana ya muundo rasmi na hatimaye tutaingia katika kiini cha swali ambapo tutakubaliana na swali kwa kutumia uthibitisho wa nduni (sifa) za lugha ya mazungumzo jinsi zinavyofanya lugha ya mazungumzo isiwe na muundo rasmi. Yaani tutaangalia ni kwa vipi sifa za lugha ya mazungumzo zinavyopelekea lugha ya mazungumzo kukosa sifa ya kuwa na muundo rasmi. Na mwisho tutatoa hitimisho.Massamba (2009) anaeleza kuwa, lugha ni mfumo wa sauti nasibu ambazo zimekubaliwa na jamii kwa madhumuni ya mawasiliano yao.Mgullu (1999) kama alivyomnukuu Trudgil (1974) anafafanua kuwa, lugha ni mfumo wa sauti za nasibu zinazotumiwa kwa mawasiliano miongoni mwa watu wa jamii fulani wenye utamaduni wake.Kwa ujumla tunaweza kusema kwamba, lugha ni mfumo wa sauti nasibu ambazo zimebuniwa na jamii kwa madhumuni ya mawasiliano miongoni mwao.Dhana yingine tuliyoiangalia kulingana na swali hili ni lugha ya mazungumzo. Kwa mujibu wa Wikipedia, wanasema lugha ya mazungumzo ni utaratibu wa kuongea baina ya pande mbili, kwa kawaida wahusika ni watu. Lugha ya mazungumzo huwa na mitindo mbalimbali kama vile rejesta, misimu, jagoni na agoti.Kisha tukaangalia dhana ya muundo, kwa mujibu wa Concise Oxford Dictionary (2001) (toleo la 10) muundo ni mpangilio na uhusiano wa vitu katika kuunda kitu kizima;Katika muktadha wa mazungumzo, muundo rasmi ni ule mpangilio unaohusisha kanuni na taratibu zilizowekwa katika uzungumzaji ambapo kila mzungumzaji hana budi kuzingatia wakati wa mazungumzo.Vilevile tunapozungumzia muundo rasmi katika lugha huangalia mpangilio wa maneno na muundo wa sentensi na namna maneno na sentensi hizo zinavyopangiliwa na kuleta mtiririko wenye maana na uliokamilika na unaoweza kueleweka na watu wote.Kutokana na fasili hii lugha ya mazungumzo haina muundo rasmi, hii ni kwa sababu haizingatii vigezo hivyo wakati wa uzungumzaji na hivyo kuonekana kutokuwa na muundo rasmi na hii ndiyo sifa mojawapo kati ya sifa zinazojidhihirisha katika lugha ya mazungumzo.Hivyo basi tunaweza kuthibitisha kauli hii kwamba, lugha ya mazungumzo haina muundo rasmi kwa kujikita katika sifa au nduni za lugha ya mazungumzo kama ifuatavyo;Kwa mujibu wa King’ei (2010), anaorodhesha sifa zinazojitokeza katika lugha ya mazungumzo ambazo ni kama ifuatavyo;Ubadilikaji wa kila mara wa maudhui, na uteuzi usiotabirika wa maneno, kauli au usemi. Hivyo katika sifa hii tunaona kwamba hakuna muundo rasmi kutokana na kwamba mzungumzaji ana uteuzi wa maneno na kauli zisizotabirika, hivyo anaamua mwenyewe nini cha kusema bila kufuata muundo au kanuni zozote. Mfano anaweza kuanza na aina yoyote ya neno katika sentensi.Utokezaji wa makosa wa aina tofauti katika mazungumzo, mfano kukosea matamshi, kusitasita, kusahau baadhi ya maneno, kuchanganya hoja, wazungumzaji kusema kwa pamoja na hivyo kupoteza uzi au mtiririko sahihi wa mazungumzo. Jambo hili hutokea kutokana na kukosekana kwa muundo rasmi unaowaongoza wazungumzaji. Kimsingi muundo rasmi hufuata kanuni madhubuti na utokeaji wa makosa haupo kwa sababu ya urasmi wake.Pia kuwepo kwa uradidi / marudio na msisitizo kwa wingi katika mazungumzo na pia mazungumzo kukatishwa kwa vichekesho, miguno ama matumizi ya lugha ya ishara, hali hii hutokana na kutokuwepo na muundo maalum unaomwongoza mzungumzaji, ndiyo maana wazungumzaji hujikuta wakirudia rudia maneno wakati wa mazungumzo.Masahihisho ya kila namna na pia ufafanuzi na maelezo hutolewa mara kwa mara pale utata unapotokea. Hii ni kwa sababu ya kutokuwepo kwa muundo maalum kama vile mpangilio wa mawazo, sentensi na mtiririko wa mawazo katika mada ndivyo vinapelekea kutokea kwa utata na kusababisha masahihisho ya mara kwa mara.Matumizi ya sentensi fupi fupi, sentensi za neno moja moja au maneno yasiyokamilika hutokea kwa wingi katika mazungumzo pindi mzungumzaji anapozungumza kwa huweza kutumia sentensi fupi fupi, au kutumia maneno yasiyokamilika. Yote hii hutokana na kutokuwepo kwa muundo rasmi wa lugha ya mazungumzo. Katika hali ya muundo rasmi hauruhusu udondoshaji wa maneno au tungo au matumizi ya sentensi fupifupi ambazo hazijajitosheleza.Msamiati mwepesi na unaofahamika kwa urahisi, pindi mzungumzaji wa lugha anapoongelea mada fulani mbele ya hadhira yake huangalia mandhari pamoja na uhusiano baina yake na wasikilizaji wake, hivyo anaweza kubadilika kulingana na hali halisi anayokutana nayo. Hii haijidhihirishi katika muundo rasmi kama vile lugha ya maandishi, mwandishi hazingatii muktadha au uhusiano baina yake na wasomaji wake, yeye huandika kazi yake bila kujua watakaosoma ni akina nani. Hivyo basi ubadilikaji huu wa msamiati kulingana na hadhira ya mzungumzaji unatuthibitishia kwamba lugha ya mazungumzo haina muundo rasmi.Vilevile kuna uvunjaji wa kanuni za sarufi na matumizi sanifu kutegemeana na uhusiano wa wazungumzaji, katika lugha ya mazungumzo hakuna kanuni ambazo zinamfanya/kumbana mzungumzaji, hivyo basi kwa sababu ya kutokuwepo kwa kanuni hizo ni wazi kwamba lugha hii haitakuwa na muundo rasmi unaomuongoza mzungumzaji ndiyo maana mzungumzaji hujikuta akivunja kanuni. Mfano; mtu anaweka viambishi sehemu ambayo haihitajiki kiambishi kama vile neno nilikuwepo – nilikuwepogi, alimpaga au hakunaga. Pia wapare husema thatha ni thaa thaba kamili wakimaanisha kuwa sasa ni saa saba kamili. Vilevile Wahaya husema ngombe badala ya ng’ombe.Pia katika lugha ya mazungumzo hakuna muda au nafasi ya kufikiria jambo la kuzungumza, hapa mzungumzaji hana muda wa andalio la anachotaka kusema, hutamka tu bila kufikiria jambo analotamka. Jambo hili la kutokuwa na muda wa kujiandaa ndilo hupelekea kutokea kwa miguno na makosa ya kimantiki. Lakini katika muundo rasmi mambo haya huwa hayajitokezi kwa sababu kuna maandalizi ya kutosha.Kwa kuhitimisha tunaweza kusema kuwa, muundo wa lugha ya mazungumzo hauwezi kujidhihirisha moja kwa moja kwa watumia lugha isipokuwa huweza kuhusisha utaratibu fulani unaozingatia mada, muktadha na mahusiano ya wazungumzaji. Aidha hoja inasisitiza kuwa hakuna mada rasmi zilizozoeleka na zinazotumika na watu wote, vivyo hivyo kwa muktadha na mahusiano. Pia lugha hiyo haiwezi kuwa na mpangilio maalum wa kile kinachozungumzwa na maelezo yake kwa wazungumzaji baina yao.MAREJEO:Smith, T. (2001). Concise Oxford English Dictionary. (10th Edt). Oxford University Press. UK.King’ei, K. (2010). Misingi ya Isimujamii. Taasisi ya Taaluma za Kiswahili. Chuo Kikuu cha Dar es salaam.Massamba, D.P.B. (2009). Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha.TUKI, Dar es Salaam.Mgullu, R.S. (1999). Mtalaa wa isimu: Fonetiki, Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili. Longhorn publishers. Ltd. Nairobi
MBINU
MBALIMBALI ZA KUBAINI AU KUTAMBUA FONIMU.
Katika kujadili mada hili sehemu ya kwanza tutajikita katika kuangalia maana ya fonolojia na fonimu kwa mujibu wa wataalamu mbalimbali, katika sehemu ya pili tutaangalia mbinu mbalimbali za kubainisha fonimu kwa mujibu wa wataalamu mbalimbali na sehemu ya tatu tutahitimisha na mwisho marejeo.Kwa kuanza na maana ya fonolojia imejadiliwa na wataalam mbalimbali kama ifutavyo:-Massamba, (2004), Habwe na Karanja (2007) kama walivyomnukuu Ladefoged (1975:23) wanaelekea kuwa na fasili zinazokaribiana kuhusu fonolojia. Wanafafanua kuwa fonolojia ni tawi la isimu ambalo hushughulika na ufafanuzi , uchunguzi na uchanganuzi wa mfumo wa sauti za lugha mahsusi.Hivyo basi tunaweza kusema fonolojia kwa ujumla tunaweza kufasili kama ni nyanja mojawapo ya isimu inayoshughulika na uchambuzi, uchunguzi wa sauti za lugha mahususi kama vile fonolojia ya Kiswahili, Kingereza, Kisafwa na Kihehe.Pia dhana ya fonimu imejadiliwa na wataalamu mbalimbali kama ifuatavyo;Massamba (2004) anasema fonimu ni kipande kidogo kabisa katika mfumo wa sauti za lugha ambacho kina sifa pambanuzi za kuweza kukitofautisha na vipande vingine vya aina yake.Habwe na Karanja, (2007) wanasema kuwa fonimu ni kipashio kidogo kabisa cha sauti katika lugha kinachokuwa na uwezo wa kubadili maana ya neno.Massamba na wenzake (2004) wanaema kuwa fonimu ni kipande sauti ambacho hutumika katika kujenga maneno ya lugha, kwa mfano vitamkwa kama /p/,/b/, /u/, /m/, /t/,/d/,/a/,/k/ na /n/ tunaweza kujenga maneno kama tunda, pumba, taka, muda, dunda, kama na kuta.Hivyo kwa ujumla fonimu tunaweza kufasili kama kipashio kidogo kabisa cha kifonolojia ambacho huwa na uwezo wa kujenga neno mfano /k/, /a/ na /a/ zinajenga neno “kaa,” /t/,/i/ na /a/-zinajenga neno “tia” au kubadili maana ya neno moja na nyingine mfano pia, bia,tia, kata,pata na bata,hivyo fonimu /p/, /b/, /t/ na /k/ zinabadili maana ya neno moja na jingine.Wataalamu mbalimbali wamebainisha mbinu mbalimbali za kubainisha fonimu, mbinu hizo ni kama zifuatazo:-Mgawanyo wa kimtoano au mgawanyo kamilishani, Mgullu (1999) akimnukuu Hyman (1975) anaeleza utoano kuwa ni dhana ambayo hutumiwa kuelezea uhusiano uliopo baina ya sauti mbili au zaidi za fonimu moja ambazo haziwezi kutokea katika mazingira sawa, hii ina maana ya kwamba kila sauti huwa na mazingira yake maalumu ya utokeaji ambayo hayawezi kukaliwa na sauti nyingine,kwa mfano kutoka lugha ya Kiingereza sauti /ph/ yenye mpumuo na /p/ isiyo na mpumuo haziwezi kutokea katika mazingira yanayofanana mfano tunaona kuwa /ph/ yenye mpumuo mara zote hutokea mwanzoni mwa maneno tu kwa mfano /put/, /pin/ na /pen/ na /p/ isiyokuwa na mpumuo hutokea sehemu nyingine yoyote katika neno isipokuwa mwanzoni mwa neno, kwa mfano /spell/na /spin/.Pia mbinu hii imeungwa mkono na Massamba (2010) akimnukuu Hocket (1958) anasema kwamba sauti mbili zinaweza kuwakilisha fonimu zinazofanana kama zitakua na mazingira tofauti ya utokeaji, sauti zinazotokea katika mgawanyo kamilishani hujulikana kama alofoni za fonimu moja. Mfano kutoka lugha ya Ci-Ruuri:Imbusi “mbuzi”Oguβusi “mbuzi mkubwa”Imbogo “nyati”oguβogo “nyati kubwa”Kutokana na mifano ya maneno hayo, tunaona kuwa fonimu /b/ na /β/ hugawana mazingira ya utokeaji, sehemu ambapo /b/ hutokea, /β/ haiwezi kutokea, huwa /β/ hutokea katikati ya irabu na mahala pengine popote, wakati /b/ hutokea tu pale inapokuwa imetanguliwa na nazali kama vile /m/.Mpishano huru , kwa mujibu wa Mgullu (1999) akimnukuu Martinent anaeleza kuwa dhana ya mpishano huru ni maneno mawili yanayoweza kuwa na tofauti ya fonimu moja tu lakini tunapozitazama fonimu hizo zilizotofauti, tunaona wazi kuwa kwanza fonimu hizo ni tofauti sana Kifonetiki au haziwezi kuwa alofoni za fonimu moja, pia tunaona kwamba fonimu hizo zilizotofauti kifonetiki hazipo katika ule uhusiano wa kimtoano, yaani zote zinaweza kutumika katika mazingira yaleyale kwenye neno lakini fonimu hizo ingawa ni tofauti hazisababishi tofauti za maneno katika maneno zinamotokea yaani kila moja inaweza kutumiwa badala ya nyingine (katika maneno maalumu) bila kubadili maana katika maneno hayo.Mifano:Alimradi ilimradi /a/ na /i/Baibui buibui /a/ na /u/Amkia amkua /i/ na /u/Bawabu bawaba /a/ na /u/Wasia wosia /a/ na /o/Benua binua /e/ na /i/Heri kheri /h/ na /kh/ au /x/.Mfanano wa kifonetiki, Mgullu (1999) akimnukuu Jones (1957) anaeleza kuwa fonimu fulani katika lugha fulani huwa ni ujumuisho wa udhahanishaji wa sauti kadhaa au tuseme kundi la sauti zinazofanana sana kifonetiki ni sauti zilizo na sifa bainifu zinazofanana. Kwa mfano irabu huwa na sifa zake bainifu ambazo ni tofauti na konsonanti, mfano irabu /i/ na /u/ hatuwezi kusema kuwa ni fonimu moja kwa sababu sauti hizi zinatofautiana sana kifonetiki, kwa hiyo hizi ni fonimu mbili tofauti.Mfano;/i/ /u/+ irabu +irabu+mbele +nyuma+juu +juu-mviringo +mviringoHivyo irabu /i/ na /u/ zinafanana tu katika sifa mbili ambapo zote ni irabu na zote ni irabu za juu na zinatofautiana katika sifa mbili ambapo irabu /i/ ni irabu ya mbele si viringe na irabu /u/ ni irabu ya nyuma viringe. Hivyo hatuwezi kusema zinafanana kifonetiki kutokana na kutofautian kwa baadhi ya sifa bainifu.Besha (2007) anasema kuwa uainishaji wa fonimu tunaangalia mfanano wa kifonetiki. Anasema kuchanganua mifumo ya sauti za lugha mbalimbali mfanano wa kifonetiki kati ya sauti ni muhimu sana kwa vile mahusiano ya kifonetiki, kanuni pamoja na minyumbuo yote inategemea katika sifa hii kuainisha sauti za lugha ili kugundua zipi ni fonimu za lugha hiyo pamoja na alofoni zake. Umuhimu huwekwa katika kuangalia uhusiano uliopo katika makundi ya sauti kufuatana na mahali pa kutamkia na namna za utamkaji , makundi makubwa yanayohusiana sana ni matatu ambayo ni Vipasuo, vikwamizi na ving’ong’o,ndani ya makundi haya umuhimu mkubwa huwekwa katika mahali pa kutamkia . Hivyo basi mifano inayotolewa na wataalamu mbalimbali haibainishi mfanano wa kifonetiki kwani sifa za kila sauti zinatofautiana na nyingine, sifa kuu ya mfanano wa kifonetiki ni lazima sauti hizo zifanane kwa sifa zote.Jozi sahili / jozi ya mlinganuo finyu, kwa mujibu wa mgullu (1999) kama alivyomnukuu Fischer (1975) anasema mlinganuo finyu ni tofauti ndogo kabisa ya kifonolojia iliyopo baina ya maneno fulani,aghalabu maneno hayo huwa yana idadi sawa za fonimu, fonimu zinazofanana isipokuwa fonimu moja na mpangilio wa fonimu ulio sawa.Katika lugha ya kiswahili maneno kama /pia/ na /tia/ ni mfano wa mlinganuo finyu kwa sababu idadi ya fonimu ni sawa, aina ya fonimu zilizopo ni zilezile isipokuwa moja, maneno yote yana /a/ na /i/ isipokua tofauti katika fonimu /p/ na /t/ na mpangilio wa sauti ni sawa ambapo /p/ na /t/ zipo mwanzoni mwa neno zikifatiwa na irabu /a/ na irabu /u/.Pia kutoka lugha ya kiswahili maneno kamapata na batakata na katidua na tuaKatika maneno haya fonimu /p/, /b/, /a/, /i/,/d/ na /t/ ndio zinazotofautisha maana za maneno baina ya neno moja na jingine. Mbinu hii pia imeungwa mkono na wataalamu wengine kama Besha (2007) na Massamba (2010) kwani wametoa maelezo yao na mifano inayofanana sana na ya Mgullu (1999) alivyonukuu kutoka kwa Fischer (1975)Kwa kuhitimisha,ni vigumu kubainisha fonimu kwa kutumia mbinu moja, hivyo basi ni vyema fonimu zikabainishwa kwa kujumuisha mbinu zote kama zilivyobainishwa na wataalam mbalimbali ili kuweza kupata mbinu moja ambayo ni sahihi katika kubaini fonimu.MarejeoBesha, R.M. (2007) Utangulizi wa Lugha na Isimu.Macmillan Aidan L.t.d: Dar es Salaam.Habwe, J. na Karanja, P (2007) Misingi ya Sarufi ya Kiswahili.Phoenix: NairobiMassamba, D.P.B (2004) Phonological Theory: History and Development. TUKI: Dar es SalaamMassamba, D.P.B (2010) Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha. TUKI: Dar es SalaamMassamba, D.P.B na wenzake (2004) Fonolojia ya Kiswahili Sanifu (FOKISA). TUKI: Dar es Salaam.Mgullu, S.R. (1999), Mtalaa wa Isimu.Longhorn:Nairobi
KWA KUWA MSAMIATI MWINGI ULIOPO KATIKA LUGHA YA KISWAHILI UNATOKANA NA LUGHA YA KIARABU NI DHAHIRI KUWA LUGHA HII INATOKANA NA KIARABU. JADILI.
Katika kujadili swali hili tutaanza na utangulizi kwa kueleza maana ya asili, maana ya msamiati na baada ya hapo tutaangalia jinsi kigezo cha msamiati kinavyotumiwa kudai kuwa Kiswahili ni kiarabu na tutaonesha udhaifu wake na mwisho tutakanusha madai haya kwa kuonesha kuwa Kiswahili ni kibantu na sio kiarabu.Mjadala kuhusu asili ya Kiswahili umejadiliwa na wataalam mbalimbali na wametumia vigezo mbalimbali kuthibitisha madai yao. Wapo wanaodai kuwa Kiswahili ni kiarabu, wanaoshadidia dai hili, kigezo kimojawapo wanchokitumia ni kigezo cha msamiati, kwamba lugha ya Kiswahili ina msamiati mwingi wa kiarabu na kwa hiyo kwa kuwa Kiswahili kina msamiati mwingi wa kiarabu basi pia Kiswahili ni kiarabu, kwa kweli dai hili halina mashiko. Kabla hatujaanza kufafanua kwamba kwa nini dai hili halina mashiko ni vema tukaangalia fasili ya dhana muhimu kama zinavyojitokeza katika swali la mjadala. Dhana hizo ni kama zifuatazo:‘Istilahi asili,’ kwa mujibu wa Massamba na wenzake (1999) asili ni jinsi kitu au jambo lilivyotokea au lilivyoanza. Fasili hii ni nzuri na inajitosheleza kwa maana kwamba jambo au kitu kinaweza kutokea kibahati kama ilivyo katika lugha au linaweza kuanzishwa.Msamiati pia unaelezwa na TUKI (2004) kuwa ni jumla ya maneno katika lugha. Fasili hii iko wazi kwamba jumla ya maneno yote katika lugha ndio huunda msamiati wa lugha husika.Wataalam wanaodai kuwa Kiswahili ni kiarabu kwa kutumia kigezo cha msamiati, hoja zao ni kama zifuatazo:Khalid (2005) anasema kuwa neno lenyewe Kiswahili limetokana na neno la kiarabu sahil katika umoja ambalo wingi wake ni sawahili likiwa na maana ya pwani au upwa. Hivyo kutoka na jina la lugha hii ya Kiswahili kuwa na asili ya neno la kiarabu sahil hivyo hudai kuwa Kiswahili ni kiarabu.Khalid anaendelea kusema kuwa Kiswahili kina msamiati mwingi wenye asili ya kiarabu. Hapa ni baadhi ya mifano ya msamiati wa Kiswahili wenye asili ya kiarabu kama alivyobainisha Khalid:Maneno yanayoonesha muda.Asubuhi dakikaWakati alfajiriKarne alasiriMagharibi saaManeno yanayowakilisha namba.Nusu roboSita sabaTisa ishiriniThelathini arubainiHamsini sitiniSabini themaniniTisini miaElfuMtandao wa jamiiforum pia wameonesha mifano ya msamiati wa Kiswahili wenye asili ya kiarabu kama ifuatavyo:Kiswahili KiarabuDirisha drishaKaratasi kartasiDebe dabbaSamaki samakMustakabali mustakabalMadrasa madrasaLodh (2000) naye anasema kiasi kikubwa cha nomino za Kiswahili zimetokana na mizizi ya maneno ya kiarabu. Mifano ya maneno hayo ni kama yafuatayo:Hesabu/hisabu mahisabu/hisabatiHarka harakatiSafiri - msafiriSafari - msafaraFikiri - fikara/fikraHata hivyo kigezo hiki cha msamiati kina udhaifu; Massamba (2002) ameonesha udhaifu wa kigezo hiki kuwa ni pamoja na kwamba:Hakuna ushahidi wowote wa kitakwimu ambao unaonesha idadi ya maneno ya kiarabu yaliyopo katika lugha ya Kiswahili yanayoweza kuhitimisha kuwa Kiswahili ni kiarabu.Kigezo cha msamiati peke yake hakijitoshelezi kuelezea kuwa Kiswahili ni kiarabu, walipaswa waangalie vigezo vingine kama vile kigezo cha kihistoria kwa kuchunguza masimulizi mbalimbali ya kale na kigezo cha kiisimu; katika kigezo hiki walipaswa kuchunguza fonolojia, mofolojia , na sintaksia ya Kiswahili kwa kulinganisha na kiarabu na ndipo wangepata hitimisho sahihi la madai yao.Vilevile kigezo hiki cha msamiati hakina mashiko kwa sababu lugha ina tabia ya kuathiriana, lugha huathiriana na lugha nyingine endapo kutakuwa na mwingiliano baina ya wanajamii lugha hizo. Kwa mfano Kiswahili kimetokea kuathiriana na kiarabu kutokana na uhusiano uliokuwepo hapo zamani katika biashara kati ya waarabu na watu wa upwa wa Afrika Mashariki na hii ikapelekea msamiatia wa kiarabu kuingia katika lugha ya Kiswahili, hivyo kwa hoja hii hatuwezi kusema Kiswahili ni kiarabu kwa sababu msamiati wa kiarabu unaonekana katika lugha ya Kiswahili.Hata hivyo si lugha ya kiarabu tu ambayo msamiati wake unaonekana katika lugha ya Kiswahili vilevile kunamsamiati wa lugha zingine za kigeni katika lugha ya Kiswahili kwa mfano, neno lenye asili ya kireno katika Kiswahili ni kama vile meza, leso pia yapo maneno yenye asili ya kijerumani kwa mfano schule kwa Kiswahili shule na maneno yenye asli ya kiingereza ni kama vile mashine, televisheni, sekondari, redio, kompyuta na maneno mengine yenye asli hiyo. Basi ingekuwa msamiati wa kigeni kuonekane kwenye lugha fulani huifanya hiyo lugha kuwa na asili ya lugha ya kigeni basi tungesema pia Kiswahili ni kiingereza kwa sababu tu msamiati mwingi wa kiingereza unonekana katika Kiswahili.Pia kigezo hiki kinaonekana kuwa ni dhaifu kwa sababu hawakufanya utafiti katika nyanja zote za matumizi ya lugha kwa mfano msamiti unaotumika katika nyanja ya elimu, afya, utamaduni na kadhalika. Kwa hiyo madai haya yanaonekana kutokuwa na mashiko kwa ufinyu wa utafiti wake.Kutoka na kigezo hiki cha msamiati kutokuwa na mashiko kuhitimisha kuwa Kiswahili ni kiarabu, basi hatuna budi kusema kuwa Kiswahili sio kiarabu bali ni kibantu. Katika kuthibitisha madai haya tutajikita zaidi katika kigezo cha kiisimu ambacho tunaamini kuwa ni kigezo pekee kinachoweza kutupatia taarifa sahihi kwani ni kigezo cha kisayansi lakini pia tutaangalia kwa ufupi vigezo ambavyo vinatoa ushahidi juu ya ubantu wa Kiswahili ambavyo ni ushahidi wa kihistoria, kiakiolojia na kiethinolojia.Kigezo hiki cha kiisimu kimetumiwa na wataalam mbalimbali katika kuonesha ubantu wa Kiswahili Massamba (ameshatajwa) amewataja wataalam mbalimbali ambao wamehusika na utafiti juu ya ubantu wa Kiswahili, wataalam hao ni pamoja na Carl Meinhof katika kitabu chake cha Introduction to the phonology of the Bantu language, Duke (1935 – 1945), Malcom Guthrie (1967), Dereck Nurse na Thomas Spear (1985). Hawa walijadili ubantu wa Kiswahili kwa kutumia kigezo cha kiisimu, kihistoria na kiakiolojia.Kwa kuanza na kigezo cha kiisimu tutaangalia vipengele kama vile kufanana kwa msamiati wa msingi, muundo wa kifonolojia, muundo wa kimofolojia, muundo wa kisintaksia mpangilio wa ngeli za majina.Mizizi ya msamiati wa msingi wa lugha za kibantu na Kiswahili hufanana kwa kiasi kikubwa, mifano ifuatayo huweza kuonesha ukweli huu.Mfano,
Kiswahili Kikurya Kinyiha Kijita Maji Amanche Aminzi Amanji Jicho Iriso Iryinso ElisoKatika mifano hiyo hapo juu tunaona mifano hiyo hapo juu tunaona kuwa mizizi maji, manche, minzi, manji inafanana kwa kiasi kikubwa, kwa hiyo huu ni ushahidi tosha kutuonesha kuwa kuna uhusiano wa kinasaba kati ya Kiswahili na lugha za kibantu.Pia mofolojia ya Kiswahili na lugha za kibantu hufanana kwa kiasi kikubwa, yaani mfumo wa maumbo ya maneno ya lugha ya Kiswahili na lugha za kibatu hufanana. Kwa mfano, namna viambishi vinavyopachikwa katika mzizi wa maneno hufuata kanuni ileile kama inavyotumika katika lugha ya Kiswahili yaani viambishi vinaweza kupachikwa kabla au baada ya mzizi na uwa na uamilifu bayana. Hebu tuchunguze mifano ifuatayo:
Kiswahili Kisukuma Kisimbiti Kinyiha A-na-lim-a a-le-lem-a a-ra-rem-a i-nku-lim-a a-na-chek-a A-le-sek-a a-ra-sek-a a-ku-sek-aKwa kuangalia mifano hii utagundua kwamba katika kutenganisha viambishi hufuata kanuni moja kwamba mahali kinapokaa kiambishi kwa mfano cha njeo, ndipo pia hukaa kwa upande wa lugha za kibantu, kwa mfano –na- na –ra- katika lugha ya kisimbiti. Hivyo tunaweza kusema kuwa kuna unasaba baina ya lugha hizi.Vilevile sintaksia ya lugha ya Kiswahili na lugha za kibantu hufanana kwa karibu sana. Kwa mfano jinsi ya mpangilio wa vipashio na kuunda sentensi hufanana yaani mpangilio wa maneno hufuata kanuni maalum ambazo hufanana katika Kiswahili na lugha za kibantu. Katika Kiswahili sentesi ina kuwa na pande mbili yaani upande wa kiima na upande wa kiarifu, katika upande wa kiima kipashio chake kikuu ni nomino na katika upande wa kiarifu kipashio chake kikuu ni kietnzi. Hii inamaana kwamba katika kuunda sentensi ni lazima nomino ianze na baadaye kitenzi. Hebu tuangalie mifano ifuatayo:
Kiswahili Mama / anakulaN (K) T (A) Kijita Mai / kalyaN(K) T (A) Kihehe Mama/ ilyaN(K) T(A) Kihaya Mama / nalyaN(K) T(A)Katika mifano hii tumeona kwamba muunndo wa kiima-kiarifu katika lugha za kibantu unafanana sana na ule wa Kiswahili yaani nomino hukaa upande wwa kiima halikadhalika kitenzi hukaa upande wa kiarifu, kwa hiyo kwa mifano hii tunaweza kusema kuwa lugha ya Kiswahili ni jamii ya lugha za kibantu.Pia mfumo wa sauti (fonolojia) wa lugha za kibantu unafana sana na ule wa Kiswahili, yaani mpangilio wa sauti katika kuunda silabi, na miundo ya silabi kwa ujumla hufanana. Kwa mfano katika lugha ya Kiswahili hakuna muundo wa silabi funge yaani silabi ambayo inaishia na konsonanti, muundo asilia wa silabi za Kiswahili ni ule unaoishia na irabu vilevile katika lugha za kibantu hufuata muundo wa silabi wazi, yaani silabi zote huishia na irabu. Mifano ifuatayo hufafanua zaidi:
Kisawhili Baba K+I+K+I Kikurya Tata K+I+K+I Kiha Data K+I+K+I Kijita Rata K+I+K+I Kipare Vava K+I+K+ITanbihi: K= konsonanti I= irabu.Kwa mifano hii tunaona kwamba mifumo ya sauti katika lugha za kibantu hufanana na ule wa Kiswahili, kwa hiyo tunaweza kuhitimisha kwa kusema kuwa lugha hizi ni za familia moja.Pia vilevile mfumo wa ngeli za majina katika lugha ya Kiswahili hufanana sana na ule wa kibantu hususani katika upachikaji wa maumbo ya umoja na wingi na maumbo ya upatanisho wa kisarufi. Katika lugha ya Kiswahili viambishi vya umoja na wingi hupachikwa mwanzoni kabla ya mzizi wa neno, hivyohivyo katika lugha za kibantu. Kwa mfano:
Umoja Wingi Kiswahili m-tu wa-tu Kikurya mo-nto abha-nto Kiha umu-ntu abha-ntu Kikwaya mu-nu abha-nuMifano hiyo hapo juu inadhihirisha wazi kwamba vipashio vyote vya umoja na wingi hujitokeza kabla ya mzizi wa neno, hivyo ni dhahiri lugha hizi zina uhusiano wa nasaba moja.Vilevile katika upatanisho wa kisarufi lugha za kibantu na Kiswahili huelekea kufanana viambishi vya upatanisho wa kisarufi hususani viambisha vya nafsi.Kwa mfano:
Kiswahili Mtoto a-nalia Kizanaki Umwana a-rarira Kisukuma Ng’wana a-lelela Kikurya Omona a-rakuraTunaona hapo juu kwamba kiambishi ‘a’ cha upatanisho wa kisarufi hujitokeza katika lugha zote, hivyo tunashawishika kusema kuwa Kiswahili kina uhusiano mkubwa na kibantu.Pamoja na ushahidi wa kiisimu kutupatia vithibitisho tosha juu ya ubantu wa Kiswahili pia kuna ushahidi mwingine kama vile ushahidi wa kihistoria, kiakiolojia na kiethinolojia.Ushahidi wa kihistoria huchunguza masimulizi na vitabu mbalimbali vya kale ambavyo huelezea asili na chimbuko la wakazi wa upwa wa Afrika Mashariki. Vilevile ugunduzi wa kiakiolojia huonesha kuwa kulikuwa na wakazi wa asili wa upwa wa Afrika Mashariki ambao walikuwa na utamaduni wao na maendeleo yao hata kabla ya kuja kwa wageni. Katika ushahidi wa kiethinolojia, huchunguzwa tarihi mbalimbali zinazojaribu kutoa historia ya watu pwani ya Afrika Mashariki na lugha yao.Kwa ujumla vyanzo hivi vyote huonesha kuwa pwani ya Afrika mashariki ilikuwa na wakazi wake wa asili ambao walikuwa na lugha yao, utamaduni wao na pia maendeleo yao, vyanzo hivi pia huhitimisha kwa kusema kuwa lugha ya wakazi hawa ilikuwa ni Kiswahili.Kwa hiyo, kwa hoja hizi tunaweza kuhitimisha kwa kusema kuwa, madai ya kusema kwamba msamiati mwingi wa kiarabu katika lugha ya Kiswahili hayana mashiko; Kwani hakuna ushahidi wa kutosha kusimamia hoja hiyo. Kama ilvyojadiliwa hapo juu,vigezo vya kiisimu, kihistoria, kiakiolojia na kiethnolojia ndivyo vitoavyo ushahidi wa kina na kutoa hoja za mashiko kuthibitisha kuwa Kiswahili sio kiarabu na bali ni kibantu.MAREJEO.Khalid (2005) “Swahili words of Arabic origin” katikaLodh, A.Y (2000) Oriental influences in Swahili: A study in language. Götenbog. Sweden.Massamba, D.P.B na wenzake (1999) Sarufi miundo ya Kiswahili Sanifu. TUKI. Dar es salaam.Massamba, D.P.B (2002) Historia ya Kiswahili 50BK hadi 1500BK. The Jomo Kenyatta Foundation.TUKI (2004) kamusi ya Kiswahili sanifu. TUKI. Dar es salaam.
TOFAUTI KATI YA NYANJA ZA ISIMU NA MATAWI YA ISIMU KATIKA KISWAHILI.
Katika makala hii tutaangalia kwa kifupi maana ya Isimu, maana ya nyanja za Isimu, maana ya Matawi ya Isimu kisha tutaeleza tofauti za nyanja za isimu na matawi ya Isimu.
Wataalamu mbalimbali wanajaribu kueleza maana ya isimu kama ifuatavyo; Mgullu, (2010) kama alivyomnukuu Richard na wenzake (1985) anasema kuwa isimu ni mtalaa ambao huchunguza lugha kama mfumo wa mawasiliano ya wanadamu.
Habwe, J na P. Karanja, wanasema kuwa katika lugha isimu ni taaluma inayochunguza lugha ya mwanadamu kisayansi.
Msanjila na wenzake (2011) wanasema kuwa isimu ni taaluma ya sayansi ya lugha inayoshughulika na nadharia, uchunguzi na uchambuzi wa vipengele mbalimbali vya lugha.
Kwa ujumla, tunaweza kufasili isimu kuwa ni taaluma ya kuchunguza lugha ya binadamu kisayansi, usayansi wa uchunguzi huu unajitokeza kwa sababu hufuata sifa za kisayansi ambazo ni utoshelevu wa kiuteuzi, utoshelevu wa kiuchunguzi, kiufafanuzi, uchechefu na uwazi.
Baada ya kuona maana ya Isimu, sasa tueleze kwa kifipi maana ya Nyanja. TUKI (2004) Kamusi Sanifu ya Kiswahili, inasema kwamba Nyanja ni wingi wa uwanja, ambapo uwanja ni maeneo ya fani za kitaaluma. Hivyo tunaweza kusema Nyanja za isimu ni taratibu zinazomwezesha mtu kujua lugha au ni taarifa ya lugha. mfano; fonolojia, mofolojia, sintaksia na semantiki.
Besha, R. (2004) anasema matawi ni tanzu za kiisimu zinazotumika katika kufafanua lugha, mfano; Isimu fafanuzi, Isimu jamii, Isimu Linganishi, Isimu Nadharia, Isimu Historia, Isimu Kompyuta, Isimu Nurolojia, Isimu Nafsia, Isimu Hisabati na Isimu tumizi. Hivyo matawi ya Isimu ni mikabala inayochanganua sayansi ya lugha.
Zipo tofauti mbalimbali baina ya Nyanja za Isimu na Matawi ya Isimu. Tofauti hizo ni kama ifuatavyo;
Maana: maana za Nyanja na Matawi ya Isimu zinatofautiana. Kwani Nyanja za Isimu ni fani za kitaalima au uwanja unaomwezesha mtu kujua lugha au maarifa ya lugha. Mfano; fonolojia, mofolojia, sintaksia, na pragmatiki. Wakati Matawi ya Isimu ni kama tanzu za tanzu za Isimu zinazotumika katika kufafanua lugha. Kwa mfano; Isimu fafanuzi, Isimu Jamii, Nafsia, Hisabati, Kompyuta na Nurolojia nk.
Idadi: idadi ya Nyanja za Isimu ni chache na zijulikana kwani zipo tano “5” ambazo ni fonolojia, mofolojia, sintaksia, semantiki na pragmatiki. Wakati matawi ya Isimu ni mengi, hayana idadi maalum. Mfano; Isimu jamii, Isimu Nadharia, Kompyuta, Historia, Isimu Falsafa, nk. Hutegemea ubunifu, udadisi katika uainisho wa wanaisimu.
Malengo: malengo ya Nyanja za Isimu ni kumwezesha mtumiaji wa lugha fulani kujua kanuni na taratibu za utumiaji wa lugha husika. Mfano; maumbo, miundo, matamshi, na maana, wakati Matawi ya Isimu yanalengo la kuchunguza, kuchambua na kufafanua lugha kulingana na tawi husika;- mfano Isimu jamii huchunguza uhusiano uliopo kati ya lugha na jamii husika. Isimu nafsia huelezea jinsi binadamu anavyojifunza lugha. Isimu kiafrika imejikita katika kuchunguza lugha mbalimbali zinazozungumzwa barani Afrika.
Utegemezi: hatuwezi kujifunza matawi ya Isimu bila kuwa na ujuzi wa Nyanja za Isimu Ila tunaweza kujifunza Nyanja za Isimu bila kuwa na ujuzi wa Matawi ya Isimu. Wakati matawi ya Isimu hutegemea Nyanja za Isimu ili kuweza kufafanua lugha mfano Isimu fafanuzi inategemea uwepo wa Nyanja za Isimu; kama vile fonolojia, mofolojia, sintaksia, semantiki na pragmatiki ili uweze kufafanua lugha husika katika vipengele hivyo.
Ujifunzaji Umilisi au Umahiri: Nyanja za Isimu kujifunza kwake hutegemea kawaida za jamii juu ya kanuni na taratibu za utumizi wa lugha husika. Mfano;
Kiswahili: Msichana mzuri. N V Kiingereza : Beautiful
girls P N
Hivyo tunaona katika Kiswahili nomino huweza kutangulia kivumishi, ni kawaida za jamii ya waswahili na taratibu zao zinazoitofautisha na jamii vyingine kama zile za kizungu zinazoweza kuruhusu kivumishi kiwe kabla ya nomino. Wakati matawi ya Isimu ujifunzaji, umilisi na hatimaye umahiri watasnia ya matawi mbalimbali ya Isimu hutegemea udadisi na ubunifu binafsi wa mhusika/mchunguzi. Mara nyingine huwa hakuna uhusiano wa moja kwa moja kwa baadhi ya matawi baina ya jamii na tawi husika ambalo mdadisi hudadisi. Mfano; Isimu Kompyuta na Kiswahili.
Mpangilio wa kingazi: Nyanja za Isimu ziko katika mpangilio wa kingazi yaani kuanzia fonolojia mpaka pragmatiki na zote hutegemeana, huhusiana na hukamilishana kuanzia ngazi ya chini kabisa mpaka ngazi ya juu kabisa.
Hivyo tunaona kwamba fonolojia, mofolojia, sintaksia, semantiki na pragmatiki ni taaluma zinazotawala msingi wa lugha mahususi na hizi ndizo Nyanja za Isimu. Nyanja za Isimu na Matawi ya Isimu vinauhusiano ambao unatimiliza kukamilishana baina yake. Kwa mfano;
Mofolojia inahusiana na Isimu changanuzi kwani zote huchunguza maumbo ya maneno. Kwa mfano neon a-na-pig-a. Sintaksia inahusiana na Isimu fafanuzi kwani zote huangalia muundo wa sentensi katika lugha. Semantiki na Pragmatiki zinauhusiano na Isimu jamii kwani zote huangalia jinsi lugha inavyotumika, nani amesema, kwa nini, wakati gani, juu ya nini. Maswali haya yote hushughulikiwa na Semantiki, Pragmatiki na Isimu jamii.
Dhana ya fonimu ni dhana ambayo imejadiliwa na wataalamu mbalimbali wakitumia mitazamo tofauti tofauti. Wataalamu wafuatao wameeleza maana ya fonimu:-
Massamba, (2004) anasema fonimu ni kipande kidogo kabisa katika mfumo wa sauti za lugha ambacho kina sifa pambanuzi kuweza kukitofautisha na vipande vingine vya aina yake. Sauti pambanuzi katika mfumo wa lugha.
Massamba na wenzake, (2004) wanasema fonimu ni kitamkwa kilicho bainifu katika lugha fulani maalumu.
Mgullu, akimnukuu Jones, (1975) anaeleza kuwa Fonimu ni kundi la sauti katika lugha fulani, lenye sauti muhimu (phonemes) pamoja na sauti zinazohusiana na ambazo hutumiwa mahali peke katika muktadha maalumu.
Tunaweza kusema kuwa wataalamu hawa wametofautiana katika kuelezea dhana nzima ya fonimu, wakati Massamba (2004), anasema fonimu ni kipande kidogo kabisa katika mfumo wa sauti za lugha, Jones (1975) akinukuliwa na Mgullu anasema kuwa fonimu ni kundi la sauti katika lugha fulani.
Hivyo tunaweza kusema kuwa fonimu kipashio kidogo cha kifonolojia kinachoweza kubadili maana ya neno katika lugha fulani (mahususi). Kwa mfano pata – baba.
Dhana ya fonimu kuvuka mipaka na kuingia katika fonimu nyingine ni pale fonimu fulani inapoliacha umbo lake la asilia na kuingia katika umbo jingine. Dhana hii imenukuliwa na Massamba (2010) kutoka kwa mtaalamu Bloch (1941).
Bloch (1941) anashawishi kwa kiasi kikubwa kuwa fonimu kuvuka mipaka ni tukio la kawaida katika lugha ya asili kutokana na ushahidi kuwa alofoni za fonimu moja zinaweza kutofautiana kwa kiasi kikubwa kifonetiki. Wakati mwingine zinakuwa na uhusiano na alofoni za fonimu nyingine tofauti na fonimu zilimotokea. Vile vile kifonetiki, sauti fulani inaweza kutokea kuwa katika fonimu mbili au zaidi katika lugha moja. Anaendelea kusema kuwa kuna aina mbili za fonimu kuvuka mipaka ambazo ni:-
Uvukaji mipaka usiokamili, unaamanisha hali ya fonimu ya aina moja kutokea katika fonimu mbili katika mazingira ya hali tofauti.
Kwa mfano:Udogo Ulimi LoaUndugu Ndimi NdoanaNduguHivyo katika Kiswahili sauti /d/ hujitokeza kama /d/ wakati mwingine huvuka mipaka na kuwa /l/. Sauti /l/ huwa /d/ endapo inatanguliwa na nazali /n/. Endapo tutajikita kifonetiki ni ngumu kutabiri /d/ kama ni alofoni ya fonimu /d/ au fonimu /l/ itakuwa rahisi.Mfano mwingine wa Kiswahili ni pale:Ki + ti = ki+eusi (kiti cheusi) katika mifano ya Kiswahili tutaona mabadiliko ya kifonimu yakijitokeza katika mfano wa fonimu /k/ inapofuatiwa na irabu halafu kuwa katika mpaka wa mofimu kisha ikafuatiwa na irabu /e/ hubadilika na kuwa /ch/ yaani (ki+eusi) = cheusi.Mfano mwingine katika Kiswahili ni:-N + buzi (mbuzi) /n/ inakuwa /m/ ikifuatiwa na /b/N+dama (ndama) /n/ inabakia kuwa /n/ ikifuatiwa na /d/N+gombe (ng’ombe) /n/ inabadilika na kuwa /n’g/Pia tunaona kuwa nazali /n/ inapofuatiwa na kitamkwa /b/ hubadilika na kuwa /m/ inapofuatiwa na kitamkwa /d/ hubakia kuwa /n/ inapofuatiwa na kitamkwa /g/ hubadilika na kuwa [ ŋ ]. Hii inamaana kuwa katika mazingira haya sauti /m/, /n/ na [ŋ] ni alofoni za fonimu /N/Uvukaji wa mipaka uliokamili. Huu ni uvukaji wa mipaka wa sauti moja kwenda sauti nyingine katika mazingira ya aina moja.Kwa mfano:-Katika lugha ya kiingereza uvukaji wa mipaka uliokamili unahusisha fonimu /t/ na /d/ inapotokea katikati ya irabu. Wamarekani hutamka sawa sauti ya ufizi [d].Mfano:- Butter, Betting, Kitty ukiyatofautisha na Budden, Bedding, Kiddy katika mifano yote hiyo fonimu /t/ na /d/ hutamkwa sawa.Kwa mfano:- /betting/ - [ beDiŋ] na /bedding/ = [beDiŋ]. Unapotamka haya maneno hautamki moja kwa moja /d/ wala /t/ bali inakuwa sauti katikati ya /t/ na /d/. Kwa msingi huo fonimu /t/ na /d/ hupoteza uhalisia wake katika matamshi. Baada ya ule uhalisia kupotea sauti inayokuja huziwakilisha haizitofautishi sauti /t/ na /d/. aina hii ya uvukaji ndio huitwa uvukaji wa mipaka wa fonimu uliokamili.Kutokana na mifano tajwa hapo juu ni dhahiri kuwa fonimu inaweza kutokea katika umbo lake asilia na kwenda katika umbo jingine la fonimu au alofoni ambazo hutokana na fonimu moja. Hii husababishwa na mazingira ya utokeaji wake au sifa za kifonolojia.MAREJEO:Massamba, D.P.B. (2004). Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha. Taaasisi yaUchunguzi wa Kiswahili. Dar es salaam.Massamba, D.P.B na wenzake. (2004). Fonolojia ya Kiswahili Sanifu. Taasisi yaUchunguzi wa Kiswahili. Chuo Kikuu cha Dar es salaam.Massamba, D.P.B. (2010). Phonological Theory: History and development.TUKI. Dar es saalam.
USHAMIRISHAJI
KATIKA LUGHA YA KISWAHILI.
Makala hii itaangazia kwa kifupi maana ya ushamilishaji kwa mujibu wa wataalamu wanavyojaribu kuielezea, tutaangalia maana ya uelekezi kwa mujibu wa wataalamu ambao ndio hutupa mwelekeo wa uelewa zaidi dhana nzima na sifa pamoja na viashiria vya ushamirishaji, pia tutaeleza aina za ushamirishaji pamoja na makundi ya ushamilishaji.
Kwa kuanza na maana ya ushamilishaji wataalamu wameifasili kama ifuatavyo;
grammar.about.com/old/dg/complent. Wanaeleza ushamilishaji ni hali ya kishazi tegemezi kusaidia kueleza au kufafanua maana kamili ya nomino au kitenzi katika sentensi. Fasili hii imejikita kuonesha ushamirishaji wa nomino na kitenzi bila kuangalia au kueleza ushamilishaji wa vivumishi, vihusishi na vitenzi kwa hata vivumishi vinaweza kutosheleza na kishazi tegemezi.
O’grady na wenzake (1996) wanaeleza ushamilishaji kwa kutoa maneno ambayo yanaweza kufanyiwa ushamilishaji kama vile nomino, kivumishi, kitenzi, kihusishi ambayo yanaweza kutoshelezwa na vishazi tegemezi. Mapungufu ya hoja hii ni kwamba hawajaonesha ushamirishaji wa kielezi lakini ukweli ni kwamba ni maneno yanaweza kufanyiwa ushamirishaji.
Hivyo tunaweza kusema ushamirishaji ni mchakato unaofanywa na vishazi tegemezi kutosheleza kitenzi, nomino kivumishi kielezi na kihusishi kinachotokea kwenye upande wa kiarifu au kutoa maelezo yaliyo ya lazima kukamilisha taarifa ya za kitenzi, nomino, kivumishi, kihusishi na kielezi.
Baada ya kufasili maana ya ushakilishaji sasa tunaweza kueleza kwa kifupi maana ya uelekezi. Wataalamu wameeleza maana ya uelekezi kama ifuatavyo;
Massamba (2004) anaeleza uelekezi kuwa ni kuwa ni hali ya uhusiano uliopo baina ya kitenzi na vijenzi vingine vya muundo wa sentensi vinavyohusiana nacho. Kiini chake hasa ni kitenzi kuhitaji au kutohitaji yambwa. Hii ina maana kuwa anaposema kuwa kitenzi kuhitaji yambwa ana maana kuwa kitenzi kuambatana na kipashio kingine kilicho cha lazima.
Mfano: mwalimu anasoma kitabu
Juma anacheza mpira
Hivyo katika sentensi hizi vipashio vilivyo vya lazima ni kitabu na mpira.
Katika kutohitaji yambwa (si elekezi) ana maana kuwa kutoandamana na kipashio kingine au kutoandamana lakini hakuna ulazima.
Mfano: Rajabu amelala usingizi.Hivyo neno “usingizi” si kipashi cha lazima katika sentensi hii.Habwe na karanja (2004) wanasema kitenzi elekezi ni vitenzi vinavyoashilia vitendwa na hali ambayo huvuka mipaka na kuathiri maneno mengi ya sentensi. Maneno yanayoathiriwa huitwa yambwa tendwa au tendwa.Mfano: jesse anampiga mamaBaba anakula machungwa.Hivyo basi kitenzi “anampiga” kinauliza swali la nani na “anakula” swali “nini” hivyo vitenzi hivi ni elekezi ambapo vinaandamana na maneno yaliyo ya lazima kama vile “mama” na “machungwa”.Pia vitenzi si elekezi, wanaelezea kuwa ni vitenzi ambavyo huwa havihitaji yambwa. Kwa maana kwamba vinajitoshereza katika matumizi yake.Mfano: jamesi amesinziaAsha anakimbiaHivyo vitenzi (amesinzia) na (anakimbia) si elekezi kwa maana havihitaji yambwa. Hivyo basi uelekezi tunaewza kusema ni mchakato wa kitenzi kuchukua au kubeba au kutoandamana na yambwa.Baada ya kufasili au kueleza maana ya uelekezi tuangalie tuangalie sifa za ushamirishaji: sifa hizo ni kama zifuatazo.Kishazi tegemezi bebwa, huwa kinafanya kazi ya kuarifu pia kufanya kazi ya kutosheleza kitenzi, nomino, kitenzi na kihusishi. Ni lazima kitokee baada ya maneno haya kwa lengo la kujibu maswali ya kwa nini na nani kama yale yanayotokea kwenye uelekezi.Hivyo baada ya kuangalia sifa hizi za usharishaji tuangalie viashiria vya ushamiklishaji:Black (1998) na O’glady na wenzake (1996) wanatueleza kuwa viashiria vya ushamirishaji ni kama vile ya, kuwa, kwamba,kappa, kama lakini kuna kiashiria kingine kama vile (ku). Blacka (1998) amezungumzia suala la ushamirishaji wa vitenzi peke yake hajatuelezea wa vitenzi, nomino,vivumishi, vihusishi na vivumishi kama O’glady na wenzake.Baaba ya kuangalia viashiria vya ushamirishaji tuangalie ushamirishaji unaweza kujidhihirisha katika vitenzi, nomino, vivumishi, vihusishi na vielezi. Hivyo tukianza na :Ushamirishaji wa vitenzi, ni ushamirishaji unaotokana na vitenzi vinapohitaji kutoshelezwa si kwa nomino za kawaida bali kishazi tegemezi ambacho lazima kitokee kwa lengo la kitenzi husika kukamilisha taarifa/ utoa taarifa zinazojitoshelezaMfano: Baba alimwambia [asha] kuwa mama hatarudi nyumbani.Mwalimu alihuzunika kuwa wanafunzi walifeli somo lake.Kishazi tegemezi kilichotokea baada ya yambwa “Asha” na kitenzi “alihuzunika” vinafanya kazi ya kutosheleza vitenzi / kukamilisha taarifa ya kitenzi.Ushamirishaji wa vitenzi umegawanyika katika makundi manne ambayo ni kama ifuatavyo:Vitenzi vya kusema, ni vile vitenzi ambavyo huwa vinatoa ripoti, matangazo, kuarifu jambo, kuambia au kueleza jambo au tukio fulani.Mfano: Rais aliwatangazia wananchi kuwa atavunja baraza la mawaziri.Komba alituambia kwamba wanafunzi wanaojituma kusoma watafaulu.Katika sentensi hizi kishazi au vishazi vinavyotokea baada ya kitenzi “aliwatangazia” na “alituambia” vinafanya kazi ya kushamirisha vitenzi hivi au kukamilisha taarifa ya vitenzi.Vitenzi vya kudadisi au kutaka kujua, ni vile vitenzi ambavyo huwa vinafanya kazi ya uchanganuzi, kuuliza na kufanya upelelezi kuhusu kitu fulani au jambo.Mfano: Juma alitaka kujua kwamba nani anafuja mali za ummaAsha alichunguza kuwa wanafunzi wengi wanaishi kwa kutegemea fedha ya mkopo.Vishazi tegemezi vilivyopigiwa msitari vinafanya kazi ya ushamirishaji wa vitenzi “alitaka” na “alichunguza”.Vitenzi vya kutendesha, hivi ni vitenzi vya kuamuru, kuagiza, kuruhusu, kulazimisha, au omba kufanyika kwa jambo fulani.Mfano: Wazazi aliwasihi watoto kusoma kwa bidii ili wafaulu mitihani yao.Rais aliamuru kwamba wanajeshi walinde mipaka ya nchi.Hivyo vishazi hivi vinafanya kazi ya kushamirisha “waliwashawishi” na “aliamulu” ambapo vinafanya kazi ya kutoshereza vitenzi.Vitenzi vya kuhisina kuamua, hivi ni vitenzi vya pande, furahi, kataa, jaribu, thubutu, fikiria na kusudiaMfano: Wanafunzi walikataa kuwa hawawezi acha kudai haki zao.Mama alimkataza Juma kuwa asichezee karibu na kisima.Vishazi hivyo vinafanya ya kutosheleza “walikataa” na “alimkataa”.Ushamirishaji wa nomino, ni mchakato ambao kishazi tegemezi hufanya kazi ya kuelezea au kufafanua au kutosheleza nomino ambayo inakuwa hijakamilika inayotokea katika sehemu ya kirifu.Mfano: ameacha maagizo kwamba mwanae amfuate.Kishazi tegemezi kilichotokea baada ya nomino “maagizo” kinafanya kazi ya kutosheleza namino “maagizo”Ushamilishaji wa nomino unafanana na ushamilishaji wa vitenzi vya kusema, kudadisi na kutendesha. Hivyo tunaweza kugawa nomino katika makundi matatu. Makundi hayo nia kama vile:Nomino za kutendesha, ni nomino ambazo huwa ambazo huwa zinaonesha hali ya kuamuru, kuruhusu, kuagiza kutaka, kulazimisha na kuomba.Mfano: Imetolewa amri kwamba wamanchi wasichechee migomo ya vyimbo vya dola.Ametoa maagizo kuwa wanafunzi wote tuondoke kesho hapa chuoni.Vishazi vilivyotokea baada ya nomino “amri”na” maagizo” vinafanya kazi ya kutosheleza nomino hizi.Nomino za kudadisi au kutaka kujua, ni nomino ambazo huwa ziafanya kazi ya kuchunguza, kuuliza au kuliza jambo fulani.Mfano: sina uhakika kama maelezo aliyatoa ni ya kweliSina mashaka kama maelezo yake si sahihi.Sina uhakika kama uufafanuzi wako unajitosheleza.Vishazi vinavyotokea baada ya nomino vinafanya kazi ya kutosheleza nomino “uhakika” na “mashaka”.Nimino za kusema, ni nomino zinazotoa ripoti, tangaza, arifu, ambia, na eleza jambo au tukio fulani.Mfano: Ametoa matangazo kwamba watu wote wafike kwenye mkutano.Tumetoa taarifa kwamba wanawake wengi ni wavivu.Vishazi vinavyotokea baada ya nomino vinafanya kazi ya kushamirisha nomino husika au kutosheleza nomino hii.Ushamilishaji wa vivumishi, ni mchakato ambao kishazi tegemezi hufanya kazi ya kutosheleza kivumishi kinachotokea kwenye kiarifu. Ushamilishaji huu hufanana na ushamilishaji wa vitenzi vya kuhisi au kuamuru.Mfano: haikuwa rahisi kumuua Simba kwa mishale.Ni vigumu kumwamini msichana ambaye humfahamu historia yake ya maisha.Hivyo vishazi vinavyotokea baada ya kivumishi “rahisi” na “vigumu” inatumika kutosheleza vivumishi hivi ambavyo havikamilishi maana ya tungo.Ushamirishaji wa vihusishi, ni mchakato ambao kishazi tegemezi hufanya kazi ya kutosheleza kihusishi kinachotokea upande wa kiarifu ambacho huwa ni lazima kitokee baada ya kihusishi.Mfano: Juma alifaulu kwa kusoma kwa bidiiMwalimu alituambia ya kwamba tusipokuwa makini tutafeli vibaya mitihani.Neno la Mungu linasema ya kuwa kumcha bwana ni chanzo cha maarifa.Hivyo vishazi hivo vinafanya kazi ya kazi ya kutosheleza kihusishi.Ushamilishaji wa vielezi, ni mchakato ambao kishazi tegemezi hufanya kazi ya kutosheleza kielezi kinachotokea upande wa kiarifu ambacho huwa na lazima kutokea baada ya kihusishi.Mfano: John anatembea polepole kama mgonjwa anyeumwa miguu.Asha anakula harakaharaka kama mtu ambaye hajawahi kula siku kumi.Hivyo vishazi vinafanya kazi ya kutosheleza kielezi.Hivyo basi ushamirishaji katika Kiswahili unasaidia kuondoa maswali ya nini? Na nani?. Hivyo ushamirishaji unafanya kazi ya kutoa taarifa zilizo kamilika.MAREJEOBlack, C.A (1998) A step by Introduction to The Government and Biding Theory of Syntax. SIL-Mexico Branch and Univerisity of North Dakota.grammar.about.com/od/c/g/complement.Habwe, J na Karanja, P (2004) Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Nairobi: Phoenix.Massamba, D.P.B (2004) Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha. Dar es Salaam: TUKI.O’Grady, W. na Wenzake(1996) Contemporary Linguistics. An Introduction. United Kingdom Pearson Education Limited.
UMILISI WA LUGHA UNAVYODHIHIRIKA KUPITIA VIPENGELE VYA KISARUFI.
Katika makala hii kwanza tutaeleza maana ya lugha kwa kifupi, maana ya sarufi kwa mujibu wa wataalamu mbalimbali, maana ya umilisi na maana ya umilisi wa lugha kama ulivyoelezwa na baadhi ya wataalamu. Kisha tutachambua vipengele vya kisarufi na nanma umilisi unavyojidhihirisha kupitia vipengele vyote vya kisarufi. Na mwishoni tutahitimisha makala hii kwa maoni na mapendekezo.
Tukianza na maana ya lugha; Massamba (2009) ameeleza lugha ni mfumo wa sauti nasibu ambazo zimekubaliwa na jamii kwa madhumuni ya mawasiliano kati yao.
Naye Mgulu (1999) kama alivyomnukuu Trudgil (1974) yeye anasema kuwa lugha ni mfumo wa sauti za nasibu zinazotumiwa kwa mawasiliano miongoni mwa watu wa jamii fulani zenye utamaduni wake.
Kwa hiyo tunaweza tukasema lugha ni mfumo wa sauti nasibu ambazo zimebuniwa na jamii kwa madhumuni ya mawasiliano kati yao.
Baada ya kuangalia maana ya lugha ni vyema tukaangalia maana ya sarufi. Kwa mhujibu wa Massamba (2009) anaeleza kuwa sarufi ni taaluma ya lugha inayohusu uchunguzi na uchanganuzi wa kanuni za vipengele mbalimbali vya lugha.
Pia kuna baadhi ya wataalam wameeleza maana ya umilisi kama ifuatavyo;
Msanjila na wenzake (2009) wameeleza kuwa, umilisi ni ujuzi na uelewa wa kanuni zinazotawala usemaji wa lugha fulani ambao msemaji mzawa wa lugha anakuwa nao.
Chomsky (1957) anaeleza kuwa, umilisi ni ule ujuzi wa lugha ambao wazawa wa lugha fulani huwa wanao. Anasema ujuzi huu ndio ambao huwawezesha wazawa hawa kuzielewa na pia kuzitunga sentensi zote sahihi katika lugha yao pamoja na zile ambazo hawajawahi kuzisikia. Kwa maana hii umilisi ni msimbo uliopo akilini mwa mtu ambao hutumiwa wakati wote mtu anapoongea.
Kwa hiyo umilisi ni uwezo alionao mtu kuhusu kutumia kanuni za lugha fulani katika kuzungumza na kuandika kwa ufasaha.
Kutokana na fasili mbalimbali za umilisi kama zilivyoelezwa na wataalam hao tunaweza kusema kuwa umilisi wa lugha ni uwezo wa msemaji wa lugha kuweza kutunga na kuelewa tungo za lugha yake.
Umilisi wa lugha / msemaji huweza kujidhihirisha kupitia vipengele vyote vya kisarufi, ambavyo ni fonolojia, mofolojia, sintaksia na semantiki. Hivyo hujidhihirishaji huo hujitokeza kama ifuatavyo:-
Kipengele cha kwanza ni Fonolojia; fonolojia ni utanzu wa Isimu unaochunguza jinsi sauti za lugha zinavyofanya kazi katika lugha mahususi. Fonolojia hushughulikia jinsi sauti hizo zinavyotumika, zinavyounganishwa na kupangwa katika lugha yoyote mahususi ili kuunda tungo zenye maana. Kipashio cha msingi katika fonolojia ni fonimu na katika fonimu kuna konsonanti na irabu. Hivyo basi ili msemaji aweze kudhihirisha umilisi wake lazima aweze kupanga vizuri konsonanti na irabu ili kuunda silabi. Mfano; b +a ba, t + a ta
Pia msemaji anatakiwa aweze kuunganisha silabi ili kuunda neno. Mfano; ba + ta bata, ka + ka kaka.
Kipengele cha pili ni Mofolojia; mofolojia ni taaluma ya Isimu inayoshughulikia uchambuzi na uchanganuzi wa kanuni na mifumo inayohusu upangaji wa mofimu mbalimbali ili kuunda maneno katika lugha. Kipashio cha msingi cha mofolojia ni mofimu. Kwa hiyo mofolojia huchunguza masuala kama vile aina za mofimu, namna mofimu zinavyojenga maneno na namna mofimu zinavyohusiana ili kuunda neno na lenye maana. Mmilisi katika usemaji wake anatakiwa ajidhihirishe katika kipengele cha mofolojia kwa kuhusisha mofimu ili kuunda maneno yenye maana. Mfano katika vitenzi.Anacheza. A- – na – chez – a A- = kiambishi awali, nafsi ya tatu umoja. -na- = njeo ya wakati uliopo timilifu. -chez- = mzizi wa neno. -a- = kiambishi tamati maana. Katika nomino hudhihirika katika maumbo ya umoja na wingi, kama inavyojidhihirisha katika mfano ufuatao. M – t mi – ti m- = kiambishi awali umoja (ngeli) mi- = kiambishi awali cha wingi -ti = mzizi wa neno. pia mmilisi wa lugha ajue matumizi ya mofimu kapa. Kwa mfano; ᴓkuta. Hivyo kwa kuwa mofimu ni kipashio cha msingi cha mofolojia na mofimu ni maana ambayo ni sehemu ya umilisi ya mzawa wa lugha husika, maana hii hudhihirika kiutendaji ama kimaandishi.
Kipengele cha tatu ni Sintaksia; sintaksia ni nyanja ya Isimu inayojihusisha na uchambuzi na ufafanuzi wa muundo wa sentensi za lugha. Kutokana na fasili hii tunaona kuwa kila lugha ina muundo wake wa sentensi unaoamua kipashio kipi kianze na kingine kifuate. Mfano; katika lugha ya kiswahili muundo wa sentensi unaanza na nomino, ikifuatiwa na kitenzi na kuishiwa na kielezi.
Kwa hiyo mmilisi katika usemaji wake anatakiwa ajue miundo ya sentensi katika lugha husika. Mmilisi wa lugha ya kiswahili lazima ajue muundo wa sentensi za kiswahili kuwa unaanza na nomino,ukifuatiwa na kitenzi na kuishiwa na kielezi. Mfano.1 Baba analima shambani. N T E Juma amekwenda sokoni. N T E
Kwa hiyo mmlisi wa lugha hawezi kuchanganya muundo huu wa sentensi za kiswahili kwa kusema:- Mfano 2. Amekwenda Juma sokoni. T N E Shambani analima baba. E T N Kwa hiyo, kulingana na muundo wa sentensi za Kiswahili, muundo wa sentensi zilizopo katika mfano namba mbili si sahihi kwani zimekiuka sintaksia ya lugha Kiswahili.
Kipengele cha nne ni Semantiki; semantiki ni nyanja nyingine ya Isimu inayojihusisha na uchunguzi wa maana katika lugha ya mwanadamu. Semantiki hutafiti maana za fonimu, mofimu, maneno na tungo kwa ujumla. Maana hushughulikiwa katika viwango vyote vya lugha kama vile sauti, maneno na sentensi. Katika semantiki tunaangalia maana ya msingi na maana ya ziada. Maana ya msingi ni ile maana kuu ya neno, maana hiyo hupatikana katika kamusi. Mara nyingi maana hii hubadilika kulingana na athari za kimazingira au muktadha halisi. Mfano; Baba – mzazi wa kiume, Kata – kitendo cha kutenganisha kitu. Sungura – mnyama mdogo mwenye mbio. Shoga – rafiki wa kike. Nyambizi – kifaa kinachosafiri chini ya maji. Mfano ya hapo juu imeoneshwa kwa kuzingatia maana halisi/msingi. Na maana ya ziada ni ile maana ya kimuktadha au kimazingira lakini yenye kuwa na misingi, kuzalishwa na kuhusiana na maana msingi. Katika kuangalia maana ya ziada mara nyingi kile mtu anachokisema si lazima kiwe ndicho anachomaanisha bali kile anachomaanisha ni maana ya ziada. Mfano; Baba – kichwa cha familiya. Kata – kifaa cha kutekea maji. Sungura – mtu machachari na mjanja. Nyambizi – mwanamke mwenye umri mkubwa anayewataka vijana wadogo kimapenzi.
Hivyo basi mmilisi wa lugha ili aweze kufikia katika ngazi ya Semantiki ambayo inahusika na kiwango cha Semantiki ni lazima ujuzi wake wa kufahamu kanuni za lugha uanzie kwenye kiwango cha fonolojia ambapo unatakiwa kujua sauti ambazo ni Konsonanti na Irabu ambazo zikiunganishwa zinaleta silabi. Kama hatakuwa na uwezo katika kiwango hiki hataweza kufikia kwenye ngazi zingine kama Mofolojia, Sintaksia na Semantiki yaani maana.
Kwa hiyo mmilisi wa lugha katika usemaji wake ili awe mmilisi mzuri anatakiwa ajue hatua za kuunda sentensi ambayo inaanzia katika kiwango cha fonimu, mofimu, silabi, muundo na maana. Maana hiyo iwe inaendana na muktadha mahususi ili kukidhi matakwa ya wazungumzaji.
MAREJEO:Besha, R.M. (2007). Utangulizi wa lugha na Isimu. Macmillan Aidan Ltd. Dar es Salaam.Chomsky, N. (1957). Syntactic Structures. Mouton The Hague.Habwe, J na Peter K (2007). Msingi ya sarufi ya Kiswahili.Phoenix Publishers. Nairobi.Massamba, D.P.B. (2009). Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha.TUKI. Dar es Salaam.Mgullu, R.S. (1999). Mtalaa wa Isimu: Fonetiki, Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili. Longhorn Publishers Ltd. Nairobi.Msanjila na wenzake. (2009). Isimujamii: Sekondari na vyuo.TUKI. Dar es Salaam.
KUFANANA NA KUTOFAUTIANA KWA FONOLOJIA NA MOFOLOJIA.
Katika kujadili swali hili tutaanza kufasili dhana kuu zilizojitokeza ambazo ni fonolojia na mofolojia. Ambapo wataalamu mbalimbali wamefasili dhana hizi huku kila mmoja akitoa fasili yake. Pia tutatalii kwa kina juu ya kuhitilafiana na kufanana kwa fonolojia na mofolojia na mwisho ni hitimisho.Kwa kuanza na mofolojia, wataalamu mbalimbali wamefasili mofolojia kama ifuatavyo,
Massamba na wenzake (2009) wanafasili mofolojia kuwa ni kiwango cha sarufi kinachojishughulisha na uchambuzi wa mfumo wa maneno katika lugha yaani jinsi maneno ya lugha yoyote iwayo inaundwa.
Besha (2007) anasema mofolojia ni taaluma inayojishughulisha na kuchambua muundo wamaneno katika lugha. Misingi ya wataalamu hawa wawili wanaonekana kuingiliana katika kuonyesha namna ya taaluma ya mofolojia inavyojihusisha na muundo wa maneno katika lugha. Mofimu ndio kipashio cha msingi katika mofolojia.
Pia Rubanza (1996) anaonekana kuungana nao kwa kusema mofolojia kuwa ni taaluma inayoshuhulika na vipashio vya lugha na mpangilio wake katika uundaji wa maneno.mtaalamu anaongezea namna vipashio vinavyotumika katika kupangilia mfumo wa muundo wa maneno katika lugha. Kipashio cha msingi katika mofolojia ni mofimu.
Hivyo basi fasili ya mofolojia imeonekana kugusia uundaji wa maneno katika lugha kwa mpangilio maalumu. Hivyo mofolojia inaweza kuelezwa kwamba ni taaluma inayoshughulika na uchunguzi na uchambuzi wa maumbo mbalimbali ya maneno katika lugjha.
Baada ya kuangalia taaluma ya mofolojia, kuna wataalamu mbalimbali ambao wamefasili dhana ya fonolojia, wataalamu hao nia kama wafuatao.
Habwe na Karanja (2007) wanafafanua fonolojia kuwa ni taaluma inayoshughulika jinsi sauti zinavyotumika, zinavyounganishwa na kupangwa katika lugha yoyote mahususi ili kuunda tungo zenye maana. Wanaeleza kuwa sauti hizo zinazotumika katika lugha hiyo mahususi hujulikana kama fonimu.
TUKI (2004) wanaifasili fonolojia kuwa ni tawi la isimu ambalo linajishughulisha na uchambuzi wa mfumo wa sauti katika lugha.
Vilevile Kihore ne wenzake (2004) wanafasili fonolojia kuwa ni tawi la isimu ambalo hujishughuliah na uchunguzi, uchambuzi na uainishaji wa sauti pambanuzi ambao hutumika katika mifumo mbalimbali ya sauti za lugha za binadamu. Katika fonolojia kipashio cha msingi kinachohusika ni fonimu.
Kwa ujumla fasili zilizoelezwa hapo juu ni za msingi katika taaluma ya fonolojia kwani wataalamu wote wanaelekea kukubaliana kuifasili fonolojia kuwa ni ni uwanja waisimu unaojisgughulisha na uchunguzi na uchambuzi wa sauti za lugha mahususi.
Kimsingi taaluma ya mofolojia na fonolojia hufanana na kuhitilafiana kwa kiasi kikubwa.
Taaluma hizi zina ufanano kama ifuatavyo; (fonolojia na mofolojia).
Kwanza, vipashio vya kifonolojia ndivyo vinavyouna vipashio vya kimofolojia, kwa kutumia fonimu ambacho ndio kipashio cha msingi katika fonolojia huweza kuunda mofimu ambayo ndiyo kipashio cha msingi cha kimofolojia.
Mfano: /h/,/p/,/t/,/k/,/g/,/m/,/n/,/o/,/u/,/e/,/s/,/a/. fonomu hizo zinzweza kuunda mfuatano wa maneno kama ifuatavyo.
Pat-a =pataTak-a =takaTes-a =tesa
Maisha Uhusiano mingine ni kuwa kanuni za kifonolojia zaweza kutumika kuelezea maumbo ya kimofolojia Kanuni hizi si kwa kuelezea maumbo tu pia huweza kubadili umbo la neno yaani umbo la ndani na umbo la nje. Kanuni hizo za kifonolojia ni udondoshaji, uyeyushaji, muungano wa sauti, nazali kuathiri konsonanti, konsonanti kuathiri nazali na tangamano la irabu.
Udondoshaji, kanuni hii inahusu kuachwa kwa sauti fulani katika matamshi wakati mofimu mbili zinapokaribiana yaani katika mazingira hayo hayo ya sauti ambayo ilikuwepo hapo awali hutoweka.hapa kuangalia umbo la ndani la neno na umbo la nje. Umbo la ndani ni jinsi neno lilivyoundwa na mofimu zake mbalimbali na umbo la nje ni jinsi neno lisikikavyo linapotamkwa.
Mfano;
umbo la ndani umbo la nje
Muguu mguu
Mutu mtu
Mujapani mjapani
Mara nyingi irabu “u” katika mofimu “mu” ikabilianapo na na mofimu fulani hasa konsonati halisi katika mpaka wa mofimu, irabu “u” hudondoshwa lakini inapokabiliana na irabu inayofanana nayo hubaki kama ilivyo.
Mfano; Muumba- muumba Muumini- muumini Muuguzi-muuguzi Muungwana- muungwana
Uyeyushaji, hii ni kanuni inayohusu ubadilikaji wa irabu fulani kuwa nusu irabu au kama wataalamu wengine waitwavyo “viyteyusho”. Viyeyusho vinavyohusika ni /w/ na /y/. kanuni hii hutokea katika mazingira ambayo irabu “u” hukabiliana na irabu isiyo fanana nayo katika mpaka wa mofimu na kuwa /w/ lakini hubaki kama ilivyo mara ikabilianapo na irabu inayofanana nayo. Pia irabu /i/ katika mofimu inapokabiliana na irabu isiyofanana nayo hubadilika na kuwa /y/ katika mpaka wa mofimu lakini hubaki kama ilivyo inapokabiliana na irabu inayofanana nayo.
MfanoMu+ema-----------mwema Vi+ake------------vyakeMu+ana------------mwana Mu+ako------------mwakoMu+eupe---------mweupe Vi+ake-------------vyakeVi+ao--------------vyao Vi+akula----------vyakulaVi+umb-----------vyumbaTofauti naMuuguzi ------ muguzi Muumba ------- muumba
Muungano wa sauti, kanuni hii hutokea pale ambapo irabu ya mofimu moja inapokabiliana na irabu ya mofimu nyingine katika mpaka wamofimu irabu hizo huungana na kuzaa irabu moja.
Mfano;
Umbo la ndani
|
Umbo la nje
|
Wa + enya
|
wenye
|
Wa + ingi
|
wengi
|
Ma + ino
|
meno
|
Wa + izi
|
wezi
|
Wa + enzi
|
wenzi
|
Lakini kanuni hii haifanyi kazi wakati wote kwani kuna mazingira mengine ambayo haifuati hasa katika mofimu mnyambuliko
Mfano:-
Wa + igizi +a +ji -
waigizaji
|
Wa+ingereza -
waingereza
|
Wa +oko+a+ji -
waokoaji
|
Wa+ite - waite
|
Kanuni ya nazari kuathiri konsonati, kuna baadhi ya sauti ambazo huathiriwa na nazali “n” inapokuwa inaandamia yaani kuna sauti ambazo huathiriwa zinapokaribiana au karibiana moja kwa moja na nazali “n”. mara nyingi hutokea katika maumbo ya umoja na uwingi katika maumbo ya maneno
Mfano:-
Umbo la
nje
|
umbo la
ndani
|
Ulimi
|
u+limi
|
Ndimi
|
u+limi
|
Urefu
|
u+refu
|
Ndefu
|
n+defu
|
Kwa hiyo kama vile ulimi mrefu
|
Ndimi ndefu
|
Hapa tunaona kwamba sauti [ l ] na [ r ] zinapokaribiana na irabu na irabu haziathiriki lakini zinapokaribiana na nazali “n” hubadilika na kuwa “d”
Kanuni ya konsonati, kuathiri nazali; katika lugha ya Kiswahili sanifu na hakika katika lugha nyingi za kibantu umbo la sauti ya nazali huathiriwa na konsonanti inayoliandamia. Maumbo ya nazali hutokea kutegemeana na konsonanti zinazotamkiwa sehemu moja
Mfano:-
Mbawa
Mbaazi
Mbegu == /m/ na /b/ hutamkiwa mdomoni
Mbuni
Kanuni ya tangamano la irabu, huu ni mchakato wa kifonolojia ambao huhusu athari ya irabu moja kwenye irabu nyingine kiasi cha kuzifanya irabu hizo zielekee kufanana kabisa au kufanana katika sifa zake za kimatamshi. Mabadiliko hayo ya sauti husababishwa na utangamano ambao hujitokeza katika baadhi ya vitamkwa yaani kunakuwa na namna fulani ya kufanana au kukubaliana kwa vitamkwa ambavyo ni jirani.
Mfano:-
Umbo la
nje
|
umbo la
ndani
|
Pikia
|
pik+i+a
|
Pigia
|
pig+i+a
|
Katia
|
kat+i+a
|
Endea
|
end+e+a
|
Chekea
|
chek+e+a
|
Pokea
|
pok+e+a
|
Hapa tunaona kwamba kitendea -i- kinawakilishwa na maumbo mawili yaani – I - na – e - hapa tunaona kwamba – I - hujitokeza pale tu ambapo irabu ya mzizi wa neno ni ama o au e kiambishi hiki – I - hubadilika na kuwa – e -. hapa ni wazi kwamba kiambishi cha kutendea huathiriwa na irabu ya mzizi na hii ndiyo tungamano ya irabu.
Zaidi sana mofolojia na fonolojia zote ni nyanja za isimu zinazounda maarifa fulani ya lugha kwa kuchunguza sauti na maumbo ya maneno yatokananyo na sauti za lugha hiyo na mpangilio wake. Nyanja zingine za isimu ni kama fonetiki, sintaksia na semantiki.
Mfano:- Neno
Limia
-
Lina sauti tano (5) (kifonolojia) zinazounda
-
Mofimu tatu (3) (kimofolojia)
Tembea
-
Sauti nne (4)
-
Mofimu mbili (2)
Baada ya kuangalia ufanano huo kwa kina, sasa uelezwe utofauti wa taaluma hizo. Tofauti zinazojitokeza ni pamoja na hizi zifuatazo:-
Maana, katika kigezo cha maana inaonekana kwamba fonolojia hujihusisha zaidi na uchambuzi wa sauti za lugha mahususi kwa mfano sauti za lugha ya Kiswahili wakati mofolojia inajikita zaidi katika uchambuzi wa maumbo ya maneno. Hapa fonolojia huangalia kuna sauti ngapi zalizounda au zilizotumika katika neno fulani wakati mofolojia huangalia neno fulani limeundwa kwa vipende vingapi
Mfano:-Lima - sauti nne (4) /l/, /i/, /m/, /a/ (fonolojia)- Vipande au mofimu mbili (2) lim – a (mofolojia)Jamila - sauti sita (6) /j/,/a/,/m/,/i/,/l/,/a/- Kipande kimoja, jamilaMasikio - sauti saba (7) /m/,/a/,/s/,/i/,/k/,/i/,/o/- Vipande viwili (2) ma + sikio
Tofauti ya vipashio, kipashio cha msingi cha kifonolojia ni fonimu wakati kipashio cha msingi cha mofolojia ni mofimu.
Mfano:-Analima - fonimu saba (7) /a/,/n/,/a/,/l/,/i/,/m/,/a/- Mofimu nne (4) a-na-lim-aSema - fonimu nne (4) /s/,/e/,/m/,/a/- Mofimu mbili (2) sem-aBaya - fonimu nne (4) /b/,/a/,/y/,/a/- Mofimu moja
Ukongwe, taaluma ya fonolojia ni kongwe kuliko taaluma ya mofolojia ambayo ilianza baada ya kuibuka taaluma hii ya fonolojia.
Dhima ya vipashio, kipashio cha kimofolojia yaani mofimu kina uamilifu mkubwa sana katika lugha hasa kwa kuangalia mofimu huru ambazo huweza kusimama peke yake na kutoa maana kamili mfano baba, mama, safi, nzuri. Maana ya mofimu huru yaweza kuwa ya kileksika ama kisarufi. Lakini pia mofimu funge huleta utegemezi wenye maana sana katika neno ambapo ni tofauti na kipashio cha kifonolojia yaani fonimu ambayo ikiwa peke yake inakuwa haina maana
Mfano:-Alilala - kifonolojia /a/, /l/, /i/, /l/, /a/, /l/, /a/Mofimu hizo hazitakuwa na maana katika muktadha huo, ila tu zitakapoungana kuunda neno.Alilala – a- mofimu awali ya nafsi ya tatu umoja katika nafasi ya kiima-li- mofimu awali ya wakati uliopita katika nafasi ya kiima.-lal- mzizi (mofimu kiini)-a- kiambishi au mofimu tamati cha maana.
Mwisho vipashio vy akifonolojia hutengwa katika kila umbo la neno baina ya fonimu moja na nyingine wakati si kila kipande au mofimu katika umbo neno hutengwa. Kwa mfano mzizi na mofimu huru daima hazitengwi.
Mfano:-Sema - /s/,/e/,/m/,/a/- Sem-aJuma - /j/, /u/, /m/, /a/- JumaSafi - /s/, /a/, /f/, /i/- Safi
Hivyo basi pamoja na kuwepo tofauti hizo taaluma hizi mbili hukamilishana sana kwani uwepo wa taaluma moja hupelekea kuimarika kwa taaluma nyingine na kutokuwepo kwa taaluma moja hudhoofisha taaluma nyingine. Na hii ndiyo maana hatuwezi kuchunguza sauti za lugha ikiwa lugha hiyo haitakuwa na mfumo na mpangilio maalumu ya maumbo ya maneno na hatutachunguza maneno kama hatutakuwa na sauti zinazopelekea kuundwa kwa maneno hayo.
VIKOA VYA MAANA: UMUHIMU NA CHANGAMOTO ZAKE KATIKA KUELEZA MAANA YA MAANA.
Katika makala hii tujadili umuhimu wa vikoa vya maana katika semantiki, yaani kuonesha ni kwa namna gani vikoa vya maana vinaweza kufanikisha suala la kuendeleza taaluma ya semantiki ambayo hujihusisha zaidi na uchunguzi wa maana ya lugha ya binadamu. Pia tutaonyesha changamoto mbalimbali ambazo zinatokea wakati wa kuelezea maana ya maana. Kabla ya kujadili yote hayo ni vyema kwanza kujadili kwa ufupi maana ya vikoa vya maana pamoja na semantiki kutoka kwa wataalamu mbalimbali kusudi uhusiano na utofauti uliopo kati ya semantiki na vikoa vya maana.
Briton (2000) anaihusisha dhana ya vikoa vya maana na dhana ya hiponimia ambapo hiponimia ni uhusiano wa kiuwima ambapo fahiwa ya neno moja hujumuishwa katika fahiwa ya neno jingine mfano fahiwa ya mgomba, mahindi, maharage zimejumuishwa katika mimea. Anahitimisha kwa kusema kuwa maneno katika vikoa vya maana huwa na sifa sawa zinazohusiana.
Wikipedia, wanaeleza kuwa kikoa cha maana ni msamiati wa kiufundi katika taaluma ya isimu ambao unaelezea kikundi cha maneno yanayohusiana kimaana.
Dirk (2010) anaeleza kuwa vikoa vya maana ni jozi za maneno yenye maana zinazohusiana ambazo maana zake zinategemeana, na kwa pamoja zinatoa dhana ya kimuundo yenye uhalisia ndani yake.
Hivyo kikoa cha maana kinaweza kufasiriwa kuwa ni seti yeyote ile ya misamiati ambayo memba wake wanahusiana kiwima na kimlalo. Uhusiano kiwima tunaweza kusema kuwa ni namna maneno yanavyohusiana kiwima, na mlalo ni namna maneno yanavyoweza kuvutana na maneno mengine yanayoelekeana nayo na kuleta maana.
Mifano ya vikoa vya maana nikama vile; “Uandishi wa kubuni” ambapo hujumuisha hadithi fupi, tamthiliya, ushairi na riwaya.
“Michezo”: ambapo hujumuisha; mpira wa miguu, mpira wa kikapu, kuruka kamba, mpira wa pete, mpira wa meza, mpira wa mikono.
“Nguo”: ambapo hujumuisha nguo za wanawake na nguo za wanaume. Nguo za wanawake: sketi, kanga, gauni, sidiria, blauzi.
Baada ya kujadili maana ya vikoa vya maana, ni vema pia kuangalia maana ya semantiki kabla ya kujadili umuhimu wa vikoa vya maana.
Kwa mujibu wa Habwe na Karanja (2004) semantiki ni utanzu wa isimu unaochunguza maana katika lugha ya binadamu, wanaendelea kusema kuwa maana hushughulikiwa katika viwango vyote vya lugha kama vile sauti, maneno na sentensi.
Hivyo tunaona kuwa vipengele muhimu katika lugha ya binadamu ni maana kwa sababu huweza kufanikisha suala la mawasiliano na upashanaji wa habari(ujumbe).
Umuhimu wa vikoa vya maana katika semantiki ni kama ufuatao.
Huonesha uhusiano wa maneno yenye sifa sawa au zinazoelekeana kimaana. Vikoa vya maana humsaidia mwanaisimu kutambua sifa za maana mbalimbali zinazohusiana kimaana kwani huwezi kuweka neno fulani katika kikoa fulani bila kujua sifa zinazotawala neno hilo. Mfano lazima ujue ndege na sifa zake ndipo utaje ndege wanaojenga hicho kikoa kama vile Kanga, Kuku, Njiwa, Bata, Mbuni na Kware.
Hurahisisha mchakato wa ujifunzaji lugha, husaidia kumueleza mtu anayejifunza lugha fulani husika ili kujua vitu mbalimbali vilivyowekwa katika makundi husika. Mfano mtoto au mgeni wa lugha fulani huweza kujifunza dhana mbalimbali kupitia vikoa vya maana. Mfano watoto huweza kujifunza rangi mbalimbali hasa nyeusi na nyeupe kwa kupitia vikoa hivyo.
Hurahisisha mawasiliano, yaani huokoa muda baina ya wazungumzaji, kwa mfano badala ya kutaja kitu kimoja kimoja basi unataja kwa ujumla wake endapo vinahusiana mfano, ukienda sokoni utauliza “una mboga za majani” utajibiwa kuwa kuna, mchicha, chainizi, spinachi, figili na matembele. Ilhali ilitakiwa mnunuaji amuulize muhudumu kwa kutaja jina mojamoja lakini yeye ametaja kwa ujumla na jibu limepatikana na ndipo huweza kutaja kikoa kimoja alichokitarajia.
Hufanya kazi ya kustawisha maana katika tungo au sentensi, utungo huwa na maana iliyojitosheleza kisemantiki(kimaana). Vikoa vya maana vinapotumika katika utungo huo hauwezi kustawisha maana hata kama vitabadilishana nafasi na muda mwingine hupelekea hata maana ya awali kupotea lakini bado utungo utakuwa na maana. Vikoa hivyo vinaweza kujitokeza katika mfumo wa kiwima au kiulalo.
Mfano :
(a) paka amekula nyama
yote.
(b) chui amekula nyama yote.
(c) simba amekula nyama yote.
Maneno yaliyopigiwa mstari yamebadilishana nafasi kiwima lakini maana yake imebaki kama ilivyo na sentensi zimejitosheleza.
Hufanikisha shughuli za utunzi wa leksikografia, Mdee (2010), akimnukuu Wiegand anaeleza kuwa leksikografia ni shughuli au kazi ya kisanaa inayojishughulisha na utunzi wa kamusi. Leksikografia hiyo hujishughulisha na ukusanyajin wa misamiati mbalimbali ya lugha na ndiyo inayosaidia kutungiwa kamusi. Na kamusi ni kipengele cha kisemantiki kwa kuwa hutoa maneno yenye maana kwa watumiaji wa lugha na maneno hayo ndiyo vikoa vyenyewe vya maneno vyenye maana ambazo muda mwingine maana zake zaweza kuwa tofauti hatakama vikoa hivyo vinakuwa na maumbo sawa ya maneno. Mifano ya kamusi zenye vikoa vya maana ni kama vile;
-kamusi ya wanyama
-Kamusi ya mavazi
-Kamusi ya tiba ya magonjwa
-Kamusi za misuko ya nywele
-Kamusi za vyakula
Kikoa kimoja husaidia kujua na kufafanua vikoa vidogo vilivyomo ndani ya vikoa vikubwa mfano kikoa cha vyakula: ugali, ndizi, viazi, ambapo kisemantiki humsaidia mtumiaji wa lugha kuteua kikoa mahususi kwa ajili ya matumizi yake kwa wakati huo.
Husaidia kuonesha umbo la wingi ambalo lina umuhimu kisemantiki hasahasa katika upatanisho wa kisarufi kwa mfano badala ya kusema ‘kikoa cha tunda” tunasema “kikoa cha matunda” “mnyama- wanyama” “mmea- mimea” hivyo basi vikoa hivyo vikitumika kwenye sentensi huwa matunda yameiva badala ya kusema Tunda yameiva, wanyama wanakimbia badala ya kusema wanyama anakimbia.
Vikoa vya maana vina sifa ya kuwa na maana ya kileksimu na kufanya kikoa kimoja kichanuze zaidi na kuweza kupata maneno mengine yenye maana kisemantiki. Mfano kuna kikoa cha masomo ya sayansi, biolojia, fizikia, kemia, kilimo. Kikoa cha biolojia huweza hufasiliwa kuwa ni somo la kisayansi linalohusiana na viumbe hai na visivyo hai. Hivyo tunaona kuwa kikoa cha biolojia kimechanuza zaidi na kuleta maana ya kikoa hicho.
Changamoto ya vikoa vya maana katika kuelezea maana ya maana.
Kuna baadhi ya vikoa havina idadi maalumu na vingine vina idadi maalumu, hii ni kutokana na ukweli kwamba vikoa kama vile vya siku za wiki , idadi ya miezi ya mwaka na siku katika mwezi huwa na idadi maalumu lakini vikoa vya maana vingine havina idadi maalumu mfano vikoa vya matunda, wanyama, mimea. Vikoa vya matunda,wanyama mimea na vinginevyo haviewezi kuwa na idadi maalum kwa kuwa vikoa vyake huweza kujitokeza kutegemeana na mazingira. Wanajamii watatoa majina ya vikoa hivyo baada ya aina fulani kutokea katika jamii yake na hivyo kuacha vionekani kutokuwa na idadi maalumu.
Kuna baadhi ya vikoa ni changamani, hii ni kutokana na kwamba baadhi ya vikoa vya maana vinawakilisha dhana zaidi ya moja na hivyo kumfanya mtumiaji wa lugha apate utata wakati wa uainishaji wake.
Mfano: ndege kama mnyama, na ndege kama kifaa cha usafiri, pia mbuzi kama mnyama na mbuzi kama kifaa. Nyanya kama kiungo na nyanya kama mboga.
Hivyo basi vikoa hivi vya maana huweza kumchanganya mwanasemantiki na kushindwa kupata maana halisi.
Baadhi ya vikoa vya maana vinauhusiano wa karibu kiasi kwamba vinaweza kumchanganya mtu katika kutofautisha dhana mbili mfano Chui na Duma, Mbwa na Mbwa mwitu, Kuku na Kware.
Hakuna nadharia ya jumla inayohusika na upangaji wa vikoa hivi, hii inatokana na ukweli kwamba dhana hizi zipo vichwani mwa watu na kuandikwa kutokana na matumizi yake kimaana
Vilevile uainishaji unahitaji umakini zaidi katika upangaji wa vikoa kwani kuna uchomozi wa vikoa vingine, hii hutokea pale ambapo dhana moja mahususi huwa na dhana ndogondogo ndani yake ambazo nazo huweza kusimama peke yake mfano kikoa cha binadamu tunapata wanaume na wanawake, ambapo ndani ya kikoa cha wanawake tunapata bibi kizee, shangazi, mama, msichana. Pia kikoa cha mwanaume tunapata babu, mjomba, Mvulana.
Vikoa vya maana hutofautiana kutokana na eneo na utamaduni, hii inamaana kuwa kila utamaduni fulani huweza kuwa na vikoa vitumikavyo katika mazungumzo yao ambavyo vinaweza kutofautiana na utamaduni wa jamii nyingine kutokana na aina na idadi ya vitu hivyo katika jamii fulani. Mfano kikoa cha ndizi katika utamaduni wa Wanyakyusa Tukuyu Mbeya kuna vikoa vya majina ya ndizi kama vile; malinda, matoki, mkono wa tembo, haradoni, kaambani na ndyali lakini katika jamii ya Wahaya huko Bukoba kuna vikoa vya majina ya ndizi kama vile; shubili, majivu. Hivyo tunaona kuwa vikoa vya maana katika jamii ya wanyakyusa na wahaya hutofautiana.
Hivyo tunaweza kusema kuwa japokuwa kunachangamoto zinazokabili vikoa vya maana lakini vikoa hivyo vina umuhimu au mchango mkubwa katika kuendeleza taaluma ya semantiki kwa sababu wanasemantiki hufanya uteuzi mzuri wa maneno yenye maana kutoka akilini na kuyatumia katika mazungumzo na hivyo kufanya suala la mawasiliano liendelee kufanikiwa zaidi.
MAREJEO
Brinton L. J (2000) The Structure of Modern English. A Linguistic intro Illustrated Edition.
John Benjamini Publishing company.
Dirk, G (2010) Theories of Lexico Semantics. Oxford University Press: New York.
Habwe, J na Karanja, P (2004) Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Phoenix Publishers: Nairobi.
Mdee,J.S, (2010) Nadharia na Historia ya Leksikografia.Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili:
Dar es Salaam.
SAUTI ZA LUGHA ZA BINADAMU
Mchango wa Jan Baudouin de Courtenay, Ferdinand de Saussure na Noam Chomsky kuhusiana na sauti za lugha ya mwanadamu umetusogeza mbele katika kuekewa na kupata maarifa zaidi juu ya sauti za lugha ya binadamu. Kabla ya kuchambua kwa kina kuhusu mchango wa wataalamu hawa ni vema kufafanua baadhi ya dhana muhimi ili kupata uelewa zaidi juu ya lugha ni nini na maana ya sauti za lugha za binadamu. Tukianza na dhana ya lugha: dhana hii imejadiliwa na wataalam mbalimbali kama ifuatavyo;
Massamba (2009) anaeleza kuwa, lugha ni mfumo wa sauti za nasibu ambazo zimebuniwa na jamii kwa madhumuni ya mawasiliano kati yao.
Vilevile Habwe na Karanja (2007) wanasema kuwa, lugha ni mfumo wa sauti nasibu na ishara za kisarufi ambazo kwazo watu wa jamii fulani ya lugha huwasiliana na kupokezana utamaduni wao.
Naye Mgullu (1999) akimnukuu Sapir (1921), anasema kuwa, lugha mfumo ambao mwanadamu hujifunza ili autumie kuwasilishia mawazo, maono na mahitaji. Mfumo huu hutumia ishara ambazo hutolewa kwa hiari.
Wataalamu hawa wanaonekana kufanana katika kuelezea maana ya lugha, kwani wote wanakubaliana kwamba lugha ni mfumo wa sauti za nasibu zenye maana zilizokubaliwa na jamii fulani ili zitumike katika mawasiliano miongoni mwao. Mambo muhimi yanayopatikana katika fasili hii ni pamoja na mfumo wa nasibu, wenye maana, kwa lengo la mawasiliano, na hutumiwa na binadamu.
Baada ya kuangalia maana ya lugha kutokana na wataalamu mbalimbali, ufuatao ni ufafanuzi wa maana za sauti za lugha kwa mujibu wa wataalamu mbalimbali.
Habwe na Karanja (wameshatajwa), wanasema sauti za lugha ni zile sauti zinazosaidia kujenga tungo zenye maana katika lugha.
Naye Massamba (kishatajwa) anaeleza kuwa sauti lugha kwa maana ya sauti ya lugha ni sauti yoyote itumikayo katika mfumo wa lugha ya mwanadamu.
Pia Massamba na wenzake (2004) wanasema kuwa sauti za lugha ni sauti zenye kubeba maana na ambazo hutumiwa na jamii fulani ya watu kwa madhumuni ya mawasiliano kati yao. Hii ina maana kuwa sauti za lugha ya binadamu ama zinaweza kufanana sana au kwa kiasi fulani na pia zinaweza zikasigana sana au kwa kiasi fulani tu. Massamba na wenzake wameonekana kuwaunga mkono Habwe na Karanja kwa kueleza namna sauti za lugha zinavyofuata mihimili katika kujenga tungo zenye maana katika lugha. Wao wanadai kuwa kuna uunganishaji wa sauti kuunda silabi au mofimu, uunganisha wa mofimu kuunda maneno na maneno kuunda tungo kubwa zaidi (sentensi). Sauti hizo katika lugha za binadamu kwa ujumla huitwa foni na zile za lugha mahususi huitwa fonimu.
Mtazamo wa wataalam walioorodheshwa hapo juu wanatofautiana katika kuelezea sauti za lugha ya binadamu.
Kwa kuanza na Jan Boudouin de Courtenay: Huyu ni mtaalamu aliyezaliwa mwaka 1845 huko Radzymin nchini Poland. Kwa mujibu wa Jones kama alivyonukuliwa na Massamba (ameshatajwa) anadai kuwa de Courtenay alianza kushughulikia nadharia ya fonimu na mabadiliko ya kifonetiki mwaka 1868. Lengo kubwa la de Courtenay lilikuwa ni kutaka kueleza tofauti kati ya fonimu na ala sauti.
Katika nadharia yake ya fonimu na mabadiliko ya kifonetiki alidai kuwa sauti za lugha ya mwanadamu ni za aina mbili yaani foni na fonimu. Hata hivyo de Courtenay hakutumia istilahi za foni na fonimu kama zinavyotajwa sasa, bali alitumia istilahi za “anthrop phonic” kwa maana ya foni, yaani sauti za kutamkwa tu na “psycho phonetics” kwa maana ya fonimu, yaani sauti za lugha.
Anaendelea kueleza kuwa, foni zipo karibu sana na taaluma ya kumwelewa binadamu pamoja na ala sauti zake ambazo kwa hakika hutofautiana sana na za wanyama wengine. Na kuhusu fonimu alisema kuwa, zinahusu kumwelewa binadamu pamoja na akili zake na namna anavyofikiri katika akili yake. Anadai kuwa mara nyingi binadamu hupokea kinachotamkwa na kufasiliwa.
De Courtenay kama alivyonukiliwa na Mgullu (1999) anadai kuwa, “fonimu ni tukio la akilini ambalo huwa na nia ya mzungumzaji au jinsi msikilizaji anavyomwelewa mzungumzaji au vyote viwili kwa pamoja.” Anaendelea kusema kuwa, “fonimu ni dhana ya kisaikolojia. Ni kipande sauti ambacho picha yake huwa akilini mwa mtu ambaye hukusudia aitoe wakati anapoongea.”
Mtalaam mwingine ni Ferdinand de Saussure (1857-1913). Huyu ni Mswisi ambaye alizaliwa mwaka 1857 huko Geneva. Hujulikana kama baba wa Isimu mamboleo (Muundo).
Moja kati ya mchango wake mkubwa katika taaluma hii ya Isimu ni kwamba aliweza kutofautisha mfumo lugha ambao ni ‘Langue’ na utendaji ambao ndio ‘Parole’. Katika dhana ya kwanza yaani Langue kama mfumo wa lugha mahususi anaueleza kuwa ni uwezo alionao mzungumzaji wa lugha mahususi na kuzungumza na kuelewa matamshi ya mzungumzaji mwingine wa lugha hiyo hiyo. Ni sehemu ya lugha inayowakisha maarifa kati ya sauti na alama, yaani ni mfumo wa alama kwa namna ya kiufundi tu.
Dai lake la msingi ni kwamba alama inategemea vitu viwili yaani kitaja (kiashiria) na kitajwa (kiashiriwa). Kitaja na kitajwa alizieleza kama alama za kiisimu. Kitaja au kiashiria ni umbo fulani la kusema au kuandikwa ambalo huwakilisha dhana fulani. Umbo hilo la kusemwa au kuandikwa ni kitamkwa au sauti ya lugha ya kusemwa na binadamu. Anapoeleza kitajwa au kiashiria ni kitu chenyewe kilichopo katika ulimwengu halisi wa vitu na dhana ambacho huwakilishwa na kiashiria fulani. De Saussure anatumia istilahi za “signify” (kitajwa) na “significant” (kitaja).
Anaendelea kusema kuwa, hakuna uhusiano wowote uliopo kati ya kitaja na kitajwa, uhusiano uliopo ni wa kinasibu tu. Ferdinand de Saussure alionesha uhusiano huu katika mchoro kama ufuatao.
Dhana (dhahania)
Kiashiria
.…………………... Kiashiriwa
Mchoro unaonesha kwa mstari uliokatika (…………….) kuwa uhusiano kati ya kiashiria na kiashiriwa si wa moja kwa moja. Hapa tunasema kuwa kitu kinachotajwa kinaweza kuwa ni kilekile lakini kila lugha inaweza kuwa na kiashiria chake cha kukitaja, kwa mfano:
Kiashiriwa: “kiti”. kwa kiswahili ni "kiti" lakini kwa kiingereza ni "chair"
Hivyo ili mawasiliano yafanyike mfumo wa ishara lazima ufahamike na ukubaliwe na wanajamii wote.
Katika dhana ya pili ya ‘Parole’ yaani utendaji anadai kuwa ni ule usemaji wenyewe wa lugha ambao hufanywa na kila mtu. Hili ni tendo la mtu binafsi. Mtu binafsi aghalabu atazingatia mfumo lugha ili aweze kuzungumza kwa usahihi kadiri anavyoweza.
Mtaalamu wa tatu ni Noam Chomsky. Huyu ni mwanaisimu wa Kimarekani anayevuma sana kwa mchango wake katika taaluma ya Isimu kwa ujumla. Dhana za umilisi (competence) na utendaji (performance) zimemfanya awe maarufu ulimwenguni kote.
Chomsky anadai kuwa mtu anapojifunza lugha huanzia na umilisi, umilisi ni ule ujuzi wa lugha ambao wazawa wa lugha fulani huwa wanao. Ujuzi huu ndio huwawezesha wazawa hawa kuzielewa na pia kuzitunga sentensi zote sahihi katika lugha yao pamoja na zile ambazo hawajawahi kuzisikia. Kwa maana hii umilisi ni msimbo (code) uliopo akilini mwa mtu ambao hutumiwa wakati wote mtu anapoongea.
Anaendelea kusema kuwa kwa kiasi kikubwa umilisi (ujuzi) wanaokuwa nao wazawa wa lugha moja hufanana. Utendi ni udhihirishaji wa maarifa ya mtumiaji wa lugha. Hii ndio sababu inayowafanya waelewane katika mazungumzo yao. Mzungumzaji anasema kile anachotaka kusema na msikilizaji anaelewa kile kilichosemwa na mzungumzaji .
Katika sauti za lugha ya mwanadamu anazungumzia fonimu kwa mtazamo wa kisaikolojia, ambapo anadai kuwa fonimu ni tukio la kisaikolojia, hivyo zipo kichwani mwa mzungumzaji wa lugha.
Hivyo tunaweza kusema kuwa, mitazamo ya wataalamu hawa inakaribiana kuhusu sauti za lugha ya mwanadamu. Jan Boudouin de Courtenay na Noam Chomsky wanaona fonimu ni tukio la kisaikolojia kwani zipo kichwani mwa mzungumzaji wa lugha. Pia Ferdinand de Saussure anatumia istilahi za langue na parole zinazokaribiana na istilahi za utendi na umilisi zilizotumiwa na Noam Chomsky. Langue na umilisi zinahusu maarifa ya lugha na parole na utenzi zinahusu udhihirishaji wa maarifa hayo. Wataalamu hawa wamefungua njia kwetu sisi wanataaluma pamoja na wataalamu wengine kuendelea kuchunguza taaluma hii ya sauti za lugha ya mwanadamu kwa kina.
Marejeo.
Habwe, J na Peter K. (2007). Msingi ya sarufi ya Kiswahili. Phoenix Publishers. Nairobi.
Massamba, D.P.B. (2009). Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha.TUKI. Dar es Salaam.
Mgullu, R.S. (1999). Mtalaa wa isimu: Fonetiki, Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili. Longhorn publishers. Ltd. Nairobi.
TUKI, (2004). Kamusi ya Kiswahili Sanifu. (Toleo la Pili). East Africa: Oxford University Press na Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili. (TUKI)
Je wajua Fonetiki na Fonoloji upo
uhusiano wa karibu?.
Taaluma ya fonolojia haiwezi kukamilika, na hata kueleweka iwapo hakuna linalosemwa kuhusuiana na taaluma ya fonetiki. Hii nikutokana na ukweli kuwa kuna uhusiano kati ya fonolojia na fonetiki. Massamba na wenzake (2004) wanaeleza ukweli huu kwamba: Fonetiki na fonolojia ni matawi mawili tofauti ya isimu lakini yenye kuhusiana sana. Uhusiano wa matawi haya unatokana na ukweli kwamba yote mawiliyanajihusisha na uchunguzi na uchambuzi unaohusu sauti za lugha za binadamu.
Kutokana na ukweli huu, jitihada za kufasili dhana ya fonolojia inaelekea kuwa nyepesi, dhana hizi mbili zinapofasiliwa kwa mlinganyo. Tuanze na fonetiki.
Fonetikini Nini?
Tunaweza kueleza kuwa Fonetiki ni tawi la isimu linalochunguza sauti za kutamkwa na binadamu ambazo huweza kutumika katika lugha asilia. Massamba na wenzake (kashatajwa) wanafasili fonetiki kuwa ni tawi la isimu linalohusika na uchunguzi na uchambuzi wa taratibu za utoaji, utamkaji, usafirishaji, usikilizaji na ufasili wa sauti za lugha za binadamu kwa ujumla. Wanasisitiza kwamba, kinachochunguzwa katika fonetiki ni (maumbo mbalimbali ya sauti zinazoweza kutolewa na alasauti za binadamu. Kipashio cha msingi cha uchambuzi wa kifonetiki ni foni.
Foni ni sauti yoyote inayotamkwa na binadamu na inayoweza kutumika katika lugha fulani. Hivyo basi, foni ni nyingi sana na hazina maana yoyote. Wanafonetiki hudai kuwa foni zimo katika bohari la sauti ambalo kila lugha huchota sauti chache tu ambazo hutumika katika lugha mahususi. Sauti chache zinazoteuliwa na lugha mahususi kutoka katika bohari la sauti huitwa fonimu.
Ama kuhusu matawi ya Fonetiki, ipo mitazamo miwili tofauti kuhusiana na matawi ya fonetiki. Mtazamo wa kwanza ni ule unaodai kuwepo matawi matatu; na mtazamo wa pili ni ule niunaodai kuwepo matawi manne. Mtazamo wa kuwepo matawi matatu ni pamoja na fonetiki matamshi, fonetiki akustika, nafonetiki masikizi. Mtazamo wa kuwepo matawi manne ni hayo hapo juu ukijumuisha na tawi la fonetiki tibamatamshi.
Fonetiki huchunguza jinsi sauti za lugha zinavyotamkwa kwa kutumia alasauti. Hususani, huchunguza namna na mahali pa kutamkia sauti husika. Fonetiki akustika huchunguza jinsi mawimbi ya sauti yanavyosafiri kutoka katika kinywa cha mtamkaji hadi kufika katika sikio la msikilizaji. Fonetiki masikizi hujihusisha na mchakato wa ufasili wa sauti za lugha, hususani uhusiano uliopo baina ya neva za sikio na za ubongo. Na fonetiki tibamatamshi ni tawi jipya lililozuka mwanzoni mwa karne hii, ambalo huchunguza matatizo ya utamkaji ambayo binadamu huweza kuzaliwa nayo au kuyapata baada ya kuzaliwa. Ni tawi linalojaribu kutumia mbinu za kitabibu kuchunguza matatizo na namna ya kuyatatua.
Je fonolojia ni nini?
Wanaisimu wanakubaliana kuwa Fonolojia ni taaluma ya isimu inayochunguza mifumo ya sauti za kutamkwa zinazotumika katika lugha asilia mahususi za binadamu. Inapolinganishwa na fonetiki, inasisitizwa kuwa fonolojia ni tawi la isimu linalochunguza mifumo ya sauti za lugha mahususi tu, kama vile sauti za kiswahili, Kiingereza, n.k. Hata hivyo, wapo wanaisimu wanaoelekea kukubaliana kuwa kuna fonetiki ya lugha mahususi pia, na kuna fonolojia ya jumla, na fonetiki ya lugha mahususi. Mathalani, Massamba (1996) licha ya kufasili kuwa fonolojia ni taaluma ya isimu inayochunguza mfumo wa sauti za lugha mahususi, anaenda mbele zaidi na kudai kuwa fonolojia inaweza kuchunguza sauti kwa ujumla wake bila kuzihusisha na lugha mahususi.
Pia wapo wanaisimu wengine wanadokeza msimamo kama wa massamba wanapodai kwamba fonolojia inaweza kuchunguzwa kwa mitazamo miwili tofauti, ambayo ni fonolojia kama tawi dogo la isimu linalochunguza mfumo na ruwaza za sauti za lugh mahususi ya binadamu, na fonolojia kama sehemu ya nadharia ya jumla ya lugha ya binadamu inayohusika na tabia za jumla za mfumo wa sauti za lugha asili za binadamu. Katika mhadhara huu, hata hivyo tutakuwa wafuasi wa mtazamo unaoona kuwa fonolojia ni tawi la isimu linaloshughulikia mfumo wa sauti za lugha mahususi, hivyo tuna kwa mfano, fonolojia ya Kiswahili, fonolojia ya Kiingereza, fonolojia ya Kiha, fonolojia ya Kihehe, na fonolojia ya Kibena fonolojia ya kikuria na kadhalika. Kipashio cha msingi cha fonolojia ni fonimu.
Fonimu.
Ni kipashio kidogo kabisa cha kifonolojia kinachoweza kubadili maana ya neno. Hivyo basi, fonimu ina maana, kwa kuwa inaweza kubadili maana ya neno inapobadilishwa nafasi katika neno husika. Foni chache zilizoteuliwa kutoka katika bohari la sauti ili zitumike kwenye mfumo wa sauti za lugha mahususi ndiyo fonimu. Hivyo, fonimu ni chache ikilinganishwa na foni. Idadi ya fonimu za lugha hutofautiana kati ya lugha moja na nyingine. Mathalani, Kiarabu kina fonimu ishirini na nane (28), Kiswahili kina fonimu thelathini (30), Kifaransa kina fonimu thelathini na tatu (33) na Kiingereza kina fonimu arobaini na nne (44). Sauti ambayo huweza kubadilishwa nafasi yake katika neno lakini maana ikabaki ileile huitwa alofoni.
Alofoni ni kipashio cha kifonolojia kinachotaja hali ambapo fonimu moja hutamkwa na kuandikwa tofautitofauti bila kubadili maana ya neno. Mfano: Fedha na feza, Sasa na thatha, Heri na kheri
Kwa kifupi, alofoni ni matamshi tofautitofauti ya fonimu [sauti] moja.
Mitazamo juu ya Dhana ya Fonimu.
Juhudi za kufasili dhana ya fonimu zilizofanywa na wanaisimu mbalimbali zimezua mitazamo mbalimbali ya namna ya kuchambua dhana hii. Hadi sasa, mitazamo mitatu ifuatayo ndiyo hujulikana zaidi.
( a ) Fonimu ni tukio la Kisaikolojia.
Huu ni mtazamo uliokuzwa na kutetewa na wanasarufi geuzi-zalishi, mwanzilishi wake akiwa ni Noam Chomsky. Kwa mujibu wa mtazamo huu, fonimu ni dhana iliyo katika akili ya mzungumzaji wa lugha. Mtazamo huu unadai kuwa kila mzungumzaji wa lugha ana maarifa bubu ya idadi na jinsi ya kutamka fonimu za lugha yake Chomsky anayaita maarifa haya kuwa ni umilisi (competence). Anadai kuwa maarifa haya ya fonimu hufanana kwa kiasi kikubwa miongoni mwa wazungumzaji wa lugha moja husika. Kinachotofautiana ni jinsi ya kudhihirisha (kutamka) fonimu hizo, yaani utendaji (performance). Chomsky anabainisha kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kuhitilafiana baina ya umilisi na utendi kutokana na matatizo mbalimbali ambayo mzungumzaji hukabiliana nayo. Matatizo hayo ni kama vile uchovu, ulemavu wa viungo vya matamshi (alasauti za lugha), athari za mazingira, ulevi na maradhi na kadhalika . Hivyo kutoka na hali hii, fonimu hubaki kuwa tukio la kiakili, yaani kisaikolojia tu.
( b ) Fonetiki ni tukio la Kifonetiki.
Wafuasi wa mtazamo huu wanaongozwa na Daniel James. Ambaye anaiona fonimu kuwa ni (umbo) halisi linalojibainisha kwa sifa zake bainifu. Anadai kuwa fonimu huwakilisha umbo halisi la kifonetiki na inapotokea kukawa na fungu la sauti katika fonimu moja, sauti hizo huwa na sifa muhimu za kifonetiki zinazofanana.
( c ) Fonimu ni Fonolojia.
Huu ni mtazamo wa kidhanifu, ambapo huaminika kuwa fonimu ni kipashio cha kimfumo, yaani fonimu huwa na maana pale tuinapokuwa katika mfumo mahususi. Mwanzilishi wa mtazamo huu ni Nikolai Trubetzkoy. Yeye huamini kuwa fonimu ni dhana ya kiuamilifu na uamilifu huu hujitokeza tu fonimu husika inapokuwa katika mfumo wa sauti wa lugha husika. Kwa mujibu wa mtazamo huu, fonimu ni kipashio kinachobainisha maana ya neno. Mtazamo huu hutumia jozi sahihi kudhihirisha dai lake. Mathalani, maneno baba na bata yana maana tofauti kwa sababu ya tofauti ya fonimu /b/ na /t/. Mtazamo huu hujulikana kuwa ni wa kifonolojia. Na kwa hakika, mawazo haya ndiyo yaliyoshika mzizi zaidi katika taaluma ya fonolojia na ndiyo inayofunzwa hivi sasa katika sehemu nyingi ulimwenguni.
Tunaweza kuonyesha uhusiano huo hapa kati ya Fonetiki na Fonolojia
FONETIKI
|
FONOLOJIA
|
HuchungasautizakutamkwanaBinadamu
|
HuchunguzasautizakutamkwanaBinadamu
|
Ni pana {huchunguzasautinyingi}
|
Ni finyu
{huchunguzasautichachetu}
|
Ni
kongwe.
|
Ni
changa.
|
Huchunguzasautipekepeke
|
Huchunguzasautikatikamfumo.
|
Huchunguzasautikwaujumla
|
Huchunguzasautizalughamahususi,
kama Kiswahili, naKinyeramba.
|
Kipashio
cha msinginifoni
|
Kipashio
cha msinginifonimu.
|
Tofauti yaFoninaFonimu.
FONI
|
FONIMU
|
Hazimamaana
|
Zinamaana
|
Zipopekepeke
|
Zimokatikamfumo
|
Nyingi
|
Chache
|
Huwezakujitokezakamaalofoni
|
|
Zinaponukuliwa,
alama ya mabano, “[ ]” hutumika
|
Zinaponukuliwa,
alamayamabanomshazari, “/ /” hutumika
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni